CHADEMA yalaani ubaguzi wa CCM Zanzibar

CHADEMA yalaani ubaguzi wa CCM Zanzibar

Miaka yote CDM huwekwa kwenye mazingira ya kujitetea dhidi ya tuhuma za ukanda, leo hii wamekuwa maadui wakubwa wa siasa hizi chafu za udini na ukabila!. Au labda CDM wanaanza kukua kisiasa, wasomi wengi tu wamewekewa zengwe na kuondoka CDM lakini huo haukuwa ubaguzi wala ukabila. Miaka 23 ya uhai wa CDM, angekuwa ni msichana tayari keshaolewa na kuzaa angekuwa mtoto wa kiume naye tayari keshakuwa mtu mzima, anaweza kukaa faragha akaongea na Baba yake mambo ya kikubwa na akaeleweka. Ama kweli siku hazigandi, hatimaye CDM kimeanza kuwa chama chenye uwezo wa kuupinga ukabila na ukanda.
 
Kwa ufupi CCM ni janga. Rais mstaafu Abeid Aman ni Chotara, Zakia Meghj ni chotara na makada wa CCM Zbar 50% ni machotara. Ukaburu wa CCM uliotangazwa na Nape, Liziwani , Kinana na ubaguzi wa ukabila na ukanda leo wamethibitisha kupitia hilo bango lililopigiwa makofi na ccm.
 
Jecha katika ubora wake!
 
Attachments

  • ImageUploadedByJamiiForums1452616384.559848.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1452616384.559848.jpg
    64.6 KB · Views: 40
Hakuna dhambi mbaya kama hii ya ubaguzi ilayohubiriwa na ccm! Hii Ni laana kwa taifa kama itaachwa iendelee
 
Huwezi kuitenganisha CCM na dhambi ya ubaguzi!!!!! CCM ya kina Nyerere na CCM ya vijana waliotengenezwa na Kikwete ni tofauti kabisa!!!
Nami naungana nao kukemea hili la Ubaguzi...

Ila ni vema pia wangekemea na ile kauli ya Lowassa kuomba kura za Walutheri kule Tabora na kusema kwamba Tanzania haijawahi kuongozwa na Rais Mlutheri....Kwamba mwaka 2015 ilikuwa ni zamu ya Walutheri....Huu pia ni Ubaguzi
 
Miaka yote CDM huwekwa kwenye mazingira ya kujitetea dhidi ya tuhuma za ukanda, leo hii wamekuwa maadui wakubwa wa siasa hizi chafu za udini na ukabila!. Au labda CDM wanaanza kukua kisiasa, wasomi wengi tu wamewekewa zengwe na kuondoka CDM lakini huo haukuwa ubaguzi wala ukabila. Miaka 23 ya uhai wa CDM, angekuwa ni msichana tayari keshaolewa na kuzaa angekuwa mtoto wa kiume naye tayari keshakuwa mtu mzima, anaweza kukaa faragha akaongea na Baba yake mambo ya kikubwa na akaeleweka. Ama kweli siku hazigandi, hatimaye CDM kimeanza kuwa chama chenye uwezo wa kuupinga ukabila na ukanda.
Hakika unashikiwa akili na Lumumba. Hauwezi kuthibitisha hayo unayoyasema kuhusu Chadema maana hizo propaganda ni za kipuuzi zinazotumiwa na wachovuvwa akili wa ccm.

Hii leo cham cha ubaguzi kinajulukana kuwa ni ccm
 
Miaka yote CDM huwekwa kwenye mazingira ya kujitetea dhidi ya tuhuma za ukanda, leo hii wamekuwa maadui wakubwa wa siasa hizi chafu za udini na ukabila!. Au labda CDM wanaanza kukua kisiasa, wasomi wengi tu wamewekewa zengwe na kuondoka CDM lakini huo haukuwa ubaguzi wala ukabila. Miaka 23 ya uhai wa CDM, angekuwa ni msichana tayari keshaolewa na kuzaa angekuwa mtoto wa kiume naye tayari keshakuwa mtu mzima, anaweza kukaa faragha akaongea na Baba yake mambo ya kikubwa na akaeleweka. Ama kweli siku hazigandi, hatimaye CDM kimeanza kuwa chama chenye uwezo wa kuupinga ukabila na ukanda.

