utaifakwanza
JF-Expert Member
- Feb 1, 2013
- 14,193
- 2,815
Ofisi ya Chama cha demokrasia na maendeleo jimbo la kasulu mjini inashikiliwa na mwenye nyumba kwa miezi kadhaa hivi sasa baada ya chama hicho kushindwa kulipa kodi ya pango.
Akiongea kwa masikitiko makubwa mmiliki wa jengo hilo (jina limehifadhiwa) ameeleza kuwa hadi mwezi wa sita anaidai chadema tshs 600000 na kwamba kina lema walipofika kigoma na chopa hivi karibuni katika ziara yao waliahidi kulipa deni hilo lakini cha kushangaza hadi leo kimya na hakuna kinachoendelea.
Amesema kuwa anashikilia samani za chama hicho ikiwamo viti,meza,bendera na mihuri pamoja na kuitia kufuli hadi atakapolipwa fedha zake na endapo washindwa kulipa hadi mwisho wa mwezi huu atakiburuza chama hicho mahakamani.
hatua ya kushikilia samani imekuja baada ya kuzungushwa kwa muda mrefu na kwamba wale viongozi aliokuwa anawafahamu wamehamia A.C.T Tanzania hivyo ameona njia pekee ya yeye kupata haki yake ni kushikilia mali zao.
my take. Chama kipeleke ruzuku mikoani