Chagulani: Wenje ni chanzo cha migogoro Mwanza

Nyakarungu

JF-Expert Member
May 1, 2011
472
375
MUSTAKABALI WA CHADEMA MWANZA.
- Waswahili hunena, ”ukikosea fomula hakika jibu sahihi halipatikani” Wana Mwanza kwa pamoja tunawapongeza ninyi binafsi na Kamati kuu ya chama kwa kuhakikisha ya kuwa chama kinaendeshwa katika misingi inayokubalika kwa mujibu wa katiba ya chama toleo la mwaka 2006, mmefanya maamuzi magumu ambayo hayakutegemewa, yalikuwa magumu lakini yenye maslahi kwa chama na taifa kwa ujumla. Wafuasi watano Yuda Iskariote waliokuwa Arusha walipata hukumu ya haki. HERI HAMSINI NZIMA KULIKO MIA MBOVU.

MADIWANI NA WABUNGE WETU
- Mara nyingi donda lililo kichwani muuguzi wake huwa ni mkono ikumbukwe yakuwa tarehe 21/01/2011 viwanja vya furahisha katibu mkuu alitamka ya kwamba, atawasimamia Madiwani wetu wa jiji la Mwanza kuhakikisha yakuwa wananchi waone tofauti ya utawala wa kisanii na utawala makini. - Pia ikumbukwe kuwa kabla ya chadema kushinda Mwanza tulikuwa tukisema mambo kama Tarime & Karatu, kesho tulitegemea tuseme mabo kama Mwanza tukifika Sengerema, Buchosa, Sumve, Kwimba & Magu.

Takribani sasa Mwaka unakatika wa wawakilishi wetu hawa hawana sauti moja, chakushangaza na kusikitisha zaidi wamepitia mgongo wa watu wengine kushika “Tender” za Halimashauri ya Jiji! Watahoji nini? Watu kunena wana Mwanza hawakuifukuza CCM jijini Mwanza kama mlaji wa zamani, na wala hawakuichagua chadema kama mlaji mpya!

Bali walihitaji mabadiliko ya kivitendo na wala si ya kinadharia. Huenda makamanda mtashtuka kusikia maneno haya, hata kama chungu tunywe kwa kuwa inatibu. Mabadaliko Mwanza bado hayajaja kwa kuwa wawikilishi wetu hawa wanatenda kimazoea wakiongozwa na hisia zao binafsi zaidi kuliko ilani ya chadema waliyokuwa wakiinadi majukwaani. Wawakilishi wetu hawa hawana sauti moja, kila mmoja anatafuta umaarufu binafsi wamekisahau chama. makamanda wakalisheni kitako waseme tatizo ni nini?

Kwanini wavutane na kulumbana wao kwa wao?wamesahu ya kuwa vita ya panzi ni furaha kwa kunguru? Kwanini hawa wasusie kikao cha baraza la Madiwani? Na kwanini hao wabaki? kajua ndo haka.
- Tusipouanika mapema, itatulazimu tuutwange mbichi. Siku 340 wametenda au kubadilisha lipi Mwanza?

Wakati ndani ya siku mia moja mgombea urais (Dr. Slaa) alikuwa ametuahidi makuu likiwemo suala tete kwa sasa la katiba mpya!
- Mbunge aliahidi ada na stahili za wanafunzi, lakini kwa leo wanafunzi na wazazi wanadaiwa madawati. Mpango wa kuomba kibali kukata miti Misitu ya Kigoma kupitia kwa wadau wa chama waliopo Jijini Mwanza wanaofahamiana na Dr. Felician Kilahama mpaka leo hii Mbunge huyu bado hajalifanyia kazi, wakati uwezekano wa kumaliza tatizo hilo lipo. Mbunge huyu wa Nyamagana haambiliki. Watoto hawa 905 anaowasomesha Rushwa imetembezwa hadharani na wafanyakazi wa ofisi yake, wengi wao hawatoki mazingira magumu na wala si yatima kama alivyoaminishwa.

