CHADEMA yalaani ubaguzi wa CCM Zanzibar

CHADEMA yalaani ubaguzi wa CCM Zanzibar

ficha ujinga wako hapa tunajadili kuhusu ccm mnavyogawa taifa kwa udini na ukabila ukitaka tujadili kuhusu bomoa bomoa kaanzishe thread tutakujibu nyumbu wewe
Ofkoz ccm walchofanya sio kitu chema!
Lakini ubaguzi ni falsafa pana beyond hayo maandishi yaliyopo hapo!
Ubaguzi huwa ndani ya nafsi za watu, hutendwa na wengine huchochea kwa maneno, au kutoa support kwa mtendaji!
Kwa miaka hii 2 tumeuona uchochezi na ubaguzi ktk sura nyingi mno! Hata hapa JF watu wengi wametoa kauli nyingi zenye ishara hizo, labda kwa kuwa mabango yao yalikuwa ktk electronic form!
Lakini point yangu ni kuwa Mimi muungwana siungi mkono aina yeyote ya ubaguzi!
Nadhani tuitumie hii case ya Zanzibar kama turning point na kuacha kubaguana!
 
Ukiona hivyo ujue saa ya anguko kuu la utawala wa kidhalimu umewadia. CCM must go. It a disgrace kwa nchi yetu na hasa waasisi wa Tanganyika na Zanzibar
 
Ukweli tangu lini ukawa ubaguzi. Zanzibar sio nchi ya machotara ni nchi ya waafrika awa machotara wanachotaka ni kumwagwa damu watuchafulie jina kimataifa. Zanzibar aiwezi kuachwa mikononi mwa masalia ya Sultan.
Pole sana
 
Wazee wa kudandia matukio. Huwezi kuendesha chama kwa kutegemea matukio. Utafikiri ubaguzi, ukanda na ukabila hawauoni chamani mwao. Ni ngumu sana kutoa boriti kwanza eeh?

CHADEMA sasa inapigania nini? Nini falsafa yake jumuishi?

Waungwana hao wameshaomba radhi. Neext?!
 
Huwezi kuitenganisha CCM na dhambi ya ubaguzi!!!!! CCM ya kina Nyerere na CCM ya vijana waliotengenezwa na Kikwete ni tofauti kabisa!!!
Yaaah umemmaliza mkuu. Hawa ndio waasisi wa unaguzi,
 
Musishangae ubaguzi ni sera ya CCM. Unadhani ccm itaweza kusavaivu bila kukubagua wewe kwamba ni muislamu au mkiristo au mkatoliki au mchagga, ama mpemba. Na hii sasa ni mpya chotara! Duu
mbona walishavuka mipaka wakawa wanaua wapinzani hii Mimi haijanishangaza...
 
Aaagh! chadema kwenu tayari mmepata kiki!hivi huwa hamna mipango ya kimaendeleo zaidi.ya kukaa mkivizia vimambo vidogo na kuvikuuuuza! mnaboa bana! Hela za bosi wenu zilizokwenda nje hamjafuatilia!
 
Asante sana kwa bandiko lililokwenda shule Makene, sina cha kuongezea naunga mkono na kulaani vikali huu ubaguzi.
 
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

CCM WAMEDHIHIRISHA FIKRA ZA KIKABURU

Katika hali isiyokuwa ya kawaida ambayo kwa namna yoyote haiwezi isingeachwa imee katika fikra za watu achilia mbali kuachiwa itembezwe hadharani, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia katika mojawapo ya mabango yaliyobebwa na wanachama wake kuiadhimisha Sikukuu ya Mapinduzi ya Zanzibar, imedhihirisha kuwa inakumbatia fikra hatari za kikaburu.

Kupitia bango hilo ambalo kwa namna lilivyotengenezwa na lilivyobebwa ni vigumu kuamini kuwa liliibuka ghafla kama vile kitambaa cha mfukoni, mwanachama wa CCM akiwa amesindikizwa na wenzake, waliopita mlangoni mwa Uwanja wa Amani bila kuzuiliwa, kukemewa wala kubugudhiwa, ujumbe hatari wa kibaguzi umeandikwa 'MACHOTARA HIZBU ZANZIBAR NI NCHI YA WAAFRIKA'. Hizi ni fikra za kikaburu. Ni ishara ya mbegu za kibaguzi zilizokomaa na sasa zinachipua.

Kwa wafuatiliaji wa masuala ya kisiasa nchini na kipekee katika muktadha huu, siasa za Zanzibar wataelewa kuwa kauli iliyotolewa katika bango hilo, si ya bahati mbaya. Ni matokeo ya siasa za chuki zinazopaliliwa, kusimamiwa, kuratibiwa na hata kunyamaziwa na uongozi wa juu kabisa wa CCM.

