CHADEMA yaiiga ODM kuhusu Sera ya Majimbo

Mkuu unauliza swali ukiwa na jibu ambalo nazidi kusema halijatafuta ukweli kwa kutumia diagnosis yaani unachotaka kusema ni kile kile mtu anaumwa mguu unakata kichwa..
Nimesema mara millioni tunachoshindwa leo ni UONGOZI mbaya usowajibika, jambo ambalo wachumi wote duniani pamoja na Wafadhili wetu wamekwisha lifanyia Utafiti na halihusiani na muundo wa serikali kuu ama ile ya majimbo isipokuwa watu hao VIONGOZI wenyewe.

Ndio maana wakaanza na kitu kama UWAZI na kina Mkapa wakajenga biashara hadi IKULU na hakikufanya kazi, Kisha wamejaribu tena kuweka taasisi za kuzuia rushwa nazo zimeshindikana kutokana na kwamba hao hao viongozi wanaotakiwa kusimamisha sheria ndio wao mafisadi.
Hivyo kinachotakiwa sasa hivi maadam tumeshapewa majibu ya gonjwa letu ni sisi wenyewe kulitafutia dawa badala ya kutegemea vyombo vya nchi za nje wasiofahamu mazingira yetu..
Tutaweza vipi kusimamisha Good Governance ktk jamii ilokiuka kwa Ufisadi?..Sheria Sheria lazima ichukue mkondo wake na kama ipibidi kuwaondoa CCM ktk UONGOZI wa nchi ni muhimu zaidi kama vile Demokrasia inavyotangazwa duniani. Kumwondoa Dikteta mbaya siku zote ni shida lakini ikibidi hata nguvu kutumika basi ni muhimu lakini kumweka mtu huyo ktk nafasi ya aina yeyote ile hakuwezi kumwondoa umeyaona ya kina Saadam na Mugabe vikwazo vya uchumi, mbinu kama hivi ndizo zimewafanya kuwa wabaya zaidi badala ya kupunguza nguvu zao ndio kwanza ziliongezeka na madhara ni kwa wananchi wake.
Chadema wanachotakiwa sasa hivi ni kuweka mwelekeo ktk uchaguzi wa 2010 kwa kutazama vipi wanaweza kumvuta mwananchi wa kijijini ktk siasa hizi.
Majimbo yana complications nyingi sana na mifano ndio kama hivyo ya Pemba. Utamwambia vipi mtu wa kijijini kwamba Tunavunja Tanzania na kukupa Jimbo?...uwe kari bu na viongozi ambao yeye mwenyewe hawataki hasa hao wa CCM.
Mkuu ukinambia Mama Mongela awe mkuu mwenye madaraka ya juu wilayani kwangu nitazimia..Kitu kimoja usichokifahamu ni kwamba wananchi vijijini wanafahamu kuwa maendeleo yao yanakwamishwa na viongozi wao wa sehemu zao kwa sababu wanaona jinsi wanavyotumia ovyo mali za umma.. NDIVYO TULIVYO bado tunawachagua hao hao na kama tutawapa madaraka zaidi ndio tumekwisha kabisa! Kina Mama Mkapa wanaojichukulia nyumba za serikali watazuka kila Jimbo, wilaya na mkoa hasa pale mali zile ni mali za taifa ndio kabisa wananchi watakuwa hawana sauti. Please jamani deal na the real issue ya kumwondoa FISADI, wananchi wa kijijini watapata kuwaelewa zaidi kwa sababu machungu yake wanayaona. Hili la Majimbo ni swala jipya na mifano michache inayoonekana ni ishara mbaya tayari ya sera hii kuuzika kwa wananchi.
Nimemaliza... msije kuwa nyie nyote CCM mnataka kujenga hoja zenu ktk kijiwe hiki...samahani lakini.
 
Mkuu unauliza swali ukiwa na jibu ambalo nazidi kusema halijatafuta ukweli kwa kutumia diagnosis yaani unachotaka kusema ni kile kile mtu anaumwa mguu unakata kichwa..
Nimesema mara millioni tunachoshindwa leo ni UONGOZI mbaya usowajibika, jambo ambalo wachumi wote duniani pamoja na Wafadhili wetu wamekwisha lifanyia Utafiti na halihusiani na muundo wa serikali kuu ama ile ya majimbo isipokuwa watu hao VIONGOZI wenyewe.

