CHADEMA yasisitiza kufanya maandamano kesho ya amani

CHADEMA yasisitiza kufanya maandamano kesho ya amani

Leo nimeona jamaa wengi kila kona wamevaa kanzu nikajua maandamano yameanza, kuja kushtuka nikagundua ni idd leo.
Hii sms nimeipiga na sikrini shuti kabisaaaaa[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] akija waifu nimuonyeshe
 
Naanza kuelewa nini maana ya kesho aseee


Ndiyo hivyo aiseeeeh, upinzani wasela tu.
Ukianza na mzee wa gia ya angani hadi familia zao ila wanataka wale wa pangu pakavu wakavunjwe milonjo kwa virungu wakati wao wapo kwenye kiyoyozi cha chopa!!!!
 
Wakitaka maandamano yafanyike waseme tu kuwa ni ya kumpongeza sizonje kwa kazi nzuri ya kutuahidi noah pindi akashya watapolipa pesa walizoiba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndiyo hivyo aiseeeeh, upinzani wasela tu.
Ukianza na mzee wa gia ya angani hadi familia zao ila wanataka wale wa pangu pakavu wakavunjwe milonjo kwa virungu wakati wao wapo kwenye kiyoyozi cha chopa!!!!
Hapa naanza kuelewa kwa nini kenya upinzani unaheshimika

Wao wanawapizani
Sisi tuna wapingaji

Hapo utamuelewa aliesema tunahitaji miaka 40 kuwafikia kenya
 
Upinzani wa Tanzania na matamko ni kama ya waenda kuzimu maandamano yatangazwe na Katambi alafu yafanyike??
Akina myika na Lema wao wamesusa au?
Mtamkumbuka sana Dr Slaa
 
Police hawajajibu kwa kuwa bado wanasubiri maagizo ya IGP. IGP nae anasubiri Waziri mwenye dhamana aseme kabla hajawaagiza watu wake.

Waziri mwenye dhamana na yeye anasubiri msg aliyomtumia mwenye Nchi ijibiwe maana kwa hofu na woga alionao, anagwaya hata kupiga simu jumba jeupe kuomba mwongozo kwa kuhofia kuitwa mpumbavu. One man show ni tatizo kubwa.
Umemsahau mkuu wa mkoa wa Dar
 
Hapa naanza kuelewa kwa nini kenya upinzani unaheshimika

Wao wanawapizani
Sisi tuna wapingaji

Hapo utamuelewa aliesema tunahitaji miaka 40 kuwafikia kenya


Mantiki iko umo humo.

Kwa ujumla, upinzani hapo Tanzania umepoteza dira. Hawajielewi wanapaswa kufanya nini na hawajui wanataka nini!!

Wapinzani, wapo wapo tu kama kuku wa kichina.
 
Mantiki iko umo humo.

Kwa ujumla, upinzani hapo Tanzania umepoteza dira. Hawajielewi wanapaswa kufanya nini na hawajui wanataka nini!!

Wapinzani, wapo wapo tu kama kuku wa kichina.
Naanza kuuona U Profesa wa Lipumba
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA kimesisitiza kwamba maandamano ya amani ambayo yalipangwa kufanyika kesho nchi nzima yatafanyika.

Akizungumza na MwanaHalisi Online, Edward Simbeye, katibu mwenezi wa Baraza la Vijana la chama hicho (BAVICHA), amesisitiza kuwa maandalizi kwa ajili ya maandamano hayo yanaendelea vizuri na tayari chama hicho kilishaandika barua kulitaarifu jeshi la polisi kuhusiana na uwepo wa maandamano hayo katika kila mkoa nchini.

Aidha, kiongozi huyo amesema kuwa mpaka muda huu bado jeshi hilo halijajibu barua ambayo chama hicho kimeliandikia na kuongeza kuwa maandamano hayo yatafanyika hata kama jeshi hilo litakuwa halijajibu barua yao mpaka kufikia siku ya kesho.

“Maandalizi yanaendelea vizuri na hapo kesho tutatoa muongozo kwa wanachama wetu na wananchi kwa ujumla kuhusiana na mahali ambapo maandamano hayo yataanzia na kuishia katika kila mkoa nchini.” amesema Simbeye

Akifafanua kuhusiana na tabia ya jeshi la polisi kuzuia kufanyika kwa maandamano kwa sababu mbalimbali, Simbeye amesema kuwa maandamano ni haki ya kikatiba na jeshi la polisi lina wajibu wa kulinda wananchi ambao wanatumia haki yao ya kikatiba kufanya maandamano na si kuzuia maandamano na kuongeza kuwa maandamano hayo yatafanyika hata kama jeshi hilo litazuia maandamano hayo.

Wiki iliyopita, baraza hilo la vijana lilitangaza kuwepo kwa maandamano ya amani siku ya kesho ambayo waliyapa jina la “Black Thursday” yenye lengo la kushinikiza kuwepo kwa haki za kisiasa, kiuchumi, utawala wa sheria pamoja na haki za binadamu nchini.
Wafanye maandamano ya kudai katiba
 
Back
Top Bottom