Tutatoa mfano. Moja ya maskani maarufu za masuala ya kisiasa Visiwani Zanzibar inayomilikiwa na CCM iitwayo Kisonge imekuwa na kawaida ya kuandika lugha hatari zinazoashiria ubaguzi ulio wazi kabisa ulio na maudhui sawa sawa na huu uliotolewa leo kwenye Sikukuu ya Mapinduzi.

Mojawapo ya kauli ambazo ziliandikwa katika ubao ulioko katika maskani hiyo hivi karibuni wakati wa joto la Uchaguzi Mkuu uliopita, iliandikwa hivi "Katiba ni ya Unguja na nyinyi Wapemba mwende mkatengeze yenu Pemba."

Lugha hiyo na nyingine za namna hiyo kama ilivyotokea leo, zimekuwa zikitolewa mbele ya viongozi wa CCM au wanaziona lakini kwa sababu wanazozijua wao, pengine zinawasaidia katika kufikia malengo ya siasa hatarishi zinazokiuka misingi yote ya demokrasia, zimekuwa zikifumbiwa macho na kuzidi kumea vichwani mwa wanachama wao na kuleta mpasuko wa ubaguzi wa itikadi za kisiasa, rangi, kanda, kabila na hata dini, si Zanzibar pekee bali nchi nzima.

Kilichotokea leo Zanzibar, ni mwendelezo usiokuwa wa bahati mbaya bali maelekezo ya kimkakati ya kueneza propaganda za chuki miongoni mwa Watanzania ambayo ndiyo imebakia kuwa silaha pekee ya kuibeba CCM ikiwa ni dalili ya wazi ya chama kilichofilisika sera, kuacha misingi yake, kuishiwa ushawishi wa hoja na kukosa uhalali wa kisiasa hivyo kujihalalisha kwa ubaguzi kama huo.

Ni mwendelezo wa kauli za viongozi wakuu wa chama hicho ambazo hutolewa hadharani kwenye majukwaa ya siasa, wakiwabagua wanachama, wapenzi, wafuasi wa vyama vingine kuwa ni wa dini fulani, kanda fulani au kabila fulani. Wakijua kabisa hakuna kikundi chochote cha kisiasa chenye sifa hizo kwa sababu ni kinyume cha sheria na misingi ya taifa letu.

Ni mwendelezo wa kauli iliyowahi kutolewa na viongozi wa chama hicho dhidi ya viongozi wenzao na wala viongozi wakuu wa CCM hawakuthubutu hata kukaripia, tena yakiwa maazimio rasmi ya kikao kwamba "Rais wa Tanzania hawezi kutoka Kaskazini".

Kauli hiyo iliyotolewa baada ya kikao ilikuwa kauli ya kikaburu sawa sawa kabisa na ile iliyotolewa leo huko Zanzibar.

Mwalimu Nyerere, Baba wa Taifa aliwahi kusema ukaburu si rangi, ni fikra.

CHADEMA tunalaani na kupinga kwa nguvu zote mipango, mikakati, tabia na chembechembe za ubaguzi wa aina yoyote, ukiwemo huu wa kisiasa ambao sasa unaanza kusakafiwa kwa ubaguzi wa rangi kwa sababu tunaamini wanaobeba agenda hii hawataishia hapo bali watazidi kutugawa Watanzania pia kwa ubaguzi wa ukanda, ukabila na udini kama ambavyo wamekuwa wakijaribu kuchochea.

CHADEMA kwa kusimamia misingi yake na kuzingatia kikamilifu misingi ya taifa letu hasa haki, uadilifu, utu, umoja na uzalendo, haiko tayari kuona taifa likifikishwa huko na kuhatarisha maisha ya jamii nzima ya Watanzania kwa sababu ya maslahi ya kikundi cha watu wachache.

Tunamkumbusha Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Ernest Mangu kuwa kauli za namna hii ambazo zimekuwa zikipaliliwa na viongozi wa CCM na wengine wakitumia nafasi za kiserikali kuchochea ubaguzi ambao ni hatari kwa amani ya nchi na usalama wa raia na mali zao, ni ushahidi wa wazi kwa ajili ya hatua za kisheria badala ya jeshi hilo kujikita katika kubambikia wanachama, wafuasi na wapenzi wa vyama vya upinzani, hususan UKAWA tuhuma na kesi zisizokuwa msingi wowote kwa maslahi tu ya kisiasa kuisaidia CCM.

