Chakula chako mwenyewe, ruhusa ya nini?

Mundu

JF-Expert Member
Sep 26, 2008
2,707
638
Jamani, kuna suala linanisumbua kidogo. Chakula umenunua mwenyewe, umekileta nyumbani, mpishi ni wako mwenyewe, umepikiwa, chakula kimeiva, kipo mezani.
Kuna ulazima kila unapotaka kula, uombe ruhusa kwa mpishi?
 
we wanunua bidhaa au chakula?
 
rukhsa baba tafuna msosi huo wewe ndo mmiliki na mtafutaji wa hicho chakula mega mkuu bila kuomba kokote kule
 
Jamani, kuna suala linanisumbua kidogo. Chakula umenunua mwenyewe, umekileta nyumbani, mpishi ni wako mwenyewe, umepikiwa, chakula kimeiva, kipo mezani.
Kuna ulazima kila unapotaka kula, uombe ruhusa kwa mpishi?

ni ustaarabu tu.....kama kumwambia muuza duka NAOMBA SODA wakati unailipia kwa hela yako
 
kwa utaratibu mzuri nabidi uombe maana huwezi kujua kama hicho chakula ni chako au cha watoto. Inawezekana wewe unapikiwa chakula spesheli!
 
Kama watoto wamelala na chakula kipo mezani, bado uombe ruhusa?
 
Ni mazoea mazuri kufanya hivyo. Maana chakula kilichoiva na kutengwa mezani yeyote yule anaweza kukila. Hivyo pale unapofanya hilo ombi kuanza kumega, ni sawa na mtu anapodonyoa namba kwenye ATM pesa zianze kumiminika; pin number ni yeye pekee aijuaye. Basi na utamu wa kilichotengwa mezani anaufaudu yeye mwenyewe maana anakuwa anabonyeza pin namba ya kweli.
 
Steve Dii,

Hata kama ni mazoea, nakubali ni tabia njema kuomba ruhusa, Lakini ndio kila wakati? maana kama mpishi umemzoea, na mapishi yake wayajua, walahi hata chakula kinapowekwa mezani lazima utajua ni kwa ajili yako. Sasa kwanini uombe ruhusa? Au waogopa ukikifakamia bila ruhusa, ukitaka kuomba chumvi waweza nyimwa?
 
Nimekuambia kuwa lile ombi ni sawa na password tu. Mambo ya formalities na protocol mkuu. Mtu hata ukiwa na master key, bado ukitoka unafunga mlango ili ukicha baadae uchomekee ufunguo ili kufungua just incase kama kuna mwehu mwingine atakuwa amebadilisha kufuli. Ukiwa na safety box ya pesa huwezi kuicha wazi baada ya kuifungua, hata kama pesa mle ndani ni zako na hiyo sefu umenunua mwenyewe na kuiweka ndani. Kuomba kula ni moja ya protokali katika kufaudu msosi wako. Vipi iwapo kuna panya au nzi amejaribu kuonja kabla yako? Utajuaje msosi unalika usipoomba ruhusa na kupata go-ahead ya mpishi??
 
Ruksa muhimu kuomba.pengine chakula kiko mezani lakin kuna vi2 vingine mpishi pengine anataka kuongeza ndo kiwe murwa zaidi..nyama choma huez kula kavkav mpaka kachumbari..ruksa na subra mkuu.
 
Kaka jambazi mbona huyu anakataa....we unakula tu kama kimeiva na nichamoto. Kama sio cha moto ndo unawwza kuomba kipashwe moto coz unataka kumega ugali.
 
...kwahiyo hamna haja ya kuomba ruhusa ee?
 
Kama watoto wamelala na chakula kipo mezani, bado uombe ruhusa?

Naam yawezekana hawajalala vizuri, si unajua chakula ingine ni soo haifai hata mtoto kusikia.

.......................................

Amani yetu inatumiwa vibaya.
 
hehehee! Siku utakula limbwata la kumfukuza mama mkwe ndo utajuuta! Subiri ruhusa bana, sio kila siku chakula chaliwa na mkono ati!
 
mm naomba niite "tusubiri kukaribishwa" ndipo tuanze kula hata kama ni mkeo kaandaa meza. tukisema kuomba ruhusa, it sounds like unasema "naomba nile" wakati mazoea si hivyo. meza ikiwa tayari utasikia tu, baba karibu chakula huku ukilengeshewa jagi unawishwe.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom