CHADEMA yaitupa kapuni Rufaa ya Zitto

CHADEMA yaitupa kapuni Rufaa ya Zitto

Gamba la Nyoka mbona na wewe unaongea kama Zitto? how can swala la uanachama na vyeo be separate? they are inclusive and directly related, kama hatima yake itakua kuvuliwa uanachama, wakijadili rufaa na akashinda atakuwa na hivyo vyeo kwenye chama gani? yeye anajua na anaachofanya ama ni kupima upepo? ama ku confirm kwamba hatima yake katika chama iko kwenye kikaango, unaambiwa usitukane wakunga na uzazi ungalipo, sasa kafikishwa mahali pake, aende akajadili vyeo vya kutumiwa na CCM amakile chama chao cha Watu wa Kigoma wachache wenye akili kama wao
 
Nimeshasema zitto ww ni muha unatoka kigoma,hiki chama ni cha mtei wa kazkazini na mchaga yaani ukurupuke tu unataka uenyekiti ahh ndoto za mchana unaota kijana chadema ni chaga development manifesto sasa muha na mchaga wapi na wapi ni lazima tukufukuze hata ukisema hutoki utaona yaani sie tuwekeE tukikopeshe chama ww uptake uenyekiti tena ukome
 
Hatuna muda wa kusikiliza muhujumu chama kwa ss tunajenga chama chetu ili tuchukue dora 2015,chadema viva..
 
Suala la Uanachama na Uongozi vilikuwa ni separate issues. Kila kimoja kilipaswa kijadiliwe kwa muktadha wake!.
Mpaka hivi sasa Zitto Kabwe ni mwanachama halali wa Chadema
Anakata rufaa kwa sababu ya Kuvuliwa uongozi wake, Then Mwingine aakuja anasema No No No, Subiri kwanza tuone kama utavuliwa uanachama au La!!- SIJAWAHI KUONA CHAMA AMBACHO KILA MTU ANAJITAFSIRIA KATIBA APENDAVYO!
Sijui Kimesera ametumia kifungu gani cha sheria/katiba ya Chama kuzuia Mchakato huru wa Rufaa
Mkuu, ukisoma huu uzi hapa chini ambao mwandishi amejishughulisha kupindua pindua na kuisoma katiba, kanuni na itifaki za CHADEMA mpaka akapata angalizo, basi hautashangaa na maneno na matamko yanayotoka kwenye ofisi za CHADEMA hasa kuhusiana na hili sakata. Mwandishi wa Thread hizi amesema ofisi ya Makao makuu ya CHADEMA inaelezeka kwa neno moja la kiingereza ambalo ni DYSFUNCTIONAL.

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...anasiasa-wetu-watatu-mbowe-slaa-na-zitto.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...oro-wa-chadema-6-hitimsho-na-mapendekezo.html

Haya ndiyo matokeo na mwendelezo wa kuwa na ofisi yenye utendaji huo.
 
Ukiona hivyo ujue hakuna chama hapo kuna wajanja wajanja wengi waliounda chama chao kikaitwa chama cha siasa.:cool2:
 
Mkuu, ukisoma huu uzi hapa chini ambao mwandishi amejishughulisha kupindua pindua na kuisoma katiba, kanuni na itifaki za CHADEMA mpaka akapata angalizo, basi hautashangaa na maneno na matamko yanayotoka kwenye ofisi za CHADEMA hasa kuhusiana na hili sakata. Mwandishi wa Thread hizi amesema ofisi ya Makao makuu ya CHADEMA inaelezeka kwa neno moja la kiingereza ambalo ni DYSFUNCTIONAL.

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...anasiasa-wetu-watatu-mbowe-slaa-na-zitto.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...oro-wa-chadema-6-hitimsho-na-mapendekezo.html

Haya ndiyo matokeo na mwendelezo wa kuwa na ofisi yenye utendaji huo.
Ni ajabu unapomsifia mchambuzi wa katiba zaidi ya walioitunga na kuiandika.
 
Ni ajabu unapomsifia mchambuzi wa katiba zaidi ya walioitunga na kuiandika.
Majaji, mahakimu na wanasheria wanapozichambua sheria mahakamani na kuzitolea angalizo huwa wamekuwa wamezitunga?.

Kwa hiyo unataka kuniambia wabunge wanazijua zaidi sheria za nchi zaidi ya majaji/mahakimu na wanasheria kwa sababu wabunge ndiyo watungaji.

Sijui hoja yako ni ipi hapa?.
 
Hizi ni siasa huwezi kulinganisha na mambo ya kimahakama,

Kamati kuu na Mwanakijiji (spinning master) nani mwenye uelewa wa katiba ya Chadema.
 
Hizi ni siasa huwezi kulinganisha na mambo ya kimahakama,

Kamati kuu na Mwanakijiji (spinning master) nani mwenye uelewa wa katiba ya Chadema.
Ooh, nilikuwa sifahamu kama Katiba ya CHADEMA imetungwa na kuandikwa na Kamati Kuu ya CHADEMA hasa ikichukuliwa mantiki ya bandiko lako #87 .

Samahani. Siwezi kuendelea kujadiliana na wewe katika mkitadha huu kutokana na uwezo na pia mlinganyo wa chambuzi.

Nimegundua hata hufahamu unachojaribu kukijengea hoja.

I'm out of here!. Thanks.
 
Wewe ni wale wale tu spinning masters,

nani kasema katiba imetungwa na CC nilichosema kati ya CC na Mwanakijiji nani anaielewa katiba ya Chadema?

Kamati kuu wanai-practice katiba wakati Mwanakijiji yuko marekani anaisoma tu kwenye mitandao.

Kama hutaki kujadiliana changanya makalio kwanza nani anakuhitaji.
 
Kwa mujibu wa katiba ya CDM ,ZITTO anyo haki ya kukata rufaa kwa maamuzi ya kamti kuu,hayo mengine ni baadae
 
Wewe ni wale wale tu spinning masters,

nani kasema katiba imetungwa na CC nilichosema kati ya CC na Mwanakijiji nani anaielewa katiba ya Chadema?

Kamati kuu wanai-practice katiba wakati Mwanakijiji yuko marekani anaisoma tu kwenye mitandao.

Kama hutaki kujadiliana changanya makalio kwanza nani anakuhitaji.

hakika kamanda unamatatizo.......kwa akili yako ya kawaida unaamini kabisa ndani ya cc wajumbe wooote wanaimasta vizuri katiba ya chama?! kwamba haiwezekani mwenykt akainfluence baadhi ya maamuzi so long yeye ndio kiongozi mkuu pamoja na uwepo wa katiba hiyo?
By the way mwanakjj ni kweli yuko mbali (marekani) hivyo unamaanisha ili uielewe vyema katiba ya CDM sharti uwe hapa hapa TZ? mita ngapi kutoka ilipo katiba yenyewe?!
nimeamini hakuna mawaziri mizigo pekeyao, hata wanachadema mizigo wapo - wewe ni mmojawa!!
 
ZITTOKABWE.jpg
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema hakitashughulikia rufaa iliyokatwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, kwa Baraza Kuu kupinga uamuzi wa Kamati Kuu (CC) wa kumvua nyadhifa zake katika chama, hadi hapo itakapopitia utetezi wake na kuamua hatima ya uanachama wake katika chama hicho.

Pia kimethibitisha kupokea utetezi dhidi ya mashitaka 11 yanayohusisha usaliti dhidi ya chama na kuwachafua viongozi wakuu kupitia waraka wa mabadiliko.

Mashtaka hayo yanamkabili Zitto, pamoja na aliyekuwa Mjumbe wa CC, Dk. Kitila Mkumbo na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba.

Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, Victor Kimesera, alisema hayo alipozungumza na NIPASHE, ofisini kwake, jijini Dar es Salaam jana.

Kimesera, ambaye ni Katibu Mtendaji Ofisi ya Katibu Mkuu wa Chadema, alisema rufaa hiyo ni kitu kidogo, hivyo haiwezi kuanza kushughulikiwa na chama katika sakata la Zitto na watuhumiwa wenzake.

“Kuna (kitu) kikubwa cha mbele yake (rufaa),” alisema Kimesera akijibu swali la NIPASHE lililotaka kujua nini kinaendelea kwenye chama baada ya Zitto kukata rufaa.
Kimesera alisema kitu kikubwa kuliko rufaa, ambacho kitaanza kushughulikiwa na chama ni maelezo ya utetezi wa Zitto na watuhumiwa wenzake.

