SI KWELI CHADEMA yatoa pole kufuatia kifo cha Hafidh Ameir

SI KWELI CHADEMA yatoa pole kufuatia kifo cha Hafidh Ameir

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #2
View Source #2
Kumekuwepo na picha inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ikidaiwa kuwa ni taarifa kwa umma iliyotolewa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kuhusu kutoa salamu za pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufuatia kifo cha mume wake, Hafidh Ameir.
Chdmsm.jpg
 
Tunachokijua

Katika taarifa hiyo, imeelezwa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Mhe. Tundu Lissu, ametoa salamu za pole kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kufuatia msiba huo. Aidha, taarifa hiyo inasema Mhe. Lissu alitoa maelekezo ya kufikisha salamu zake za pole kupitia Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche, alipokutana naye mahakamani wakati wa kuendelea kwa kesi.

Taarifa hiyo pia inadai kuwa, kwa niaba ya wanachama wote wa CHADEMA, chama hicho kimetoa salamu za pole kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, familia, ndugu, jamaa na wote walioguswa na msiba wa Hafidh Ameir.

Hata hivyo, ufuatiliaji wa maneno muhimu pamoja kurasa rasmi za CHADEMA zimebaini kuwa chama hicho hakijatoa taarifa kwa umma yenye maudhui hayo, Aidha, ukurasa na kupitia Instagram, umekanusha taarifa hiyo.

Aidha kupitia ukurasa rasmi wa instagram wa Brenda Rupia, ambaye Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA,umekanusha taarifa kwa kuandika kuwa taarifa hizo ni potoshi

Taarifa hiii inajiri ambapo Tundu Lissu akiwa mahakamani aliuliza iwapo ujumbe wake wa pole alioutuma kwa familia ya marehemu ulikuwa umewafikia wafiwa.
CHADEMA kamwe hawawezi kumita SAMIA RAIS !Kamwe haiwezi kutokea

TEC wakiongozwa na Rais na Maaskofu wote wa Catholic church wanamtambua,wewe mlalahoi wa Tandale usipomtambua kknapungua nini.

CHADEMA mtakapofikia malengo yenu mtakuwa mmechoka sana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom