MAFILILI
JF-Expert Member
- Apr 28, 2011
- 2,377
- 1,200
Katika kile kinachoashiria anguko la kisiasa mkoani DSM, CHADEMA kimejikuta kikipoteza wafuasi, wanachama na wafadhili ndani ya kata ya Mianzini ambako waliambulia kura chache katika uchaguzi mdogo wa udiwani, uliohitimishwa kwa mgombea wa CCM, Mheshimiwa Mbwana kuibuka kidedea. Pigo takatifu kwa CHADEMA limeambatana na kufungwa kwa tawi la chama lililokuwa eneo la KAKONKO bar Majimatitu; Wiki mbili zilizopita bango la utambulisho wa ofisi ya chama lilionyesha OFISI YA CHADEMA kata ya Mianzini, hivi leo limebadilika na kuwa OFISI YA CCM tawi la Maji Matitu, POLENI akina Mwita &CO; CCM yasonga mbele kwa kasi kubwa huku CHADEMA ikirudi nyuma kwa kasi ya ajabu