CHADEMA yaonywa na JWTZ 'Leave us alone" - Army

CHADEMA yaonywa na JWTZ 'Leave us alone" - Army

Nimesoma maelezo yote hapo ya huyo msemaji wa jeshi, hakuna mahali popote amejibu hoja ya msingi ya CHADEMA kuhusu mchezo mchafu unaoendelea katika kambi za majeshi kwa askari wote kuamriwa kupeleka taarifa za vitambulisho vyao vya kupiga kura.

Huyo msemaji ametoa vitisho vitupu badala ya kujibu hoja. Jeshi sio vitisho bali jeshi ni kanuni, sheria na Utaratibu. Ni ujinga na ushamba mkubwa kwa karne hii na dunia ya sasa kuwa na jeshi linaloamini kutishia watu badala ya kujenga urafiki na mahusiano mema na raia na taasisi.

Kwa namna IGP na huyu msemaji wa Jeshi la JWTZ walivyoshindwa kutoa majibu ya msingi katika hoja nzito zilizotolewa kwao, inaashiria kabisa wamepanic sana hususani baada ya hicho kichafu walichokuwa wanakificha sasa kimeanza kuwa hadharani.

ww ni mjinga sana. Jeshi likae kutoa hoja kwa mwanasiasa??
Tatz kila kila kitu mnajifanya mnajua sana. Sasa ukitaka kuona madhara ya kutofautiana kauli na jeshi ni hayo ya kuwa wapinzan kila mwaka
 
Tell your JWTZ to provide an answer to the allegations...!!

Allegation without proof is as good as nothing. . . . . .The response was just to send a message that "we hear what you say". . . . the proof has been asked for. . . .Pick the challenge and man up!!!

That simple. . . .
 
chadomo wanachezea kiwembe, kikiwakata wasilalamike.
pic.jpg


Kwa mbali nakumbuka kauli ya Mnadhimu Mkuu wa Jeshi Luteni Jenerali Abdulrahman Shimbo tarehe 2/10/2010 kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010. Tunakaribia Uchguzi Mwingine na kuna kila dalili ya historia kujirudia. Kwa sasa Shimbo ni balozi wetu China.
 
Ni kawaida kukanusha hata kama kuna ukweli tunatambua vyombo vyetu vya dola.
 
Ulielewa akiposema oviously Kura za wanajeshi zitaenda kwa kwa potential people ?

Sasa hapo potentiality ya mtu we unaipimaje. . . . . .Subjective term unataka kui -objectify???!!
Acha usingizi amka. . . . .Kaweka wazi kuwa kila mtu ana haki ya kuchagua mtu anayeona anafaa kama una unalolijua peleka ushahidi katoa nafasi hiyo. . .
 
Ni kawaida kukanusha hata kama kuna ukweli tunatambua vyombo vyetu vya dola.

Mahakama kubwa kabisa ni wananchi, ushahidi uanikwe tu baas wananchi siku hizi wameamka sana huhitaji tochi ili wakuletee sindano iliyodondoka, wataipata na giza hivyo hivyo. . . . . . .
 
kiujumla vyombo vyetu vya dola vimeathiriwa sana na mfumo wa chama kimoja. hili linaonekana kote toka polis, jw,na hata usalama wa taifa. kiukweli kama ukawa wakafanikiwa kuchukua madaraka kunatakiwa kufanyike transformation kubwa kwenye vyombo hivi ili viendana na mfumo wa vyama vingi wa taifa letu.
 
Nchi hii ni ya Watanzania wote jeshi ni kwa kodi zetu kama wameongea CDM wao wakanushe
 
ww ni mjinga sana. Jeshi likae kutoa hoja kwa mwanasiasa??
Tatz kila kila kitu mnajifanya mnajua sana. Sasa ukitaka kuona madhara ya kutofautiana kauli na jeshi ni hayo ya kuwa wapinzan kila mwaka

haa haa kwa hiyo kazi ya jeshi ni kuingiza vyama madarakani?
 
walioko jeshini ndo wanalaumu mnawafosi kuchukua vitambulisho vyao...na ukwel mfano wanadai hata wenyewe wameichoka ccm...wanadai muwaachie uhuru...muwaachie wanchi uhuru pia wafanye yao

Creame yote ya viongozi wa kisiasa wa Taifa hili ni wanajeshi akiwamo huyo Lowasa na Rais anaye maliza muda wake. Wapo miongoni mwao mabalozi (Shimbo, Adadi Rajabu) wakuu wa mikoa, wilaya na wabunge, sasa wamemchoka nani! ?
 
Tanzania ndio maana tunafail vitu vingi sana mbn jamaa hawajajibu hoja kabisa.
 
Waache waendelee kuropoka dawa yao ipo jikoni... kwa style hii hata wafanyeje hawatakaa wainufaishe nchi ni wapuuzi sana hawa jamaa kila kukicha heshima yangu kwao inashuka kwasababu ya ujinga kama huu. Sijui lowassa kawapa nini walahi siwezi toa kura yangu kwa watu wanafanya wananchi ni wajinga kama chadema. Watawashika masikio hao hao wasiotaka shule wala kazi kutwa kuandamana kama manyumbu na uvivu wao kusubiri wanasiasa ambao ni wafanya biashara kuwaletea maendeleo.




