CHADEMA yasisitiza kufanya maandamano kesho ya amani

CHADEMA yasisitiza kufanya maandamano kesho ya amani

Hakuna tamko LA CHADEMA hata moja liliwahi kutekelezwa hebu watuambie M4C iko wapi? Operation Sangara iko wapi? Ushindi SAA NNE asubuhi ya Lowasa iko wapi? Maandamano ya Kupinga Udikteta yako wapi?

Maandamano ya TLS yaliyosisitizwa na Tundu Lissu Juzi yako wapi? Maandamano ya Kuziba Midomo bungeni yako wapi? UKAWA yenyewe iliishia wapi kama kila Chama kilisimamisha mgombea uchaguzi wa mwaka 2015, " Ukistaajabu ya Mbowe utashangaa ya Lissu
Wekeni pembeni Vyombo vya dola, Wakuu wa Miko/Wilaya kisha mpande kwenye majukwaa tupambane.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akitangulia mbowe mbele na mgombewa wa 2020 mimi nitakua nyuma yao

Sent using Jamii Forums mobile app
Watoto wa lowasa, sumaye, mbowe, lisu na godless lema, sugu na vigogo wengine wa chadema watakuwemo kwenye hayo maandamano? Au ni vijana watoto wa walalahoi tu? Kuwa maandamano yakifanyika wenyewe watakuwa na hawara zao Beach wakila maraha?
 
mtikila alisema chadema ni magabacholi wanaotetea mafisadi na ni manyani sema hawana manyoya
 
maandamano ya kiwogawoga!! Endeleeni kujipanga weee mwishoni mtaambiwa hakuna kuandamana! na hapo mikia yoote chuki.
tusisumbuane kujiandaa na maandamano yasiyo na kichwa,kweli shida na hasira ni nyingi lkn tuandamane kwakujipanga na kumaanisha
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA kimesisitiza kwamba maandamano ya amani ambayo yalipangwa kufanyika kesho nchi nzima yatafanyika.

Akizungumza na MwanaHalisi Online, Edward Simbeye, katibu mwenezi wa Baraza la Vijana la chama hicho (BAVICHA), amesisitiza kuwa maandalizi kwa ajili ya maandamano hayo yanaendelea vizuri na tayari chama hicho kilishaandika barua kulitaarifu jeshi la polisi kuhusiana na uwepo wa maandamano hayo katika kila mkoa nchini.

Aidha, kiongozi huyo amesema kuwa mpaka muda huu bado jeshi hilo halijajibu barua ambayo chama hicho kimeliandikia na kuongeza kuwa maandamano hayo yatafanyika hata kama jeshi hilo litakuwa halijajibu barua yao mpaka kufikia siku ya kesho.

“Maandalizi yanaendelea vizuri na hapo kesho tutatoa muongozo kwa wanachama wetu na wananchi kwa ujumla kuhusiana na mahali ambapo maandamano hayo yataanzia na kuishia katika kila mkoa nchini.” amesema Simbeye

Akifafanua kuhusiana na tabia ya jeshi la polisi kuzuia kufanyika kwa maandamano kwa sababu mbalimbali, Simbeye amesema kuwa maandamano ni haki ya kikatiba na jeshi la polisi lina wajibu wa kulinda wananchi ambao wanatumia haki yao ya kikatiba kufanya maandamano na si kuzuia maandamano na kuongeza kuwa maandamano hayo yatafanyika hata kama jeshi hilo litazuia maandamano hayo.

Wiki iliyopita, baraza hilo la vijana lilitangaza kuwepo kwa maandamano ya amani siku ya kesho ambayo waliyapa jina la “Black Thursday” yenye lengo la kushinikiza kuwepo kwa haki za kisiasa, kiuchumi, utawala wa sheria pamoja na haki za binadamu nchini.
Mngetoa ratiba leo, otherwise mnabip tu naona.
 
Hakuna mtu mwenye kufikiri kwa kutumia kichwa anaweza kuwaamini hao chadema.Wanaona bomoa bomoa inachukua habari zao,wameamua wakapigwe virungu kinguvu
 
chama kiko ICU ha ha eti maandamano, mngekua mnaandamana kuhusu pesa,kuiamrisha serikali kusambaza maji ya bomba nchi nzima, madawa hospitalini hapo ngewaunga moyo
 
mhh anayetaka kuvunja miguu athubutu kutoka! awamu hii [HASHTAG]#vyumavimekaza[/HASHTAG]
 
maandamano yanaanza saa ngapi ndugu zanguni tuanze kuchungulia kwenye madirisha yetu.......
 
Back
Top Bottom