Chakula gani ulikula mara moja na kwa mara ya kwanza hadi leo hutaki tena kukila?

1.Hoho iliyopikwa (on salads it's ok)
2.Macaroni
3.Dagaa(omena)
4.Kamba(harufu ya mafuta yake)
5.Nyama ya mafuta au utumbo original-ile Soft on both sides - (ule upande wa nywele nywele hivi, sina shida nikila)

Salamu toka nchi jirani ✌️
 
Mpaka sasa vyakula vinavyoongoza kwa kuchukiwa:
1. Kabichi: Kabichi tatizo lake kubwa ni mapishi. Haitakiwi ipikwe yenyewe, lazima itiwe vikorombwezo hasa nazi au ichanganywe na nyama nk ndio italika. Pia kabichi ni nzuri kama una mboga nyingine mf maharage
2. Choroko: Choroko japo sio nzuri saana, ila kidogo zikipikwa na nazi nyingi zinavumilika na unaweza kula na wali tu, sio ugali pls! Pia ukiwa na mboga ya majani pembeni itasaidia zaidi
3. Mlenda: Mimi binafsi kama mlenda ndio chakula pekee kilichobaki duniani, basi mi ntakufa njaa tu sitakua na namna nyingine
4. Njugu mawe + mbaazi: hizi kwakweli tukubaliane tuu hata mimi mwenyewe hazipandi ni kula usife mradi siku kuzisogeza
5. Kongoro: Kongoro lile hua halina mapishi mengine zaidi ya hayo, kwahiyo kama huliwezi unaacha tu, haina kubembelezana
6. Utumbo: Utumbo una sheria mbili kuu za kuupika ili ulike: 1) Kabla ya kuupika hakikisha UNAUOSHA SANA ikiwezekana tumia sabuni, jiki, stili waya nk we osha tuu! 2) Chemsha sanaa kuanzia masaa manne na kuendelea hakikisha umelainika kabisa ndembendembee! Ukizingatia hayo, utahitaji kitunguu swaumu na kitunguu maji tu unapata bonge la kituu.. au unaunga na kabichi/mchicha na nazi unakula ugali mkubwa hivi.....!

Itaendelea
 
Hapo namba sita, dah. Utumbo waupitisha kwa waya na sabuni, wewe dingi kweli! 🤣 🤣 🤣
 
Siku moja tumetoka shule, nlikuwa f3 kama sikosei. Kulikuwa na jamaa anaitwa amani alikuwa anakula sana kuber na nlikuwa namwona mjanja kwani madem walikuwa wanamshobokea balaaa maana mda wote macho mlegezo anakuwa kama kalewa hivi.
Basi bwana siku tumetoka shule mchana kabla ya lunch.
Nikamwambia nataka kutest kidogo kuber ya kienyeji, maana yy alikuwa anapiga ya kutengenezwa locally sababu ashakuwakonkord ya dukani imepozwa.
Akanichotea vidole vitatu akaniambia weka kwenye fizi.
Nikawa nanyonya maji baadae nikaimeza. Bwanabwana kama nusu saa hivi nikahisi kizunguzingu utumbo kama kuna mtu anakoroga na mwiko yaan nlitaka kufa sijui. Nikaenda kulala hata sikula.
Toka hapo nikisikia harufu ya kuba nahosi kichefuchefu
 
Back
Top Bottom