Chaguzi ndogo 16/6 na 14/7 majumuisho na tathmini

ciril ndugu yangu, huwezi kutoa andishi bila kujali hisia. ila hisia haziruhusiwi kufifisha ukweli na uhalisia wa chochote kinachojadiliwa.
labda nianze kwa kulitetea jeshi la polisi na jinsi ambavyo chadema wanalionea na kulidhalilisha wakati jeshi hilo linafanya kazi kwa mujibu wa sheria. ni mzandiki tuu atakayekataa kuwa jeshi la pilisi tulilonalo sasa ni bora kiutendaji kuliko kipindi chochote tangu uhuru, na ndio jeshi la polisi pekee miongoni mwa nchi za SADC na EAC. polisi ya tz chini ya said mwema imejipenyeza mpaka miongoni mwa raia kupitia polisi jamii na ulinzi shirikishi kiasi ambacho askari polisi wa tz sio kiumbe cha kuogopwa zaidi ya kuonekana rafiki wa watu. nenda katika nchi zinazotuzunguka au hata SOUTH AFRICA kisha uje ulinganishe na TZ.
tatizo la CHADEMA ni PROVOCATION! mnawa-provoc polisi kwa makusudi ili watimize wajibu wao ili mpate platform ya kulalamika. tunajua kabisa kuwa MAANDAMANO, MIKUTANO na uhuru wa kutoa maoni ni haki ya kikatiba ya kila mtanzania...
ni kwa nini sasa inalazimika polisi kupewa taarifa?? ni kwa sababu mikutano na maandamano yatahitaji ulinzi toka jeshi la polisi.sasa polisi wakiwa hawana askari wa kutosha kutoa ulinzi katika mkutano/maandamano husika ni wajibu wao kupiga marufuku. tatizo lenu kubwa mnafanya siasa huku mkidhani ninyi ni weledi wa kila kitu(hili ni tatizo la wanasiasa wooote wa africa), mnajiona kuwa ni wataalamu wa SHERIA,UCHUMI,USALAMA,VITA,HABARI,ELIMU,UVUVI,HIFADHI,UHANDISI na kila kitu kiasi cha kuingilia hata mamlaka za kiutawala. hebu jiulize kwa kutenda haki kabisa,, hivi ni chama gani kinachoongoza kwa kufanya mikutano ya hadhara na maandamano ndani ya miaka mitatu iliyopita??? hivi kweli kama serikali na jeshi la polisi wangekuwa wana dhamira mbaya ya kukandamiza democrasia kama mnavyotaka tuamini, hayo yote yangewezekana??????? jibu utakuwa nalo moyoni hata kama humu utajibu tofauti na moyo wako...
kuhusu mauaji ya MWANGOSI, nadhani lile llikuwa ni kosa la kimedani na kwa kutambua hilo, serikali ilichukua hatua kwa mujibu wa sheria na yule askari nadhani sisi wote ni mashahidi kuwa yuko mahakamani, tatizo ni kwamba hata katika matukio ya kijeshi mnataka maamuzi yatolewe kisiasa kwa matakwa yenu ili mwisho wa siku mje humu na kujitapa kwamba serikali inaendeshwa kwa amri za chadema.
kuhusu bomu la arusha>>>>> mtanisamehe saaana kama mtapenda lakini kwa mtu yeyote mwenye akili isiyoendeshwa na ushabiki hawezi kuihusisha serikali wala CCM katika mlipuko ule. na kuna kila sababu ya kuihusisha CHADEMA na tukio lile na hata matukio baada ya mlipuko ule yanathibitisha dhana hiyo. hivi labda nikuulize, ni kwa maslahi gani CCM/SERIKALI itaayapata kwa kulipua bomu kwenye mkutano wa chadema!!!?????? ni mwendawazimu tu ambae ataacha kuihusisha serikali/ccm kama mlipuko ukitokea kwenye mkutano wa chadema(kama mnavyoihusisha sasa).Na hivyo basi ili kuichafua serikali/ccm NI LAZIMA WALE WENYE MALENGO HAYO(CHADEMA) wafanye tukio kama lile ili mwisho wa siku lawama zielekezwe kwa serikali/ccm kama jinsi mnavyojitahidi kutuaminisha.
lakini vilevile ukiangalia na kutafakari kauli za viongozi wa chadema baada ya mlipuko wa pale soweto, kuna kitu kinajionyesha. kwa nini mkutano ule waliandaa vifaa maalum(bullshit) vya kurikodi matukio??? kwa nini walengwa wa lile bomu hawakuwa na dhamira ya kuwalenga viongozi?? kwa nini camera iliyochukua tukio haikushituliwa na mlipuko wa bomu lile??? kwa nini yalikuwa yamelengwa maeneo maalum kwa mpiga picha kuchukua matukio???na LA MSINGI KABISA, KWA NINI USHAHIDI WA MLIPUKO ULE MPAKA SASA UNAJULIKANA NA WATU WATATU TUU NDANI YA CHADEMA???? KWA NINI HATA VIKAO VYA JUU VYA CHAMA VIMESHINDWA KUDAI NA KUPEWA (japo kwa kuonyeshwa tuu) USHAHIDI HUU???? KWA NINI HATA WANASHERIA WA CHAMA (ambao ndio haswaa waliostahili kukaa na ushahidi huo kwa ajili ya taratibu za kisheria) MAPAKA LEO HII HAWAJUI HUO USHAHIDI UNAOONGELEWA NI UPI????
jiulize kwa nini wale watu makini kabisa ndani ya chama chenu kama akina ZZK,KITILA MKUMBO,TUNDU LISSU, PRO SAFARI NA PROF BAREGU wamejitenga kabisa na upuuzi wa bomu la pale soweto???? amini nakwambia, something is cooking and when the right time comes, mtalalamika kuwa mnahujumiwa... ona yanayotokea kwa KILEO kule igunga, imechukua miaka mingapi kwa ukweli kuja kujulikana???? ni muda tu kaka na mlipuko wa arusha utapata mwenyewe.
kwangu mimi naona ni upuuzi kwa mzalendo yeyote wanchi hii atakaposimama na kusema"""eti tuzingatie na kutatua kero za wananchi na sio kujaribu kuiangamiza chadema'''' mimi naamini kabisa kuwa SIASA ZA CHADEMA ZA HIVI SASA NI TATIZO KUBWA KATIKA NCHI YETU KULIKO MATATIZO YOOOTE YANALOLIKABILI TAIFA hata kama chadema yenyewe sio tatizo.
ni halmashauri ngapi mnazoziongoza ambazo manawakataza wananchi kushiriki na kuchangia shughuli za maendeleo???
ni kwa kiasi gani mnawashawishi na kuwa-organise wamachinga wafanye biashara maeneo mabayo ni kinyume cha sheria?
ni kwa kiwango gani mnajaribu kuzipaka matope juhudi za serikali (hata kama hazitoshi) katika kutimiza ahadi na malengo yake????
ni kwa kiwango gani mnajaribu kuuteketeza na kuuangamiza uzalendo tokamioyoni mwa watanzania na kuwashawishi kuichukia nchi yao tz na kuipenda chadema kama vile chadema/ccm zinaweza kuwepo bila tanzania???????
'' DEMOCRACY IS NOT ALL ABOUT ELECTIONS, IT'S ABOUT NATIONAL STABILITY AND PATRIOTISM''
kumbuka HAMMAS, MUSLIM BROTHERHOOD, MDC na CUF..hivi vyama vilishinda uchaguzi lakini havikupewa nchi.unajua ni kwa nini???? havikuwa vinawakilisha matakwa na hatma ya mataifa husika

