CHADEMA yalaani ubaguzi wa CCM Zanzibar

CHADEMA yalaani ubaguzi wa CCM Zanzibar

TAARIFA KWA UMMA
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesikitishwa
sana na ujumbe wenye maudhui ya ubaguzi
ulioandikwa kwenye moja ya Bango lililobebwa na
mmoja wa wananchi waliojitokeza katika
maadhimisho ya Sherehe za Miaka 52 ya
Mapinduzi ya Zanzibar.
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaomba radhi
kwa ujumbe huo, kinapinga na kinakemea kabisa
fikra, hisia na mitazamo yoyote yenye maudhui ya
kibaguzi.
Ujumbe huo sio tu kuwa una maudhui ya kibaguzi
bali pia unaenda kinyume kabisa na falsafa na
Shabaha ya waasisi wa Mapinduzi hayo Matukufu
ya mwaka 1964 na unapingana na misingi na
itikadi ya CCM inayohimiza Umoja na
Mshikamano wa Kitaifa.
Daniel Chongolo
Mkuu wa Mawasiliano na Umma CCM.
12/01/2016
CCM ni chama cha wabaguzi wanaokumbatia majipu...
 
Haya, mmepata TOPIC ya kuongea angalau! Hakikisheni mnaiwekea mafuta la sivyo kesho hamtakuwa na topic ya kupata airtime, ALAFU KUMBE MLIKUWA MNAFUATILIA, nilidhani mmezira! Kumbe mnajifungia chumbani na popcorns kisha hampitwi na jambo!
 
Ubaguzi wowote ule ni unyama...Wa rangi, wa ukabila, wa ukanda, wa udini n.k....Wote ni ubaguzi...

Nafarijika kuona CCM waamelitmbua kosa na kutoa haraka taarifa ya kukemeaa kauli hizo za kibaguzi....

CHADEMA walikaa kimya Lowassa alivyohubiri udini kule Tabora....
You are missing my point dude! Nimekuuliza Kikwete aliposema mara hii ni zamu ya mwanamke kuwa Speaker ina maana alibaguwa?

Unaposema mara hii ni zamu ya fulani, haina maana unabagua. Kubagua ni kusema musiwachague fulani.
 
Kuimba Radhi kunapunguza nini. Ukweli upo pale pale. Ni sawa na ile ya kufuta kauli bungeni ilhal umesema message Sent
Mkuu, ni kweli hujui thamani ya kuomba msamaha/radhi unapokosea hapa duniani au unatania tu? Warusi juzi juzi hapa ndege yao imedunguliwa na Uturuki wamepigana kufa na kupona Uturuki iwaombe radhi halafu we unasema kuomba radhi haibadilishi cho chote? Are you serious? Kwani CCM walikuwa na ulazima wa kufanya hivyo hasa ukizingatia kuwa hili ni bango tu la wanachama na siyo tamko wala falsafa ya chama? Tumeona mabango mangapi yenye jumbe za kutatanisha kutoka kwa wanachama wa kila chama lakini hayakutolewa matamko wala kuombewa msamaha? Hili la Zanzibar lina upekee upi?

Ujasiri wa kuomba msamaha hasa katika siasa siyo jambo la kawaida na linaonyesha "good will" na hata kukomaa kwetu kisiasa.
 
Haya, mmepata TOPIC ya kuongea angalau! Hakikisheni mnaiwekea mafuta la sivyo kesho hamtakuwa na topic ya kupata airtime, ALAFU KUMBE MLIKUWA MNAFUATILIA, nilidhani mmezira! Kumbe mnajifungia chumbani na popcorns kisha hampitwi na jambo!
Lini tulikosa agenda...
 
Hamkumkana yule mwanamke wa Zanzibar aliyesema nchi ya kimapinduzi haipewi kwa kura leo museme Bango ni lake. Lile Bango Lilikuwa linawakilisha chama chake ndo maana hakuzuiwa hakubughudhiwa na alivaa uniform za chama
Mkuu hata sielewi unajaribu kusema nini.

Ina maana mtu akipigwa picha akiwa amevaa nguo let us say za CHADEMA huku amebeba bango lenye ujumbe tata kwenye maandamano ndo tuchukulie moja kwa moja kuwa anawakilisha chama? Ina maana kabla ya maandamano vyama viwe vinakagua mabango yote yaliyobebwa na waandamanaji na kuyahakiki kama hayana jumbe tata?
 