Huenda hizi sifa binafsi ndizo zinamfanya Wenje akwamishe ilani ya Chama ya Elimu bure kwa wote.Chadema tunawabunifu wepesi wa kusahau.
- Wenje anamfumbia au hupuuza taarifa anazopewa ndani ya Jiji (zero response). Akipewa taarifa hazifuatilii, huenda anakwamishwa na deni alilonalo kwa mkurugenzi baada ya kumkopesha pesa za kulipia watoto 905. tulipanga tupate utafiti wa mapato halisi ya Jiji ili bajeti inapokuja tufanye uwiano halisi Mbunge huyu bado haonyeshi ushirikiano.

Hivyo hivyo na katibu wa chama mkoa yuko tayari kuomba au kufuata mchango wa fedha lakini mchango wa kimawazo kama ujenzi wa ofisi ya mkoa hayuko tayari.
- Wenje alipewa majinaya madiwani kadhaa wa chadema ambao tayari mkurugenzi wa jiji amekwishawakamata kwenye himaya yake Mbunge huyu hakufuatilia. - Tax property na service levy ni pesa ambazo bado Kabwe (Mkurugenzi Jiji la Mwanza) anakula na wawakilishi wetu hawajui zinakusanywa kiasi gani. Hata ukiwauliza mmoja mmoja nyumba ngapi kwenye kata yake zinalipa kodi Halmashauri na kiasi gani kinapatikana bado kazi ipo.

Chukulia mfano mabilioni ya fedha yaliyotolewa na EU (jumuia ya ulaya) ili kuziunganisha nyumba 5,000 kwenye mfumo wa maji taka Jijini Mwanza ni nyumba 1200 tu ndizo zilizounganishwa.
- Kauli za Wenje kuhusu machinga Mwanza ndizo zinazochochea vurugu. Mbunge huyu ni tatizo kwa chama mkoa. Wenje amepoteza mwelekeo, anahamasisha uvunjaji wa sheria akiwalazimisha wananchi kujichukulia sheria mkononi. Suala la machinga na suala la sharifu wanaofanya kazi ya kuzoa taka na usafi wa mazingira aliwahamasisha wananchi wawapige mawe pindi waingiapo kwenye nyumba zao kufanya ukaguzi akisahu kuwa sisi chadema tunaongoza Halmashauri.

Wajumbe huenda wawakilishi wetu hawakujiandaakuongoza ndiyo maana wanapuyanga. Diwani wa viti maalumu ambaye pia ni mwenyekiti wa BAWACHA Jimbo la Nyamagana ni tatizo katika Chama, mamlaka haya anayatoa wapi? Yatupasa tutanabaishe kama yeye ni kiongozi wa Chama Proper, BARAZA au ni katibu wa ofisi ya Mbunge? Mamlaka haya yanatoka wapi nayeye kuwa juu ya viongozi wa nafasi husika?

MIGOGORO YA CHAMA
- Niliposoma gazeti la majira la tarehe 20/08/2011 lenye kichwa cha habari kilichosomeka, “MONGELA AMWEKEA PINGAMIZI MACHEMLI” nilifadhahika kukuta taarifa za kujihuzulu kwa viongozi wote wa Wilaya ya Ukerewe na Kamati tendaji. Chanzo walidai mgombea wao Bw. Simon Mabagala Mtobesya kukataliwa na Kamati kuu ya Chama. Namshukuru Mungu kwa chadema Kusimama imara na kushinda kiti cha Ubunge na kuiongoza Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe.

- Mtaalamu mmoja wa masuala ya Uongozi na Utawala aliwahi kuainisha baadhi ya vyanzo vya Migogoro kwamba ni pamoja na ukiukaji wa kanuni na taratibu ndani ya Chama (Katiba), uongozi wa kibabe, ubinafsi, na upendeleo bila kufuata kanuni (sisi tumesema), na kutowajibika kwa viongozi wa Chama.

