CHADEMA, Zitto, wataka ripoti BoT iwekwe hadharani

60B9185C-4C08-4779-85FE-DE33F42BF7B6.jpeg
 
Rais Samia alikabidhiwa ripoti hiyo kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere, kama alivyoagiza uchunguzi ufanyike wa fedha zilizotolewa benki hiyo kati ya Januari na Machi, mwaka huu.

Wakitoa maoni yao baada ya kuzungumza na Nipashe jana kwa nyakati tofauti, baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani walitaka serikali iiweke hadharani ripoti hiyo.

Jumatatu ya wiki hii, Rais Samia wakati akizungumza na wahariri na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali aliahidi kuwa ripoti hiyo itatolewa.

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika alidai upo ukweli unaelekea kufichwa kuhusu ufisadi kwenye matumizi ya fedha za serikali.

“Badala ya taarifa fupi kwa vyombo vya habari iliyotolewa ni muhimu ripoti kamili ikawekwa hadharani. Taarifa ya kuwa kuna matumizi ya fedha yamefanyika mara mbili ilipaswa kuambatana na majina yao kuchukuliwa.

“Ikiwa ni uchunguzi wa kweli na wa kina utafanyika hakuna namna aliyekuwa mlipaji mkuu wa serikali na aliyekuwa Waziri wa Fedha watakwepa kuhusika na kashfa hii,” Mnyika alidai.

Kauli ya kutaka ripoti hiyo iwekwe hadharani pia iliungwa mkono na Kiongozi wa Chama cha ACT - Wazalendo, Zitto Kabwe, ambaye alisema mpaka sasa ripoti hiyo wameiona kwa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari.

“Binafsi sijaisoma na mara nyingi huwa sitoi maoni kwenye jambo ambalo silijui, kwa hiyo ninachoweza kusema kwa sasa kwa kuwa Rais aliahidi kwamba ripoti hii itawekwa wazi basi iwekwe wazi ili tuisome na baadaye tuweze kutoa maoni, kwa sasa ni vigumu kuyatoa kwa sababu hatujui chochote kilichopo ndani ya ripoti hiyo,” alisema.

Taarifa hiyo iliyopokelewa juzi na Rais Samia inatokana na agizo lake alilolitoa Machi 28, mwaka huu, alipopokea ripoti ya CAG kwa mwaka wa fedha 2019/20.

Katika taarifa ya ukaguzi maalum ambayo Rais Samia alipokea juzi, Kichere alisema ukaguzi uliofanyika umebaini fedha zilizotolewa BoT katika kipindi hicho zilifuata taratibu zote, isipokuwa baadhi ya malipo yalikuwa yanatoka Hazina Kuu kwenda katika taasisi mbalimbali za serikali yalibainika kuwa na upungufu.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, upungufu huo unajumuisha baadhi ya taasisi kama vile Wakala wa Barabara (TANROADS) na Mamlaka ya Bandari (TPA) kufanya malipo mara mbili kwa kazi moja au kuchelewa kutumia fedha zilizoidhinishwa kwa ajili ya malipo ya kazi husika.

Chanzo: Nipashe
Wamekwapua mabilioni alafu wanatuongezea kodi na tozo
 
Back
Top Bottom