CHADEMA yasambaza PikiPiki nchi nzima

CHADEMA yasambaza PikiPiki nchi nzima

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA Kamanda Freeman Mbowe ametangaza mkakati wa Uchaguzi mkuu wa 2015 na moja ya mkakati huo ni kumwaga pikipiki katika tarafa zote nchini kwa lengo la kuwafikia wananchi na kueneza elimu ya uraia.Pikipiki hizo zitakuwa na vipaza sauti maalumu ambazo zitawasaidia viongozi wa chama hicho kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

Mbowe aliyasema hayo mjini Hanang jana wakati akiwa anazungumza na viongozi wa chama na wadau wakuu wa CDM mjini hapa.

Mbowe alisema wameanza mkakati wa kuhakikisha chama kinawafikia wananchi kila mahali.Kiongozi huyo machachari amesema lengo kubwa ni kutaka kusikiliza matatizo ya wananchi na hata kule ambako kuna shida ya usafiri basi kwa pikipiki chama kitafika.

Mbowe alisema upatikanaji wa pikipiki hizo unatokana na Ruzuku ya chama pamoja na ufadhili kutoka kwa wanachama na marafiki wa chama chake walioko nje ya nchi.Huku mikakati yote hii ikiwa inasimamiwa na yeye mwenyewe chini ya uratibu wa Katibu mkuu wa chama hicho Dr Wilbroad Slaa.

Source:Mwananchi Jumatatu
 
Jambo jema kujipanua zaidi vijijini ambako bado wananchi hawajafikiwa na fikra mbadala.
 
CCM waliambiwa eti CDM inapendwa Arusha na vijana kwa sababu iligawa pikipiki. Alipokuja JK akagawa pikipiki 10 kwa umoja wa vijana wa Bodaboda ili kujibu mapigo na kuzima nguvu za CDM kwa vijana. Sina hakika kama alifanikiwa au utafiti huo wa akina Magesa Molongo ulikuwa na ukweli.

Kwa hili nalo utasikia wanaiga maana wao hawajambo kwa kucopy & kupaste.
 
Big up CDM the earlier the better! Madereva waende mafunzo sio kununua leseni maana watakufa kabla ya 2015. Vilevile wafundishwe jinsi ya kufanya service ili vyombo vidumu beyond 2015.
 
safi sana, ila nilitaka kujua operation sangara imeishia wapi? make tuliambiwa kipindi fulani ilisimamishwa kupisha ile tume ya wakina Nchimbi, na baada ya hapo ingeendelea lakini hadi leo kimya, vipi kulikoni?
 
Ni jambo zuri, ila ingefaa hizo Pikipiki zingepelekwa haswa vijijini watu wakafanye kazi huko mjini watu ni waelewa sasa hazina haja sana ni mtazamo tu!
 
Usimwage mtama (mkakati) kwenye kuku wengi CCM mmesikia hiyo jipangeni kununua pikipiki zaidi. Mmesikia mshindani wenu anafanya nini.
 
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA Kamanda Freeman Mbowe ametangaza mkakati wa Uchaguzi mkuu wa 2015 na moja ya mkakati huo ni kumwaga pikipiki katika tarafa zote nchini kwa lengo la kuwafikia wananchi na kueneza elimu ya uraia.Pikipiki hizo zitakuwa na vipaza sauti maalumu ambazo zitawasaidia viongozi wa chama hicho kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

Mbowe aliyasema hayo mjini Hanang jana wakati akiwa anazungumza na viongozi wa chama na wadau wakuu wa CDM mjini hapa.

Mbowe alisema wameanza mkakati wa kuhakikisha chama kinawafikia wananchi kila mahali.Kiongozi huyo machachari amesema lengo kubwa ni kutaka kusikiliza matatizo ya wananchi na hata kule ambako kuna shida ya usafiri basi kwa pikipiki chama kitafika.