Ndio maana wakaanza na kitu kama UWAZI na kina Mkapa wakajenga biashara hadi IKULU na hakikufanya kazi, Kisha wamejaribu tena kuweka taasisi za kuzuia rushwa nazo zimeshindikana kutokana na kwamba hao hao viongozi wanaotakiwa kusimamisha sheria ndio wao mafisadi.
Hivyo kinachotakiwa sasa hivi maadam tumeshapewa majibu ya gonjwa letu ni sisi wenyewe kulitafutia dawa badala ya kutegemea vyombo vya nchi za nje wasiofahamu mazingira yetu..
Tutaweza vipi kusimamisha Good Governance ktk jamii ilokiuka kwa Ufisadi?..Sheria Sheria lazima ichukue mkondo wake na kama ipibidi kuwaondoa CCM ktk UONGOZI wa nchi ni muhimu zaidi kama vile Demokrasia inavyotangazwa duniani. Kumwondoa Dikteta mbaya siku zote ni shida lakini ikibidi hata nguvu kutumika basi ni muhimu lakini kumweka mtu huyo ktk nafasi ya aina yeyote ile hakuwezi kumwondoa umeyaona ya kina Saadam na Mugabe vikwazo vya uchumi, mbinu kama hivi ndizo zimewafanya kuwa wabaya zaidi badala ya kupunguza nguvu zao ndio kwanza ziliongezeka na madhara ni kwa wananchi wake.
Chadema wanachotakiwa sasa hivi ni kuweka mwelekeo ktk uchaguzi wa 2010 kwa kutazama vipi wanaweza kumvuta mwananchi wa kijijini ktk siasa hizi.
Majimbo yana complications nyingi sana na mifano ndio kama hivyo ya Pemba. Utamwambia vipi mtu wa kijijini kwamba Tunavunja Tanzania na kukupa Jimbo?...uwe kari bu na viongozi ambao yeye mwenyewe hawataki hasa hao wa CCM.
Mkuu ukinambia Mama Mongela awe mkuu mwenye madaraka ya juu wilayani kwangu nitazimia..Kitu kimoja usichokifahamu ni kwamba wananchi vijijini wanafahamu kuwa maendeleo yao yanakwamishwa na viongozi wao wa sehemu zao kwa sababu wanaona jinsi wanavyotumia ovyo mali za umma.. NDIVYO TULIVYO bado tunawachagua hao hao na kama tutawapa madaraka zaidi ndio tumekwisha kabisa! Kina Mama Mkapa wanaojichukulia nyumba za serikali watazuka kila Jimbo, wilaya na mkoa hasa pale mali zile ni mali za taifa ndio kabisa wananchi watakuwa hawana sauti. Please jamani deal na the real issue ya kumwondoa FISADI, wananchi wa kijijini watapata kuwaelewa zaidi kwa sababu machungu yake wanayaona. Hili la Majimbo ni swala jipya na mifano michache inayoonekana ni ishara mbalia ya sera hii kuuzika kwa wananchi.
Nimemaliza... msije kuwa nyie nyote CCM mnataka kujenga hoja zenu ktk kijiwe hiki...samahani lakini.

Uongozi mbaya unachangiwa na sytem mbovu kuwa expolited!
Hata kama ni biashara yako..Kama huna mipango madhubuti utaibiwa tuu!
 
Mimi nina uhakika kuwa sisi kama wadau wa nchi..Tunaweza kujadili na kuja na outcome nzuri tu kwa wananchi!
Ukisema kuwa mtu ni mbaya halafu hufanyi jitihada zozote zile zenye kuondoa mazingira yaliyopelekea yeye kuufanya ubaya huo then subiri malaika kama alivyosema Mbowe!
 
Na kama tunajua kuwa watu si malaika..Then ni sisi tutakao make sure tunaweka system na mazingira mazuri ya kuwabana wenye kutaka kui exploit system!
We unafikiri kwanini wenzetu wamefikia stage za hali ya juu za kuwabana mafisadi?
Ni muhimu kuwa na utaratibu utakao ensure haki kwa wananchi wa kawaida pale inapokuja kwenye usimamizi na uendelezaji wa rasilimali zao!
 