Haya yaliyosemwa na mtaalamu huyu japo si yote au zaidi ya haya yaliyosemwa mtaalamu huyu ndiyo chanzo cha migogoro katika chama ndani ya mkoa wa Mwanza. Majimbo ya Magu Buchosa, Nyamagana na Sengerema uongozi unayumba. Hii isimaanishe ya kwamba majimbo mengine hayana migogoro, la hasha, iliyotajwa imefikia kukipa chama doa katika jamii.

CHANZO CHA MIGOGORO
a) Uteuzi wa Madiwani viti maalumu umejenga majeraha na kuacha makovu ambayo hayatafutika. Ikumbukwe ya kuwa kovu la utotoni hufifia au huisha kabisa, lakini kovu la utu uzima hudumu daima. Makovu haya yapo Magu, Sengerema na Nyamagana, Mbaya zaidi viongozi wa chama tena siyo BAWACHA ndiyo waliyohusika kuyajenga. Bila ya kumung’unya maneno tunamtaja katibu wa Mkoa Ndugu Wilson Mushumbusi kuhusika moja kwa moja katika mizozo hii.

Makamanda leo jimbo la Magu linaviongozi waliosimamishwa na mkoa na wale waliosimikwa na mkoa wote wanafanmya kazi ofisi mbili tofauti. Hivyo hivyo na Nyamagana ambapo katika jimbo hili nafsi ya uongozi ina viongozi wawili kila upande ukiita mwingine Batili. Katibu wa mkoa anadai Kamati kuu ilifuta uongozi wa Wilaya ya Nyamagana. Hii inamaanisha Mushumbusi aliachiwa Fredy Lukanga(katibu wa baraza la wazee) peke yake kama kiongozi aliyepatikana kwa njia halali wakati huo huo alidai Kata zote za Nyamagana zilikuwa hazijafanya uchaguzi na Mkoa, Nyamagana haikuhusika? Na kama ilihusika na Mushumbusi haoni hata yeye amechaguliwa na wajumbe Batili?


b) Viongozi kuwa na makundi: hii imewajengea dhana kuamini ya kwamba baadhi ya wanachama ni wasaliti au hawana nidhamu, hivyo hata wanaposimama katika haki wao siku zote huwa ni wakosaji tu. Lakini yatupasa kuelewa yakuwa hata saa mbovu kuna kipindi husema ukweli, tujenge urafiki na wala si uadui ndani ya chama.

Kiongozi anayejenga migogoro anahitaji kuwatawanya ili awatawale viiongozi wa namna hii wamegundua ya kuwa wamepoteza mwelekeo, wanatafuta sifa binafsi ya kujilundikia mali kwa kuwa hawajui mustakabali wao ndani ya Chama kwenye nyadhifa zao.


c)
Njaa za viongozi: viongozi wengi wa Chama wanaishi kwa kuchungulia mifuko ya wawakilishi wetu, hii imewanyanga’anya wao fursa ya kusimamia kanuni, taratibu na maadili ya Chama kwa kushindwa kuwakemea wafadhili. Wameshindwa kutoa maamuzi sahihi au kukemea kutokana na kuwekwa mifukoni na wawakilishi wetu. Hii nayo imechangia kuzua migogoro miongoni mwa wanachama wetu.

d)
Upangaji safu ya wanaotajaria kugombea Ubunge & Udiwani 2015, huku wakijenga kupenyeza propaganda zenye kuchafua na kujenga mgawanyiko, kukatisha tamaa na hata kutishia kufukuzwa wanachama kwa wale wanaoonekana kukinzana na matakwa yao. Ya nini kugombania fito wakati wote tunajenga nyumba moja? Upi ni uongozi halali wa Nyamagana?

e) Wawakilishi kuwa juu ya viongozi wa Chama: viongozi wetu wa chama mkoa wamekosa sauti juu ya aidha Wabunge au Madiwani wetu wa Jiji la Mwanza. Wawakilishi hawa wamekuwa wakipanga nini chama kifanye na wale si Chama kuwapangia wao nini wafanye. Chama sasa kinawajibika kwa wawakilishi hawa.

