CHADEMA yasisitiza kufanya maandamano kesho ya amani

CHADEMA yasisitiza kufanya maandamano kesho ya amani

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA kimesisitiza kwamba maandamano ya amani ambayo yalipangwa kufanyika kesho nchi nzima yatafanyika.

Akizungumza na MwanaHalisi Online, Edward Simbeye, katibu mwenezi wa Baraza la Vijana la chama hicho (BAVICHA), amesisitiza kuwa maandalizi kwa ajili ya maandamano hayo yanaendelea vizuri na tayari chama hicho kilishaandika barua kulitaarifu jeshi la polisi kuhusiana na uwepo wa maandamano hayo katika kila mkoa nchini.

Aidha, kiongozi huyo amesema kuwa mpaka muda huu bado jeshi hilo halijajibu barua ambayo chama hicho kimeliandikia na kuongeza kuwa maandamano hayo yatafanyika hata kama jeshi hilo litakuwa halijajibu barua yao mpaka kufikia siku ya kesho.

“Maandalizi yanaendelea vizuri na hapo kesho tutatoa muongozo kwa wanachama wetu na wananchi kwa ujumla kuhusiana na mahali ambapo maandamano hayo yataanzia na kuishia katika kila mkoa nchini.” amesema Simbeye

Akifafanua kuhusiana na tabia ya jeshi la polisi kuzuia kufanyika kwa maandamano kwa sababu mbalimbali, Simbeye amesema kuwa maandamano ni haki ya kikatiba na jeshi la polisi lina wajibu wa kulinda wananchi ambao wanatumia haki yao ya kikatiba kufanya maandamano na si kuzuia maandamano na kuongeza kuwa maandamano hayo yatafanyika hata kama jeshi hilo litazuia maandamano hayo.

Wiki iliyopita, baraza hilo la vijana lilitangaza kuwepo kwa maandamano ya amani siku ya kesho ambayo waliyapa jina la “Black Thursday” yenye lengo la kushinikiza kuwepo kwa haki za kisiasa, kiuchumi, utawala wa sheria pamoja na haki za binadamu nchini.

Itakuwa vizuri mkitanguliza Wake zenu na Watoto wenu Mstari wa mbele badala ya kuwaacha nyumbani halafu mtangulize vijana Masikini washiriki mipango yenu batili ya Kuhujumu Taifa
 
Watoto wa Mbowe,Prof Safari,Sumaye,Lowassa nk wapo masomoni ulaya huku mkitaka watoto wa maskini waandamane,wapigwe na FFU,zamu hii hamumpati mtu,wazungusha mikono wameshapata akili labda muanzishe maandamano ya humu JF mtawapata wengi.
 
Daaah, best message of the week
Imewapata huyoo akina salary slip na wingine
 
Safi sana hii tupo pamoja wadhalimu lazima wapingwe na kila mwenye akili timamu
 
Hivi hawa jamaa hawana matatizo mengine? I mean hata tu kusaidia waototo wao home work?
Nyumba zimebomolewa licha ya zuio la kimahakama mtu atakaa anasaidia watoto homework wakati hata sare za shule zimepotelea kwenye bomoabomoa pamoja na madaftari,kwanini usiende kudai uwepo wa utawala wa sheria na kuwepo kwa heshima ya haki za binadamu?

Mkuu fikiri vyema.
 
Naombeni kufahamu mapema kama kibali kimepatikana, vinginevyo nijue namna ya kukabiliana na vitu vya ncha kali....
 
Yanaanzia wapi na kuishia wapi?

[emoji124]‍♂️naenda zimbobo.
 
Police hawajajibu kwa kuwa bado wanasubiri maagizo ya IGP. IGP nae anasubiri Waziri mwenye dhamana aseme kabla hajawaagiza watu wake. Waziri mwenye dhamana na yeye anasubiri msg aliyomtumia mwenye Nchi ijibiwe maana kwa hofu na woga alionao, anagwaya hata kupiga simu jumba jeupe kuomba mwongozo kwa kuhofia kuitwa mpumbavu. One man show ni tatizo kubwa.
Uko sahihi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyumba zimebomolewa licha ya zuio la kimahakama mtu atakaa anasaidia watoto homework wakati hata sare za shule zimepotelea kwenye bomoabomoa pamoja na madaftari,kwanini usiende kudai uwepo wa utawala wa sheria na kuwepo kwa heshima ya haki za binadamu?

Mkuu fikiri vyema.
..unataka kuniambia nyumba zimebomolewa Tanzania nzima?
 
Itakuwa vizuri mkitanguliza Wake zenu na Watoto wenu Mstari wa mbele badala ya kuwaacha nyumbani halafu mtangulize vijana Masikini washiriki mipango yenu batili ya Kuhujumu Taifa
Taifa hapo linahujumiwa nini? Tatizo ni walewalle walamba miguu. Woga ni kifo ujasiri utakuweka huru. Jitafakari.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi hawa jamaa hawana matatizo mengine? I mean hata tu kusaidia waototo wao home work?
mnalichukulia suala la kusaidia mtoto homework kama ni tatizo, wakati ni kitu cha kawaida kabisa kwa mzazi anayejitambua kama vile kuhakikisha mtoto amekula mlo kamili
 
Police hawajajibu kwa kuwa bado wanasubiri maagizo ya IGP. IGP nae anasubiri Waziri mwenye dhamana aseme kabla hajawaagiza watu wake. Waziri mwenye dhamana na yeye anasubiri msg aliyomtumia mwenye Nchi ijibiwe maana kwa hofu na woga alionao, anagwaya hata kupiga simu jumba jeupe kuomba mwongozo kwa kuhofia kuitwa mpumbavu. One man show ni tatizo kubwa.
Hahahaha[emoji23][emoji28][emoji23][emoji28] kama kuna kaukweri flani hivi
 
Back
Top Bottom