Uongozi mbaya unachangiwa na sytem mbovu kuwa expolited!
Hata kama ni biashara yako..Kama huna mipango madhubuti utaibiwa tuu!
Hapana mkuu sysytem mbovu hujengwa na viongozi wabaya.. hakuna system iliyojitokeza yenyewe ila kwa nguvu za mwanadamu.
Nitarudia kusema kwa nini bnado unasisitiza kukata kichwa hali tayari umeshaambiwa maradhi yako ya mguu hayatokani na madaraka ya kichwa.
Nchi zetu zote maskini tumekutwa hatuna UONGOZI mzuri ktk fani nyingi sana kwa sababu ya UHUJUMU Uchumi.. sasa nambie wewe Majimbo yatarekebisha kitu gani kuleta Good governance ikiwa swala ni MAFISADI!
We unafikiri kwanini wenzetu wamefikia stage za hali ya juu za kuwabana mafisadi?
Ni muhimu kuwa na utaratibu utakao ensure haki kwa wananchi wa kawaida pale inapokuja kwenye usimamizi na uendelezaji wa rasilimali zao!
Biula shaka sio kwa kuunda majimbo!..Ila sheria kuwa mbele ya kila kitu na Uwajibikaji.
 
Mkuu Jmushi naona umeikimbilia sana hii issue ya majimbo, lakini sidhani kama unaelewa vizuri complication zake.

Huyo Mkandara yeye anaishi nchi ambayo inaongozwa kimajimbo na kwa kweli sijaona system iliyokuwa ngumu kama hiyo na inahitaji ufanisi wa hali ya juu.

Kwa Tanzania nasema hivi, sio katika miaka ya karibuni sytem hii itafaa.

Chadema wanafanya makosa makubwa sana sababu wanaleta discussion ambayo ni very complicated wakati huu CCM iko taabani badala ya kumjali mwananchi moja kwa moja.

Wananchi asilimia 80 Tanzania wako vijijini bila elimu, sasa wewe leo unazuka na discussion ngumu kama hii ya majimbo unatazamia utasucceed vipi??

Kwa nini Chadema wasipiganie kumkomboa mwananchi kwa sera za moja kwa moja ie kilimo, elimu???

Kwa nini Chadema wasionyeshe wao watafanya nini kwenye system hii tuliyonayo tofauti na CCM ili wananchi waelewe kwa urahisi???

Mimi nadhani hii ni kama vile kufuata wapenzi wa soka uko Europe au South America, ukawaambia unataka sheria za timeouts na substitution kama za basketball!! Utafukuzwa kwa matusi na ndio Chadema wanachofanya.

Pse sijasema Majimbo ni system mbaya au nzuri lakini kuintroduce hii Tanzania ni sawa sawa na kumfuata mkulima kijijini ukamwambia usitumie kuni kupikia bali tumia majiko ya umeme wakati hata kuafford mlo mmoja hawezi!!!

My 2 cents
 
Mkuu umeongea jambo la maana sana!
Inawezekana si wakati muafaka huu kwasababu ya time factor!
Nakubali kabisa!
CHADEMA should now concentrate on changes that would allow them together with the rest of oppositision parties to win the general elections!
Halafu then wakiwa madarakani ndio wapromote hiyo idea na kuwaelimisha wananchi!
Wakiikubali sawa..Wakiikata sawa!
Ila sasa hivi inaweza kutumika kama a very divisible tool based on the time factors together with the people's ability to acknowledge the urgency and the importance of the issue!
 
Badala ya kuwa na wakuu wa mikoa 25 au zaidi pindi mikoa ikiongezwa ambao wanaongeza gharama kubwa za uendeshaji kwa serikali nadhani juzi kuliwekwa article hapa inayoonyesha gharama ya kuongeza mkoa mmoja ni shilingi bilioni 10. Kutakuwa na wakuu wa majimbo 5 au 6 tu maana kila jimbo linaweza kuwa na mikoa kati ya minne au mitano. Z'bar pamoja na kuwa ni nchi lakini pia kuna mikoa, hivyo Z'bar inaweza kuwa jimbo la visiwani. Kushusha idadi ya wakuu wa mikoa toka 25 na mashangingi yao hadi kufikia 5 au 6 kutakuwa na nafuu kubwa kwa serikali na savings itayopatikana hapo inaweza kulenga sehemu nyingine muhimu, hopefully sio mifukoni mwa mafisadi.
 
Ubatili na Ubutu wa Sera ya Chadema ya Majimbo
Chadema wana nia nzuri ya kuleta maendeleo kwa Wananchi na Taifa. Dhana ya kuwa na serikali za mitaa zilizo na nguvu kwa ajili ya maendeleo ya wananchi ni nzuri. Ama kuwepo kwa Serikali za Mikoa/Majimbo ambayo zinatokana na msukumo wa Wananchi wenyewe na si Uteuzi wa Ikulu pia ni jambo jema na ni wakati muafaka wa Wananchi kuwa na sauti kubwa zaidi ya Wabunge katika kutetea haki zao, kudai maendeleo na kurutubisha mapato na hali za maisha yao.