You are missing my point dude! Nimekuuliza Kikwete aliposema mara hii ni zamu ya mwanamke kuwa Speaker ina maana alibaguwa?

Unaposema mara hii ni zamu ya fulani, haina maana unabagua. Kubagua ni kusema musiwachague fulani.
Ndio alibagua.....

Ukweli ni kwamba hauwezi kuona 'uzito' wa hilo unalolipinga kwa sababu tu unaongozwa na hisia.....

Kuituhumu CCM kwambaa inakumbatia ubaguzi kwa bango lililoandikwa na wanachama wasiojitambua ni kutoitendea haki CCM....Na kwa bahati nzuri CCM wamelikemea hilo...Hawajakaa kimya...Wangekaa kimya sawa
 
Mkuu hata sielewi unajaribu kusema nini.

Ina maana mtu akipigwa picha akiwa amevaa nguo let us say za CHADEMA huku amebeba bango lenye ujumbe tata kwenye maandamano ndo tuchukulie moja kwa moja kuwa anawakilisha chama? Ina maana kabla ya maandamano vyama viwe vinakagua mabango yote yaliyobebwa na waandamanaji na kuyahakiki kama hayana jumbe tata?
Kumbe alikuwa anamuwakilisha mama yake...
 
Kweli hili Jambo ccm wamekosea sana lakini mtu hujulikana tabiya yake mapema sana
 
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

CCM WAMEDHIHIRISHA FIKRA ZA KIKABURU

Katika hali isiyokuwa ya kawaida ambayo kwa namna yoyote haiwezi isingeachwa imee katika fikra za watu achilia mbali kuachiwa itembezwe hadharani, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia katika mojawapo ya mabango yaliyobebwa na wanachama wake kuiadhimisha Sikukuu ya Mapinduzi ya Zanzibar, imedhihirisha kuwa inakumbatia fikra hatari za kikaburu.

Kupitia bango hilo ambalo kwa namna lilivyotengenezwa na lilivyobebwa ni vigumu kuamini kuwa liliibuka ghafla kama vile kitambaa cha mfukoni, mwanachama wa CCM akiwa amesindikizwa na wenzake, waliopita mlangoni mwa Uwanja wa Amani bila kuzuiliwa, kukemewa wala kubugudhiwa, ujumbe hatari wa kibaguzi umeandikwa 'MACHOTARA HIZBU ZANZIBAR NI NCHI YA WAAFRIKA'. Hizi ni fikra za kikaburu. Ni ishara ya mbegu za kibaguzi zilizokomaa na sasa zinachipua.

Kwa wafuatiliaji wa masuala ya kisiasa nchini na kipekee katika muktadha huu, siasa za Zanzibar wataelewa kuwa kauli iliyotolewa katika bango hilo, si ya bahati mbaya. Ni matokeo ya siasa za chuki zinazopaliliwa, kusimamiwa, kuratibiwa na hata kunyamaziwa na uongozi wa juu kabisa wa CCM.

Tutatoa mfano. Moja ya maskani maarufu za masuala ya kisiasa Visiwani Zanzibar inayomilikiwa na CCM iitwayo Kisonge imekuwa na kawaida ya kuandika lugha hatari zinazoashiria ubaguzi ulio wazi kabisa ulio na maudhui sawa sawa na huu uliotolewa leo kwenye Sikukuu ya Mapinduzi.

Mojawapo ya kauli ambazo ziliandikwa katika ubao ulioko katika maskani hiyo hivi karibuni wakati wa joto la Uchaguzi Mkuu uliopita, iliandikwa hivi "Katiba ni ya Unguja na nyinyi Wapemba mwende mkatengeze yenu Pemba."

Lugha hiyo na nyingine za namna hiyo kama ilivyotokea leo, zimekuwa zikitolewa mbele ya viongozi wa CCM au wanaziona lakini kwa sababu wanazozijua wao, pengine zinawasaidia katika kufikia malengo ya siasa hatarishi zinazokiuka misingi yote ya demokrasia, zimekuwa zikifumbiwa macho na kuzidi kumea vichwani mwa wanachama wao na kuleta mpasuko wa ubaguzi wa itikadi za kisiasa, rangi, kanda, kabila na hata dini, si Zanzibar pekee bali nchi nzima.