Alisema hiyo ni kwa sababu tayari kuna hoja ya CC, ambayo inataka ijiridhishe kama Zitto na wenzake waendelee kuwa uanachama au la.

Kwa mujibu wa Kimesera, baada ya Zitto na wenzake kuwasilisha utetezi wao, CC itaitishwa na kuyapitia na kisha itatoa maamuzi juu ya uanachama wao.
“Sasa huwezi kuongea juu ya rufaa wakati hujajua uanachama wao kwanza,” alisema Kimesera.

Hivyo, alisema rufaa ya Zitto itaendelea kuhifadhiwa kwenye jalada hadi hapo hatua ya kwanza ya kupitia maelezo yao ya utetezi na kuyatolea maamuzi itakapochukuliwa. “Lazima twende kwa hatua. Kwa hiyo, hiyo (rufaa) imekaa,” alisema Kimesera.

Mwanasheria wa Zitto, Albert Msando, alitaja sababu mbili za mteja wake kukata rufaa kuwa ni kukiukwa kwa taratibu za kuchukua hatua za nidhamu na sababu zilizotolewa kutokuwa sahihi.

Msando alitaja kifungu cha 6.5.6 cha Kanuni ya Uendeshaji ya chama hicho, akisema utaratibu uliotakiwa kufuatwa kabla ya kumchukulia hatua za kinidhamu kiongozi kwa mujibu wa Katiba na Kanuni ni kupewa kwanza mashtaka kwa maandishi ili apate nafasi ya kujibu.

Alisema kiongozi yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu bila kwanza kupewa mashtaka yake kwa maandishi na mamlaka husika na kupewa nafasi ya kujibu mashtaka kwa maandishi.

Alitaja ibara ya 5.4.3 na 5.4.4 ya Katiba kwamba mwanachama yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu ama kuonywa ama kuachishwa ama kufukuzwa uanachama bila kujulishwa makosa yake kwa maandishi na kutakiwa kutoa majibu katika muda usiopungua wiki mbili.”

Alitaja vipengele vingine ni kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya kikao kinachohusika na atajulishwa kwa maandishi uamuzi wa kikao ndani ya wiki mbili baada ya kusikilizwa.

Katika hatua nyingine, Kimesera alisema Chadema imepeleka majibu baada ya Mwigamba kupeleka barua yenye malalamiko kwa Msajili wa Vyama vya Siasa dhidi ya uongozi wa chama hicho.

Katika malalamiko yake, Mwigamba anadai kuwa katiba ya Chadema ilivurugwa na viongozi wa chama kwa kuondoa kinyume cha taratibu maelezo ya kifungu cha katiba ya chama yaliyokuwa yakiainisha ukomo wa vipindi viwili vya uongozi.

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, alithibitisha kupokea barua hiyo ya Mwigamba na kusema ofisi yake inaifanyia kazi.

Kimesera jana, kuwa walipeleka majibu dhidi ya malalamiko ya Mwigamba baada ya kuagizwa na msajili kufanya hivyo kabla ya Desemba 19, mwaka huu.

Katika barua yake, Mwigamba amemuomba msajili kutoa mwongozo kuhusu anachodai kuwa ni mgogoro wa kikatiba uliopo ndani ya Chadema kufuatia kipengele cha katiba kinachogusia ukomo wa uongozi kubadilishwa kinyume cha utaratibu.

Novemba 22, mwaka huu, CC iliwavua madaraka viongozi hao na kuwataka wajieleze kwa maandishi ndani ya siku 14 baada ya kudaiwa kuhujumu chama kwa kuandika waraka wa siri unaodaiwa pamoja na mambo mengine, kuwadhalilisha viongozi wakuu wa Chadema.

CHANZO: NIPASHE

MASKINI ZITTO KABWE CHADEMA!!!! CHAMA KIMETUPILIA MBALI RUFAA YA ZITO.....SOMA ZAIDI ~ PAPARAZI
 
Kamanda ulikuwa umelala hii habari mbona ipo toka jana humu JF au nyie pro-Chadema mkiona jina la Zitto ni kukimbilia JF kuanzisha uzi wewe mtu wa kumi leo kuleta hii habari.
 
Back
Top Bottom