muongozaji
JF-Expert Member
- Oct 9, 2009
- 1,386
- 1,003
Okay....sawa. Ila vitendo ni muhimu zaidi kuliko maneno. Tunasubiria kuona. Kumbuka 2020 sio mbali
Niseme tu ukweli napenda sana siasa za upinzani hasa baada ya kuona madhaifu mengi yaliyojitokeza katika tawala za CCM. Kuna mambo wanayafanya mpaka mtu unapata hasira, wamekuwa wakijiona ni miungu watu huku wakifanya mambo very unfair kwa wananchi na wapinzani. Sijawahi kuwa na kadi ya chama chochote ila napenda siku moja upinzani uongoze nchi hii.
Wito wangu kwa viongozi na wanachama wa upinzani mjenge vyama vyenu na viwe na utaratibu wa kitaasisi na kuwe na succession ya madaraka. Mpendane na mheshimiane, acheni siasa za unafiki muwe wapinzani na washindani wa kweli mtafanikiwa. Tuache mihemko na vurugu zisizo na msingi, najua kuna wakati wenzenu wa upande wa pili wanawachokoza. Ni ha hayo tu, keep going!
HIZI KAMAT NI USANI MTUPU CHEYO KAWAMBIA CCM NI NGUMU KUINGOA MTAKA SANA NA KAMATI MWISHO KUNAWAHatishwi Ila mkia unamchapAaaa[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Duh! wengine wanachukua kadi za chama alichopo Magu sababu wanamkubali Prezidaa na commitments zake. Wazo lenu ni zuri, ila ni muhimu ku-strategize na kuja na mbinu mbadala, otherwise mtagawana hao wanachama na chama tawala
Safi sana kamanda .Tutaendelea kuleta taarifa moja kwa moja
Una roho ngumu sana ! Unawezaje kumwamini cheyo ?HIZI KAMAT NI USANI MTUPU CHEYO KAWAMBIA CCM NI NGUMU KUINGOA MTAKA SANA NA KAMATI MWISHO KUNAWA
Naamini ipo siku kiu yetu itapata kitulizo.Ushauri wako ni mzuri mkuu. Tatizo ni kwamba hautasikilizwa na wenye haki miliki za hivyo vyama. Sisi ambao hatuna chama lakini tuna mapenzi ya dhati ya kuuona upinzani ukiwa imara zaidi tunaposhauri kwa uwazi bila unafiki wowote tunaonekana wapinzani wa UKAWA au mamluki au wasaliti....wanataka watu wanaowasifia tu hata pale wanapokuwa wanakosea !!
Ukweli mtupu mkuu .Natumai katika hilo la kipaumbele cha kuongeza idadi ya wanachama, hili la katiba mpya ya rasimu ya Tume ya Warioba watalipa kipaumbele kikubwa. Kwa sababu bila katiba mpya ya rasimu ya Warioba Tume ya MACCM ya wizi wa kura na chaguzi itaendelea kufanya uovu wake kwa miaka chungu nzima ijayo.
NILIFIKIRI HAWAPO KUMBE UPO SHIKAMOO MWANA CMS HAIUna roho ngumu sana ! Unawezaje kumwamini cheyo ?
Kudai katiba mpya linakuwaje swala jipya?Natumai katika hilo la kipaumbele cha kuongeza idadi ya wanachama, hili la katiba mpya ya rasimu ya Tume ya Warioba watalipa kipaumbele kikubwa. Kwa sababu bila katiba mpya ya rasimu ya Warioba Tume ya MACCM ya wizi wa kura na chaguzi itaendelea kufanya uovu wake kwa miaka chungu nzima ijayo.
A.K .A wanaNDONDOWamchangani fc
Makubwa kumzidi nani, uliona wapi Ng'ombe akatikiswa na mkia wake
Ha ha ha bado unaishi kwa ahadi za katika makaratasi, au Matumaini
Hicho Chama kilishakufa walipokubali kupokea makapi ya CCM. Walimeza ndoano sasa kwishneyKamati kuu ya CHADEMA leo imeingia katika siku ya pili ya kikao chake na tayari maazimio kadhaa yamefikiwa.
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya kikao hicho zinasema wajumbe hao waliojifungia kwa siku mbili wameamua mambo kadhaa na huenda yakatoa mwelekeo mpya wa siasa za nchi hususan katika kipindi hiki ambacho inaonekana demokrasia kukandamizwa.
Pia moja ya maazimio ni namna ya kukijenga chama kitaasisi zaidi na kukijenga kwa umakini mkubwa kuanzia kwenye vitongoji ili kuhakikisha walau ifikapo mwaka 2019 kiwe na wanachama hai milioni 10.
Kwa siku zote mbili wanasiasa maarufu Tanzania na mawaziri wakuu wastaafu Edward Lowassa na Fredrick Sumaye wameendelea kushiriki kikamilifu katika kikao hicho muhimu.
Wanachama kadhaa wa Chadema waliohojiwa wanasubiri kwa hamu maazimio ya kikao hicho hasa baada ya mkutano mkuu wa CCM uliomalizika jana ambapo chama hicho kiliweweseka na kuonekana kila kiongozi wa CCM ana hofu kubwa na Edward Lowassa na Fredrick Sumaye.
Mawaziri wakuu hao wastaafu walichangia kwa kiasi kikubwa kuisambaratisha vibaya CCM katika jiji kuu la DSM na sasa chama hicho tawala ni wapinzani hapa jijini.
Tayari Fredrick Sumaye ametangaza kugombea uenyekiti Kanda ya Pwani ili kiisambaratisha CCM kwa kanda nzima.
Mmh hivi yale ni makapi au ng'ombe wasio na mikia? Au majina yanatofautiana kulingana na upande ulipo?Hicho Chama kilishakufa walipokubali kupokea makapi ya CCM. Walimeza ndoano sasa kwishney
Kwa sasa wamejirudisha wenyewe baada ya kuona hawana thamani kwa kuondoka CCM. Baada ya kutubu tumewapokea kama bwana wapotevu tena!! Ni furaha kwa mkosefu mmoja kutubu dhambi zake!!Mmh hivi yale ni makapi au ng'ombe wasio na mikia? Au majina yanatofautiana kulingana na upande ulipo?
Kwa nijuavyo kapi halina thamani tena japo laweza Tengeneza samadi nzuri kwa mazao, lakini linabaki kuwa kapi...! Iweje ulipokee na kulibatiza jina lingine?