Chaguzi ndogo 16/6 na 14/7 majumuisho na tathmini

Chadema kimeendelea kupata ushindi mnono kutokana na kupendwa!. Nakijiuliza Chadema kimefanya nini kustahili kupendwa huku, sioni kitu!. Chadema kinaendelea kushinda kwa sababu CCM imechokwa, na inachukiwa, hivyo kuna maeneo hata Chadema wangesimamisha jiwe, jiwe lingeshinda!. Hivi ndivyo hali ilivyokuwa kwa baadhi ya ushindi wa Chadema kwenye uchaguzi wa 2010, kuna wabunge na madiwani wa Chadema wameshinda, ukiangalia any substance ya ushindi wao, huioni, ila wameshinda simply kwa sababu CCM imechokwa!.

All the best.
Pasco.

"Nakijiuliza Chadema kimefanya nini kustahili kupendwa huku, sioni kitu!."

Mkuu, hapa hujasema kweli!! ....yaani huoni tofauti kati ya hoja za mwenyekiti wa CCM na wa CDM? Hoja za katibu mkuu wa CCM vs CDM?! N.K hoja za wabunge wa CCM na wa CDM?......
Chama cha upinzani hakipendewi kwakuwa kimefanya nini....kinapenwa kwa hoja zake kwamba kitafanya nini? kweli PASKALI hujui?!
 
Mungu taratibu anaanza kujibu maombi ya watanzania. Uzuri ccm hawajui wafanye nini ili warudishe ari ya watanzania wanatumia polisi na mabomu!
 
Maeneo yenye umaskini Mkubwa bado ccm inaonekana kushinda kirahisi, tathmini inaonesha bado pilau na vijipesa imekuwa ni sababu ya ccm kushinda maeneo hayo

Kuichagua CCM ni kulipigia jeshi la POLISI kura, yaani unakubaliana na unyama wanaowafanyia raia wenzetu, kung'oa kucha, kung'oa meno, kutumwagia tindikali, kutufungulia kesi za uongo, kutupiga mabomu na utesaji mwingine jeshi la POLISI linalowafanyia raia kwa amri isiyo halali ya MaCCM.

Chagua Chadema Chagua Ukombozi
Chagua CCM chagua POLISI na ukatili wao

Mie nachagua polisi ili wanilindie amani, utulivu na mali zangu.

 
Uchambuzi wako ni murua, kuna kitu hapa unatakiwa ukifahamu Arusha ndiyo ngome ya Chadema kama vile Pemba na CUF lakini bado CCM wanapata kura kwa nini.

Ukiangalia kura walizopata CCM uchaguzi wa kwanza wa hizo kata nne utaona kura za CCM zinaongezea ukiangalia na uchaguzi wa jana.

Pamoja kuwa Arusha ni ngome ya Chadema bado kuna watu wanaipigia kura za kutosha CCM.
 
Mwigulu Nchemba kakimbia kimya kimya akiwa hoi bin taabani.Magamba Arusha ni chimbuko la mabadiliko katika taifa hili.
 
Yafuatayo ni matokeo ya kata zote 26 katika chaguzi zilizofanyika 16/06/2013 na 14/07/2013
WILAYA
KATA
CCM
CHDM
CUF
NCCR
DP
APPT
ADC
NRA
TOTAL
WINNER
former
Loser
Nachingwea
Stesheni
806
327
480
-----1613
CCM
CCM
Sengerema
Nyampulukano
1073
1476
38
45
----2632
CHDM
CCM
CCM lost
Sengerema
Lugata
2214
1044
------3258
CCM
CCM
Muheza
Genge
347
326
6
-----679
CCM
CCM
Muheza
Tingeni
362
244
4
-----610
CCM
CCM
Bahi
Ibungule
863
248
---9
--1120
CCM
CCM
Chemba
Dalai
1361
1027
377
----2765
CCM
CCM
Mbinga
Langiro
-
-NO
-
-C
-O
-N
-T
-E
-STCCM
CCM
Serengeti
Manchilla
676
625
16
-----1317
CCM
CCM
Mbeya
Iyela
1163
1918
-12
20
---3113
CHDM
CCM
CCM lost
Mufindi
Mbalamaziwa
1420
184
------1604
CCM
CCM
Kilolo
Ng'ang'awe
686
217
------903
CCM
CCM
Bukombe
Runzewe west
612
529
----153
1294
CCM
CCM
Temeke
Mianzini
1283
315
494
---25
9
2126
CCM
CCM
Ulanga
Minepa
1196
1029
------2225
CCM
TLP
TLP lost
Kilombero
Ifakara
3746
4106
------7852
CHDM
CCM
CCM lost
Kilosa
Masanze
948
638
------1586
CCM
CCM
Monduli
Makuyuni
1547
360
------1907
CCM
CCM
Arusha
Themi
326
678
313
-----1317
CHDM
CHDM
Arusha
Kimandolu
1169
2665
------3834
CHDM
CHDM
Arusha
Kaloleni
389
1019
169
-----1577
CHDM
CHDM
Arusha
Elerai
1239
1715
213
-----3167
CHDM
CHDM
Babati
Bashnet
1130
2008
------3138
CHDM
CCM
CCM lost
Mbulu
Dangobesh
968
1558
5
-----2531
CHDM
CCM
CCM lost
Singida
Iseke
791
831
96
-----1718
CHDM
CHDM

