CHADEMA yasambaza PikiPiki nchi nzima

CHADEMA yasambaza PikiPiki nchi nzima

Mkuu Majanikv

Ndipo utakapoona uzuri wa JF.Maoni haya mazuri yalitolewa hapa JF na viongozi wakuu wanayafanyia kazi.

Sitachoka kutoa maoni kuna kitu naandaa kama tukifuata ushindi wetu 2015 mpaka january kitakua tayari sema nahitaji data fulani kutoka sehemu sijui nipata
 
Nimewahi kutabiri ushindi wa brazil kombe la dunia mwaka 2002 na kwamba wangeifunga ujeruman 2:0.pia nilitabiri kuwa jk akichaguliwa rais mwaka 2005 atakuja chukiwa na wananchi kuliko alivyokuwa anapendwa wakati huo.mimi nilimuunga mkono salmu ahmed salimu.na ninatabiri sasa:chadema watachukua nchi 2015.kumbukeni maneno haya.
 
Safi kamanda Mbowe, lakini usiseme, usimwage mchele kwenye kuku wengi, huwezi jua maadui watapanga nini, we nyamaza watu waone vitendo tu!

Mkuu Chuakachara

Jambo jema huwa halifichiki.Mikakati yote ya kimaendeleo ni lazima wanachama wajulishwe.Fahamu hii ni baada ya ushauri mzuri toka kwa wanachama wakiwemo walioko hapa JF.

Ni vigumu kununua pikipiki kwa siri na kwenda kuzigawa kwa siri tukihofia eti wazee wa Copy and Paste wataiga.Tutakuwa hatujatendea haki wanachama kwani ni lazima wajue ruzuku yao inafanya nini.
 
Chama makini kwa watu makini, tunashambulia kote kote angani na nchi kavu....Helicopter, magari na pikipiki...Well done
 
Mkuu Chuakachara

Jambo jema huwa halifichiki.Mikakati yote ya kimaendeleo ni lazima wanachama wajulishwe.Fahamu hii ni baada ya ushauri mzuri toka kwa wanachama wakiwemo walioko hapa JF.

Ni vigumu kununua pikipiki kwa siri na kwenda kuzigawa kwa siri tukihofia eti wazee wa Copy and Paste wataiga.Tutakuwa hatujatendea haki wanachama kwani ni lazima wajue ruzuku yao inafanya nini.......

Sisemi iwe siri kiasi hicho. Mashini zikisha fika nchini then hakuna atakaye leta obstacles. Si unajua CCM wanamiliki dola , watazua TRA, mara oh hili na lile mradi wakwamishe!
 
Sisemi iwe siri kiasi hicho. Mashini zikisha fika nchini then hakuna atakaye leta obstacles. Si unajua CCM wanamiliki dola , watazua TRA, mara oh hili na lile mradi wakwamishe!

Ok.Nimeipata hoja yako mkuu.
 
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA Kamanda Freeman Mbowe ametangaza mkakati wa Uchaguzi mkuu wa 2015 na moja ya mkakati huo ni kumwaga pikipiki katika tarafa zote nchini kwa lengo la kuwafikia wananchi na kueneza elimu ya uraia.Pikipiki hizo zitakuwa na vipaza sauti maalumu ambazo zitawasaidia viongozi wa chama hicho kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

Mbowe aliyasema hayo mjini Hanang jana wakati akiwa anazungumza na viongozi wa chama na wadau wakuu wa CDM mjini hapa.

Mbowe alisema wameanza mkakati wa kuhakikisha chama kinawafikia wananchi kila mahali.Kiongozi huyo machachari amesema lengo kubwa ni kutaka kusikiliza matatizo ya wananchi na hata kule ambako kuna shida ya usafiri basi kwa pikipiki chama kitafika.

Mbowe alisema upatikanaji wa pikipiki hizo unatokana na Ruzuku ya chama pamoja na ufadhili kutoka kwa wanachama na marafiki wa chama chake walioko nje ya nchi.Huku mikakati yote hii ikiwa inasimamiwa na yeye mwenyewe chini ya uratibu wa Katibu mkuu wa chama hicho Dr Wilbroad Slaa.

Source:Mwananchi Jumatatu

Ni mjini Katesh wilaya ya Hanang
 
inapokuja suala la ngawira mwenyekiti anataka kusimamia!! sasa katibu mkuu afanye nini? yaani kale ka-umangi hakakutoki tu Mbowe? siku ukiwa rais nadhani wizara ya fedha itakuwa chini yako!! hahahahahahaha!!
 
Hii nzuri sana, but do it quickly wengi vijijini bado uelewa hautoshi. Uchaguzi mdogo wa madiwani wiki chache zilizopita unadhihirisha hilo.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA Kamanda Freeman Mbowe ametangaza mkakati wa Uchaguzi mkuu wa 2015 na moja ya mkakati huo ni kumwaga pikipiki katika tarafa zote nchini kwa lengo la kuwafikia wananchi na kueneza elimu ya uraia.Pikipiki hizo zitakuwa na vipaza sauti maalumu ambazo zitawasaidia viongozi wa chama hicho kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

Mbowe aliyasema hayo mjini Hanang jana wakati akiwa anazungumza na viongozi wa chama na wadau wakuu wa CDM mjini hapa.

Mbowe alisema wameanza mkakati wa kuhakikisha chama kinawafikia wananchi kila mahali.Kiongozi huyo machachari amesema lengo kubwa ni kutaka kusikiliza matatizo ya wananchi na hata kule ambako kuna shida ya usafiri basi kwa pikipiki chama kitafika.

Mbowe alisema upatikanaji wa pikipiki hizo unatokana na Ruzuku ya chama pamoja na ufadhili kutoka kwa wanachama na marafiki wa chama chake walioko nje ya nchi.Huku mikakati yote hii ikiwa inasimamiwa na yeye mwenyewe chini ya uratibu wa Katibu mkuu wa chama hicho Dr Wilbroad Slaa.

Source:Mwananchi Jumatatu
 
inapokuja suala la ngawira mwenyekiti anataka kusimamia!! sasa katibu mkuu afanye nini? yaani kale ka-umangi hakakutoki tu Mbowe? siku ukiwa rais nadhani wizara ya fedha itakuwa chini yako!! hahahahahahaha!!

Mkuu wangu Papa D

Onyesha kidogo walau hekima yako kwenye mijadala ya msingi.Usipende sana kuonyesha upeo wako utakaosababisha kudharauliwa na mtoto wa chekechea.
 
Amechelewa jamvini, karamu imeshaliwa:
9.jpg

sipati picha
nikitazama juu kuna chopa,pembeni kuna hilux za m4c,pale pikipiki,kule makamanda wengine wako kwa mguu wanapiga door by door..
Ccm itapona kweli..???
 
HAMA YA MATOKEO YA KATA 29 IMEANZA HAWA JAMAA HAMUWAWENZI WANA PROPAGANDA ZA KISAYANSI WAKATI NYIE MNA PROPAGANDA ZA kinafki
 
Back
Top Bottom