CHADEMA yaishitaki YANGA kwa barua kwenda FIFA

Abdul Said Naumanga

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2024
Posts
745
Reaction score
1,470
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimewasilisha malalamiko rasmi kwa FIFA Ethics Committee dhidi ya Klabu ya Young Africans SC (Yanga). Malalamiko hayo yanahusu mchango wa TZS milioni 100 uliotolewa na Yanga kwa chama cha siasa (CCM) katika hafla ya Gala Dinner iliyofanyika Mlimani City, Dar es Salaam, tarehe 12 Agosti 2025. Katika malalamiko hayo, CHADEMA inadai kuwa kitendo hicho kilichofanywa na Yanga ni uvunjaji wa moja kwa moja wa kanuni za FIFA zinazolinda misingi ya political neutrality na uhuru wa vyama vya michezo dhidi ya ushawishi wa kisiasa.

Kwa mujibu wa barua hiyo, kitendo cha Rais wa Yanga, Eng. Hersi Said, kutangaza mchango huo mbele ya viongozi wa kitaifa wa chama tawala wakati wa kampeni za uchaguzi, ni tendo linalotafsiriwa kama explicit political alignment. Kwa maneno mengine, klabu imejipambanua hadharani kisiasa. FIFA Statutes, hasa Articles 4, 14, 19 na 20, pamoja na FIFA Code of Ethics (Articles 15 na 20), zinaweka wazi kwamba klabu na viongozi wake wanapaswa kubaki huru dhidi ya ushawishi wa kisiasa, na marufuku hii inalenga kulinda hadhi ya michezo kama jukwaa la umoja wa kijamii bila kujali imani au itikadi.

Tatizo kubwa siyo tu uvunjaji wa kanuni, bali athari za kijamii na kitaasisi zinazoweza kutokea. Yanga ni taasisi ya kijamii yenye mashabiki na wanachama wanaotoka pande zote za kisiasa. Mara klabu inapojitokeza wazi kuunga mkono chama fulani, inawa alienate mashabiki na wanachama wanaotoka nje ya mstari huo. Hii inavunja msingi wa michezo kama chombo cha umoja, inahatarisha taswira ya klabu katika soko la wadhamini, na inaweza kuibua mfarakano wa ndani. Zaidi ya hapo, inaleta mfano hatari unaoweza kufuatiwa na vilabu vingine, na hatimaye kugeuza sekta ya michezo kuwa uwanja wa siasa za vyama.

Kwa mantiki hiyo, hoja ya CHADEMA mbele ya FIFA si hoja nyepesi ya siasa za ndani, bali ni hoja ya kulinda misingi ya utawala bora wa michezo duniani. FIFA mara nyingi imeonyesha msimamo mkali dhidi ya ushawishi wa kisiasa, ikiwahi hata kuzuia mashirikisho ya kitaifa kushiriki michuano pale ambapo serikali au vyama vya siasa vimeonekana kuingilia maamuzi ya michezo. Ikiwa FIFA itaona uzito wa malalamiko haya, hatua dhidi ya Yanga au viongozi wake zinaweza kuwa fundisho kubwa kwa vilabu vyote Afrika na kwingineko, kwamba siasa na michezo lazima zibaki na mipaka yao.

Kwa mtazamo wangu, hili si jambo la kupuuzwa. Hata kama ndani ya Tanzania linaweza kuonekana kama jambo la kawaida la kisiasa, kwenye mizani ya sheria za michezo za kimataifa ni suala linaloweza kupelekea adhabu kali, kuanzia onyo, faini, kufungiwa viongozi husika, au hata kuathiri ushiriki wa klabu kimataifa endapo TFF itabainika kushindwa kudhibiti wanachama wake. Hivyo basi, hatua ya CHADEMA imefungua ukurasa mpya wa mjadala; Je, Tanzania tupo tayari kulinda michezo yetu dhidi ya ushawishi wa kisiasa, au tutaendelea kuziacha klabu zetu zibebeshwe ajenda za vyama?​

==========================
IMG_5955.jpeg
IMG_5956.jpeg

IMG_5957.jpeg

IMG_5958.jpeg
 
Ni kweli wanayanga Imetuuma Ml.100 yetu ya Tofali,lakini anachotaka Chadema kufanya ni ushenzi na kuharibu Timu yetu! Chadema akifanya hivyo atambue Kuna Wana Yanga Pia ni wanachadema. So Anguko analolitafuta Chadema anayeshitaki dhidi ya Yanga litamdhalilisha yeye na Yanga itasonga mbele. Nashauri Chadema wasidandie vita ambayo uhakika wa ushindii haupo.
 
