Tatizo wa bongo mgao Kama haujaenda vizuri lazima makelele yatasikika
"Majugu si Mtaji"
Nilipofika mwz nilishauriwa kupima sana marafiki wa kuwa nao, kwani ni mkoa wenye majungu sana.Hapo awali sikuliona hilo lakini muda unavyokwenda nazidi kuamini.Vijiwe vya Majungu mwanza viko,Mwanza Institute, Shooters, Kirumba Resort.(Hiki cha Kirumba resort kinabeba wana ccm wengi hasa Vijana,Shooters kinabeba wachezaji wastaafu na vijana wapenda mpira na pamoja na wanaccm-kwa mtizamo wangu,Mwanza Institute hiki ni mchanganyiko wa vijana -madreva taxi,wafanyakazi, wafanya biashara na baadhi ya wafanyakazi, ijapokua kimechoka kidogo siku hizi.Hivyo ni vijiwe ambavyo ukipita tu,ushafahamika.Nilifika Mwanza siku ya kwanza usiku nikapelekwa na mwenyeji wangu Villa.Kesho kutwa yake niliporipoti ofcn kujitambulisha kwa boss ,akaniambia umeonekana viwanja kadhaa vya jijini mwz.I was surprised.
back to Ulingo wa siasa,habari za Wenje kutokushinda 2015,ukipita kwenye hivi vijiwe utazipata, kwa mara ya kwanza nilizipata, Ile siku CCM walipobeba watu kwa Malori kusherehekea kuzaliwa kwao,maana tulipata msosi katika kijiwe cha Shooters.lakini ukijaribu kuangalia kiini hasa cha kulaumiwa hukipati zaidi ya kusema ,siku hizi anafanya biashara za kwenda nje ya nchi,mara alishinda kwa ajili tu ya kupata mtaji hata yeye anajua na mengine mengi.
Nilichojifunza ni hawa madiwani wawili, walikua wakijitahidi kumpiga sana majungu huyu bwana kwa kushirikiana na madiwani wa CCM.Niliwahi kuandika humu ndani siku moja nilipokutana na huyo diwani kwa mara ya kwanza,akiwa na dogo mmoja aliyetambulishwa kwangu kama katibu wa Chacha Wangwe R.I.P, na walikua na jamaa mwingine ambaye ni mwl.Adam naye alijitambulisha kama mwalimu wa shule ya Nganza.walipiga majungu kuhusiana na uongzi wa CDM.
Juzi usiku hawamadiwani walikua katika hotel ya Sparrow Ghana, wakamwita rafiki yangu niliyekua naye kwa furaha huku Adam akimwambia huyo rafiki yangu," Umeona Highness alivyo jificha chini ya meza?" huyo rafiki akamwambia sikuona,akamwambia hujaona taarifa ya habari?wakati huo walikua wakiongea na yule mmiliki wa hiyo hotel.Nikajaribu kuunganisha Dots zangu, mmiliki huyo wa hotel kwa redio mbao ni rafiki wa Ritz1 ,alifahamiana naye kupitia kuunganishwa na jamaa wa Villa Park.Na pale hotel walikua wakiongelea kuhusiana na hayo mambo ya kisiasa, kwa hiyo ni ka hisi kuna uwezekano haya mambo yanafanyika kwa kusaidiwa na watu fulani.
Kwa ujumla hawa watu hawafai.Nilipenda kauli ya CDM ilikua very straight kwamba ,wamefukuzwa kwa kwa kukihujumu chama,hilo nilikubaliana nalo na nikaamini CDM wanapata taarifa sahihi.
lengo langu ni kuwafahamisha wana jf kuwa siasa za mwanza ziko kimajungu majungu sana, hivyo muwe makini sana mnapopata taarifa za mwz wakati wa kuzijadili.