Hii ni zaidi ya kulala na Bundi.
CHADEMA kimepata pigo kubwa baada ya aliyekuwa Katibu Mwenezi wa chama hicho Kata ya Mkuza Abdallah Maja kuhama chama hicho na kujiunga na CCM.
Maja pamoja na wanachama wengine wa CHADEMA akiwemo Yusuph Komba walirudisha kadi za Chama hciho kwenye mkutano wa hadhara wa Mwenyekiti wa CCM Kibaha Mjini Maulid Bundala uliofanyika Mkuza Kibondeni wilaya ya kibaha wakati wa ziara yake inayoendelea kwenye mji huo kuangalia utekelezaji wa Ilani ya Chama.
Akizungumza mara baada ya kuhamia CCM, Maja alisema kuwa kule Chadema hakuna lolote kwani siasa zake ni za kibabaishaji. "kule hakuna lolote zaidi ya ujanja ambao hautaweza kuleta maendeleo kwa wananchi. Mimi nilipata matatizo lakini walishindwa kunisaidia hadi nikasaidiwa na CCM, nimeona kuwa chama cha ukweli ni Cha Mapinduzi pekee" Alisema Maja.
Source: Majira jumatatu septemba 30, 2013. Ukurasa wa 10:
Baada ya Habari hiyo ya kusisimua napenda kumpa pole ya dhati kabisa Mwenyekiti wa Chadema Taifa Bw. Freeman Aikaeli Mbowe kwa kufiwa na Ndugu yake Grace Aikaeli Mbowe, ambaye amefariki katika ajali ya Gari iliyotokea eneo la Kabuku Jana.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina la Bwana Lihimidiwe. Pole mara mbili Mheshimiwa.