Hii ina ushahidi gani kama imetoka FFU, mbona limeandikwa kama tangazo la kuuza viwanja huko mbande na sio amri,tuache kupanda chuki tuweke ukweli hapa.Nimekaa JKT miaka miwili, sijawahi kuona hawa jamaa wakitumia neno tangazo, labda mtu binafsi anauza kitu chake ndiyo huweka tangazo
chadomo wanachezea kiwembe, kikiwakata wasilalamike.
Unaumizwa na constitutional rights??! Hao mashabiki wa Magufuli hawakukeri? Kushabikia magaeuzi ni ujinga na kutokwenda shule?Umekula maharage ya wapi wewe?Waache waendelee kuropoka dawa yao ipo jikoni... kwa style hii hata wafanyeje hawatakaa wainufaishe nchi ni wapuuzi sana hawa jamaa kila kukicha heshima yangu kwao inashuka kwasababu ya ujinga kama huu. Sijui lowassa kawapa nini walahi siwezi toa kura yangu kwa watu wanafanya wananchi ni wajinga kama chadema. Watawashika masikio hao hao wasiotaka shule wala kazi kutwa kuandamana kama manyumbu na uvivu wao kusubiri wanasiasa ambao ni wafanya biashara kuwaletea maendeleo.
"Mwnyekiti wa chama cha
CHADEMA Freeman Mbowe
amesema kuna vijana watatu
wametoka jeshini wataalamu
wa mambo ya Kompyuta
wamenda Tume ya Taifa
Uchaguzi kushughulika na
BVR na wakiwa pale
hawajitambulishi kama
wanajeshi".
Mbowe amesema ushahidi
upo na kama Mwamunyange
akibisha atamuekekeza kambi
wanaotoka, wameanza kazi
tarehe ngapi na majina yao
na wapo NEC kwa kazi ipi.
Amesema jaji Lubuva naye
ajitokeze asema vijana hao
wako ofisini kwake kwa
malengo yapi..
Mbowe aliyasema hayo
alipokuwa kwenye mkutano
wa kutambulisha mgombea
urais kwa tiketi ya CHADEMA
Edward Lowasa jana kwenye
uwanja wa furahisha
ulioudhuriwa na umati
mkubwa sana wa watu.
Chanzo: Tanzania Daima
Umeona wapi kitu kinachoitwa chadomo....kiwembe kazi yake kunyolea nywele zote uzijuazo na sio kukatia gogo.
Angalia na maneno yako hayo.
Nimesoma maelezo yote hapo ya huyo msemaji wa jeshi, hakuna mahali popote amejibu hoja ya msingi ya CHADEMA kuhusu mchezo mchafu unaoendelea katika kambi za majeshi kwa askari wote kuamriwa kupeleka taarifa za vitambulisho vyao vya kupiga kura.
Huyo msemaji ametoa vitisho vitupu badala ya kujibu hoja. Jeshi sio vitisho bali jeshi ni kanuni, sheria na Utaratibu. Ni ujinga na ushamba mkubwa kwa karne hii na dunia ya sasa kuwa na jeshi linaloamini kutishia watu badala ya kujenga urafiki na mahusiano mema na raia na taasisi.
Kwa namna IGP na huyu msemaji wa Jeshi la JWTZ walivyoshindwa kutoa majibu ya msingi katika hoja nzito zilizotolewa kwao, inaashiria kabisa wamepanic sana hususani baada ya hicho kichafu walichokuwa wanakificha sasa kimeanza kuwa hadharani.
walioko jeshini ndo wanalaumu mnawafosi kuchukua vitambulisho vyao...na ukwel mfano wanadai hata wenyewe wameichoka ccm...wanadai muwaachie uhuru...muwaachie wananchi uhuru pia wafanye yao
Viongozi wa juu tu lkn maprivate hawaungi mkono hujuma
Truth pains but must be told.
Ni kweli majeshi yetu pamoja na polisi walichukua vitambulisho vya kupigia kura vya mapolisi na wanajeshi wote na kwenda kuvinakili namba kwa sababu zinazojulikana.
Acheni demokrasia ichukue mkondo wake kihalali.
Iko wazi kuwa taasisi zote za ulinzi na usalama wameamriwa kupeleka number za vitambulisho vyao vya kupigia kura, huyu anaekanusha anashiriki tu ktk kufunga bao la mkono!
Tanzania ikiingia kwny machafuko ya kisiasa mi wazi CCM ndio watakuwa wamesababisha!
Bado tunataka majibu toka kwa CDF kama alivyouliza Mbowe, wale maafisa wa IT wamjeshi wameenda kufanya kazi gani ya siri Tume ya Uchaguzi? Hakuna mamlaka isiyohojiwa katika nchi inayoendeshwa kidemokrasia hivyo lazima tupate majibu na sio vitisho.
Mbowe kauliza kwa uthabiti mkubwa kabisa na uwazi. Kwa nini kuwe na siri kati ya Tume na Jeshi? Kwa nini vyombo vya dola vichukue namba za askari za shahada zao?