Jamani, kuna suala linanisumbua kidogo. Chakula umenunua mwenyewe, umekileta nyumbani, mpishi ni wako mwenyewe, umepikiwa, chakula kimeiva, kipo mezani.
Kuna ulazima kila unapotaka kula, uombe ruhusa kwa mpishi?
Bidhaa ni universal set, na chakula ni member wa hiyo universal set........we wanunua bidhaa au chakula?
vipi tena, mbona waguna?Mmmhhh!
Jamani, kuna suala linanisumbua kidogo. Chakula umenunua mwenyewe, umekileta nyumbani, mpishi ni wako mwenyewe, umepikiwa, chakula kimeiva, kipo mezani.
Kuna ulazima kila unapotaka kula, uombe ruhusa kwa mpishi?
Kama watoto wamelala na chakula kipo mezani, bado uombe ruhusa?kwa utaratibu mzuri nabidi uombe maana huwezi kujua kama hicho chakula ni chako au cha watoto. Inawezekana wewe unapikiwa chakula spesheli!
Steve Dii,Ni mazoea mazuri kufanya hivyo. Maana chakula kilichoiva na kutengwa mezani yeyote yule anaweza kukila. Hivyo pale unapofanya hilo ombi kuanza kumega, ni sawa na mtu anapodonyoa namba kwenye ATM pesa zianze kumiminika; pin number ni yeye pekee aijuaye. Basi na utamu wa kilichotengwa mezani anaufaudu yeye mwenyewe maana anakuwa anabonyeza pin namba ya kweli.
Steve Dii,
Hata kama ni mazoea, nakubali ni tabia njema kuomba ruhusa, Lakini ndio kila wakati? maana kama mpishi umemzoea, na mapishi yake wayajua, walahi hata chakula kinapowekwa mezani lazima utajua ni kwa ajili yako. Sasa kwanini uombe ruhusa? Au waogopa ukikifakamia bila ruhusa, ukitaka kuomba chumvi waweza nyimwa?
...kwahiyo hamna haja ya kuomba ruhusa ee?Kaka jambazi mbona huyu anakataa....we unakula tu kama kimeiva na nichamoto. Kama sio cha moto ndo unawwza kuomba kipashwe moto coz unataka kumega ugali.
Kama watoto wamelala na chakula kipo mezani, bado uombe ruhusa?