CHADEMA yawapa raha watanzania: Taifa Lazizima

CHADEMA yawapa raha watanzania: Taifa Lazizima

Wakuu zangu,

Kwanza kabisa ningependa kutoa shukran kwa uongozi wa Chadema na watu wote walioshiriki ktk mchakato wa katiba mpya. Nachopenda kufahamu ni kwamba muswada uliopita unakubalika na wananchi?.. Je, marekebisho yaliyofanywa yamefanywa kwa kuzingatia hoja za wananchi na kwa kiasi gani tunakubaliana na sheria itakayopitishwa.

Mkandara,hakika hata mimi nimefurahi.Hakika kwa kiasi fulani madai makubwa yaliyokuwa yanapigiwa kelele yametekelezwa.Tusubiri tuone hii dhamira njema kama itatekelezwa ipasavyo.
 
leo kwa machozi ya furaha nampongeza dr slaa,lissu,mbowe,mama nkya,jukwaa la katibu,deus kiwanga,wanaCDM wote duniani,mh col.jakaya m kikwete,katibu mkuu mpya,regia mtema/RIP,mwisho watz wote kwa kuipa mamlaka cdm itupiganie wanyonge..tulisema watawale toka ikulu,cdm itawale toka mioyoni mwa watu...namlaani selina,AG,na mama kilango waliokuwa wamepanga kutupeleka kwenye vita ya kijinga...mama kilango ulisema..hata cdm ikitoka bungen,wanaccm wanatosha kujenga katibu...yako wapi sasa?CHALIII! ASANTE CDM,ASA
 
Peopleeeeeeeeeeeeeeezzzzzzzzzzzzzzzzzzzzz!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!...........................................
 
Wakuu zangu,

Kwanza kabisa ningependa kutoa shukran kwa uongozi wa Chadema na watu wote walioshiriki ktk mchakato wa katiba mpya. Nachopenda kufahamu ni kwamba muswada uliopita unakubalika na wananchi?.. Je, marekebisho yaliyofanywa yamefanywa kwa kuzingatia hoja za wananchi na kwa kiasi gani tunakubaliana na sheria itakayopitishwa.
Mkandara

Elewa nothing is perfect in this world, hakuna hata siku moja ambayo wote kwa pamoja tutakuja kukubaliana,

kwa hiyo watu mnapokubaliana kwa jambo fulani lazima mshukuru Mungu na mpongezane.
 
Nawapongeza wakuu wote mliyoona yaliyofanywa na hawa wana mapinduzi. CHAGUA CHADEMA CHAGUA MAENDELEO.
 
Kweli wewe msomaji tu!
Big up kwa pongezi zako na nasaha
Watanzania wenzangu! mimi nimsomaji tu humu na sijawahi kuchangia sana ila naomba na mimi kwa hili niingie kwenye historia ya wawakilishi wachache wataopata fursa ya kupongeza viongozi wetu makini waliofanikisha marekebisho haya kupita kwa ajili tu ya masilahi ya Watanzania.. Kwanza kabisa napenda kwa dhati kumshukuru na kumpongeza RAIS wetu J M Kikwete kwa ujasiri na pengine moyo wa usaliti aliouonyesha kwa chama chake na kuweka maslahi na uzalendo mbele kuridhia mawazo na mapendekezo yaliyowasilishwa kweke na CHADEMA. Ni ukomavu wa hali ya juu sana katika ulimwengu wa waliostaarabika. ni dhahiri siasa za dunia ya tatu ni tete mbovu hasa kwenye masuala ya msingi kitaifa kama hili. Ni historia Rais na utaishi na raha hiyo milelePili Nachukua fursa hii kuwapongeza CHADEMA NA WANA CHADEMA kwa kazi nzuri inayofanywa kuinua taifa letu changa linaloelekea kupotoshwa na kuyumbishwa na walafi wachache! ni hatua ya hali ya juu iliyotukuka inayokifanya CHADEMA kuimarika kila kukicha pale inapokumbatia Utaifa na uzalendo wa kweli kwa kila wazo au jambo linalofanywa. Nawapongeza sana na ninawahakikishia historia itachukua mkondo wake pale muda utakapotimia.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Wakati tunawapongeza waliofanikisha kupigwa kwa hatua hii ndogo, tutie vichwani mwetu kuwa kuna safari ndefu sana na changamoto nyingi mno kufikia kupata katiba inayohitajika kwa taifa hili... Lazima tuwe macho zaidi, hila ni nyingi na zitazidi kuwa nyingi zaidi. Bado wananchi wanatakiwa kuamshwa na kuelimishwa zaidi juu ya maana na umuhimu wa zoezi hili. Kumbukeni ccm hawaaminiki... Kama wamegeuka waonyeshe ktk kila nyanja kuwa kweli wamebadilika.
 
