CHADEMA yasisitiza kufanya maandamano kesho ya amani

CHADEMA yasisitiza kufanya maandamano kesho ya amani

hakikisha mama zenu na wake zenu plus nyinyi mnaongoza hayo maandamano ili ilete maana kiitifaki
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA kimesisitiza kwamba maandamano ya amani ambayo yalipangwa kufanyika kesho nchi nzima yatafanyika.

Akizungumza na MwanaHalisi Online, Edward Simbeye, katibu mwenezi wa Baraza la Vijana la chama hicho (BAVICHA), amesisitiza kuwa maandalizi kwa ajili ya maandamano hayo yanaendelea vizuri na tayari chama hicho kilishaandika barua kulitaarifu jeshi la polisi kuhusiana na uwepo wa maandamano hayo katika kila mkoa nchini.

Aidha, kiongozi huyo amesema kuwa mpaka muda huu bado jeshi hilo halijajibu barua ambayo chama hicho kimeliandikia na kuongeza kuwa maandamano hayo yatafanyika hata kama jeshi hilo litakuwa halijajibu barua yao mpaka kufikia siku ya kesho.

“Maandalizi yanaendelea vizuri na hapo kesho tutatoa muongozo kwa wanachama wetu na wananchi kwa ujumla kuhusiana na mahali ambapo maandamano hayo yataanzia na kuishia katika kila mkoa nchini.” amesema Simbeye

Akifafanua kuhusiana na tabia ya jeshi la polisi kuzuia kufanyika kwa maandamano kwa sababu mbalimbali, Simbeye amesema kuwa maandamano ni haki ya kikatiba na jeshi la polisi lina wajibu wa kulinda wananchi ambao wanatumia haki yao ya kikatiba kufanya maandamano na si kuzuia maandamano na kuongeza kuwa maandamano hayo yatafanyika hata kama jeshi hilo litazuia maandamano hayo.

Wiki iliyopita, baraza hilo la vijana lilitangaza kuwepo kwa maandamano ya amani siku ya kesho ambayo waliyapa jina la “Black Thursday” yenye lengo la kushinikiza kuwepo kwa haki za kisiasa, kiuchumi, utawala wa sheria pamoja na haki za binadamu nchini.
Maigizo haya chadema 2020 hamtobaki salaama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi hawa jamaa hawana matatizo mengine? I mean hata tu kusaidia waototo wao home work?
Waandamane tu wasaidie kuwakumbusha watawala mambo muhimu ikiwemo suala la elimu ili wazazi wawe na uhakika kuwa watoto wao wanapata elimu bora na sio wenyewe ndio wageuke walimu!
 
Mnaandamana kwa lipi mnaloliitaji uchumi so ukafanye kazi uupate unafikili ukivunjwa hiyo milonjo yako utapata msaada#we kama unataka kuishi bila bugdha pambana na hali yako usipambane na serikali upo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Police hawajajibu kwa kuwa bado wanasubiri maagizo ya IGP. IGP nae anasubiri Waziri mwenye dhamana aseme kabla hajawaagiza watu wake. Waziri mwenye dhamana na yeye anasubiri msg aliyomtumia mwenye Nchi ijibiwe maana kwa hofu na woga alionao, anagwaya hata kupiga simu jumba jeupe kuomba mwongozo kwa kuhofia kuitwa mpumbavu. One man show ni tatizo kubwa.
haaaah! jesh la mtu mmoko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamani, hivi matatizo mengi tuliyonayo nchini kama ya ajira kwa vijana , umeme, maji na huduma za afya ila hao upinzani wameona maandamano ndiyo solutions!?

Waambieni waache utoto tunahitaji sera safi za maendeleo na Taifa lenye amani.
 
Haki zipi mnazotaka kudai au na nyie mnataka kuolewa kama ni haki ya kuishi mnayo, haki ya kuzungumza na kutoa maoni mnayo, haki ya kufanya kazi kukuza uchumi mnayo, haki ya kufanya kila kitu mnayo, haki ya kulala segerea mnayo. Je nyie mnataka kudai haki zipi? Tahadhari, kwa yeyote anayejua anao uwezo wa kufanya chochote akafanye lakini sio kuchochea maandamano au kama mnataka haki ya kuoana wanaume kwa wanaume hiyo haipo mnapoteza muda wenu tu kwanza karibuni sana mvua Nazi zinakaribia kunyesha mashamba ya magereza hayana mazao kwa sasa hivyo mkiandamana mtakaopatikana mtaenda kusaidiana na walipo kule kuipatia nchi chakula kingi. Usithubutu kuandamanaaaaaaaaa.........usidanganywe na mtu coz anayekudanganya uandamane yy hatoandamana kama una akili utajua nina maanisha nini
 
Tunataka vijana wenye ujasiri aina ya simbeye

Simbeye ni kijana ambaye huongea kwa kumaanisha

mchana toch ,usiku magogo tufanyaje?
 
