Chahali na Uenyekiti wa Mbowe CHADEMA

Chahali na Uenyekiti wa Mbowe CHADEMA

Tuwekee hapa kipengele cha katiba ya ccm kinachoruhusu uhuni huu wa kutokuwa na uchaguzi wa ushindani ndani ya ccm ngazi ya Taifa.

Pili tueleze Mtuliabna Dr Mollel ni lini walichukuwa fomu zankuomba kugombea ubunge na lini kura za maoni zilipigwa na ni lini kikao cha kamati kuu ya ccm kilikaa kufanya uteuzi?

Na kwenye chama hakuna kitu kinachoitwa utamaduni, chama kinaendeshwa kwa katiba na kanuni zake.

Upuuzi huu wa utamaduni waeleze mazuzu wenzako wanaotumia tumbo kufikiri ambao wanawahubiria vijana kujiajiri wakati wao wenyewe ni majobles wanaishi kwa kitegemea kujipendekeza uvccm ili wapate posho na ukatibu wa wilaya.
Twende kwenye mada kaka! Suala mezani ni Ukomo wa Mwenyekiti wa CHADEMA.

Haya nimajibu ya John Mnyika katika uzi aliouandika Pascal Mayalla mwaka 2015 (Bofya hapa kusoma zaidi)

"Pasco, Pamoja na marekebisho niliyoeleza kuhusu majibu ya Dr Slaa kwamba katiba ya 2004 iondolewe kwenye orodha kama nilivyochangia hapo awali. Katiba ya mwaka 2004 haiwezi kuwa ushahidi wa hayo madai yasiyokuwa ya kweli. Katiba ya mwaka 2004 mimi ninayo hapa nilipo, kwenye kifungu cha 6.3.2 kina kipengele cha 'muda usiozidi vipindi viwili katika cheo kimoja kwa ngazi moja'. Hata hivyo, huu sio ushahidi wa kwamba kipengele hiki kimeondolewa 'kinyemela'.

Hii ni kwa sababu tatu; Mosi, 2006 hatukuwa tunafanya marekebisho ya katiba kwa maana ya kuondoa au kuacha kifungu cha katiba ya mwaka 2004. Tuliandika katiba upya, ndio maana tarehe 13 Agosti 2006 pale PTA tukafanya uzinduzi wa katiba mpya ya CHADEMA.

Kwenye mchakato wa kukusanya maoni ya katiba mpya na hatimaye maandalizi ya rasimu ya katiba mpya, hili suala halikuingia kabisa.

Halikupitishwa kwenye mapendekezo ya sekretariati, kamati kuu, baraza kuu na hata mkutano mkuu kwa kadiri ya kumbukumbu zangu. Hivyo huwezi kuzungumzia 'kuondoa kinyemela' kipengele ambacho hakikuingia.. JJ"
 
"Kirefu cha CHADEMA ni Chama cha DEMOKRASIA na Maendeleo. Sasa ni demokrasia gani hiyo ambayo inaruhusu mwenyekiti mmoja kuwa madarakani milele? What if “uenyekiti wa milele” ni miongoni mwa vikwazo kwa maendeleo ya chama hicho?" Evarist Chahali
Hii inatoka Lumumba baada ya kuona Kiongozi wa kambi rasmi bungeni amewamudu vizur
 
na ukiwasema unalaaniwa eti

Katiba ya CHADEMA "x. CHADEMA itashughulikia matatizo ya viongozi nawanachama kwa kufuata taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa Katiba ya Chama, wala hata siku moja haitashughulikia mambo kama hayo Mahakamani. Mwanachama atakayeshindwa kufuata taratibu na ngazi za Chama hatavumiliwa na atafukuzwa uanachama."
 
Chadema ni kama kanisa la kilokole, mwenye kanisa ndio askofu wa maisha. Kwa mfano unamtofautishaje Mbowe na Gwajima?!......wote ni viongozi wa kudumu!
Navipi kuhusu ccm kutawala tangu Uhuru hiyo wee haikusumbui?
 