Tuache kwanza inyeshe ndo tutajua wapi inavuja
 
View attachment 3444032
View attachment 3444033
View attachment 3444034
Saaafi sana
 
Ni kweli wanayanga Imetuuma Ml.100 yetu ya Tofali,lakini anachotaka Chadema kufanya ni ushenzi na kuharibu Timu yetu! Chadema akifanya hivyo atambue Kuna Wana Yanga Pia ni wanachadema. So Anguko analolitafuta Chadema anayeshitaki dhidi ya Yanga litamdhalilisha yeye na Yanga itasonga mbele. Nashauri Chadema wasidandie vita ambayo uhakika wa ushindii haupo.
Mi mwanayanga ila naunga mkono Yanga kushtakiwa.
 
Chama Cha siasa kinashtaki klabu ya mpira kujihusisha na siasa. Je, kwa wao kushtaki si kujihusisha na mpira?
Bora, mtu independent toka Chadema angeshtaki badala ya chama kizima kujihusisha.
Kwanza Kuna wanayanga ni Chadema na hapo conflict inaanza.
 
Chama Cha siasa kinashtakinklabu ya mpira kujihusisha na siasa. Je, kwa wao kushtaki si kujihusisha na mpira?
Bora, mtu independent toka Chadema angeshtaki badala ya chama kizima kujihusisha.
Kwanza Kuna wanayanga ni Chadema na hapo conflict inaanza.
C unajua tena chadema kwa kudakia mambo ili nao wasikike masikioni mwa watu 😂
Kumbe nao wanaifatilia ccm bhana 😂
 
CHADEMA wameitumia FIFA barua rasmi ya malalamiko yao dhidi ya Klabu ya Yanga wakihusishwa kuwa na Ushirika wa karibu na CCM katika barua hiyo iliyotiwa saini na Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Diaspora wa Chama hicho ni kuwa wameweka matakwa yafuatayo:

1- Uchunguzi ufanywe na FIFA kuhusu ushirika wa Yanga katika masuala ya kisiasa.

2- Yanga ikumbane na rungu mara moja kama klabu lakini Viongozi wake pia wapokee adhabu kali kulingana na taratibu za FIFA.

3- Kusisitiza na kuzuia soka la Tanzania kushirikiana na masuala ya kisiasa. CHADEMA wapo tayari wakati wowote kutoa Ushahidi pale ambapo FIFA watahitaji.

Screenshot_20250817_154714_Instagram.jpg
 
Katika barua hiyo, CHADEMA wanawasilisha malalamiko rasmi dhidi ya Klabu ya Yanga (Young African Sports Club) kwa madai kwamba klabu hiyo imejihusisha na siasa za vyama nchini Tanzania.

CHADEMA wanadai hatua hizo za Yanga zinakiuka moja kwa moja misingi ya FIFA inayotaka vilabu vya mpira wa miguu kubaki huru na visijihusishe na siasa, kwa kuwa FIFA inapinga upendeleo wa kisiasa na inalinda misingi ya uhuru na kutokuwa na upande wa kisiasa.

Kwa hiyo, barua hii ni ombi la CHADEMA kwa FIFA ichukue hatua za haraka dhidi ya Yanga kwa madai ya kuvunja kanuni hizo.
1799105340.jpg
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimewasilisha malalamiko rasmi kwa FIFA Ethics Committee dhidi ya Klabu ya Young Africans SC (Yanga). Malalamiko hayo yanahusu mchango wa TZS milioni 100 uliotolewa na Yanga kwa chama cha siasa (CCM) katika hafla ya Gala Dinner iliyofanyika Mlimani City, Dar es Salaam, tarehe 12 Agosti 2025. Katika malalamiko hayo, CHADEMA inadai kuwa kitendo hicho kilichofanywa na Yanga ni uvunjaji wa moja kwa moja wa kanuni za FIFA zinazolinda misingi ya political neutrality na uhuru wa vyama vya michezo dhidi ya ushawishi wa kisiasa.

Kwa mujibu wa barua hiyo, kitendo cha Rais wa Yanga, Eng. Hersi Said, kutangaza mchango huo mbele ya viongozi wa kitaifa wa chama tawala wakati wa kampeni za uchaguzi, ni tendo linalotafsiriwa kama explicit political alignment. Kwa maneno mengine, klabu imejipambanua hadharani kisiasa. FIFA Statutes, hasa Articles 4, 14, 19 na 20, pamoja na FIFA Code of Ethics (Articles 15 na 20), zinaweka wazi kwamba klabu na viongozi wake wanapaswa kubaki huru dhidi ya ushawishi wa kisiasa, na marufuku hii inalenga kulinda hadhi ya michezo kama jukwaa la umoja wa kijamii bila kujali imani au itikadi.