Unasikitisha sana mkuu!
 
Nchi inakabidhiwa by vetting not by votting!.
Rais wa nchi ndiye amiri jeshi mkuu wa majeshi yetu ya ulinzi na usalama!. Hata ikitokea chama fulani kikamsimamisha a very popular linatic, akachaguliwa, jee atakabidhiwa?!. Utawala wa nchi una change hands kwa exchange of instrumetns of power ikiwemo kuapishwa na kukabidhiwa vyombo vya dola, wanaofanya hayo ni wale wapiga kura au nu yule mwenye navyo?!. JK ndie rais aliyeyepo, na whoever atakaye chaguliwa, JK ndiye mkabidhi!, jee atajikabidhia tuu kwa sababu wananchi wamesema au?!.

Kwa taarifa tuu matokeo halali ya uchaguzi, sio zile kura zilizopigwa bali ni zile zitakazo tangazwa!. Nasisitiza mshindi kupatikana by vetting, hata kama votting imesema ni fulani, vetting ndio itaamua atangazwe nani!. Waulizeni CUF wawaambie kilichikuwa kinatokea kwenye chaguzi zote Zanzibar na kilichukuwa kinatangazwa!.

Washaurini viongozi wa Chadema, waanze kuzungumza in good terms na Mwamunyange, Rashid Othman na Saidi mwema, ili pia wapite kwenye vetting!.. vinginevyo...!

Pasco.

Najikumbusha tuu, hii ni ya mwaka 2013.
Tumeshuhudia mtu anashinda by voting halafu vetting imegoma!.

Pasco
 
Back
Top Bottom