Unalidhika na ccm Kuwa madarakani
Katiba ya chadema kabla ya kufanyiwa marekebisho mwaka 2006 yaliyoondoa kipengele hiki kwa kisingizio cha kuweka katiba mpya
ukomo-wa-uongozi-ulionyofolewa-kinyemela-2006-png.233613
 
Billicanas hajaporwa ni kujigeuzia mali ya umma kuwa ya kwake kwa kutegemea huruma za wananchi! Eti Mwenyekiti afu hutaki lipa kodi!
Suala la kujichukulia maamuzi ya kulima kwenye catchment area siliungi mkono hata kidogo.
Suala la muundo wa upatikanaji kiongozi lisikupe shaka ni desturi ya chama kupokezana vijiti kila ufikapo ukomo wa uongozi na inafahamika hivyo na iko wazi katika katiba ya chama!

HOJA: Niambie uongozi wa CHADEMA katika nafasi ya uenyekiti ni miaka mingapi mingapi kwa muhula mmoja?
Ni lini amewahi itisha hata uchaguzi wa uongo uongo ili mpige kura ya kuchagua au kupendekeza mwenyekiti?
NI muundo upi wa demokrasia unayoizungumzia mliyoitumia kumpitisha LOWASA kuwa mgombea wenu wa uraisi kupitia CHADEMA na UKAWA kwa ujumla?
Vipi ccm Kutawala kwa nguvu tangu Uhuru hii kwako sio Shida?
 
Unazungumzia kipindi tumetoka kupata uhuru nionavyo mimi b4 tanzania ikombolewe ikombolewe kwanza chadema kutoka mikononi mwa familia kiwe chama huru cha wanachama
Kwanini tusianze kuikomboa Nchi kutoka kwa Mkoloni mweusi Kwanza ccm
 
Navipi kuhusu ccm kutawala tangu Uhuru hiyo wee haikusumbui?
CCM ni taasisi na inafuata katiba yake, na ndio maana wananchi wamekuwa wakiiamini na kuipa dola. Na tangu uhuru viongozi wanabadilishwa kwa kuzingatia katiba ya chama na katiba ya JMT
 
Mshana unalidhika na muda wa mwenyekiti mamlakani?, ni Kweli Mbowe si kikwazo kwa maendeleo ya chadema Kwa sasa?, du!

Inakubidi uelewe kuwa CHADEMA mpaka sasa ina miaka 26 na imeshakuwa na wenyeviti watatu. Hiyo ni wastani wa miaka 8 kwa kila mwenyekiti wakati CCM/TANU ina miaka 64 na ishakuwa na wenyeviti 5 mpaka sasa na hivyo kuwa na wastani wa miaka 13 madarakani akiwemo na JPM. Sasa sijui hizi kelele zako ni miluzi au mbinja?
 
Kukalia madaraka kwa muda mrefu kama anavyofanya Mbowe si sahihi kwenye zama hizi ambazo Demokrasia inapiganiwa nchini Tanzania.ni kweli kuwa Mbowe amefanya mageuzi makubwa ndani ya chama hicho, lakini hiyo haiwezi kuwa sababu ya yeye kuwa mwenyekiti wa maisha. Chadema ni taasisi, tunaamini ndani ya chadema kuna watu wengi wenye uwezo wa kufanya mageuzi zaidi ili kuipeleka mbele zaidi chadema
Vipi kuhusu cccm kutawala kwa nguvu tangu Uhuru hii huamini kama ni tatizo la Nchi hii?
 
wanampora mpaka wabunge!
Hivi ni ahadi gani Zitto Kabwe hajakutimizia mpaka umemgeuka kiasi hiki? Au ni kweli hii ID ilikuwa ni taasisi kama ID ya Tuntemeke?

Maana aliyekuwa anamiliki ID hii ya Waberoya kipindi kile alikuwa kichwa hasa na mfuasi hasa wa Zitto, lakini siyo Waberoya huyu mrenda kichwa kimejaa fungus.
 
Back
Top Bottom