Wali maharageBeef lasagne ni utopolo.
Chicken pizza ni takataka!
Wali maharage best food ever
Duh, karibu nicheke! 🤣 🤣 🤣Wali maharage
samaki nchanga, nlikula nachingwea, nikauliza mbona mishkaki mwekundu namna hii?Mambo vipi wanaJF natumai mko poa. Kwenye misosi kuna kuwa na kile chakula una hamu nacho au tu umekuta sehemu kimepikwa kwasababu hujawahi kula unaamua kula huo msosi kwa mara ya kwanza lakini chakula hicho kina kushinda kabisa hata kukupelekea kujisikia vibaya.
Mimi miaka ya nyuma nilikuwa nasikiaga kuhusu supu ya kongoro siku na mimi nikaamua nijue ikovipi hiyo supu nikaenda sehemu nzuri tu nikaulizia nikaambiwa ipo basi nikaletewa pale nikaanza kuipiga lakini kidogo tu nilikula kama vipande viwili tu vya ile nyama nikajisikia kuchefuchefu vibaya sana hata hiyo nyama kumeza haimezeki nikaacha supu karibia yote pale hadi leo hii sitaki tena kusikia kuhusu hiyo supu
Nyingine hii ilikuwa ni juisi ile ya rozela nilikuta imetengenezwa sehemu nikanywa glasi moja ilikuwa na ladha nzuri tu lakini baada ya hapo nilijisikia vibaya sana kama kizunguzungu mara kama mwili unataka ku vibrate mara jasho linatoka japo kulikuwa na feni yaani ilikuwa ni shida mpaka leo nikiiona hiyo juisi naipitia mbali kabisa. Hata juisi ya miwa ilinishinda kabisa ni bora nile muwa kama muwa
Vipi kwa upande wenu wadau ni kitu gani ulikula lakini baada ya hapo hutaki tena kukila.
Ila we jamaa fix kweli. Tka lini hujui kiswahili na tunashinda wote kwenye mbege kila ckSawa sawa mkuu ila fanya utembelee bongo usije ukasahau kabisa asili yako.
Hii kitu ni hatari usijaribuKuna kitu moja ya kichaga inaitwa kitalolo 🤮🤮🤮
Hukuona dunia inazunguka chini juu juu chini 😂Nilionja ugoro hadi leo sitamani kabisa hata harufu yake
Mlenda kwakweli hata mimi ulinishinda.Mimi juice ya miwa na mlenda hivyo vitu siwezi
Chorokopia mimi hazipandi, na kabichi. Nikiwa ugenini nitakula tu kwa kujitahidi nisionekane mimi namna gani lakini kwakweli sipendiChoroko nilipata shida sana kuzimeza na nilikua ugenini