CHADEMA Yazindua Kanda ya Zanzibar

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,491
2,000
Chama cha Demokrasia na Maendeleo - CHADEMA kimezindua rasmi kanda ya Zanzibar ya chama hicho.

Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo alikuwa Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Hamad Yusuf.Uzinduzi huo ulifanyika katika ukumbi wa Jamat Khan mjini Unguja.

Viongozi mbalimbali wa mikoa, wilaya,matawi na Makamanda wa chama hicho upande wa Zanzibar walihudhuria.Pia walikuwepo wabunge wa viti maalum Zanzibar.

Akizungumza katika uzinduzi huo Naibu Katibu Mkuu huyo aliwataka wanachama wa chama hicho kushikamana na kuzidi kuisimika Chadema Zanzibar.

Pia Kiongozi huyo aliwamiminia sifa viongozi wakuu wa chama hicho Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa kwa kazi kubwa wanayofanya huku akisema viongozi hao wamekuwa kama Nembo ya chama hicho.

Uzinduzi huu wa Kanda ya Zanzibar umefanyika baada ya kukamilika zinduzi za Kanda za Tanzania Bara.
 

fikirikwanza

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
7,448
2,000
hongereni sana, CDM ikishika kasi Zanzibar wanzanzibari watapata kile wanachodai kila mwaka kutoka CCM na CUF bila mafanikio
 

Marire

JF-Expert Member
May 1, 2012
12,060
2,000
tuje tufanye tathimini ya hizi kanda tujue faida yake
kama kanda ya kusini sijawahi kusikia makeke yake kabisa.
cc: Molemo
 
Last edited by a moderator:

manning

JF-Expert Member
Apr 1, 2013
3,524
1,250
NYOTA MPYA YA UHURU WA ZANZIBAR Imeanza kuwaka kupitia CHADEMA Wanzanzibar acheni siasa za mazoea kipeni ushirikiano mpate mnachotaka.
 

kistwangara

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
656
195
tundu lissu alishasema zanzibar siyo muhimu kwa chadema kulikoni tena.

duuuuhh!? Naona babako kakurithisha ujinga ndo umekuwa mjinga zaid. Hv ww tukiuliza una zaid ya semi mia mbili umezipata wapi? Hayo ndo unayokumbuka mbona haukumbuki ubakaji wa kada wenu kapuya?
 

masanjasb

JF-Expert Member
Aug 11, 2011
2,364
1,195
Nilijiunga cdm kwa ushawishi wa dr slaa na sasa naipenda chadema kama taasisi..... .lets move on
 

Ruttashobolwa

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
47,865
2,000
chama cha demokrasia na maendeleo - chadema kimezindua rasmi kanda ya zanzibar ya chama hicho.

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa naibu katibu mkuu zanzibar hamad yusuf.uzinduzi huo ulifanyika katika ukumbi wa jamat khan mjini unguja.

Viongozi mbalimbali wa mikoa, wilaya,matawi na makamanda wa chama hicho upande wa zanzibar walihudhuria.pia walikuwepo wabunge wa viti maalum zanzibar.

Akizungumza katika uzinduzi huo naibu katibu mkuu huyo aliwataka wanachama wa chama hicho kushikamana na kuzidi kuisimika chadema zanzibar.

pia kiongozi huyo aliwamiminia sifa viongozi wakuu wa chama hicho freeman mbowe na dr wilbroad slaa kwa kazi kubwa wanayofanya huku akisema viongozi hao wamekuwa kama nembo ya chama hicho.

Uzinduzi huu wa kanda ya zanzibar umefanyika baada ya kukamilika zinduzi za kanda za tanzania bara.

sifa gani amewamiminia?
Akitaka kuwajua chadema chumbani na sebureni ajaribu kuutaka urais au uenyekiti wa mbowe na slaa.

Hivi amezungumziaje swala la campaign ya gongo?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom