CHADEMA yasambaza PikiPiki nchi nzima

CHADEMA yasambaza PikiPiki nchi nzima

Nilijua wanatoa za mkopo tuwalipe kidogo kidogo, bt anyway hakijaharibika kitu sababu ni jitihada za kujihakikishia ushindi hyo 2015
 
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA Kamanda Freeman Mbowe ametangaza mkakati wa Uchaguzi mkuu wa 2015 na moja ya mkakati huo ni kumwaga pikipiki katika tarafa zote nchini kwa lengo la kuwafikia wananchi na kueneza elimu ya uraia.Pikipiki hizo zitakuwa na vipaza sauti maalumu ambazo zitawasaidia viongozi wa chama hicho kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

Mbowe aliyasema hayo mjini Hanang jana wakati akiwa anazungumza na viongozi wa chama na wadau wakuu wa CDM mjini hapa.

Mbowe alisema wameanza mkakati wa kuhakikisha chama kinawafikia wananchi kila mahali.Kiongozi huyo machachari amesema lengo kubwa ni kutaka kusikiliza matatizo ya wananchi na hata kule ambako kuna shida ya usafiri basi kwa pikipiki chama kitafika.

Mbowe alisema upatikanaji wa pikipiki hizo unatokana na Ruzuku ya chama pamoja na ufadhili kutoka kwa wanachama na marafiki wa chama chake walioko nje ya nchi.Huku mikakati yote hii ikiwa inasimamiwa na yeye mwenyewe chini ya uratibu wa Katibu mkuu wa chama hicho Dr Wilbroad Slaa.

Source:Mwananchi Jumatatu

Duuu nawaonea huruma CHADEMA, mmejitahidi weeee kuelimisha watu, mmejitahidi kufichua mafisadi, mmejitahidi kufuatilia walioiba fedha wakaficha nje; Kwa jitihada zote hizo mlitakiwa mtuongoze na wanaotuhumiwa wapigwe chini lakini mwisho wa siku wananchi wanawapa madiwani 5 kati ya 29. Huenda kuna kitu hamjawajulia hawa wapiga kura au mbaya wenu hamjamjulia. Ila msikate tamaa mungu yupo pamoja nanyi. Kuna siku ndoto yenu itatimia na mtafurahi nasi watanzania tunaopenda haki tutashangilia na kufurahi huku tukinwa wine zetu.
 
VIVA CHADEMA. Tunazisubiri na huku Iramba mashariki hasa maeneo ya Kirumi, Mkalama, Nkinto, Mwangeza, etc.
 
safi sana, ila nilitaka kujua operation sangara imeishia wapi? make tuliambiwa kipindi fulani ilisimamishwa kupisha ile tume ya wakina Nchimbi, na baada ya hapo ingeendelea lakini hadi leo kimya, vipi kulikoni?

sasa si imekua replaced na M4C??
 
Wazo jema!!!
Nashauri mgawanyo ulenge Jographia ya Maeneo husika. Kuna Tarafa nyingine ni kubwa sawa na Wilaya kiasi kwamba pikipiki moja nisawa na hakuna kwani itakuwa vigumu kuwafikia walengwa. Kata zingine Pia tuongoze nguvu hiyo katika MAENEO MKAKATI ambayo twaweza kumiliki majimbo yote yawe ni ngome za kuiteka nchi nzima.
Mfano; Jimbo/Kanda la Magharibi - Mwanza na Shinyanga.
Jimbo/Kanda la Nyanda za Juu Kusini - Mbeya.
Jimbo/Kanda la Kaskazini - Arusha na Kilimanjaro.
Jimbo/Kanda la Pwani/Mashariki - Dar es Salaam.
Jimbo/Kanda la Kati - Singida.
Jimbo/Kanda la Magharibi - Kigoma.
Jimbo/Kanda la Kusini - Mtwara.
Kwa Pemba na Ungija - Waungwana ongezeni.

Ngazi ya jimbo kuwe na Kurugenzi zenye kusimamia shughuli zote za chama ktk Chaguzi na Uenezaji wa Chama.

Nawasilisha!

Mkuu Molemo ugawaji wa pikipiki ni jambo moja matumizi yake ni jambo lingine.
 
Last edited by a moderator:

Mkuu Asante sana

Mara nyingi ushauri kama huu kupitia JF ndiyo inayowasaidia viongozi kujua ni nini kifanyike na kwa maslahi ya nani.

Nina imani ushauri wako umefika kunakohusika.
 
Mkuu Molemo ugawaji wa pikipiki ni jambo moja matumizi yake ni jambo lingine.

Mkuu wangu Ngongo

Umetoa tahadhari nzuri na muhimu ambayo naamini itafanyiwa kazi.
 
Last edited by a moderator:
Zile pick up za M4C nasikia zinabebea majani ya ng'ombe Moshi.
 
Hahahahahahahahahaaa!! MOLEMO!!!
DON'T be obsessed by politics of poor Countries like Tanzania! utaishia kujitia kiberiti!!
Ningesema maneno ya aina hiyo hiyo dhidi ya JK ungeshangilia au kutoa maneno matamu ya kuunga mkono!
Kwa taarifa yako Katibu mkuu wa CHADEMA ndo mtendaji mkuu wa chama!! hata ma-auditor wanamhoji yeye kuhusu matumizi si mbowe. Kubaliana nami kuwa Mbowe kapotoka kwa kauli yake hiyo hasa katika kipindi hichi ambacho chama chake ndo kinasimika mizizi!! You must learn to be flexible!! ccm wapo rigid ndo sababu wanayumba. sasa nanyi mkiwa rigid kama wao hakika tutashuhudia mnavyosambaratika!!

BY THE WAY: MBOWE ANGEPUNGUKIWA NINI KAMA ANGESEMA CHAMA KITASIMAMIA UZAMBAZAJI WA HIZO PIKIPIKI KWA KARIBU ZAIDI? BADALA YA KU-PERSONALIZE USIMAMIZI WA HIZO PIKIPIKI?. CHEO CHA MWENYEKITI NI TAASISI SI MTU BINAFSI. KITENDO CHA KUSEMA YEYE KAMA MBOWE ATASIMAMIA IS DEADLY WRONG!! HASA KWA CHAMA MAKINI KAMA CHADEMA!!

MTU anapojitangaza kuwa yu-professor, sisi tunauangalia huo u-prof. chadema ikisema ni chama makini nasi twaangalia huo umakini. kama vile ccm wanavyojigama ni chama cha wafanyakazi na wakulima ambapo tumeshawakataa kwa kuwa si chama cha hao watu tena bali ni chama cha wafanyabiashara!!

Mkuu wangu Papa D

Onyesha kidogo walau hekima yako kwenye mijadala ya msingi.Usipende sana kuonyesha upeo wako utakaosababisha kudharauliwa na mtoto wa chekechea.
 
tunaomba hizi mali za chama zifatiliwe na zitumiwe kwa malengo yalokusudiwa isije hujumiwa hii mitambo ...gud move
 
Vyovyote uonavyo mkuu wangu.

Mimi nilijua hizo pikipiki ni kwa ajili ya kuwasaidia wakina mama wajawazito na wagonjwa maeneo husika, kumbe kwa ajili ya viongozi wa chadema kufika huko na kuwapa watu elimu ya uraia,lengo likiwa ni kuikataa CCM na kuchagua Chadema 2015.Helicopter vipi haziwezi kufika huko.Kweli ndugu zangu mpo katika Strategic Dialema ya hali ya juu.Mzee Sabodo umri umekwenda sana yule,Shauri zenu.Tumieni rasilimali kidogo mlizonazo kwa kutatua kero za wananchi lazima watawachagua tu,lakini siyo kwa namna hii ya kuzunguka kama Kikwete(Vasco da Gama)
 
Hili jambo jema, lakini pia kwakuwa katika ngazi ya tarafa hatuna uongozi wa kikatiba, itabidi tuwe na makatibu waenezi ngazi ya tarafa watakao simamiwa na kaitubu mwenezi wa wilaya, pia sustainability ya vifaa hivyo iwe well planned ili kusiwe na uharibifu wa mapema! CCM wataiga tu kwasababu wana hela lakini hawana mawazo! Ndio maana wameshindwa kutumia kodi zetu kutuletea maendeleo!
 
Ni jambo zuri kupeleka pikipiki za kichina hatahivyo zoezi la kusambaza pikipiki liende sambamba na ufunguzi wa ofisi hasa maeneo ya Pwani na Kusini; Msije rudia makosa yaliyofanyika kata ya Mwawaza, Shinyanga mjini kumteua mgombea udiwani mtu ambaye ni kibaka hiyo yote ilitokana na siasa za zimamoto
 
Mimi nilijua hizo pikipiki ni kwa ajili ya kuwasaidia wakina mama wajawazito na wagonjwa maeneo husika, kumbe kwa ajili ya viongozi wa chadema kufika huko na kuwapa watu elimu ya uraia,lengo likiwa ni kuikataa CCM na kuchagua Chadema 2015.Helicopter vipi haziwezi kufika huko.Kweli ndugu zangu mpo katika Strategic Dialema ya hali ya juu.Mzee Sabodo umri umekwenda sana yule,Shauri zenu.Tumieni rasilimali kidogo mlizonazo kwa kutatua kero za wananchi lazima watawachagua tu,lakini siyo kwa namna hii ya kuzunguka kama Kikwete(Vasco da Gama)

Akili yako haina akili! Hayo unayoyasema ni ya maana sana, lakini elimu ni muhimu zaidi ili kujenga taifa la watu wanaoweza kuiwajibisha serikali ya CHADEMA au yoyote iliyoko madarakani, nyie CCM mnafurahia ujinga wa wananchi maana mnautumia kufanikisha malengo yenu ya kisiasa! Sasa unaenda kuwaambia wananchi ukweli! Hilo mnaliogopa sana magamba!
 
Back
Top Bottom