Huo ukanda na ukabila umekuwa ukihubiriwa na ccm, sasa bango limewavua nguo! Pole Sana kama ulisombwa na hizo propaganda! Leo wabaguzi wameonekana wazi!
 
Dunia iweke vikwazo kwa CCM
Duh....

Iweke vikwazo kwa CCM kwa kauli ya wanachama/wafuasi ambao si wasemaji wa Chama.....Na bahati nzuri CCM Makao makuu wamelikemea hili na kuliaani...

Mbona hamkukemea ile kauli ya Lowassa kuomba kura za Walutheri kule Tabora na kusema kwamba Tanzania haijawahi kuongozwa na Rais Mlutheri....Kwamba mwaka 2015 ilikuwa ni zamu ya Walutheri....Huu pia ni Ubaguzi...Double standards
 
Na sasa hivi chadema wana kazi ngumu ya kusubiria matukio ili watoe matamko..andiko reeefu
 
Nami naungana nao kukemea hili la Ubaguzi...

Ila ni vema pia wangekemea na ile kauli ya Lowassa kuomba kura za Walutheri kule Tabora na kusema kwamba Tanzania haijawahi kuongozwa na Rais Mlutheri....Kwamba mwaka 2015 ilikuwa ni zamu ya Walutheri....Huu pia ni Ubaguzi
Ina maana Kikwete alipokuwa bungeni mwaka 2010 na kusema safari hii ni mwaka wa mwanamke kuwa Speaker alikuwa ni mbaguzi wa jinsia? Hata Wamarekani walikuwa wanasema safari hii ni zamu ya raisi mweusi.

Mkuu, unajuwa kuna tofauti baina ya kusema fulani si Watanzania ama si wafuasi wa chama fulani au hawawezi kuwa na cheo fulani na ukisema safari hii ni zamu ya kabila fulani ama jinsia fulani. Hii haimfanyi aliyesema kumbaguwa mwengine ila anatumia fursa ile kujaribu kueleza fairness ama kuwakumbusha audience kwamba hawa watu wa kabila ama jinsia fulani musiwasahau pia na wao wanayo haki ya kuongoza
 
Hakuna dhambi mbaya kama hii ya ubaguzi ilayohubiriwa na ccm! Hii Ni laana kwa taifa kama itaachwa iendelee
Ile kauli ya kibaguzi si ya chama mkuu....Ni baadhi tu ya wana CCM wasio kuwa na akili ndio waliandika huo upuuzi....

Mbona Lowassa alivyohubiri udini kule Tabora haukukemea??

TAARIFA KWA UMMA
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesikitishwa sana na ujumbe wenye maudhui ya ubaguzi ulioandikwa kwenye moja ya Bango lililobebwa na mmoja wa wananchi waliojitokeza katika maadhimisho ya Sherehe za Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaomba radhi kwa ujumbe huo, kinapinga na kinakemea kabisa fikra, hisia na mitazamo yoyote yenye maudhui ya kibaguzi.

Ujumbe huo sio tu kuwa una maudhui ya kibaguzi bali pia unaenda kinyume kabisa na falsafa na Shabaha ya waasisi wa Mapinduzi hayo Matukufu ya mwaka 1964 na unapingana na misingi na itikadi ya CCM inayohimiza Umoja na Mshikamano wa Kitaifa.

Daniel Chongolo
Mkuu wa Mawasiliano na Umma CCM.
12/01/2016
 
Ina maana Kikwete alipokuwa bungeni mwaka 2010 na kusema safari hii ni mwaka wa mwanamke kuwa Speaker alikuwa ni mbaguzi wa jinsia? Hata Wamarekani walikuwa wanasema safari hii ni zamu ya raisi mweusi.

