Mkuu Candid Scope,
Labda hapa kama unabisha for the sake of kubisha.
Residency hapo inaongelea kitu kimoja tu ambacho ni makazi, mambo mengine yote ni kujidanganya bure. Makazi yana maana nyingi kuanzia makazi ya muda mpaka makazi ya kudumu.
Kwa mtu wa Commonwealth inatakiwa awe na makazi yake UK wakati anapiga kura. Hawezi kuwa TZ na akatumiwa forms za kupiga kura za UK. Ni raia tu ndio hata akiwa nje ya nchi anaweza kutumiwa karatasi za kupiga kura au akaenda ubalozi.
Kama bado unataka kujua basi chukua email hii na waandikie wahusika kwa mfano kwenye mji wa Swindon, namba ya help line ni +441793 464601, email
elecreg@swindon.gov.uk waulize swali lolote unalotaka kuwauliza kuhusu sheria za uchaguzi UK.
In fact hapa UK huwa tunawashauri vijana wanaokuja toka TZ kujakusoma kwamba wajiandikishe mara moja kupiga kura kwani kama hujajiandikisha hata uwe na credit score nzuri kiasi gani unaweza usipate vitu kama credit card. Database wanayochunguza kwanza ni hiyo list ya wapiga kura.
Hata mtu aliyekuja kutembea tu UK kutoka nchi za Modola kama yuko hapa wakati wa kupiga kura, huwa anapiga kura, bora awe amejiandikisha kabla ya siku ya mwisho kujiandikisha.