Tatizo kubwa siyo tu uvunjaji wa kanuni, bali athari za kijamii na kitaasisi zinazoweza kutokea. Yanga ni taasisi ya kijamii yenye mashabiki na wanachama wanaotoka pande zote za kisiasa. Mara klabu inapojitokeza wazi kuunga mkono chama fulani, inawa alienate mashabiki na wanachama wanaotoka nje ya mstari huo. Hii inavunja msingi wa michezo kama chombo cha umoja, inahatarisha taswira ya klabu katika soko la wadhamini, na inaweza kuibua mfarakano wa ndani. Zaidi ya hapo, inaleta mfano hatari unaoweza kufuatiwa na vilabu vingine, na hatimaye kugeuza sekta ya michezo kuwa uwanja wa siasa za vyama.

Kwa mantiki hiyo, hoja ya CHADEMA mbele ya FIFA si hoja nyepesi ya siasa za ndani, bali ni hoja ya kulinda misingi ya utawala bora wa michezo duniani. FIFA mara nyingi imeonyesha msimamo mkali dhidi ya ushawishi wa kisiasa, ikiwahi hata kuzuia mashirikisho ya kitaifa kushiriki michuano pale ambapo serikali au vyama vya siasa vimeonekana kuingilia maamuzi ya michezo. Ikiwa FIFA itaona uzito wa malalamiko haya, hatua dhidi ya Yanga au viongozi wake zinaweza kuwa fundisho kubwa kwa vilabu vyote Afrika na kwingineko, kwamba siasa na michezo lazima zibaki na mipaka yao.

Kwa mtazamo wangu, hili si jambo la kupuuzwa. Hata kama ndani ya Tanzania linaweza kuonekana kama jambo la kawaida la kisiasa, kwenye mizani ya sheria za michezo za kimataifa ni suala linaloweza kupelekea adhabu kali, kuanzia onyo, faini, kufungiwa viongozi husika, au hata kuathiri ushiriki wa klabu kimataifa endapo TFF itabainika kushindwa kudhibiti wanachama wake. Hivyo basi, hatua ya CHADEMA imefungua ukurasa mpya wa mjadala; Je, Tanzania tupo tayari kulinda michezo yetu dhidi ya ushawishi wa kisiasa, au tutaendelea kuziacha klabu zetu zibebeshwe ajenda za vyama?​

==========================
View attachment 3444032
View attachment 3444033
View attachment 3444034
Badala mje kugombea huku kwenye uchaguzi.mnapenda kesi nyie
 
Kwa mustakabali wa maisha yetu, bila kutazama upenzi wa Yanga au Simba. Watanzania tuungane na CHADEMA katika hili.
 
Katika barua hiyo, CHADEMA wanawasilisha malalamiko rasmi dhidi ya Klabu ya Yanga (Young African Sports Club) kwa madai kwamba klabu hiyo imejihusisha na siasa za vyama nchini Tanzania.

CHADEMA wanadai hatua hizo za Yanga zinakiuka moja kwa moja misingi ya FIFA inayotaka vilabu vya mpira wa miguu kubaki huru na visijihusishe na siasa, kwa kuwa FIFA inapinga upendeleo wa kisiasa na inalinda misingi ya uhuru na kutokuwa na upande wa kisiasa.

Kwa hiyo, barua hii ni ombi la CHADEMA kwa FIFA ichukue hatua za haraka dhidi ya Yanga kwa madai ya kuvunja kanuni hizo.
View attachment 3444174
Wekeni pia barua mlio jibiwa na FIFA jana
 
Likawe funzo, huu ni ujinga ko sisi wamayangq tusio wana CCM wametuweka kundi gani?
 
Walio andika barua toka Chadema kwenda FIFA kuhusu mchango wa 100m, unao ihusisha yanga SC, uwezo wao wa kufikiri ni mdogo

Jibu la mfano:
FIFA wanakuruhusu mkojo wako utoke mwilini mwako lakini usiingie mwilini mwako

Tafsiri wanaruhusu hata wachezaji wajenge makanisa na misikiti kama alivyofanya Mbwana Samatta, wanasiasa kualikwa kwenye michezo, vile Vile wanaruhusu Vilabu vya mpira na mchezaji mmoja mmoja kujihusisha na mambo ya kijamii pamoja na hayo ya kisiasa

FIFA wanaruhusu pia Chama cha siasa kimiliki timu ya mpira ila kisiingize mambo ya siasa kwenye mpira hata kama timu ni yakwao

FIFA hawaruhusu wanasiasa kuingilia mambo ya mpira hata wachezaji wakiwa kwenye mpira waka onyesha mabango ya NERNE ama October wana pata,(✓)
 
Back
Top Bottom