Kilichotokea leo Zanzibar, ni mwendelezo usiokuwa wa bahati mbaya bali maelekezo ya kimkakati ya kueneza propaganda za chuki miongoni mwa Watanzania ambayo ndiyo imebakia kuwa silaha pekee ya kuibeba CCM ikiwa ni dalili ya wazi ya chama kilichofilisika sera, kuacha misingi yake, kuishiwa ushawishi wa hoja na kukosa uhalali wa kisiasa hivyo kujihalalisha kwa ubaguzi kama huo.

Ni mwendelezo wa kauli za viongozi wakuu wa chama hicho ambazo hutolewa hadharani kwenye majukwaa ya siasa, wakiwabagua wanachama, wapenzi, wafuasi wa vyama vingine kuwa ni wa dini fulani, kanda fulani au kabila fulani. Wakijua kabisa hakuna kikundi chochote cha kisiasa chenye sifa hizo kwa sababu ni kinyume cha sheria na misingi ya taifa letu.

Ni mwendelezo wa kauli iliyowahi kutolewa na viongozi wa chama hicho dhidi ya viongozi wenzao na wala viongozi wakuu wa CCM hawakuthubutu hata kukaripia, tena yakiwa maazimio rasmi ya kikao kwamba "Rais wa Tanzania hawezi kutoka Kaskazini".

Kauli hiyo iliyotolewa baada ya kikao ilikuwa kauli ya kikaburu sawa sawa kabisa na ile iliyotolewa leo huko Zanzibar.

Mwalimu Nyerere, Baba wa Taifa aliwahi kusema ukaburu si rangi, ni fikra.

CHADEMA tunalaani na kupinga kwa nguvu zote mipango, mikakati, tabia na chembechembe za ubaguzi wa aina yoyote, ukiwemo huu wa kisiasa ambao sasa unaanza kusakafiwa kwa ubaguzi wa rangi kwa sababu tunaamini wanaobeba agenda hii hawataishia hapo bali watazidi kutugawa Watanzania pia kwa ubaguzi wa ukanda, ukabila na udini kama ambavyo wamekuwa wakijaribu kuchochea.

CHADEMA kwa kusimamia misingi yake na kuzingatia kikamilifu misingi ya taifa letu hasa haki, uadilifu, utu, umoja na uzalendo, haiko tayari kuona taifa likifikishwa huko na kuhatarisha maisha ya jamii nzima ya Watanzania kwa sababu ya maslahi ya kikundi cha watu wachache.

Tunamkumbusha Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Ernest Mangu kuwa kauli za namna hii ambazo zimekuwa zikipaliliwa na viongozi wa CCM na wengine wakitumia nafasi za kiserikali kuchochea ubaguzi ambao ni hatari kwa amani ya nchi na usalama wa raia na mali zao, ni ushahidi wa wazi kwa ajili ya hatua za kisheria badala ya jeshi hilo kujikita katika kubambikia wanachama, wafuasi na wapenzi wa vyama vya upinzani, hususan UKAWA tuhuma na kesi zisizokuwa msingi wowote kwa maslahi tu ya kisiasa kuisaidia CCM.

Wakati tukimtaka Rais John Magufuli kutimiza kwa vitendo kauli yake ya kwamba Serikali yake haitawabagua watu kwa misingi ya kisiasa (huku Waziri Mkuu wake akitoa maagizo kinyume kabisa na kauli hiyo) tunakitaka CCM, kupitia kwa Mwenyekiti wake, Jakaya Kikwete kama hakiko nyuma ya agenda hizo za kibaguzi na fikra hizo za kikaburu, kichukue hatua za haraka mara moja kuwawajibisha viongozi wake waliosimamia na kuachia jambo lililotokea leo huko Zanzibar.


Imetolewa leo Jumanne, Januari 12, 2016 na;

Tumaini Makene

Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Habari
CHADEMA


Kweli nyani
aoni kundule,mmeacha ubaguzi mlioufanya kwenye ubunge wa viti maalum mnashabikia ilo bango aisee CHADEMA kweli ziizzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzz
 
Back
Top Bottom