Chaguzi ndogo 16/6 na 14/7 majumuisho na tathmini

ivi aiwezekani wapinzani kuungana wakaweka pembeni itikadi zao tukajenga nchi,nimeona kata ya mnima huko mtwara imeonesha wapinzani wananguvu kuliko chama tawala tufike mahali wa tz tubadilike ukombozi wakweli auwezi kuja kwa itikadi ya vyama
 
Mtu wa Shamba umeeleweka vizuri sana natumia simu ningekungoea like

hii naiprint ikae kwenye hard copy
 
Pasco umebaki muda mfupi tu kabla ya chadema haijakabidhiwa nchi huo ukuu wa wilaya unaoutafuta utausikia kwa wenzako kwa muda uliobaki,lkn pia una fikra kwamba chadema bado changa ok! Nijuavyo mm mamayako akikwambia huyu ni baba yako hata kama hana ndevu yakupasa ukubali tu.
 
Tathmini nzuri na hii ya kudhorora kwa kwa ccm naifananisha na production life circe ya kwenye uchumi kwa sasa ni wakati wao wa kudetorerate n wasipotafuta alternative approach basi watakuwa wakipoteza jimbo moja baada ya jingine na mwisho wake ikulu na ndicho tukitamanicho wapenda mabadiliko
 
Pasco,

CCM haijengi flyover ni kodi za wananchi wote, hata rapid transport ni kodi zetu, CCM yako inatoka wapi Mzee wa bonafide genuine?
 
Asante sana,mchanganuo mzuri sana,mwenye macho haambiwi tazama,kwa tathmini yangu CHADEMA ndicho chama pekee sasa kinachokubalika,hawajapoteza kata hata moja kwa zile walizokuwa wanakubalika awali lakini pia wamewanyang'anya CCM kata 3 na upinzani mwingine kata 2.Wamepata kata mpya 5!Ni ushindi wa kishindo!
 
mkuu hizi ndio mambo tunazohitaji sio maneno mingi vitendo 0.001.. hongereni wote mlioshinda chaguzi na poleni wote mliopigwa chini jipangeni 2015 mnaweza shinda..
 
Pasco umebaki muda mfupi tu kabla ya chadema haijakabidhiwa nchi huo ukuu wa wilaya unaoutafuta utausikia kwa wenzako kwa muda uliobaki,lkn pia una fikra kwamba chadema bado changa ok! .
Mkuu Pelekete, huwezi amini, kuna type fulani ya watu wachache wa aina yangu ambao kwetu ukuu wa wilaya sio deal kabisa!. Kwa ukaribu nilionao na hozo top corridors, ingekuwa U DC kwangu ni deal, ningeshakuwa siku nyingi!, ningeanzia tuu na kukata kadi ya CCM, mengine yote yangefuatia!, maskini Pasco mimi, hata kadi ya CCM sina, leo ukuu wa wilaya upi ninaupumulia?!.

Nimeipenda hii ya kwenye bold, kumbe unatambua kuna kukabidhiwa nchi!, wakati wewe ukiconcentrate kusubiria kukabidhiwa, mimi ninamuimagine huyo mkabidhi, atamkabidhi nani?. Kabla mkabidhi hajakabidhi, kwanza anamtathmini mkabidhiwa, ataweza kuubeba huo mzigo anaotaka kukabidhiwa?!. Ili mkabidhiwa aweze kukabidhiwa, lazima aonyesha utayari wa kuubeba huo mzigo!, tena utayari ni kitu mimoja na uwezo wa kubeba ni kitu kingine!. Kwanza aonyeshe utayari tuu, akabidhiwe ndipo aonyeshw uwezo!, hayo yote kwa Chadema wewe umeyaona?!.
Pasco.
 
hiki ndicho kinachofaa kufanya,yaani uchambuzi wa matukio bila kumung'unya maneno.
analysis yako nimeikubali mkuu
 
Wakati wana wa Arusha wakitoa funzo kwa maeneo mengine ya nchi, watawala na makada lukuki wa CCMkwamba upole si ujinga, mie nitapendelea kuzungumzia kupungua kwa idadi ya wapiga kuraunaokadiriwa kufikia asilimia 60.
Zipo sababu nyingizinazoweza kutolewa, lakini mimi nimeona sababu moja kubwa kwamba MBINU yaserikali kuachia mnyama wa mbuga ya GOMBE kurandaranda katika maeneoya jiji la Arusha, (kama suprise kwa wasiotembelea mbuga za wanyama) hasa wakati wa kampeni ya nyumba hadi nyumba.
Wataalamu wamesemahili limesababisha mambo mawili:
1. Wapiga kura wengi ambao mnyama huyo hakwaamefika majumbani mwao, walibaki majumbanimwao ili mgeni asiwakose.
2. Wapiga kura wengine waliogopa kutokamajumbani mwao kwa kuhofia kukutana na mnyama huyo ambaye japo anafanana nabinadamu, bado anatisha kwa mwonekano wake.
Kwa upande wa CCM,wao walijikita katika kueneza propaganda za kipuuzi kabisa katika jiji laArusha ikiwemo kudaiwa kusambaza vijana wao wa GREEN GUARDS kupanga na kuanzisha fujoili kuwasingizia vijana wa CHADEMA. Kwa kuwa fujo ni mtego wa panya, watuwengi waliofia usalama wao.
La mwisho, kupunguakwa wapiga kura ni dalili tosha kwamba CCM imechokwa. Nasema imechokwa kwasababu kwa kawaida KADA wa CCM huwa hakosi kwenda kupiga kura. Ni kosa kubwakwa mwana CCM kutoenda kituoni siku ya uchaguzi. Na kama kura zilizotolewazinamaanisha hilo:
1. CCM imeendelea kukosa ushawishi miongonimwa wanachama wake.
2. CCM imepunguza wapiga kura kwa kadritunavyoelekea 2014/2015.
Hizo ndizo nilizowezakuona, wengine mnaweza kuongezea.
HONGERA wana ARUSHA.
HONGERA CHADEMA.
 
CCM haijengi flyover ni kodi za wananchi wote, hata rapid transport ni kodi zetu, CCM yako inatoka wapi Mzee wa bonafide genuine?
"Mlilala hundingwa ndingwa, mwemacho haambiwi tule", 2015 inakuja, chakula kinawekwa mezani, subiria sasa kujua aliyelala ni nani na aliye macho ni yupi!. Atakayecheka mwisho ndio atakayecheka zaidi na atakae lia mwisho ndie atakaye lia sana!. Sisi wote tupo humu, subiria 2015 ni nani atacheka na nani atalia mwisho, tutakumbushana!.
Pasco
Mzee wa BG!.
 
Back
Top Bottom