Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 16,987
- 20,271
Leo tarehe 01/12/2013 Chama kimezindua rasimu ya sera mpya ya mabadiliko ya Tabia ya nchi. Akizindua Sera hiyo Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano ya Ndani wa Chama Mh. John John Mnyika (Mb) ambaye aliambata na Katibu wa Baraza la Wanawake la Chama Mh. Naomi Kaihula, Afisa wa Sera na Utafiti wa Chama Mh. Mwita Waitara pamoja na Maafisa wengine wa Chama; Mh. Mnyika amesema CHADEMA ndio taasis ya kwanza kuzindua sera hiyo hapa nchini.
CHADEMA ndio Chama cha kwanza hapa nchini na Afrika kuwa na Sera ya Mabadiliko ya Nchi. Hata serikali yetu pamoja na kuwa Rais na Viongozi wengi wa Serikali wameshashiriki mikutano mingi kuhusu athari za Mabadiliko ya Tabia ya nchi lakini mpaka leo Tanzania haina Sera ya kukabiliana na janga hili Alisema Mnyika.
Mh. John John Mnyika
Mh. John John Mnyika
Mnyika aliongeza kuwa Rais ameshashiriki mikutano mingi akitolea mfano mkutano wa hivi karibuni uliofanyikanchini Scotland ambapo Rais alihudhuria ukiwa ni mkutanowa 19. Mikutano hiyo inayojulikana kwa jina la CORP imekuwa ikifanyika kila mwaka katika nchi mbalimbali ambapo mwaka juzi ulifanyikia Daban Afrika Kusini, mwaka jana ulifanyikia Doha Qatar na mwaka huu umefanyikia Scotland.
Mnyika ameongeza kuwa kilichozinduliwa leo ni rasimu iliyoandaliwa baada ya kukusanya maoni kwa wadau mbalimbali wakiwemo wataalam wa mazingira na sasa kitakachofanyika ni kukusanya maoni kutoka kwa Watanzania kwa muda wa mwezi mmoja na baadae Sera kamili itazinduliwa.
Sera hiyo inapatikana katika tovuti yetu katika kipengele cha Sera za Chama. Unaweza kuisoma na kutoa maoni yako kwa anuani zinazoonekana katika tovuti yetu au hapa hapa kwenye tovuti