f) Kupwaya kwa Baraza la uongozi Mkoa: huenda unusu wa baraza hili au kufanya kazi kimezoea leo hii takribani mwezi mmoja sasa chama kinachoenda kushika Dola 2015 hakina ofisi ya chama Mkoa. Katiba ya chama toleo la 2006 ibara ya 7.8.1.4 & 7.8.1.5 zinatamka bayana kuwepo ofisi ambayo Mkoa utawajibika kulipa gharama ya pango.

Licha ibara ya 7.8.3.2 kuhitaji ofisi za wilaya na Mikoa ziwe angalau na mtu mmoja na wakudumu wakufunga na kufungua ofisi kila siku Mwanza hili halijawahi kutendeka. Huenda kutokuwepo kwa M/kiti wa chama Mkoa na M/kiti wa BAWACHA kwa kipindi kirefu sasa huku Finias Magesa akitumia “remote control” kuongoza Mkoa kumechangia Mkoa kuyumba, kukosa ofisi na hata kutoa maamuzi yanayokinzana na katiba katika suala la kesi ya Diwani viti maalumu Sengerema.

Katiba ya Chadema uk 95 kipengele cha X kinazuia matatizo ya chama kupelekwa mahakamani, lakini cha ajabu kesi ilifunguliwa Nov, 2010, Baraza la uongozi tarehe 14/07/2011, Magnum Hotel Baraza la Mkoa lilitoa siku 14 kesi hiyo iwe imeondolewa makamani ama sivyo wahusika bila kuwataja hadharani wangechukuliwa hatua. maamuzi haya yalitoka kifungu kipi cha katiba? Huku Magesa akijinasibu ya kwamba, familia isiyo na utaratibu lazima itasambaratika.

Pamoja na siku hizo 14 kesi haikufutwa hadi mwezi Septemba ndipo ilipofutwa uongozi wa Wilaya ya Sengerema ilijinasibu ya kuwa Dr. Slaa ametoa “Go ahead” Dr. Slaa haijui katiba ya Chadema! Kumrudisha M/kiti wa (J) Sengerema aliyejihuzulu kwa hiyari yake,bila yeye mwenyewe kuomba kurejea kwa zaidi ya kipindi cha mwaka mmoja Baraza la uongozi mkoa halikusoma barua iliyotajwa na CC juu ya viongozi wa Wilaya ya Ukerewe waliojuhuzulu au baraza la uongozi mkoa linatenda kwa mazoea.

SULUHISHO LA MGOGORO

- lazima tubadilishe mtazamo kwa sasa, heri tulinde kiwanda chetu hata kwa mabomu kuliko kukisahau tukalinda kwa rada magari yaliyozalishwa na kiwanda chetu. Tujenge chama kuliko kumjenga mtu ambaye leo tunaye na kesho hatunaye - wawakilishi wetu wapewe mafunzo na semina wajue chama hakikutokana na wao bali wao ndio wametokana na chama hivyo popote penye mgogoro au mvutano chama kitatamalaki wajue upi ni wajibu wao kwa chama na ipi haki yao kutoka kwenye chama.

- Mushumbusi na Wenje ni chanzo cha Migogoro Mwanza, wanakwamisha kukua na kuenea kwa Chama, hivyo wakae wajitathimini ama sivyo waachie ngazi kwani siasa siyo hisia binasfi, bali ni utashi wenye kushirikisha mawazo ya wengine – waswahili husema “mjinga wa kweli huwa hajui kama ni mjinga hivyo hajui anachokipoteza” - Ili kubaini ukweli na kupata ufumbuzi viongozi wa kata zote za Jiji Wakutanishwe kubaini kinachoendelea na kiini cha migogoro wakutanishwe na viongozi wakuu.

RAI

- Uchaguzi wa viongozi ufanyike haraka kwenye majimbo yenye migogoro na yasiyo na uongozi kabisa kama jimbo la Sumve, ili kazi ya kukieneza chama ianze haraka iwezekanavyo. Pia Uongozi wa Mkoa ambao kwa sasa unapwaya aidha uvunjwe na uchaguzi uitishwe au nafasi zinazopwaya kwa sasa zijazwe.

- Iletwe semina ya viongozi wa Chama ngazi ya Jimbo, Wilaya na Mikoa ili kuwajengea uwezo wa kufanya kazi wakijua mipaka yao kwani inajidhihilisha yakuwa migogoro mingi inatokana na ukiukwaji wa katiba huku ule utendaji wa kimazoea ukipewa kipaumbele - Tunaomba Madiwani wakutanishwe na uongozi wa Wilaya hizi mbili yaani Ilemela na Nyamagana,pia katibu mkuu ahamishe ofisi yake DAR kwa muda na aje awasimamie Madiwani wetu hawa.

- Meya wa Jiji aondolewe kwa maana ameshindwa kujirekebisha nakuisimamia Halmashauri - Wakurugenzi wa chama Taifa nao ni tatizo, kwani hawarejeshi taarifa sahihi na halisi wanazokuja kutafiti majimboni. Hutumiwa na baadhi ya watu kupika repoti. Taarifa zao ziwe zinachujwa. Rejea Uchaguzi wa Meya wa Jiji la Mwanza na uchaguzi wa chama Ukerewe 5/01/2011. Benson alionywa akakaidi, lakini matokeo ya utemi wake aliyaona.rejeeni pia ripoti yake kuhusu uchunguzi wa uhalali wa viongozi wa Nyamagana alimhoji nani, lini, na wapi kubaini kama uchaguzi haukufanyika.

- Ofisi ya chama Taifa izingatie haki za wanachama kwani hata maonyo yanatolewa kimya kimya yanawavunja nguvu wanachama. Katiba ya chama toleo la 2006 ibara 6.3.6 (a) – (f) imekuwa ikikiukwa sana na chama, kiongozi wa Jimbo/Wilaya anasimamishwa uongozi na katibu Mkuu kwa katiba ipi na ibara ipi inayompa mamlaka kutenda hayo?

Pia ubatirishaji wa uteuzi wa wawakilishi wa chama kama wabunge CC iwe inawapa taarifa walioenguliwa na sababu za kuwaengua. Rejea yaliyotokea kwa NYAMAGANA(Chacha Okong’o).

- Chama kimekuwa na mfumo mbovu wa mawasiliano, kwani mawasiliano yanatoka chini kwenda juu. Wabunge wetu wamekuwa wakitumia nafasi ya ukaribu na ukatibu mkuu kuwakandamiza wale wasio na nafasi ya karibu kuongea na katibu mkuu, huku wakitoa taarifa zenye kupotosha. Shilingi ina pande 2.

- Makamanda pigieni kelele wafadhili wanapotoa fedha zisiingie hazina, badala yake ziingie mfuko maalumu ili usimamizi uwe wa makini kuliko sasa, kwani zinatumiwa vibaya na serikali ikibidi hata walete msimamizi wao kama MCC.

- Wadau wa Chadema Mwanza wakutanishwe na Viongozi wakuu (viongozi) ilikusikia nao wanatushauri yapi ili kukipeleka chama mbele maana viongozi wetu hawasemi ukweli wa yale yanayojili.

- makamanda, hata asiye na kiuno huvua mbele yawengine, nasi tumevua, popote palipo na mvutano au migogoro baina ya pande mbili historia itatuhukumu na wakati utatuambia nani Alikuwa sahihi na nani hakuwa sahihi.
Wasalaam

Katibu (BAVICHA) Mkoa wa Mwanza Naibu katibu Baraza la Wazee Wilaya
ya Nyamagana

………………………………….. ………………………………………
SALVATORY MAGAFU PATRICK SAMSON


Nakala

- Mwenyekiti wa Taifa
- Katibu taifa
- Naibu katibu mkuu taifa bara na visiwani
- Wajumbe wa Kamati kuu.
- Makamu mwenyekiti bara na Zanzibari.



