CHADEMA yazindua Sera Mpya

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,985
20,263
Leo tarehe 01/12/2013 Chama kimezindua rasimu ya sera mpya ya mabadiliko ya Tabia ya nchi. Akizindua Sera hiyo Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano ya Ndani wa Chama Mh. John John Mnyika (Mb) ambaye aliambata na Katibu wa Baraza la Wanawake la Chama Mh. Naomi Kaihula, Afisa wa Sera na Utafiti wa Chama Mh. Mwita Waitara pamoja na Maafisa wengine wa Chama; Mh. Mnyika amesema CHADEMA ndio taasis ya kwanza kuzindua sera hiyo hapa nchini.

“CHADEMA ndio Chama cha kwanza hapa nchini na Afrika kuwa na Sera ya Mabadiliko ya Nchi. Hata serikali yetu pamoja na kuwa Rais na Viongozi wengi wa Serikali wameshashiriki mikutano mingi kuhusu athari za Mabadiliko ya Tabia ya nchi lakini mpaka leo Tanzania haina Sera ya kukabiliana na janga hili” Alisema Mnyika.

Mh. John John Mnyika
Mh. John John Mnyika

Mnyika aliongeza kuwa Rais ameshashiriki mikutano mingi akitolea mfano mkutano wa hivi karibuni uliofanyikanchini Scotland ambapo Rais alihudhuria ukiwa ni mkutanowa 19. Mikutano hiyo inayojulikana kwa jina la CORP imekuwa ikifanyika kila mwaka katika nchi mbalimbali ambapo mwaka juzi ulifanyikia Daban Afrika Kusini, mwaka jana ulifanyikia Doha Qatar na mwaka huu umefanyikia Scotland.

Mnyika ameongeza kuwa kilichozinduliwa leo ni rasimu iliyoandaliwa baada ya kukusanya maoni kwa wadau mbalimbali wakiwemo wataalam wa mazingira na sasa kitakachofanyika ni kukusanya maoni kutoka kwa Watanzania kwa muda wa mwezi mmoja na baadae Sera kamili itazinduliwa.

Sera hiyo inapatikana katika tovuti yetu katika kipengele cha Sera za Chama. Unaweza kuisoma na kutoa maoni yako kwa anuani zinazoonekana katika tovuti yetu au hapa hapa kwenye tovuti
 
Vizuri sana.
Chadema inazidi kuonyesha ni kwa namna gani kilivo tofauti na vyama vingine,Kwa kuchambua sera zinazolenga kuleta suluhu ktk Jamii nzima.
 
Mnyika jumbo lako ubungo limekushinda hakuna maendeleo yoyote uliyofanya maneno tu kweli siasa ni uongo tu na huu ndio mwisho wako hatukuchagui tena katafutesha ulime
 
Mabadiliko ya nchi au mabadiliko ya chama chenu?
Kweli nyie mmechanganyikiwa.
 
Mnyika jumbo lako ubungo limekushinda hakuna maendeleo yoyote uliyofanya maneno tu kweli siasa ni uongo tu na huu ndio mwisho wako hatukuchagui tena katafutesha ulime

Nyinyi Mazuzu wa Mwigulu, hamna akili kabisa. Wakati watu wanazungumzia issues zinazohusu matatizo wanayopata watu nyinyi mnahangaika kuiremba Div. 0 kuwa div. Five. Kwanza hujui kazi ya mbunge, mnafikiri kazi mbunge ni kugawa Tshirt na Kanga, kama wanavyofanya maCCM yanu.

JJ Mnyika ubungo hamuwezi kumtoa hata kwa dawa
 
Musitutoe nnje ya MADA,Watu wanataka demokrasia ndani ya Chama.

You peole be serious! I d'nt imagine to find even schoolars to be ignorant over what is democracy! Free and fair electing of an office bearier is just a small part of an organ to exercise democracy.
 
Demokrasia ndo nini? Je Mkiti wa magamba mpinzani wake alikuwa nani?

Demokrasia si lazima uwe na mpinzani we mufilisi demkrasia ni kuifata misingi iliyokubalika na wengi ktk maamuzi ya jambo so kama mwenyekiti wa magamba anapatikana kwa kupigiwa kura ya kuwa au kutokuwa na imani ndio wameamua hivyo maadam hawakiuki walichokubaliana. Waambie na wenzio maana imekuwa single hii
 
Back
Top Bottom