Lakini jinsi CHADEMA walivyowasilisha huu mchakato wa Sera ya Majimbo, kuna upungufu mkubwa sana wa kisera na kiutendaji ambao unaifanya Sera hii iwe Butu na hata Batili.

Chadema wamefanya kazi nzuri kubainisha mapungufu na matatizo ya migongano ya kiutawala katika nazi za mikoa wilaya na hata Serikali za mitaa kutokana na mvutano wa kiimla, kiutendaji na nguvu za kiutawala.

Walichoshindwa Chadema kukifanya katika kuwasilisha maoni yao kwa Wananchi, ni kuonyesha ni jinsi gani mfumo wao wa Utawala wanaoupendekeza unaweza kuleta ufanisi na kuhamasisha uzalishaji mali na kuwa kichocheo cha maendeleo. Aidha wameshindwa kuoanisha mfumo wao kwa kutoa ama takwimu au vitendea kazi ambavyo vinaweza kuonyesha kuwa mfumo wao utakuwa bora kuliko wa sasa wa kiutawala.

Zaidi, Chadema wameshindwa kuwa makini kwa kujikanganya mno katika kubainisha chimbuko la kudumaa kwa maendeleo ya Taifa, kudai kuwa mfumo wa uongozi na utawala ni mbaya na hatimaye kudai mfumo wao wa utawala utakuwa ni bora na kwa manufaa ya Taifa na jamii.

Hii kauli ya Majimbo na hata kuundwa kwa majimo haya katika manifesto ya Chadema ni sawa na ile Sera ya TANU tulioishupalia na kuipiga vita ya Vijiji vya Ujamaa.

Wengine wenu/wetu, tunashupalia sera lakini bado hatujakaa chini na kuchanganua ni kwa nini bado tuna umasikini, bado hatuna maendeleo madhubuti na kadhalika.

Kama kawaida yetu, tumejiunga na wale wanaotafuta kila sababu kulaumu kushindwa kwa maendeleo ya Taifa. Tulianza na Fikra za Nyerere, tukaja Siasa ya Ujamaa, tukaegemea kwenye mambo ya Ruksa na sasa ni Ufisadi na Utawala.

Lakini hizi ni sababu nyingi kama kete za drafti au bao. Hatujakaa chini kujiuliza je Mtanzania anataka maendeleo ya namna gani? hatujamhoji Mtanzania kujua tafsiri yake ya maendeleo ni nini!

Kama Chadema wangetamka kuwa wataboresha mfumo wa uongozi na utawala kwa kutumia vigezo vilivyopo sasa na kuleta maendeleo, ningewaelewa.

Lakini Sera hii ni kama kibwagizo cha kujinadi ili wapewe kura. Kiutendaji, kamwe haitafanikiwa!

Ili kufanikisha Sera hii ambayo wengine tunaishabikia bila kutafakari kunabidi kwanza kuwepo kwa mabadiliko ya Katiba ya Nchi. Hili Chadema wameligusia juu juu kwa kudai tuliunda katiba ya kumuiga mkoloni, lakini hawajaliweka mbele kuwa ili kuleta mabadiliko ya maana ya Kidemokrasia, Uongozi na Utawala ili Taifa liweze kuanza safari mpya ya maendeleo ni kubadilisha Katiba. Chadema hawajathubutu hata kidogo kuonyesha wazi kuwa kuna haja ya kuwa na Katiba mpya kwanza ambayo itasawazisha makosa yaliyopo sasa hivi ambayo yanadumaza maendeleo ya Taifa, yanapunguza Uwajibikaji na kuwa na Serikali yenye Nguvu nyingi zisizo milikiwa na Wananchi.

Chadema hawajazungumzia wazi kwa wananchi kuwa mfumo huu ni Utashi wao (Chadema) na si wa Wananchi au mjumuiko wa Vyama vya Kisiasa. Sijawahi sikia kuwa Chadema walikusanya kura za maoni na kuwauliza Watanzania wanataka mfumo gani wa Utawala au Ushirikishi. Hivyo basi, Chadema wanataka kunda Sera ya kujenga mfumo mpya wa Utawala ambao kikija Chama kingine cha Siasa ambacho hakikubaliani na mfumo huo, basi Watanzania itabidi tujifunge mikanda na kujiandaa kuishi na kuongoza na mfumo mpya wa Kiserikali. Na hili ndilo linaloonekana wazi kuwa Chadema haikubaliani na mfumo wa sasa ambao tuliuunda baada ya Uhuru.