Mkuu, unajuwa kuna tofauti baina ya kusema fulani si Watanzania ama si wafuasi wa chama fulani au hawawezi kuwa na cheo fulani na ukisema safari hii ni zamu ya kabila fulani ama jinsia fulani. Hii haimfanyi aliyesema kumbaguwa mwengine ila anatumia fursa ile kujaribu kueleza fairness ama kuwakumbusha audience kwamba hawa watu wa kabila ama jinsia fulani musiwasahau pia na wao wanayo haki ya kuongoza
TAARIFA KWA UMMA
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesikitishwa sana na ujumbe wenye maudhui ya ubaguzi ulioandikwa kwenye moja ya Bango lililobebwa na mmoja wa wananchi waliojitokeza katika maadhimisho ya Sherehe za Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaomba radhi kwa ujumbe huo, kinapinga na kinakemea kabisa fikra, hisia na mitazamo yoyote yenye maudhui ya kibaguzi.

Ujumbe huo sio tu kuwa una maudhui ya kibaguzi bali pia unaenda kinyume kabisa na falsafa na Shabaha ya waasisi wa Mapinduzi hayo Matukufu ya mwaka 1964 na unapingana na misingi na itikadi ya CCM inayohimiza Umoja na Mshikamano wa Kitaifa.
Daniel Chongolo

Mkuu wa Mawasiliano na Umma CCM.
12/01/2016
 
Wazee wa kudandia matukio. Huwezi kuendesha chama kwa kutegemea matukio. Utafikiri ubaguzi, ukanda na ukabila hawauoni chamani mwao. Ni ngumu sana kutoa boriti kwanza eeh?

CHADEMA sasa inapigania nini? Nini falsafa yake jumuishi?

Waungwana hao wameshaomba radhi. Neext?!

Kuimba Radhi kunapunguza nini. Ukweli upo pale pale. Ni sawa na ile ya kufuta kauli bungeni ilhal umesema message Sent
 
Ina maana Kikwete alipokuwa bungeni mwaka 2010 na kusema safari hii ni mwaka wa mwanamke kuwa Speaker alikuwa ni mbaguzi wa jinsia? Hata Wamarekani walikuwa wanasema safari hii ni zamu ya raisi mweusi.

Mkuu, unajuwa kuna tofauti baina ya kusema fulani si Watanzania ama si wafuasi wa chama fulani au hawawezi kuwa na cheo fulani na ukisema safari hii ni zamu ya kabila fulani ama jinsia fulani. Hii haimfanyi aliyesema kumbaguwa mwengine ila anatumia fursa ile kujaribu kueleza fairness ama kuwakumbusha audience kwamba hawa watu wa kabila ama jinsia fulani musiwasahau pia na wao wanayo haki ya kuongoza
Ubaguzi wowote ule ni unyama...Wa rangi, wa ukabila, wa ukanda, wa udini n.k....Wote ni ubaguzi...

Nafarijika kuona CCM waamelitmbua kosa na kutoa haraka taarifa ya kukemeaa kauli hizo za kibaguzi....

CHADEMA walikaa kimya Lowassa alivyohubiri udini kule Tabora....
 
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

CCM WAMEDHIHIRISHA FIKRA ZA KIKABURU

Katika hali isiyokuwa ya kawaida ambayo kwa namna yoyote haiwezi isingeachwa imee katika fikra za watu achilia mbali kuachiwa itembezwe hadharani, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia katika mojawapo ya mabango yaliyobebwa na wanachama wake kuiadhimisha Sikukuu ya Mapinduzi ya Zanzibar, imedhihirisha kuwa inakumbatia fikra hatari za kikaburu.