Mkuu sina cha kuongeza! Tusipokuwa makini hadi UDINI utatumika ili kufanikisha malengo ya wapuuzi fulani. Kimsingi, ndio vita ya Katiba imeanza na ni vita ngumu ajabu.
 
Nina pata wasiwasi na uwezo na upeo wako wa kufikiri. Ungeliangalia bunge leo wakati wanapitisha muswada huu , wazi kuwa CDM walikuwa wanaomba huruma ya CCM , kwa Lissu mishipa ilikuwa inamtoka mpaka Jaji Werema alikuwa anamwonea huruma. Na kama umesoma waraka wa Kafulila juu ya suala hili ni wazi kuwa CDM wamelamba garasa badala ya dume. Kwa taarifa yako ni mapendekezo yasiyozidi 5% ndio yamefanyiwa kazi, sasa hapo mtu amepata 5% unampa pongezi ya nn badala yakumsikitikia?

Yaani ktk ***** ne vihio ww ni kiongozi wao...
 
fmpiganaji, tunashukuru kwa kutupa mwelekeo mzima wa mambo yanavyokwenda mpaka sasa, lkn kama mkereketwa wa vuguvugu la mabadiliko ya kisiasa yanayoendela kutokea nchini Tanzania, naomba ufafanuzi kuhusu tukio la wabunge wa CDM kutoka nje ya bunge siku ambayo Rais Kikwete alipozindua bunge. Ninachokumbuka ni kwamba kitendo kile kilifanyika kama ishara ya kuonyesha kwamba wana-CDM hawakukubaliana na matokeo ya uchaguzi wa Rais, na kwa maana hii walitoka nje ya bunge kwa sababu ya kutomtambua Rais ambaye aliandaliwa kwa ajili ya uzinduzi wa bunge hllo. Kinachonichanganya zaidi ni kitendo cha viongozi wa CDM kuomba kukutana na Rais, ambae hapo mwanzo walitangaza kutomtambua, kwa ajili ya kumshauri kuhusu mambo ya katiba. Swali langu, au ufafanuzi ninaohitaji kuupata toka kwenu wanaJF, hasa wana-CDM, ni huu: Je, vuguvugu la wana-CDM kutomtambua Rais kikwete limeishia wapi?, na hivi nini tamko rasmi la CDM kuhusu kutomtambua Rais Kikwete
 
Walishatoa ufafanuzi na wakaeleza kwamba kutoka kwao Bungeni kipindi kile ilikuwa ishara ya "KUPINGA UTARATIBU ULIOMUWEKA MADARAKANI RAIS KIKWETE" na kilio kikuu kikiwa KATIBA iliyozaa TUME MBOVU YA UCHAGUZI. Tena wakasema, Kikatiba (kwa katiba hiyo mbovu) Kikwete ni Rais halali wa Tanzania. Umeelewa Mkuu?
 
Asante sana mkuu.., nimekuelewa.
 
ni hatua nzuri, asante mchambuzi kwa thread nzuri, nategemea kumuona PASCO wa JF kwenye hii thread, nakumbuka alivyomponda Lissu na kifungu chake cha kanuni ya 57.
 
Mkuu fmpiganaji u made an outstanding analysis and fabulous observation. Kwann baba Mwanahawa hakuoni akupe ajira pale magogoni? Big up cdm, big up baba mwanahawa and big up jf members, only those who are not leftists i mean riz, rejao, madam foxy and their company. Mkuu u made my day. 😛oa :focus:
 
Pamoja na pongezi kwa CDM, binafsi naanza kumpopngeza JK, mambo mengi nimekuwa nikimuona JK anapotoka sana lakini katika hili, naweza kukiri kuwa akilisimamia vizuri basi naye atajiandikia historia katika siasa za Tanzania. Tulikotaka kwenda kama si busara za CDM na uungwana wa JK katika hili naamini tungefika pabaya. Ninachomhurumia tu JK asipokuwa makini na ndumilakuwili kama A. Kilango itakula kwake, big up JK kwa kuwa mbayuwayu(naamini walikushauri wahafidhina lakini ukatumia na zako).
:A S 465::A S 465:
 
...KWA KWELI WANASTAHILI PONGEZI KUBWA SANA....Na hii inanifanya niamini kuwa kila jambo linalofanyika kwa taabu mwisho wake huwa ni mzuri...wamekuwa wakiitwa vichaa,wendawazimu,wapumbavu,wabishi,wapenda fujo...lakini hata wakati wa kupigania uhuru Nyerere na wenziye walipitia ugumu wa aina hiyo wa kutokuaminiwa hadi mafanikio yalipopatikana...CHADEMA NI CHAMA MAKINI,IMARA NA MADHUBUTI...KINA VIONGOZI WENYE UPEO WA KUONA MBALI NA UTAALAM WA HALI YA JUU,WENYE KUTHUBUTU KUDHALILIKA KWA AJILI YA UKOMBOZI WA TANZANIA....MUNGU AWABARIKI SANA!
 
Back
Top Bottom