Ama Chadema haitamki rasmi na wazi gharama kubwa za kuwa na mfumo kama huu. Chadema haitamki hatima ya hiyo mikoa ambayo itakusanywa kama fungu la nyanya kuunda Jimbo. Je Chadema imefanya tathmini gani kuona kuwa Singida na Dodoma ziko tayari kuunda Serikali ya mseto ya Jimbo? Je ni mfumo gani utatumika kugawa madaraka kwa hii mikoa itakayounda jimbo?

Nitaleta jambo moja ambalo laweza kumuamsha Mkandara na kunikoromea, lakini hili ni muhimu wakati tunatafakari huku kuundwa kwa majimbo.

Kanisa la Kilutheri Tanzania (KKKT) lilikuwa na majimbo (Dayosisi na Sinodi) ambayo yalikuwa sawa na hayo majimbo nane yanayotangazwa na Chadema. Baada ya miaka nenda rudi, waumini katika majimbo hayo, wakakataa kuwepo kwa muungano wa mikoa na hovyo kuishia karibu kila mkoa au sehemu kuunda jimbo (Dayosisi au Sinodi) yake!

Je tutaweza kuwaweka Wahaya, Wakurya,Wakerewe, Wajaluo, Wajita Wasukuma na Wanyamwezi kama Jimbo moja?

Chadema inazungumzia rasilimali na mapato yatumike kwa majimbo yaliyovuna. Hili ni sawa, lakini bado Chadema haijatueleza ni vipi Serikali kuu itajiendesha ama kuratibu Uendeshaji wa majimbo na hata mapato ya Taifa.

Chadema inasema Serikali kuu itakuwa na Wizara nne tu, Hata Marekani yenye Majimbo/Mikoa 50 yanayojiendesha yenyewe, Serikali kuu inaongozwa na kadiri Wizara 12 za kudumu. Sisi tutajenga nchi gani isiyo na wizara ya mawasiliano na miundo mbinu, wizara ya sheria, wizara ya afya, wizara ya elimu, wizara ya biashara na viwanda, wizara ya kilimo? Ni nchi gani au Serikali gani ya Kitaifa tutaijenga yenye wizara za mambo ya nje, mambo ya ndani, fedha na ulinzi pekee?

Huu ni udhaifu mkubwa sana ambao Chadema wanaonyesha katika kujiuza kwa wananchi na kama hili ndilo tegemeo lao kushika madaraka na kuongoza nchi, basi Mtanzania atasema heri tuendelee na CCM yetu maana hawa Chadema hawaeleweki.

Kinachotakiwa si kubadilisha mfumo kila mara tunapoona mambo hayaendi sawa na yanakwenda kombo. La kujiuliza ni hili, je Chadema kwa kutumia mfumo uliopo watahakikishaje kuwa Ufanisi, Uwajibikaji, Ubunifu, Uchapa kazi, Mipango bora na Uadilifu vinakuwa ndio vigezo kamili vya kuleta maendeleo kwa Taifa letu?

Mike Huckabee amesema juzi kuwa kama Wananchi hawawezi kujidhibiti, kujisukuma na kujitawala kwa uadilifu na kuchapa kazi, kamwe hawatakuwa huru na kuwa na maendeleo, hishia kuwa na Serikali inayoburuza, kuratibu na kutawala kwa nguvu ma kuamuru kila kitu.

Tunahitaji sera na mwamko wa Uongozi ambao unafuata Haki, unajali Utu, ni Fanisi, Hodari, Nyenyekevu, Mahiri, Wenye Juhudi, Wajibikaji, Fuatiliaji, Bunifu, yenye Uwazi na hamasishaji. Hatuhitaji mfumo mpya wa Kiutawala ikiwa matokeo yatakuwa ni yale yale kwa kushindwa kutibu magonjwa yaliyopo.

