Kwa hiyo swala sio Majimbo yenywe isipokuwa who do you answer to.. kwa hiyo kwa nini isiwe kila mikataba iwekwe who to answer to badala ya kwenda kwa rais kwani tatizo hapa ni madaraka ya RAIS sio ukubwa wa nchi..
Kisha ikiwa ubadhilifu unatokana na rais kwa nini tunamchagua rais asiyeweza kuongoza nchi yenye watu millioni 40 tu ukubwa wa nchi sawa na state moja ya Marekani ama serikali nyinginezo. za Africa!
Hivi we BISKUTI mbona hauwi straight?
Unazunguka zunguka nini hapa?
Ama unataka biskuti iliwe?
Sema unachotaka kusema na si ulete kizunguzungu hapa!
Unajua siyo kosa lako jmushi1, kwani inaonekana kama mtu haja-drop buzz-words kama CCM, fisadi, Zitto, CHADEMA na kadhalika kwenye postings zake basi kwako binafsi mtu huyo hajazungumza lolote la maana.
BP Biscuit mane,
Mkuu hata sikuelewi unakojaribu kwenda, samahani sana nipo kizani kabisa! ebu nieleze kwa kina unachojaribu kuzungumza ktk hoja hii ya Majimbo.
Kwa kifupi ninachojaribu ku-argue hapa ni kwamba sera ya majimbo ielekezwe kwenye kufua (kwa maana ya ku-exploit) nguvu mwanana ya ukabila kwa manufaa ya maendeleo ya Wananchi waishio kwenye majimbo hayo. Na ukabila, kama tunavyofahamu ni natural instinct na jadi ya binadamu wote popote duniani kama viliyo dhana za nuclear family, extended family na clanship (au ukoo). Hata Ulaya utaona mataifa karibia yote kwa ujumla yamegawanyika kutokana na vigezo vya lugha na ukabila.
a) Jimbo la Kaskazini litaundwa na Mikoa ya Arusha, Manyara na
Kilimanjaro.:Humu kuna wachagga,wamasai,wameru etc etc! Tena kuna wahamiaji wengi tu ambao si makabila hayo! The same applies to letters b-h
b) Jimbo la Kusini litaundwa kwa kuunganisha mikoa ya Lindi na Mtwara.
c) Jimbo la Ziwa litaundwa kwa kuunganisha mikoa ya Kagera, Mwanza, Shinyanga na Mara.
d) Jimbo la Mashariki mkoa wa Tanga na visiwa vyake.
e) Jimbo la Pwani -litaundwa kwa kuunganisha Mikoa ya Morogoro, Pwani na Dar- es-salaam.
f) Jimbo la Kati litaundwa na Mikoa ya Dodoma na Singida.
g) Jimbo la Magharibi litaundwa na mikoa ya Tabora, Rukwa na Kigoma.
h) Jimbo la Nyanda za Juu Kusini litaundwa kwa kuunganisha Mikoa ya Iringa na Mbeya
Mkuu wale viongozi wa Majimbo wqatashindwa nini kujilimbikiza mali wao?.. unajua mkuu kama ungeweza kunijibu direct swali langu la KUTOWAJIBIKA nadhani tungekuwa hatuzunguki mbuyu huu.
Ni kitu gani kitakacho wahakikishia wananchi kwamba hapatakuwepo na miungu wadogo ktk Majimbo?.. hawa marais wadogo wenye tamaa ya kujilimbikiza mali lakini hawajapata mwanya huo.
kuwa aswerable to the people ni neno tu ambalo hata leo tunaambiwa lipo ktk katiba ya nchi lakini halitekelezwi. Je, hayo majimbo yatabadilisha vipi kitabia hiki cha kujilimbikiza mali.. kuiba mbegu zetu, kwani mtoto wa nyoka ni myoka!
b) Tutabadili mfumo wa sasa wa utawala na kuanzisha mfumo mpya wa utawala utakaokuwa na muundo mpya wa serikali kuu na serikali za majimbo. Serikali za mitaa zitakuwa sehemu ya serikali za majimbo.
4) Serikali kuu na serikali za mitaa zina mahusiano na maingiliano makubwa katika utekelezaji wa majukumu yake. Kazi na majukumu ya serikali za mitaa zimeainishwa kwenye sheria ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa ya mwaka 1982. Kwa mfano, sehemu ya 111 na 118 ya sheria za Mamlaka za Mijini (Urban Authorities) zimeainisha huduma zinazotolewa na serikali za mitaa kama ifuatavyo.
a) Huduma zinazotolewa na serikali za mitaa kwa usimamizi wa serikali kuu. Huduma hizi ni elimu ya msingi, huduma za afya, maendeleo ya kilimo na mifugo, maji, na ujenzi na ukarabati wa barabara.
b) Huduma zinazotolewa na kusimamiwa na serikali za mitaa yenyewe. Huduma hizi ni ukusanyaji wa taka, usafi wa mazingira, maegesho ya magari na vifaa vinginevyo, masoko na nyinginezo.
