Chakula cha baba kitengwe pembeni kama zamani?

Miss Natafuta

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
25,546
45,835
Kuna familia moja naifahamu ina mke, mume, mtoto mmoja, mdogo wa mke wa kike, wa kiume, binamu wa mke beki tatu, mtoto wa dada wa mke na pia kuna ndugu wawili wa mume.

Huyu mume ana mchepuko. Nimenotisi kule kwa mchepuko jamaa anakula vizuri mno maana mchepuko uko peke yake.

Mimi sio mmbea ilitokea tu nikajua. Nilimuuliza mchepuko kwanini unatembea na mume wa mtu tena unaemjua? Akaniambia jamaa anampenda mno akimuacha atakufa njaa.

Mimi sielewi ila ndo hivo mlio na familia ndefu mjipange chakula cha baba mtenge kwa special hot pot mtaachwa.

Inaelekea jamaa home kwake hali vizuri maskini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbunye ndiyo yenyewe, mwanaume hachepuki kwa kufuata kula basi tungekuwa tunashinda kwa akina mama lishe
 
Back
Top Bottom