Mkuu Kishoka,

Kwenye majimbo tukiingiza ukabila basi kamwe hayatafanikiwa, lakini tukisema majimbo haya ni ya Watanzania bila kujali wanatoka kabila lipi basi naamini yanaweza kuwa na mafanikio makubwa zaidi hasa kama watapewa uhuru mkubwa wa kujiamulia mambo ambao wakuu wa mikoa hawana. Mfano wa mafanikio ya Watanzania ni hii JF, imagine hapa ukumbini kama tungeweka mbele ukabila badala ya Utanzania, sidhani kama JF ingekuwa na mafanikio makubwa kama iliyoyapata hadi sasa.
 
Sera ya majimbo itatuwezesha kuwa karibu na viongozi through smooth chain of commands na uwakilishi!
Badala ya Mwanakijiji kusubiri maamuzi ya rais kwenye utekelezaji wa sera muhimu za maendeleo..Wanakuwa na wawakilishi wenye nguvu kwenye maamuzi yenye kuhusika na shughuli za kimaendeleo!

Kwani Watu wa Kijiji, Kata, Tarafa na Mbunge kazi zao ni nini? hao si first line katika chain of command na uwakilishi au ni vipi?
 
Hawabanwi na wananchi kwasababu they answer straight to the president rather than THE PEOPLE! Hawa wanahaki ya kujibu kwa raisi tu! Hakuna fundamental procedures zenye ku assure accountability under the current system na ndio maana tuna suasua kuwashughulikia mafisadi!
Nini kigumu hapo jamani?

Isn't the President answerable to the people? Who elects the president?
 
Ubatili na Ubutu wa Sera ya Chadema ya Majimbo

Chadema wana nia nzuri ya kuleta maendeleo kwa Wananchi na Taifa. Dhana ya kuwa na serikali za mitaa zilizo na nguvu kwa ajili ya maendeleo ya wananchi ni nzuri. Ama kuwepo kwa Serikali za Mikoa/Majimbo ambayo zinatokana na msukumo wa Wananchi wenyewe na si Uteuzi wa Ikulu pia ni jambo jema na ni wakati muafaka wa Wananchi kuwa na sauti kubwa zaidi ya Wabunge katika kutetea haki zao, kudai maendeleo na kurutubisha mapato na hali za maisha yao.​

Lakini jinsi CHADEMA walivyowasilisha huu mchakato wa Sera ya Majimbo, kuna upungufu mkubwa sana wa kisera na kiutendaji ambao unaifanya Sera hii iwe Butu na hata Batili.​

Chadema wamefanya kazi nzuri kubainisha mapungufu na matatizo ya migongano ya kiutawala katika nazi za mikoa wilaya na hata Serikali za mitaa kutokana na mvutano wa kiimla, kiutendaji na nguvu za kiutawala.​

Walichoshindwa Chadema kukifanya katika kuwasilisha maoni yao kwa Wananchi, ni kuonyesha ni jinsi gani mfumo wao wa Utawala wanaoupendekeza unaweza kuleta ufanisi na kuhamasisha uzalishaji mali na kuwa kichocheo cha maendeleo. Aidha wameshindwa kuoanisha mfumo wao kwa kutoa ama takwimu au vitendea kazi ambavyo vinaweza kuonyesha kuwa mfumo wao utakuwa bora kuliko wa sasa wa kiutawala.​

Zaidi, Chadema wameshindwa kuwa makini kwa kujikanganya mno katika kubainisha chimbuko la kudumaa kwa maendeleo ya Taifa, kudai kuwa mfumo wa uongozi na utawala ni mbaya na hatimaye kudai mfumo wao wa utawala utakuwa ni bora na kwa manufaa ya Taifa na jamii.​

Hii kauli ya Majimbo na hata kuundwa kwa majimo haya katika manifesto ya Chadema ni sawa na ile Sera ya TANU tulioishupalia na kuipiga vita ya Vijiji vya Ujamaa.​

Wengine wenu/wetu, tunashupalia sera lakini bado hatujakaa chini na kuchanganua ni kwa nini bado tuna umasikini, bado hatuna maendeleo madhubuti na kadhalika.​

Kama kawaida yetu, tumejiunga na wale wanaotafuta kila sababu kulaumu kushindwa kwa maendeleo ya Taifa. Tulianza na Fikra za Nyerere, tukaja Siasa ya Ujamaa, tukaegemea kwenye mambo ya Ruksa na sasa ni Ufisadi na Utawala.​

Lakini hizi ni sababu nyingi kama kete za drafti au bao. Hatujakaa chini kujiuliza je Mtanzania anataka maendeleo ya namna gani? hatujamhoji Mtanzania kujua tafsiri yake ya maendeleo ni nini!