Huyu jamaa alipaswa kujibu habari za kukusanya kadi za wapiga kura wanajehsi.

Kazi ya jeshi ni ulinzi wa mipaka ya nchi. Ina taratibu zake na mara zote hatuingilii masuala ya usalama wa nchi .

Suala la uchaguzi wa viongozi wa nchi ni la kiraia wala si la kijeshi. Linapaswa kufanyika kwa taratibu na sheria zilizopo na wala halina matinki yoyote ya ujeshi.

Kama wanajeshi waliona hawawezi kufanya siasa, kuchagua viongozi wa nchi na Watanzanai wenzao, wangeweka miiko ya kazi ili watu wao wasijiandikishe na wakakae huko huko maporini wakisubiri vita.

Habari ya viongozi wao kuleta ubabe kwenye siasa hata wanapotuhumiwa kuvunja taratibu kwa kisingizio kwamba wao wana uwezo wa kuua watanzania wote, haiwajengi wao wala chama chao. Mtu mweye ufahamu na uelewa wa siasa, suala la kiraia alipaswa kutambua haki za kiraia za wanajenshi walionyang'anywa kadi, na mipaka ya jehsi katika masuala ya kiraia, na hivyo kuwapa uhuru wa kupiga kura kama raia wengine bila vitisho.

Msemaji wa jeshi alipaswa kutoa hoja aidha kukanusha tuhuma ama ku justify na si kutishia. Na ninasikitika kuona viongozi wa jeshi wanaonyesha kuiuinga mkono ccm ambayo ilikataliwa na wanajeshi wengi sana mwaka 2010. Hii tarayi inaashirika mgawanyiko ndani ya jeshi ambao kama busara haitatumika, likitokea la kutokea, jeshi linagawanyika mara moja na wenye akli wanaeewa nini ninasema.

Jeshi kama limeamua kuhusika na siasa za nchi, lisiingize ujeshi wake kwenye siasa. Lifuate taratibu na sheria za nchi a hivyo kuacha kukusanya kadi za wapiga kura kwa vitisho amri na kadhalika. Linapokiuka sheria za nchi, na kuhojiwa vitendo vyake hivyo, liache ubabe, badala yake, likanushe ama kutoa ufafanuzi na si vitisho. Huku kwenye kura siyo jehsini na hatuhitaji karinye karinye zao.

Vinginevyo, ninachokiona ni ule ule mwendelezo wa tabia za wanajeshi wanaofahamika kwa matumizi mengi ya nguvu, kuliko mbegu za juu.


Majibu haya yamenikumbusha amuri kwa kruter waazimane appetite, ili wote wapate chakula. . Ninakumbuka namna tu tunavyoweza kutoa " C" yaani mapumziko kwa kuruta anayesema ana uongonjwa unaoitwa " Chronic Chlorophyll of the Mitochondria ".

Au tunavyoweza kumpa mtu kibali cha special diet kwa kuwa ana "Vascular Bundles" kwenye mikono na tena akae mbali na wenzake maana huo ni ungojwa hatari sana wa kuambukiza.

Narudia tene kusema, nilitegemea afande ajibu hoja badala ya vitisho. Asisahau hao aliowachukulia kadi zao ndio wapiganaji na wana uhuru na utashi wako wa kumchagua kiongozi wanayemtaka. Jeshi halimiliki nafsi za hao wapiganaji.

Akumbuke pia sababu za jeshi kugawanyika na madhara yake ndipo aamue kusema na kufanay anchotaka. Asisahau wanajeshi wanandugu zao wengi abao huwa hawako "BARAKIS" ambao wanahitaji kuwalinda na kuwatetea.

Ni vema aktumia maarifa kuliko ubabe maana sasa athari zake, wenye akili wanaziona ziko dhahiri.
 
Msemaji anayajua maneno lakini maana yake hajui! hilo ni ONYO batili na la kijinga, hakuna chombo cha umma kilichoko nje nje ya wigo wa public probity, hakuna. Umma una haki ya kufuatilia mwenendo wao kama unakidhi maslahi ya umma. Sasa wamefumaniwa wanatoa vitisho badala ya kujibu hoja. Kama wamesingiziwa sana sana wanaweza kwenda mahakamani kushtaki kama chombo na raia mwengine YOYOTE!, hawana haki wala Uhuru wa "kupigana vita na Chadema"!?, kitendo kingine zaidi ya kwenda mahakamani ni uhalifu kama uhalifu huo wanaotuhumiwa kuufanya na hatua za kushughulikia wahalifu wankijeshi zipo kimataifa including ICC!



TPDF_refuste1-aug15-2015.jpg

Director of Information and Public Relations in the Tanzania People's Defence Forces (TPDF), Colonel Ngemela Lubinga (C) stresses a point during a press conference in Dsm yesterday.