Mtwara
Mnima
918
206
626
414
----2164
CCM
CUF
CUF Lost
Kura kata zote27233
25293
2837
471
20
9
178
9
56050
Asilimia49%
45%
5%
1%
0%
0%
0%
0%
100%

Positions of the Parties before and After.
CCMCHADEMACUFTLPTOTAL
Wards Before1951126
Wards After16100026

Gainers and Losers
Losers (Former Seats lost)
Gainers (New seats gained)
Net Final position
TLP  Lost 1 to CCM
CHADEMA  Gained 5 from CCM
CHADEMA GAINED 5
CUF  Lost 1 to CCM
CCM - Gained 2 (From TLP and CUF)
CCM LOST 3
CCM  Lost 5 to CHADEMA

TLP  LOST 1
CHADEMA - none

CUF  LOST 1

Ni matumaini yangu kuwa namba zinajieleza vizuri.

1. Asilimia ya Kura:
CCM wamepata 49%, Chadema 45%, CUF 5% vyama vingine 1%

2. Ushindi wa Jumla wa Kata:
CCM wameshinda kata 16 (moja wameshinda bila kupiga kura kwa kuwa hakukuwa na wagombea wa upinzani) na Chadema wameshinda kata 10.

3. MLINGANISHO NA HALI ILIVYOKUWA BAADA YA UCHAGUZI 2010
  • Chadema wameongeza viti 5
  • CCM wamepoteza viti 3
  • TLP na CUF wamepoteza kiti kimoja kimoja.
4. MAMBO YA KIMKAKATI YA KUZINGATIA KWA VYAMA HUSIKA.
a. Vyama vya Upinzani.
Ukiangalia majimbo ya Stesheni (Nachingwea) na Mnima (Mtwara) wapanzani wakijumlisha kura zao walipata kura nyingi zaidi kuliko CCM, lakini CCM ameibuka mshindi. Hali hii ilikuwepo Kenye pia katika chaguzi mbili za kwanza za vyama vingi ambapo KANU ilikuwa inashinda, lakini kura za upinzani ni nyingi. Hapa ndipo inabidi kufikiria mkakati wa ushindi.

Niwakumbushe tu, wakati wa vita ya pili ya dunia Uingereza iliunda ushirika na Urusi, kwa kuwa waliona nguvu za Ujerumani wasingeziweza wakiwa wametengana. Japo kwa kweli hakukuwa na urafiki mwingine wowote wa dhati kati ya nchi hizi, lengo la ushindi kwa wote liliwaunganisha. Maadui huungana na kuwa rafiki wanapokuwa na tishio la pamoja. Vyama vya upinzani visipoona hivyo, CCM itaendelea kudumu miaka mingi sana ijayo, japo kwa kura kidogo zaidi na zaidi.

Wapinzani Tanzania kama wanahitaji ushindi, wanahitaji kufikiria hili. Ukiangalia jumla ya kura zilizopigwa, CCM wana 49% lakini wana viti vingi zaidi ya 50% vilivyogombaniwa. Hakika CUF ingeungwa mkono na CHADEMA NA NCCR Mageuzi Mtwara na Nachingwea CCM wangepoteza. Kadhalika CUF ingeunga mkono Chadema Kata ya Dalai Dodoma wangewashinda.

Hata hivyo kila chama kinapaswa binafsi kuendelea na kampeni za kujijenga kule ambako bado hawafahamiki, huku wakijitahidi kuhudumia vema wale waliowapa uwakilishi.

b. Chama cha Mapinduzi.
Kwa kweli chama chetu kikongwe Tanzania kinahitaji kujitafiti. Uchaguzi mdogo wa madiwani wa Oktoba 2012, CCM ilipoteza viti kadhaa. Kwa haraka haraka nakumbuka walipoteza Kata 4 zikiwemo ya Daraja Mbili Arusha, Kata ya Ipole wilayani Sikonge - Tabora, na kata ya Lengali wilayani Ludewa. Katika uchaguzi huu CCM wamepoteza kata 5 zilizokuwa mikononi mwao, na kupata mpya mbili zilizokuwa TLP na CUF.

