CHADEMA yaleta AMANI MBEYA baada ya risasi na Mabomu kushindwa

Magamba wamejifunza nini gapo? Kwamba mabomu na bunduki si lolote si chochote mbele ya uonevu na ukandamizaji
 
Mbeya wanajambo kubwa la kufanya SASA.

Wakowapi wasomi wa Mbeya hata wanakubali watoto wao kuharibiwa msingi wa kiuchumi?(wengi wamesoma kwa wao ama wazazi wao kupika pombe, kuuza ndizi, kuuza sukari, kuuza bagia, kuuza mahindi, kuuza nguo, n.k)

Wako wapi watumi.shi wa Mbeya hata wanakubali ndugu zao kukandamizwa na kufanywa maskini? (watumishi wengi wa Mbeya ni wazawa wa Mkoa huo, wanajua fika wao na majirani zao wanavyopata shida kuitafuta shilingi. Wanajua fika walioshambuiwa Mbalizi, Mwanjelwa hadi Uyole ni watu wenye mtaji mdogo si kama wale wa Uhindini, along Sai, etc

Wako wapi waliokuwa viongozi toka Mbeya hata kukubali ndugu zao, vijana wao, binti zao na wajukuu zao kuishi kwa hofu hali wakijaa hasira,ghadhabu na chuki kwasababu ya uvivu wa kufikiri na kulewa madaraka kwa viongozi waliopo? (ukichanganya madhila ya kuungua masoko, mgogoro wa wafanyabiashara ndogo ndogo, na hili; namna yalivyoshughulikiwa hayawezi ondosha chuki ya wananchi dhidi ya Serikali upesi. Watakuwaje na furaha ilhali kila wanapotaka kufanyabiashara au kukuza mitaji wanapigwa kwenzi kurudi kwenye ufukara)

Wako wapi wazee wasiokubali kusikia vilio na kuyaona machozi ya watoto wao, vikipazwa majumbani na mitaani; kuziona damu za wana wao kutokana na majeraha ya risasi, virungu na mabuti ya Polisi; kuyaona macho yao yakishuhudia mfululizo wa udhalimu huu juu ya wana wao baada yao ambayo ni fahari yao? (Mahangaiko yao yote ktk ujana na utu uzima wao ni kuwa kizazi baada yao kinapata furaha zaidi yao, lakini leo ni huzuni na uchungu ambao hata wao hawakuuonja)

Wako wapi wanausalama wazawa wa Mbeya, wasiokubali bunduki, risasi na mabomu vitumike dhidi ya ndugu zao kwasababu ya uvivu wa kufikiri wa watu wachache wapenda sifa kwa Kkwete na CCM? Je wanaweza kusema inatosha na kuhakisha watu hao pamoja na Kandoro wanahamishwa Mbeya?

Wako wapi viongozi wa dini waliouona udhalimu huu dhidi ya viumbe wa Mwenyezi Mungu, na wao kusimama na kusema INATOSHA! INATOSHA! INATOSHA! UDHALIMU HUU KUENDELEA KUFANYWA NA WATAWALA WALEVI WA MADARAKA.
 
Huyu ni Mh Mbilinyi waliyemuita muhuni, muimba muziki tu, asiye na elimu, asiye na busara, hafai kuwa mbunge, na kadha wa kadha....

Leo anarudi kuwa sababu ya tumaini na faraja kwa watu wake kutokana na madhila asiyoyasababisha yeye ila wale wanaomchukia.

Simama Kandoro na wenzako na mjipime kama mwaweza lingana na huyo "muhuni" ktk mioyo ya wana-Mbeya. Kinyume cha hekima ni upumbavu, mwawezaji kusema ninyi mna hekima kwa kusababisha vurugu kubwa kwa zaidi ya masaa 30 bila suluhuhisho, lakini huyo "muimba muziki tu" akatatua kwa masaa machache.

Mh Mbilinyi, watu wa Mbeya wanakuheshimu sana. Ni mtoto wao, ni ndugu yao, ni kaka yao. Tembea ukijua upo mioyoni mwao. Wengine wamekuita SUGU, hawa wanakuita "Mwana wa Faraja" Songa mbele kuwahudumia, kuwatumikia na kuwaongoza watu wako. Always be in their hearts.
 
Mkuu,

Maelezo yameenda shule. Nimeamua kuya-EDIT na kuyaweka vizuri zaidi.

Ukweli ni kuwa, ukiona unafikiri hivi, basi haupo CCM. Sintashangaa mimi/wewe tukiingia huko, tutaanza kufikiri hivyohivyo.

Kwa wafuatiliaji wa michezo. Wakati ule timu ya Taifa ya Togo iliposhambuliwa wakielekea kwenye 'world cup' kapteni wao 'Adebayor' alisema namnukuu "MWAFRIKA HANA THAMANI AFRIKA".

Hivi kulikuwa na haja gani kusubiri fujo na uharibifu ufikie kiwango hicho?

Hivi hakuna watanzania wanaoweza ku-predict reaction ya wananchi kwenye maamuzi yahayohusu maisha yao!!?

Au ndo imebakia "tufanye tulichoamua na waki-react tunawapiga mpaka watulie".

KAZI IPO
 
Nilicho gundua viongozi wengi wakiafrika wanajifanya vipofu kwa kuacha kutatua tatizo na kutumia mabavu
hivi unawatimua machinga wasijitafutie riziki unataka waende wapi wakati huja waandalia eneo mbadala lakufanyia biashara
 
Nafikiri ndio hao walipelekwa apolo na ni imani yangu watarudishwa kwenye box
 
Back
Top Bottom