Jamani hivi watu wengine bwana hivi mtu unaposema eti unaandamana kwa lengo la kudai haki ni haki zipi ambazo hauna? Kana ni haki ya kufanya kazi yoyote unayotaka unayo, haki ya kuzungumza na kutoa maoni unayo ili mradi usivuke mipaka, haki ya kuishi unayo, haki ya kuoa unayo, haki ya kushauri unayo, haki ya haki ya kwenda segerea unayo, haki ya kufa unayo, haki ya kuhoji unayo, haki ya kuhubili injili unayo, haki ya kulima unayo, haki ya kufanya Siasa kwa kipindi husika unayo, haki ya kupiga kura unayo. Je we unayetaka kuandamana unataka nn? au una maana yako nyingine? sasa kwa taarifa yako we sembeye hauungwi mkono ng'o saivi tumekuwa wajanja mnataka sie tuvunjwe miguu nyie mpate cha kuzungumza. Anzeni kwanza nyie sisi tufuata awamu nyingine, mnadhani sie hatujipendi mmechemshaaàa, hadanganywi mtu apa mpoh.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jirani yako akipata shida huwezi kujua, subiri siku yakikufika, ndio utaelewa.
 
Nyumba zimebomolewa licha ya zuio la kimahakama mtu atakaa anasaidia watoto homework wakati hata sare za shule zimepotelea kwenye bomoabomoa pamoja na madaftari,kwanini usiende kudai uwepo wa utawala wa sheria na kuwepo kwa heshima ya haki za binadamu?

Mkuu fikiri vyema.
Ndio waende kwenye maandamano ya bavicha? Ha ha ha.
 
Mungu ibariki Bavicha , Taasisi pekee ya vijana inayovuma kwenye eneo la maziwa makuu .
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA kimesisitiza kwamba maandamano ya amani ambayo yalipangwa kufanyika kesho nchi nzima yatafanyika.

Akizungumza na MwanaHalisi Online, Edward Simbeye, katibu mwenezi wa Baraza la Vijana la chama hicho (BAVICHA), amesisitiza kuwa maandalizi kwa ajili ya maandamano hayo yanaendelea vizuri na tayari chama hicho kilishaandika barua kulitaarifu jeshi la polisi kuhusiana na uwepo wa maandamano hayo katika kila mkoa nchini.

Aidha, kiongozi huyo amesema kuwa mpaka muda huu bado jeshi hilo halijajibu barua ambayo chama hicho kimeliandikia na kuongeza kuwa maandamano hayo yatafanyika hata kama jeshi hilo litakuwa halijajibu barua yao mpaka kufikia siku ya kesho.

“Maandalizi yanaendelea vizuri na hapo kesho tutatoa muongozo kwa wanachama wetu na wananchi kwa ujumla kuhusiana na mahali ambapo maandamano hayo yataanzia na kuishia katika kila mkoa nchini.” amesema Simbeye

Akifafanua kuhusiana na tabia ya jeshi la polisi kuzuia kufanyika kwa maandamano kwa sababu mbalimbali, Simbeye amesema kuwa maandamano ni haki ya kikatiba na jeshi la polisi lina wajibu wa kulinda wananchi ambao wanatumia haki yao ya kikatiba kufanya maandamano na si kuzuia maandamano na kuongeza kuwa maandamano hayo yatafanyika hata kama jeshi hilo litazuia maandamano hayo.

Wiki iliyopita, baraza hilo la vijana lilitangaza kuwepo kwa maandamano ya amani siku ya kesho ambayo waliyapa jina la “Black Thursday” yenye lengo la kushinikiza kuwepo kwa haki za kisiasa, kiuchumi, utawala wa sheria pamoja na haki za binadamu nchini.
OK.... ni CHADEMA.... au ni wing ya vijana BAVICHA au Binamu zao TLS???
 
Back
Top Bottom