Kipropaganda ni rahisi kuhesabu viti kuwa kati ya kata 26 mmeshinda kata 16. Kimoyomoyo mnajua kuwa mnawakilisha kata chache zaidi sasa kuliko awali. Ni vizuri kujiuliza kama chama iwapo mambo yako sawa ndani ya Chama. Je ni sera? Je ni watendaji? Je ni kubweteka? Je ni mbinu ambazo badala ya kujenga mvuto kwa watu zinazidi kuwafanya watu wakichoke na kukichukia chama hiki tawala? Je ni timu ya kampeni?

Kwa vyovyote vile ni lazima mfanye tafakari. Mfahamu pia kuwa mbinu za kutisha watu kwa vyombo vya dola na kufungua kesi za kubambikiziana, na kujaribu ku criminalize the opposition zinafanya wananchi wawachukie zaidi kuliko kuwapenda.

Hiyo ni tathmini yangu. Nakaribisha mjadala.

Kuna kata ya Mianzini na Majimatitu sijaziona kwenye bandiko lako.
 
"Nakijiuliza Chadema kimefanya nini kustahili kupendwa huku, sioni kitu!."
Mkuu, hapa hujasema kweli!! ....yaani huoni tofauti kati ya hoja za mwenyekiti wa CCM na wa CDM? Hoja za katibu mkuu wa CCM vs CDM?! N.K hoja za wabunge wa CCM na wa CDM?......
Chama cha upinzani hakipendewi kwakuwa kimefanya nini....kinapenwa kwa hoja zake kwamba kitafanya nini? kweli PASKALI hujui?!
Mkuu Mzizi wa Mbuyu, solid reasons are given na sio za kuuliza kama mtu anaona au haoni!. Hili swali la solid reasons nimekuwa nikiliuliza tangu ushindi wa Chadema wa 2010 kwenye baadhi ya maeneo, nikasema Chadema imeshinda kwa sababu CCM imechokwa ns sio imeshinda kwa sababu imejipanga kwa ushindi huo kwa sababu maalum za kushinda!.

Kuelekea 2015, we need more than this!, we need solid reasons why Chadema, not why not CCM!.
Kama unazo sababu why Chadema besides why not CCM ndizo zianze kuhubiriwa sasa kuelekea 2015, Chadema ikabidhiwe Ikulu kwa sababu hizo na sio kwa sababu CCM imeshindwa kufanya abcd bali kwa sababu Chadema itafanya abcna d kwa kutumia resources kuytoka abcd, ether kwa kubana matumizi abcd, hivyo kuokoa kiasi abcd cha fedha kitakacho tumika kufan ya abc na d, au CCM imekuwa haikusanyi kodi abcd katika maeneo haya abcna d au Chadema itaanzisha vyanzo vipya vya mapato abcd, vitakavyozalisha abcd na kayatumia mapato hayo kufanya abcd etc, etc, giving out reasons za kuichagua Chadema!.

Hizi ndizo mimi ninazoziita politics of sustainability na sio just politics of politiking!.

Pasco.
 
Mtu wa shamba asante.cdm tusikie na kufanyia maoni kazi.the future is bright; the road is rough!
 
hakuna mahali nimeona CCM imeinyang'anya kiti CHADEMA, misuli ya chadema nani atAiweza??
 
thathmini iliyo fanywa katika uzi huu ni mjarab! hilo ndiyo neon ambalo naweza kulitumia. wana jf kama tungejikita kwenye tathmini za kipembuzi na kuacha m.a.t.u.s.i., tungejijenga sana kisiasa. vijana ktk nchi nyingine wanatumia mitandao ya kijamii kufanya tathmini zilizokwenda shule. mambo ya magamba, magaidi, maliberali, ccm b nk..... hayatotufikisha mbali. wake up guys!
 
Uchambuzi wako ni murua, kuna kitu hapa unatakiwa ukifahamu Arusha ndiyo ngome ya Chadema kama vile Pemba na CUF lakini bado CCM wanapata kura kwa nini.

Ukiangalia kura walizopata CCM uchaguzi wa kwanza wa hizo kata nne utaona kura za CCM zinaongezea ukiangalia na uchaguzi wa jana.