1. Dira.
Kuwa na taifa linaloendelea kwa haraka na kwa usawa, lenye haki, umoja na mshikamano wa kweli
2. Dhumuni Kuu.
Kujenga mfumo na muundo wa utawala unaotoa nguvu na mamlaka zaidi kwa umma katika kujiongoza na kutumia raslimali zao kwa usawa kujiletea maendeleo.
3. Malengo Mahsusi.
(1) Kupunguza ukubwa wa serikali kuu kimuundo na kimajukumu pamoja na gharama zake za uendeshaji na kuachia raslimali nyingi kutumika moja kwa moja kwa maendeleo ya wananchi.
(2) Kurahisisha uongozi wa nchi kwa kuiunganisha mikoa kuwa majimbo ambayo viongozi wake watapatikana na kuongoza kwa ridhaa ya wananchi.
(3) Kupunguza urasimu wa kufikia maamuzi na kuongeza ufanisi na usimamizi wa karibu zaidi katika utoaji huduma kwa jamii chini ya tawala za majimbo.
(4) Kuondoa matabaka kwa kuweka mgawanyo mzuri na matumizi mazuri ya raslimali kati ya eneo moja la nchi na lingine.
(5) Kuimarisha mfumo na muundo wa Serikali za Mitaa kwa kuingiza ngazi ya Mkoa katika muundo huu.
(6) Kuondoa migongano ya kiutendaji kati ya Serikali Kuu na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa pande zote kufanya kazi katika eneo moja la kijiografia na katika jamii ile ile moja.
(7) Kuanzisha vyombo vya uwakilishi wa wananchi ndani ya utawala wa majimbo na kuboresha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Muundo Mpya wa Serikali za Mitaa huu:
Serikali za mitaa zitakuwa sehemu ya serikali za majimbo na zitawasiliana na serikali kuu kupitia uongozi wa jimbo. Muundo mpya wa serikali za mitaa utahusisha ngazi zifuatazo;
a) Halmashauri za wilaya/Miji.
b) Wakuu wa Idara katika Halmashauri. Idara hizi ni kama idara za mipango, kilimo, elimu, maji, maliasili, maendeleo ya jamii n.k).
c) Ofisi ya Kata itakayokuwa chini ya Katibu Kata na Kamati ya Maendeleo ya Kata.
d) Serikali ya Kijiji/Mtaa itakayoundwa pia na Ofisa mtendaji wa Kijiji na Halmashauri ya Kijiji.
QUOTE=Mkandara;198528]Mkuu wale viongozi wa Majimbo wqatashindwa nini kujilimbikiza mali wao?.. unajua mkuu kama ungeweza kunijibu direct swali langu la KUTOWAJIBIKA nadhani tungekuwa hatuzunguki mbuyu huu.
Ni kitu gani kitakacho wahakikishia wananchi kwamba hapatakuwepo na miungu wadogo ktk Majimbo?.. hawa marais wadogo wenye tamaa ya kujilimbikiza mali lakini hawajapata mwanya huo.
[/QUOTE]kuwa aswerable to the people ni neno tu ambalo hata leo tunaambiwa lipo ktk katiba ya nchi lakini halitekelezwi. Je, hayo majimbo yatabadilisha vipi kitabia hiki cha kujilimbikiza mali.. kuiba mbegu zetu, kwani mtoto wa nyoka ni myoka!
[/QUOTE]QUOTE=Mkandara;198536]Jmushi1,
Mkuu nitarukia tena swali hili pamoja na kwamba yale yaliyotangulia halikupata ufumbuzi
Hivi mapato ya tuseme mgodi wa dhahabu Shinyanga utawasaidia vipi wakazi wa Bukoba chini ya Majimbo ikiwa leo wananchi wa Shinyanga wanalalamika mali zao kuchukuliwa na serikali kuu. Kisha hao Shinyanga watakuwa na upendo gani tofauti kuona kwamba utajiri wao unapelekwa Bukoba hali Bukoba hawana kitu zaidi ya ndizi na kahawa siyokuwa na soko nje. Msukuma wa Shinyanga hali ndizi wala hana mahusiano ya kutaka chochote toka Bukoba utamwambia kitu gani ikiwa shinyanga itarudi nyuma kimaendeleo. hayo Makao makuu ya Jimbo sijui yatakuwa Mwanza. Je, hiyo Mwanza ikijengwa kwa chumi za mikoa mingine mtawaeleza nini wananchi wa sehemu zinazozalisha ujenzi wa makao makuu hayo..