Mbowe alisema upatikanaji wa pikipiki hizo unatokana na Ruzuku ya chama pamoja na ufadhili kutoka kwa wanachama na marafiki wa chama chake walioko nje ya nchi.Huku mikakati yote hii ikiwa inasimamiwa na yeye mwenyewe chini ya uratibu wa Katibu mkuu wa chama hicho Dr Wilbroad Slaa.

Source:Mwananchi Jumatatu

mkuu huo mkakati ndo tulikuwa tunausubiria kwa muda mrefu sana! Bila shaka cdm itawafikia vzr watanzania wengi zaidi! Akina nepi watasoma namba yaan!
 
Salute kwa hiyo mikakati; wadau tunapaswa tuisupport kwa kuprovide mafuta na matengenezo! Salute again CDM!
 
safi sana, ila nilitaka kujua operation sangara imeishia wapi? make tuliambiwa kipindi fulani ilisimamishwa kupisha ile tume ya wakina Nchimbi, na baada ya hapo ingeendelea lakini hadi leo kimya, vipi kulikoni?.....

OS au M4C?
 
Big up CDM the earlier the better! Madereva waende mafunzo sio kununua leseni maana watakufa kabla ya 2015. Vilevile wafundishwe jinsi ya kufanya service ili vyombo vidumu beyond 2015.....

Good idea!
 
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA Kamanda Freeman Mbowe ametangaza mkakati wa Uchaguzi mkuu wa 2015 na moja ya mkakati huo ni kumwaga pikipiki katika tarafa zote nchini kwa lengo la kuwafikia wananchi na kueneza elimu ya uraia.Pikipiki hizo zitakuwa na vipaza sauti maalumu ambazo zitawasaidia viongozi wa chama hicho kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

Mbowe aliyasema hayo mjini Hanang jana wakati akiwa anazungumza na viongozi wa chama na wadau wakuu wa CDM mjini hapa.

Mbowe alisema wameanza mkakati wa kuhakikisha chama kinawafikia wananchi kila mahali.Kiongozi huyo machachari amesema lengo kubwa ni kutaka kusikiliza matatizo ya wananchi na hata kule ambako kuna shida ya usafiri basi kwa pikipiki chama kitafika.

Mbowe alisema upatikanaji wa pikipiki hizo unatokana na Ruzuku ya chama pamoja na ufadhili kutoka kwa wanachama na marafiki wa chama chake walioko nje ya nchi.Huku mikakati yote hii ikiwa inasimamiwa na yeye mwenyewe chini ya uratibu wa Katibu mkuu wa chama hicho Dr Wilbroad Slaa.

Source:Mwananchi Jumatatu.......

Safi kamanda Mbowe, lakini usiseme, usimwage mchele kwenye kuku wengi, huwezi jua maadui watapanga nini, we nyamaza watu waone vitendo tu!
 
Ni jambo zuri, ila ingefaa hizo Pikipiki zingepelekwa haswa vijijini watu wakafanye kazi huko mjini watu ni waelewa sasa hazina haja sana ni mtazamo tu!......

Mkuu mkakati huu umelenga vijijini zaidi japokuwa lengo ni kila tarafa ipate pikipiki.

Viva CHADEMA.
 
safi sana, ila nilitaka kujua operation sangara imeishia wapi? make tuliambiwa kipindi fulani ilisimamishwa kupisha ile tume ya wakina Nchimbi, na baada ya hapo ingeendelea lakini hadi leo kimya, vipi kulikoni?....

Mkuu Chasha,

Usiwe na wasiwasi operation M4C itaendelea tena kwa nguvu kubwa.Ni mipango tu inawekwa sawa.
 
Nafurahi sana nikiona moja ya maoni ya wanachama yanafanyiwa kazi......

Mkuu Majanikv

Ndipo utakapoona uzuri wa JF.Maoni haya mazuri yalitolewa hapa JF na viongozi wakuu wanayafanyia kazi.
 
Back
Top Bottom