CHADEMA VEMA
PEOPLE’S POWER
 
Ni mtu mjinga pekee anayeweza kumlamu Wenje.Wenje ni Katapila linaloangusha vibaraka wote wa ufisadi.
 
Chadema wameonyesha udhaifu wa hali ya juu katika masuala ya utawala katika Jiji la Mwanza, wakazi wa Mwanza waliwapa kura kwa imani mtaijenga Mwanza kinyume chake ni ufisadi tu na vita vya kugombea madaraka.
 
Hapa JF hapaitaji hiyo barua kwa sababu mwandishi ajaonyesha kama wanapewa nakala. Wapelekee wale wahusika waliopewa nakala, umeonyesha kuwa uliyeleta hii barua umefanya mahojiano na Chagulani hivyo vikao vya chama vitakaa kuwasuruhisha.
 
Chadema wameonyesha udhaifu wa hali ya juu katika masuala ya utawala katika Jiji la Mwanza, wakazi wa Mwanza waliwapa kura kwa imani mtaijenga Mwanza kinyume chake ni ufisadi tu na vita vya kugombea madaraka.
ritz hiyo barua ni ya majungu na wewe unapenda majungu yatokee ndani ya cdm hiki siyo chama cha mabastola,ccm inatumia akina matata kuivuruga chama ila hapo watagonga mwamba
 
Ni mtu mjinga pekee anayeweza kumlamu Wenje.Wenje ni Katapila linaloangusha vibaraka wote wa ufisadi.
Mkuu mleta mada ana mantiki hizi ni changamoto kwa uongozi swala la mwanza kuna mengi yanahitaj majibu
 
Mwanza kuna tatizo sio siri. Hizi chokochoko zitatugharimu sana huko mbele. Nashauri ofisi ya Katibu Mkuu bila upendeleo ifanye utafiti wa kina wa nini chanzo cha purukushani hizi. Najua wale madiwani waliofukuzwa wana mkono kwenye hizi fujo!
 
Kwa mwenye taarifa tafadhali.Dr slaa yuko wapi wakati chama kinayumba

Ulitaka na slaa atangaze jf kwamba anafuatilia kujua chanzo cha mgogolro wewe unaweza kumlingani slaa na hiki kimeo cha binadamu kisichojua hata sehemu ya kupeleka malalamiko.Yule anaitwa DR.SLAA ni mtaalamu wa ku-deal na issues siyo persons.get tuned you gonna see how dr.slaa is the best in dealing with disputes
 
Chagulani kaa utulie ili upate busara ya kufanya maamuzi yenye faida kwa ajili ya mustakabali wako wa kisiasa. Leo hii ndio unapata akili ya kumuandikia mwenyekiti malalamiko haya wakati ulipewa kila nafsi ya kuyasema lakini hukuweza.

Hii tabia ya kudhani kwamba unaweza ukagain political popularity kwa kumshambulia Wenje haitakusaidia kamwe. Alishindwa Masha utaweza wewe mtoto mdogo ambae bado unajifundisha siasa. Hao watu wa ccm wanaokudanganya wanakupoteza na mwisho wako kisiasa hauko mbali kama hautobadilika. Zile siasa za vyuoni zilishakwisha ni wengi tulizifanya lakini tulipofika mtaani tukaswitch kuendana na hali halisi ya maisha na siasa za nchi hii.

Na mwanachadema yeyote anayeshabikia huu upuuzi wa chagulani atambue kwamba hatutamuonea haya katu, lazima atawajibika kwa matendo yake.
 
