CHADEMA Yazindua Kanda ya Zanzibar

Chadema ni kama maji usipokunywa utayaoga, sio bara sio Zanzibar TWENDE KAZI NGUVU YA UMMA.

Kusini mmekushindwa mtaweza Zenji!?. Babu yenu Slaa ashawaharibu na Gongo yake. Padre mzima anasupport Gongo!,MAJANGA.
 
Molemo tunasubiri picha mkuu.
jf haijazuia picha.
 
Last edited by a moderator:
Kanda hiyo na iwe chachu ya kuwapatia wazanzibar madaraka kamili juu ya nchi yao...
yaani ukiongea tu hii lugha basi umefungua mioyo ya wazanzibar na wanakuwa wasikivu kweli kweli kama ndani yake itakua hakuna hidden agenda.
 
Tundu Lissu alishasema Zanzibar siyo muhimu kwa Chadema kulikoni tena.

Umeiona ile shule yenu ya Bagamoyo ambayo wanafunzi 12 wamefauru kwa miujiza! Basi nguvu yote kapeleke kule kuliko kujikaribisha ktk mambo yasiyo kuhusu!
 
Zanzibar kunakubalika vyama viwili tu navyo ni CUF na CCM hatutaki vyama vya wakristo lakini kupachika bendera zao hilo sio tatizo.
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo - CHADEMA kimezindua rasmi kanda ya Zanzibar ya chama hicho.

Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo alikuwa Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Hamad Yusuf.Uzinduzi huo ulifanyika katika ukumbi wa Jamat Khan mjini Unguja.

Viongozi mbalimbali wa mikoa, wilaya,matawi na Makamanda wa chama hicho upande wa Zanzibar walihudhuria.Pia walikuwepo wabunge wa viti maalum Zanzibar.

Akizungumza katika uzinduzi huo Naibu Katibu Mkuu huyo aliwataka wanachama wa chama hicho kushikamana na kuzidi kuisimika Chadema Zanzibar.

Pia Kiongozi huyo aliwamiminia sifa viongozi wakuu wa chama hicho Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa kwa kazi kubwa wanayofanya huku akisema viongozi hao wamekuwa kama Nembo ya chama hicho.

Uzinduzi huu wa Kanda ya Zanzibar umefanyika baada ya kukamilika zinduzi za Kanda za Tanzania Bara.

Kwani chadema mmeshaitambua Zanzibar kama ni nchi? Si mnampango wa kuvunja muungano! Ha!
 
Kazi kweli kweli mpaka 2015 tutaona vitu vingi sana,chadema inazidi kupanda juu Mungu yuko upade wetu kila la heri.
 
Back
Top Bottom