Kupitia bango hilo ambalo kwa namna lilivyotengenezwa na lilivyobebwa ni vigumu kuamini kuwa liliibuka ghafla kama vile kitambaa cha mfukoni, mwanachama wa CCM akiwa amesindikizwa na wenzake, waliopita mlangoni mwa Uwanja wa Amani bila kuzuiliwa, kukemewa wala kubugudhiwa, ujumbe hatari wa kibaguzi umeandikwa 'MACHOTARA HIZBU ZANZIBAR NI NCHI YA WAAFRIKA'. Hizi ni fikra za kikaburu. Ni ishara ya mbegu za kibaguzi zilizokomaa na sasa zinachipua.

Kwa wafuatiliaji wa masuala ya kisiasa nchini na kipekee katika muktadha huu, siasa za Zanzibar wataelewa kuwa kauli iliyotolewa katika bango hilo, si ya bahati mbaya. Ni matokeo ya siasa za chuki zinazopaliliwa, kusimamiwa, kuratibiwa na hata kunyamaziwa na uongozi wa juu kabisa wa CCM.

Tutatoa mfano. Moja ya maskani maarufu za masuala ya kisiasa Visiwani Zanzibar inayomilikiwa na CCM iitwayo Kisonge imekuwa na kawaida ya kuandika lugha hatari zinazoashiria ubaguzi ulio wazi kabisa ulio na maudhui sawa sawa na huu uliotolewa leo kwenye Sikukuu ya Mapinduzi.

Mojawapo ya kauli ambazo ziliandikwa katika ubao ulioko katika maskani hiyo hivi karibuni wakati wa joto la Uchaguzi Mkuu uliopita, iliandikwa hivi "Katiba ni ya Unguja na nyinyi Wapemba mwende mkatengeze yenu Pemba."

Lugha hiyo na nyingine za namna hiyo kama ilivyotokea leo, zimekuwa zikitolewa mbele ya viongozi wa CCM au wanaziona lakini kwa sababu wanazozijua wao, pengine zinawasaidia katika kufikia malengo ya siasa hatarishi zinazokiuka misingi yote ya demokrasia, zimekuwa zikifumbiwa macho na kuzidi kumea vichwani mwa wanachama wao na kuleta mpasuko wa ubaguzi wa itikadi za kisiasa, rangi, kanda, kabila na hata dini, si Zanzibar pekee bali nchi nzima.

Kilichotokea leo Zanzibar, ni mwendelezo usiokuwa wa bahati mbaya bali maelekezo ya kimkakati ya kueneza propaganda za chuki miongoni mwa Watanzania ambayo ndiyo imebakia kuwa silaha pekee ya kuibeba CCM ikiwa ni dalili ya wazi ya chama kilichofilisika sera, kuacha misingi yake, kuishiwa ushawishi wa hoja na kukosa uhalali wa kisiasa hivyo kujihalalisha kwa ubaguzi kama huo.

Ni mwendelezo wa kauli za viongozi wakuu wa chama hicho ambazo hutolewa hadharani kwenye majukwaa ya siasa, wakiwabagua wanachama, wapenzi, wafuasi wa vyama vingine kuwa ni wa dini fulani, kanda fulani au kabila fulani. Wakijua kabisa hakuna kikundi chochote cha kisiasa chenye sifa hizo kwa sababu ni kinyume cha sheria na misingi ya taifa letu.

Ni mwendelezo wa kauli iliyowahi kutolewa na viongozi wa chama hicho dhidi ya viongozi wenzao na wala viongozi wakuu wa CCM hawakuthubutu hata kukaripia, tena yakiwa maazimio rasmi ya kikao kwamba "Rais wa Tanzania hawezi kutoka Kaskazini".

Kauli hiyo iliyotolewa baada ya kikao ilikuwa kauli ya kikaburu sawa sawa kabisa na ile iliyotolewa leo huko Zanzibar.

Mwalimu Nyerere, Baba wa Taifa aliwahi kusema ukaburu si rangi, ni fikra.