Kama Chadema wangetamka kuwa wataboresha mfumo wa uongozi na utawala kwa kutumia vigezo vilivyopo sasa na kuleta maendeleo, ningewaelewa.

Lakini Sera hii ni kama kibwagizo cha kujinadi ili wapewe kura. Kiutendaji, kamwe haitafanikiwa!​

Ili kufanikisha Sera hii ambayo wengine tunaishabikia bila kutafakari kunabidi kwanza kuwepo kwa mabadiliko ya Katiba ya Nchi. Hili Chadema wameligusia juu juu kwa kudai tuliunda katiba ya kumuiga mkoloni, lakini hawajaliweka mbele kuwa ili kuleta mabadiliko ya maana ya Kidemokrasia, Uongozi na Utawala ili Taifa liweze kuanza safari mpya ya maendeleo ni kubadilisha Katiba. Chadema hawajathubutu hata kidogo kuonyesha wazi kuwa kuna haja ya kuwa na Katiba mpya kwanza ambayo itasawazisha makosa yaliyopo sasa hivi ambayo yanadumaza maendeleo ya Taifa, yanapunguza Uwajibikaji na kuwa na Serikali yenye Nguvu nyingi zisizo milikiwa na Wananchi.​

Chadema hawajazungumzia wazi kwa wananchi kuwa mfumo huu ni Utashi wao (Chadema) na si wa Wananchi au mjumuiko wa Vyama vya Kisiasa. Sijawahi sikia kuwa Chadema walikusanya kura za maoni na kuwauliza Watanzania wanataka mfumo gani wa Utawala au Ushirikishi. Hivyo basi, Chadema wanataka kunda Sera ya kujenga mfumo mpya wa Utawala ambao kikija Chama kingine cha Siasa ambacho hakikubaliani na mfumo huo, basi Watanzania itabidi tujifunge mikanda na kujiandaa kuishi na kuongoza na mfumo mpya wa Kiserikali. Na hili ndilo linaloonekana wazi kuwa Chadema haikubaliani na mfumo wa sasa ambao tuliuunda baada ya Uhuru.​

Ama Chadema haitamki rasmi na wazi gharama kubwa za kuwa na mfumo kama huu. Chadema haitamki hatima ya hiyo mikoa ambayo itakusanywa kama fungu la nyanya kuunda Jimbo. Je Chadema imefanya tathmini gani kuona kuwa Singida na Dodoma ziko tayari kuunda Serikali ya mseto ya Jimbo? Je ni mfumo gani utatumika kugawa madaraka kwa hii mikoa itakayounda jimbo?​

Nitaleta jambo moja ambalo laweza kumuamsha Mkandara na kunikoromea, lakini hili ni muhimu wakati tunatafakari huku kuundwa kwa majimbo.​

Kanisa la Kilutheri Tanzania (KKKT) lilikuwa na majimbo (Dayosisi na Sinodi) ambayo yalikuwa sawa na hayo majimbo nane yanayotangazwa na Chadema. Baada ya miaka nenda rudi, waumini katika majimbo hayo, wakakataa kuwepo kwa muungano wa mikoa na hovyo kuishia karibu kila mkoa au sehemu kuunda jimbo (Dayosisi au Sinodi) yake!​

Je tutaweza kuwaweka Wahaya, Wakurya,Wakerewe, Wajaluo, Wajita Wasukuma na Wanyamwezi kama Jimbo moja?​

Chadema inazungumzia rasilimali na mapato yatumike kwa majimbo yaliyovuna. Hili ni sawa, lakini bado Chadema haijatueleza ni vipi Serikali kuu itajiendesha ama kuratibu Uendeshaji wa majimbo na hata mapato ya Taifa.​

Chadema inasema Serikali kuu itakuwa na Wizara nne tu, Hata Marekani yenye Majimbo/Mikoa 50 yanayojiendesha yenyewe, Serikali kuu inaongozwa na kadiri Wizara 12 za kudumu. Sisi tutajenga nchi gani isiyo na wizara ya mawasiliano na miundo mbinu, wizara ya sheria, wizara ya afya, wizara ya elimu, wizara ya biashara na viwanda, wizara ya kilimo? Ni nchi gani au Serikali gani ya Kitaifa tutaijenga yenye wizara za mambo ya nje, mambo ya ndani, fedha na ulinzi pekee?​

Huu ni udhaifu mkubwa sana ambao Chadema wanaonyesha katika kujiuza kwa wananchi na kama hili ndilo tegemeo lao kushika madaraka na kuongoza nchi, basi Mtanzania atasema heri tuendelee na CCM yetu maana hawa Chadema hawaeleweki.​