Pamoja kuwa Arusha ni ngome ya Chadema bado kuna watu wanaipigia kura za kutosha CCM.
Mkuu Ritz naomba basi utuwekee idadi ya kura kwenye uchaguzi wa kwanza kwenye hizi kata kama unazo ili tuweze kufanya uchambuzi mbadala.
Thanks
 
Last edited by a moderator:
Kuna kata ya Mianzini na Majimatitu sijaziona kwenye bandiko lako.
Mianzini ipo, angalia Wilaya ya Temeke, kati ya Bukombe na Ulanga.

Majimatitu naomba unisaidie kunipa data. Mimi najua June 16 uchaguzi ulikuwa umepangwa kufanyika kata 26, na nimeziweka zote 16 zilizofanya uchaguzi.
WILAYA
KATA
CCM
CHADEMA
CUF
ADC
NRA
TOTAL
WINNER
FORMER
LOSER
Temeke
Mianzini
1283
315
494
---25
9
2126
CCM
CCM
 
Kama Nape Nnauye kajitokeza kujkubali kushindwa, sioni ni kwanini wengine wasite kuipongeza Chadema kwa ushindi mnono walioibuka nao Arusha. Mara zote nimesema kwamba CCM inakufa kifo cha kamongo. Kamongo ni samaki wa aina yake. Anapovuliwa asubuhi, huanza kuuzwa muda huo huo. Kwa kawaida hukatwa vipande. Kila mnunuzi anapofika, anakatiwa kipande. Cha ajabu ni kwamba hadi jioni, hata kama kimebaki kichwa, bado huwa kinaachama licha ya ukweli kwamba kiwiliwili chote kimeshapikwa na kuliwa na wateja wa awali. CCM inapiga miayo kama kamongo! Hiyo haina maana kwamba haielekei kufa! La hasha, CCM inakabiliwa na wakati mgumu. Vijana wanataka mabadiliko bila kujali CCM imefanya mangapi mabaya na mazuri.
 
Safi sana mtu wa shamba kwa achambuzi wako wa kina, kumbe maneno mengi yote hayo ni kwamba CCM inazidi kudorora, mimi sijali nani kapata nini nachoangalia ni idadi ya kura zilizopigwa katika kata zote 26 kwa vyama viwili tu CCM na CDM.

Yaani mbwebwe zote la Nape na jamaa zake kumbe ni tofauti ya kura 1,940 tu, ambayo ni tofauti ya 2%. Hongera sana CDM kwa kazi nzito. Huu ni ushindi mkubwa, na ushindi unapimwa kwa idadi ya wapiga kura.

Tofauti ya Kura ni 1,940 tu. Pamoja na changamoto zote za kugoma kuboresha daftari la wapigakura, matumizi mabovu ya vyombo vya dola, kutumia ma DC, RC kama wapiga debe wa CCM kutisha wananchi, Rushwa nk

CDM mnaruka viunzi -- so far so good - wanalainika hawa mbona!!!
Kura kata zote
27233

25293
Asilimia
49%
45%
 
mi naona tuc waze tena hiki chama cha ccmmafisadi tuwaze mabadiliko ya nchi ye2 nilazima cha che2 cha cdm kisheke dola tuone mabadiko ccm tumeichoka haina jipya sasa tunaanza na mungu na tutamaliza na mungu

ccm kimebaki chama cha viongozi na jamaa zao.wanagawana utajiri wa nchi yetu na wawekezaji kupitia mikataba feki na ya siri.huwezi amini!!!!!!!!!!kibaya zaidi wanapofanya ujangili huu wanalindwa na dola.CDM tumeanza na mungu tutamaliza na mungu.
 
Huko Serengeti waliwakamata vijana wote wa CHADEMA wakawaweka ndani hadi uchaguzi ulipopita... Vipi ikiwa uchaguzi huu ungekuwa huru na wa haki, mambo yangekuwaje?

Uko sahihi, na inasemekana kazi hii iliratibiwa na DC. Hatua iliyochukuliwa na NEC kwenye uchaguzi wa ARS ya kupiga marufuku RC na DC kujihusisha na shughuli zote za uchaguzi inahitaji kuwa moja ya ibara katika sheria au kanuni za uchaguzi. Kisheria, RC au DC hawana majukumu yoyote yanayohusu uchaguzi, na kibaya zaidi wote ni makada wa ccm. NEC wakiamua kumbe wanaweza, angalu wametuonyesha kupitia uchaguzi wa ARS. Pamoja na mapungufu kadhaa yaliyojitokeza, wanastahili hongera kwa hili.
 
Back
Top Bottom