CHADEMA tunalaani na kupinga kwa nguvu zote mipango, mikakati, tabia na chembechembe za ubaguzi wa aina yoyote, ukiwemo huu wa kisiasa ambao sasa unaanza kusakafiwa kwa ubaguzi wa rangi kwa sababu tunaamini wanaobeba agenda hii hawataishia hapo bali watazidi kutugawa Watanzania pia kwa ubaguzi wa ukanda, ukabila na udini kama ambavyo wamekuwa wakijaribu kuchochea.

CHADEMA kwa kusimamia misingi yake na kuzingatia kikamilifu misingi ya taifa letu hasa haki, uadilifu, utu, umoja na uzalendo, haiko tayari kuona taifa likifikishwa huko na kuhatarisha maisha ya jamii nzima ya Watanzania kwa sababu ya maslahi ya kikundi cha watu wachache.

Tunamkumbusha Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Ernest Mangu kuwa kauli za namna hii ambazo zimekuwa zikipaliliwa na viongozi wa CCM na wengine wakitumia nafasi za kiserikali kuchochea ubaguzi ambao ni hatari kwa amani ya nchi na usalama wa raia na mali zao, ni ushahidi wa wazi kwa ajili ya hatua za kisheria badala ya jeshi hilo kujikita katika kubambikia wanachama, wafuasi na wapenzi wa vyama vya upinzani, hususan UKAWA tuhuma na kesi zisizokuwa msingi wowote kwa maslahi tu ya kisiasa kuisaidia CCM.

Wakati tukimtaka Rais John Magufuli kutimiza kwa vitendo kauli yake ya kwamba Serikali yake haitawabagua watu kwa misingi ya kisiasa (huku Waziri Mkuu wake akitoa maagizo kinyume kabisa na kauli hiyo) tunakitaka CCM, kupitia kwa Mwenyekiti wake, Jakaya Kikwete kama hakiko nyuma ya agenda hizo za kibaguzi na fikra hizo za kikaburu, kichukue hatua za haraka mara moja kuwawajibisha viongozi wake waliosimamia na kuachia jambo lililotokea leo huko Zanzibar.

Imetolewa leo Jumanne, Januari 12, 2016 na;

Tumaini Makene

Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Habari
CHADEMA

Kwa vyovyote vile, kazi ya wapinzani ni kupinga kila jambo la chama tawala. Hayo maneno yalitarajiwa.
 
Tangu lini nyani akaona kundule? Mtu kaandika bango lake wameshupaa utafikiri ndiyo falsafa ya chama duh. Kuishi kwa kudandia vitukio ni shida!

Hamkumkana yule mwanamke wa Zanzibar aliyesema nchi ya kimapinduzi haipewi kwa kura leo museme Bango ni lake. Lile Bango Lilikuwa linawakilisha chama chake ndo maana hakuzuiwa hakubughudhiwa na alivaa uniform za chama
 
wangesikitishwa pia na lowasa kuomba kura kidini / lutheran ,
kuna kuomba kura na kupata kura. Wapo waliomba kwa kuwabagua wakaazi wengine wasio wazawa wa mikoa yao tena kwa lugha mama zao. Leo hii ZNZ ina watu Wa rangi zote, wake, mama, baba wa viongozi ni asili ya kiarabu. Eg Salim.
 
Duh....

Iweke vikwazo kwa CCM kwa kauli ya wanachama/wafuasi ambao si wasemaji wa Chama.....Na bahati nzuri CCM Makao makuu wamelikemea hili na kuliaani...

Mbona hamkukemea ile kauli ya Lowassa kuomba kura za Walutheri kule Tabora na kusema kwamba Tanzania haijawahi kuongozwa na Rais Mlutheri....Kwamba mwaka 2015 ilikuwa ni zamu ya Walutheri....Huu pia ni Ubaguzi...Double standards

Ilishatolewa kauli Tanzania haiwezi pata Raisi toka Kaskazini. Hiyo vipi?
 
Back
Top Bottom