Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,625
Wakuu weekend inaendaje?

Usafi ni muhimu kila sehemu, na linapokuja suala la chakula mkazo zaidi unahitajika, maana ukizembea kidogo tu unaweza kuathiri vibaya walaji wako hata kupelekea kifo uchafu aliokutana nao hapo ni mkubwa na kutengeneza sumu kali.

Umeshawahi kukagua sehemu unayokula ukaangalia kama maji wanayotumia kuosha vyombo na kupikia ni masafi, kama vyombo unavyotumia vinasafishwa vizuri, au hayakuhusu ukifika unakula tu unasepa zako?

IMG_1129.jpeg

Pichani, ni sehemu ya chakula Dar ambako ilikuwa sehemu pendwa ya kupata mbuzi. Siku moja nikaona hayo maji kwa uzuri, maji ambayo yalikuwa yakitumika kusafishia visu vinavyokatia nyama, ndimu, pilipili, na ndio maji hayo walikuwa yanatumika kusafisha meza na sehemu ambayo nyama (ya ng’ombe, mbuzi, kuku) inawekwa kwaajili ya kukata vipande vya mteja.

Ili kusafisha anachovya kitambaa ambacho nacho rangi inaenda kufanana na maji hayo kwa kuuzoea uchafu huo.

Maji hayo kama unavyoyaona yalivyomachafu, bado kunakuwa na vimabaki vya chakula ambayo vinakuwa vinaanguka hapo akiwa anajiandaa kumfungia mteja, na kuna kisabuni kwa mbaliii!

Siku hiyo nikamfata jamaa aliyekuwa anawasimamia kumuuliza kwanini hawabadilishi maji wanayofanyia usafi hapo mpaka yanakuwa machafu hivyo, jamaa akasema akasema unajua hiyo ni leo tu yanabadilishwa sasa hivi, nilijua anadanganya ila nikamwambia sawa, nitafatilia jambo hilo. Nilichukua picha lakini niliipoteza, hivyo nikarudi siku nyingine maana nlijua ntakuta tu maji machafu.

Siku nyingine niliyoenda ndio nikachukua na picha hii, ambayo kwakweli uchafu ni ule ule tu.

Hii ni hatari, kama tumbo lako hoya hoya unaweza kupigwa na sumu ya chakula matata sasa. Mabwana afya huwa wanapita kweli sehemu hizi za vyakula na kuhakikisha usafi unafuatwa?

Sehemu unayokula ikoje Mkuu, usafi ni wa hali ya juu au tumemjachia mungu?
 
Mimi sio mpenzi wa kula migahawani ila tu ikitokea nikala nje ntaenda kwenye hotel ya hadhi kiasi
Muonekano wa hotel nzuri utaijua tu. Wahudumu walivyo na hata chef alivyo

Napenda usafi sana hata hotel za kulala huwa Nakagua kwanza kama haijaniridhisha naaga kwa heshima tu naenda nyingine
 
si wanasema ukimchunguza sana bata huwezi kumla
Nakazia… kuna mazingira yako wazi yanaogopesha, kuna mazingira yamejificha mpk uchokonoe… ndio maana kabla ya kula tunapaswa kuombea chakula 😂😂

kule Morombo kwenye mbuzi panaitwaje? mshamba_hachekwi nilienda mara 1, namna nilikuta hata kwenye gari sikushuka, na tokea hapo sijawahi kurudipo.
 
Sikumbuki nimeenda mara 1 tu😂
 
Mimi sio mpenzi wa kula migahawani ila tu ikitokea nikala nje ntaenda kwenye hotel ya hadhi kiasi
Muonekano wa hotel nzuri utaijua tu. Wahudumu walivyo na hata chef alivyo

Napenda usafi sana hata hotel za kulala huwa Nakagua kwanza kama haijaniridhisha naaga kwa heshima tu naenda nyingine
Hakuna hotel za ovyo kama hizo unazoita za heshima. Njoo tule kisinia Kwa Sele bonge
 
Niliona muuzaji anapiga chafya kwenye mbonga ya majani anayochambua bila kuzibq mdomo, nilichoka sana
Wengine kuchokonoa puaaa

Ndomana sehemu za kula jiko linakuwa wazi wapishi unawaona
Wanavyofanya madikodiko
Hapo angalau kidogo kuna kausalama

Ova
 
Bora umejiihami mapema 🤣🤣🤣
Ule Morena na vyakula vya usajili mpya ale nani?! Si umezoea kula mpishi na chakula chake wewe!!! 😂😂😂
Morena yenyewe Wana namba E kibao wanaotembeza msosi😁kikubwa nachokula kimetoka morena
 
Nakazia… kuna mazingira yako wazi yanaogopesha, kuna mazingira yamejificha mpk uchokonoe… ndio maana kabla ya kula tunapaswa kuombea chakula 😂😂

kule Morombo kwenye mbuzi panaitwaje? mshamba_hachekwi nilienda mara 1, namna nilikuta hata kwenye gari sikushuka, na tokea hapo sijawahi kurudipo.
Kwa morombo hivo hivo, mbona pako vizuri tu
 
Back
Top Bottom