CHADEMA yasisitiza kufanya maandamano kesho ya amani

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA kimesisitiza kwamba maandamano ya amani ambayo yalipangwa kufanyika kesho nchi nzima yatafanyika.

Akizungumza na MwanaHalisi Online, Edward Simbeye, katibu mwenezi wa Baraza la Vijana la chama hicho (BAVICHA), amesisitiza kuwa maandalizi kwa ajili ya maandamano hayo yanaendelea vizuri na tayari chama hicho kilishaandika barua kulitaarifu jeshi la polisi kuhusiana na uwepo wa maandamano hayo katika kila mkoa nchini.

Aidha, kiongozi huyo amesema kuwa mpaka muda huu bado jeshi hilo halijajibu barua ambayo chama hicho kimeliandikia na kuongeza kuwa maandamano hayo yatafanyika hata kama jeshi hilo litakuwa halijajibu barua yao mpaka kufikia siku ya kesho.

“Maandalizi yanaendelea vizuri na hapo kesho tutatoa muongozo kwa wanachama wetu na wananchi kwa ujumla kuhusiana na mahali ambapo maandamano hayo yataanzia na kuishia katika kila mkoa nchini.” amesema Simbeye

Akifafanua kuhusiana na tabia ya jeshi la polisi kuzuia kufanyika kwa maandamano kwa sababu mbalimbali, Simbeye amesema kuwa maandamano ni haki ya kikatiba na jeshi la polisi lina wajibu wa kulinda wananchi ambao wanatumia haki yao ya kikatiba kufanya maandamano na si kuzuia maandamano na kuongeza kuwa maandamano hayo yatafanyika hata kama jeshi hilo litazuia maandamano hayo.

Wiki iliyopita, baraza hilo la vijana lilitangaza kuwepo kwa maandamano ya amani siku ya kesho ambayo waliyapa jina la “Black Thursday” yenye lengo la kushinikiza kuwepo kwa haki za kisiasa, kiuchumi, utawala wa sheria pamoja na haki za binadamu nchini.
Duh, mngefanikisha hayo maandamano leo tusingelala kwa kelele zenu. Lakini Mungu mkubwa, mmenyng'onyeaa kama mmefiwa vile.
 
Maandamano huwa yanakoswa msisimko pale viongozi WA chama wanapotanguliza wengine mstari WA mbele
Wao wakiwa hawapo kabisa

Kufanya hivyo ni kutoa mhanga wengine
Viongozi wakibaki salama

nb napenda kuandamana lakini sharti langu ni hili
Viongozi wawe mstari WA mbele.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Police hawajajibu kwa kuwa bado wanasubiri maagizo ya IGP. IGP nae anasubiri Waziri mwenye dhamana aseme kabla hajawaagiza watu wake.

Waziri mwenye dhamana na yeye anasubiri msg aliyomtumia mwenye Nchi ijibiwe maana kwa hofu na woga alionao, anagwaya hata kupiga simu jumba jeupe kuomba mwongozo kwa kuhofia kuitwa mpumbavu. One man show ni tatizo kubwa.

Hamna haja ya kibali cha polisi. Kaandamaneni tu. Lissu na Sumaye na Halima waongoze
 
Maandamano yasiyoruhusiwa ni kinyume cha kanuni na utaratibu. Bora mlivyonywea mmeokoa roho zenu.
 
Wapinzani Wa Tz akili zao ni takataka,wanadai democracy wakati ndani ya vyama vyao haipo,mboe kawa mwenyekti Wa kudum,zito,mfalme,mbatia,Mali yake,halafu wangedai mambo kama dawa hospital, elim,Huduma kama umeme,maji,barabara,vitabu mashuleni,mikopo kwa wanafunzi,fire ektingisha maduka,huo ni wizi wanaibiwa watu,traffic watumie machine sio vitabu,Efd watu wanauziwa mbovu,kuna mambo wapinzani wakiyaweka wazi watu wako tayari kuunga mkono sio mambo ya udikita uchwara

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiki chama sasa kinajifia chenyewe kutoka kwenye maandamano ya ukweli wakati wa Dr. Slaa hadi maandamano ya kwenye key board! Akiri za nyumbu ni bure kabisa hivi mlitegemea Lowasa aongoze maandamano kweli? kama ameshindwa tu kuvaa magwada yenu sembuse kuandamana!
 
Back
Top Bottom