Political parties have been warned never to provoke the army, nor interfere with its operations, saying that political parties should do their job without dragging the army into their affairs.

The warning comes only a few days after the local media reported that Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) accused the army of ordering its rank and file to collect their Biometric Voters Registration cards for the purpose of favouring one of the political parties.

Tanzania People’s Defence Forces (TPDF) yesterday strongly denounced the CHADEMA allegations, warning political parties to stop provoking it.

According to TPDF, the statement issued by CHADEMA’s Deputy Secretary General - Tanzania Mainland, John Mnyika; claiming that TPDF has confiscated the BVR cards from all its soldiers and staff, and was registering cards’ numbers with the aim of cheating in the coming general election was purely rubbish.

The Army’s Director of Public Information and Communications Col. Ngemela Lubinga told a press conference in Dar es Salaam that TPDF has transparent responsibilities; adding that soldiers have constitutional and civil rights like any other Tanzanian, hence, every army member deserves to vote for whoever she/he likes.

He, however, reminded the media that soldiers were neither allowed to be members nor followers of any political party; adding that TPDF works as professional state organ as it is known world-wide.

“Whoever goes against the set arrangement, the army will not hesitate to take ethical actions against him or her. Thus, TPDF was saddened with the statement by CHADEMA; but the army urges each side to perform its duties in accordance with the law and not to interfere with each other in any way,” said Col. Lubinga.

He said that TPDF asked whoever with evidence on the CHADEMA claims to come forward and present it; adding that political parties should also seek the truth before they issue provocative statements.

Unfounded and provocative statements, according to TPDF, were nothing but aimed at triggering the breach of the national peace especially in this preparations period toward general election, set to take place in October, this year.

TPDF wanted politicians to recognise its endeavours towards encouraging their members to register and make sure they fully participate in the coming general election.

He added that political parties and the army were both building the same house, which is promoting peace in the country, thus, there was no need to scramble for building materials.

Responding on what legal actions to be taken by the army against CHADEMA’s claims and others alike, Col. Lubinga said the matter was being discussed at the relevant ministry (Defence and National Service).

Again, politicians had recently complained of setting up polling stations in the army camps; claiming that the practice was denying people the freedom to vote; but also Col. Lubinga trashed those claims as well.

He said that people should not confuse the two; voters’ registration centres and voting stations; insisting that for many years now, voting within army camps has never happened.

The same claims (confiscating staff voting cards) were also directed to Tanzania Police Force by politicians whereby the Deputy Inspector General of Police (DIGP) Abdulrahman Kaniki denied the allegations but promised to seek the truth.



SOURCE: THE GUARDIAN


 
Kiwembe kingine hiki tumekivunja:
View attachment 276852

Hii ina ushahidi gani kama imetoka FFU, mbona limeandikwa kama tangazo la kuuza viwanja huko mbande na sio amri,tuache kupanda chuki tuweke ukweli hapa.Nimekaa JKT miaka miwili, sijawahi kuona hawa jamaa wakitumia neno tangazo, labda mtu binafsi anauza kitu chake ndiyo huweka tangazo
 
Waache waendelee kuropoka dawa yao ipo jikoni... kwa style hii hata wafanyeje hawatakaa wainufaishe nchi ni wapuuzi sana hawa jamaa kila kukicha heshima yangu kwao inashuka kwasababu ya ujinga kama huu. Sijui lowassa kawapa nini walahi siwezi toa kura yangu kwa watu wanafanya wananchi ni wajinga kama chadema. Watawashika masikio hao hao wasiotaka shule wala kazi kutwa kuandamana kama manyumbu na uvivu wao kusubiri wanasiasa ambao ni wafanya biashara kuwaletea maendeleo.
watu wanakazi zao za maana wewe,acha ujinga.kura yako moja haina madhara,peleka huko
 
Hii ina ushahidi gani kama imetoka FFU, mbona limeandikwa kama tangazo la kuuza viwanja huko mbande na sio amri,tuache kupanda chuki tuweke ukweli hapa.

Ulitarajia tangazo liwe na sifagan?

Hata magari na zana zao zinasura mbaya.

Au ulitaka iandikwe kwa risasi?
 
walioko jeshini ndo wanalaumu mnawafosi kuchukua vitambulisho vyao...na ukwel mfano wanadai hata wenyewe wameichoka ccm...wanadai muwaachie uhuru...muwaachie wananchi uhuru pia wafanye yao

Kweli etii??

Kwani wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wa nchi ni makada? Siamini hivyo!

Umenikumbusha yule mnadhimu mkuu wa JWTZ mwaka wa uchaguzi 2010 sijui anaitwa nani vile......(A. Shimbo)! Alivyostaafu kadakishwa ubalozi ughaibuni!
 
Majeshi wore yamelipwa madai yao yote tena cash kitu ambacho hakijawahi tokea hapa Tanzania. Kuna walakini uchaguzi huu, CCM inataka kuwadhulumu haki ya kupiga kura kwa Uhuru Watanzani. Ila tupo macho.
 
Back
Top Bottom