Wakati tukimtaka Rais John Magufuli kutimiza kwa vitendo kauli yake ya kwamba Serikali yake haitawabagua watu kwa misingi ya kisiasa (huku Waziri Mkuu wake akitoa maagizo kinyume kabisa na kauli hiyo) tunakitaka CCM, kupitia kwa Mwenyekiti wake, Jakaya Kikwete kama hakiko nyuma ya agenda hizo za kibaguzi na fikra hizo za kikaburu, kichukue hatua za haraka mara moja kuwawajibisha viongozi wake waliosimamia na kuachia jambo lililotokea leo huko Zanzibar.


Imetolewa leo Jumanne, Januari 12, 2016 na;

Tumaini Makene

Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Habari
CHADEMA
Kwa shukrani za kipekee tumelipokea hili tamko na tunaahidi kulisimamia na kulitetea kwa nguvu zetu zoote maana kwa uzoefu tunajua wataingia wapotoshaji kutaka kulipotosha hili tamko kwa manufaa ya ccm
 
Watetea ukaburu. Wakiishawamaliza machotara watahamia makabila, unadhani uko salama?
Nimehoji ukimya wa CHADEMA ktk sakata la Bomoa Bomoa na ukisoma comment yangu nimesikitishwa pia na tabia ya ccm!
Shida yenu mnapenda kwendda nje pale mnapoulizwa maswali!
Hoja yangu ni simple hii issue ina just 48 hours mmeresond haraka, ile ya Bomoa inazaidi ya 3 weeks hamkuzungumza!
Cuf waligombana na chadema kwa kauli za kiongozi wenu ambazo znz zilitafsiriwakama kauli za kibaguzi!
Fungua Uzi wa manji na ujenzi wa coco beach, kuna comments zaidi ya 10 za kubagua wahindi!
Soma thread ya Dangote, Leopard tour, kamata kamata za wahamiaji, huko kote kuna kauli za kibaguzi!
Ubaguzi ni fikra za mtu zaidi, kuliko maandiko!
Ccm kama taasisi wanapaswa kulitolea maelezo, lkn bado haizuii Mimi kuuliza kwanini chadema walikaa kimya kwa lile tatizo jingine pia!
 
huu ubaguzi umewafurahisha ccm ndo maana waliupokea huu ujumbe wakifurahi udini na ukabila utaipeleka ccm kuzimu
hakuna umaskini mkubwa kama umaskini wa akili wewe tunakupuuzia wewe ni maskini wa akili unasapoti upuuzi

Wengi wanasupport ule ujinga hawajui ni watanzania wangapi wameathirika kisaikolojia. Naona wanasupport tu hawajui hata madhara yake.

Simshangai Samoa Suluhu yeye alishajisemea kwamba Upinzani usiende Ikulu hautasikilizwa kwa maana hiyo Samia Suluhu yupo kwa ajili ya wanachama wa CCM tu.Na tutakaotibiwa Muhimbili kama ni mpinzani basi ni fadhila tu na kama Chotara umepata favour tu.
 
Ukweli tangu lini ukawa ubaguzi. Zanzibar sio nchi ya machotara ni nchi ya waafrika awa machotara wanachotaka ni kumwagwa damu watuchafulie jina kimataifa. Zanzibar aiwezi kuachwa mikononi mwa masalia ya Sultan.
Thinking capacity yako ni# 0
 
TAARIFA KWA UMMA
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesikitishwa
sana na ujumbe wenye maudhui ya ubaguzi
ulioandikwa kwenye moja ya Bango lililobebwa na
mmoja wa wananchi waliojitokeza katika
maadhimisho ya Sherehe za Miaka 52 ya
Mapinduzi ya Zanzibar.
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaomba radhi
kwa ujumbe huo, kinapinga na kinakemea kabisa
fikra, hisia na mitazamo yoyote yenye maudhui ya
kibaguzi.
Ujumbe huo sio tu kuwa una maudhui ya kibaguzi
bali pia unaenda kinyume kabisa na falsafa na
Shabaha ya waasisi wa Mapinduzi hayo Matukufu
ya mwaka 1964 na unapingana na misingi na
itikadi ya CCM inayohimiza Umoja na
Mshikamano wa Kitaifa.
Daniel Chongolo
Mkuu wa Mawasiliano na Umma CCM.
12/01/2016
 
Siungi mkono ubaguzi wa rangi hata kidogo ila CCM haina budi kuchunguza tukio hili kwa undani..huyo kijana anaweza kuwa mwanaccm au mwanachama wa chama chochote aliyetengenezwa ili kuichafua CCM..!
 
Back
Top Bottom