Mkuu mleta mada ana mantiki hizi ni changamoto kwa uongozi swala la mwanza kuna mengi yanahitaj majibu

Katibu wa BAVICHA Mwanza,kama kweli wewe ndio umeandika haya,bila kujali yana ukweli au la,basi umeonyesha wewe ndo tatizo katika chama huko mwanza,na wewe unaesema kuwa ana mantiki huenda hujui mantiki inakwenda kwenye mantiki na wala usitegemee kwa kuandika hapa yeye kama kiongozi anatafuta suluhu na majawabu ya matatizo ya Mwanza.

Ni upuuzi mkubwa kujifanya unajua katiba na ukaanza kuchambua matatizo ya ofisini kwenu huko mwanza kupitia JF.Je KATIBA INAKUELEKEZA KUFANYA HIVI?JE HUJUI KAMA MAMBO HAYA YANA VIKAO HALALI VYA CHAMA AMBAKO NDIKO ULITAKIWA KUYAPELEKA?JE ULISHAWAHI KUMWNDIKIA KATIBU MKUU UKIMFAHAMISHA UKWELI UNAOUJUA WEWE KUHUSU MGOGORO WA KIUOGNOZI MWANZA.

Hakika hujui uongozi na nadhani uliingia CDM kwa kufuata mkumbo na upepo wa mabadiliko ulikupitia na ukajikuta umeangukia CDM.
Ungelikuwa unaijua kazi yako na unajua kuitumikia nafasi yako vema hakika usingeyaleta hapa mambo ambayo kimsingi yanapaswa kujadiliwa kwenye kikao na sio kuleta malalamiko yako kwenye JF.hii inanidhihirishia kuwa wewe ndio tatizo na umefanya hivi kwa maslahi binafsi na kundi lako. Na nakwambia hivi,wewe lazima tukushughulikie ndani ya chama,hatuwezi kuwa na mizigo kama wewe,unadhani kuna mahali au kuna kitu hakina changamoto katika kuhudumia jamii,au ulidhani CDM ni malaika hawakosei kitu?au ulidhani CDM ni sawa na Mungu?

lakini ni vipi umepata ujasiri wa kutaka kupata suluhu kupitia JF wakati wewe ni mmoja wa viongozi?tena ni kiongozi unaeongoza engine ya chama,BAVICHA ni engine ya chama unaushawishi mkubwa ni vipi leo unakuja kulalamika hapa JF?kwanza nilichoki-notice kwako ni kwamba huna nidhamu kabisa na wala you don't see beyond the curtain,for sure you think short katibu wewe.
Unaweza ukawa umeona jambo kweli,lakini solution yake ni hapa JF ukizingatia wewe ni muhusika?

Je, wanachama wako unaowaongoza ndio ulitaka waingie kwenye vikao vya chama kutafuta suluhu?jiangalie sana,wewe ni mjumbe wa kamati ya utendaji je haya umewahi kuyasema kwenye vikao?je uliwahi kumwandikia Katibu mkuu ukieleza haya?
mwisho nakutaka kuanzia leo ukome kumwambia katibu mkuu Dr Slaa hajui katiba.
 
Hold on just for a minute, I naively ignore the contents and just vaguely focus on your heading/title i.e. Wenje is a (source of the) problem....fine if he's a problem then what did you, Henry and Chagulani done?

Sio rahisi kihivyo....nadhani CCM wamewekeza sana kwa hawa double-agents hapo Mwanza ili tu kuchelewesha mabadiliko, maana hawawezi kuzuia mabadiliko chanya ya uongozi wa nchi hii.

Ushauri wa bure kwa Mataka na Chagulani (pamoja na mashabiki wenu) ni hivi; moto hauzimwi kwa kumwagia petroli.
Muda huu kama mngekuwa smart kidogo tu mngekaa kimya ili mtafakari na kujifunza pale mlipokosea (makosa yenu yako wazi tu). Hata kama kuna mahali mmeonewa kwa mchakato huo mngeweza kutafuta haki zenu ndani na/au nje ya CHADEMA. Lakini haya mnayofanya sasa hivi yanapigia mstari usahihi wa CC kuwavua uanachama 100%.
 
Back
Top Bottom