Kinachotakiwa si kubadilisha mfumo kila mara tunapoona mambo hayaendi sawa na yanakwenda kombo. La kujiuliza ni hili, je Chadema kwa kutumia mfumo uliopo watahakikishaje kuwa Ufanisi, Uwajibikaji, Ubunifu, Uchapa kazi, Mipango bora na Uadilifu vinakuwa ndio vigezo kamili vya kuleta maendeleo kwa Taifa letu?​

Mike Huckabee amesema juzi kuwa kama Wananchi hawawezi kujidhibiti, kujisukuma na kujitawala kwa uadilifu na kuchapa kazi, kamwe hawatakuwa huru na kuwa na maendeleo, hishia kuwa na Serikali inayoburuza, kuratibu na kutawala kwa nguvu ma kuamuru kila kitu.​

Tunahitaji sera na mwamko wa Uongozi ambao unafuata Haki, unajali Utu, ni Fanisi, Hodari, Nyenyekevu, Mahiri, Wenye Juhudi, Wajibikaji, Fuatiliaji, Bunifu, yenye Uwazi na hamasishaji. Hatuhitaji mfumo mpya wa Kiutawala ikiwa matokeo yatakuwa ni yale yale kwa kushindwa kutibu magonjwa yaliyopo.​

Hii makala/reply yako inachanganya sana Reverand!

Kwenye highlight!

Umezungumzia neno "maendeleo" mara nyingi mno!
Umezunguka wee...CHADEMA hivi CHADEMA vile!
Sasa inaonyesha kuwa unajichanganya..Hapo kwenye red highlight unadai wewe pia hujui nini ni maendeleo!
At the same time kwenye hihglights nyeusi umeonekana kuwa unayajua sana maendeleo!
Tena especially pale inapokuja kwenye yale maendeleo unayoyajua wewe ambayo CHADEMA hawawezi kuyaleta!
Yani hii ni kama ile speech ya Kikwete kule Singida amabayo kwa maoni yangu ni the worst of all times!
 
Hii makala/reply yako inachanganya sana Reverand!

Kwenye highlight!

Umezungumzia neno "maendeleo" mara nyingi mno!
Umezunguka wee...CHADEMA hivi CHADEMA vile!
Sasa inaonyesha kuwa unajichanganya..Hapo kwenye red highlight unadai wewe pia huji nini ni maendeleo!
At the same time kwenye hihglights nyeusi umeonekana kuwa unayajua sana maendeleo!
Tena especially pale inapokuja kwenye yale maendeleo unayoyajua wewe ambayo CHADEMA hawawezi kuyaleta!
Yani hii ni kama ile speech ya Kikwete kule Singida amabayo kwa maoni yangu ni the worst of all times!

Mushi,

Kwa nini unakuwa mgumu kutuliza bongo na kufikiri kauli za watu? Nimesoma majibu yote anayokupa Mkandara ambayo yanafanana na hoja yangu, lakini ni upofu wa makusudi ndio unaokusumbua.

Nilikuambia kule kwenye Tanzania Rich or Poor, take time to read, understand the speaker and know the speaker well, before you jump into conclusion and respond.

Moelex kakufundisha vizuri sana, hata Biskuti kabainisha wazi kuwa usipoona vijineno fulani katika hoja, unakimbilia kusema hoja ni hewa.

Mimi nimesoma huo mchakato mzima walioletya Chadema and I am being honest kuwa ni Batili na Pungufu.

Acha kuchagua maneno ya kuwekea mkazo na rangi bwana. Soma hoja uelewe.

Mimi naandika kwa nafsi nyingi na si yangu pekee (kumbuka somo la fasihi?). Naelewa maendeleo ni nini na kwa nini Tanzania haina maendeleo. Ndio maana katika aya yangu ya mwisho nauliza kama hakuna ufanisi na uwajibikaji, kuna maana gani kuja na mfumo mpya wa utawala?

Read son, read!
 
Mkuu Kishoka,

Kwenye majimbo tukiingiza ukabila basi kamwe hayatafanikiwa, lakini tukisema majimbo haya ni ya Watanzania bila kujali wanatoka kabila lipi basi naamini yanaweza kuwa na mafanikio makubwa zaidi hasa kama watapewa uhuru mkubwa wa kujiamulia mambo ambao wakuu wa mikoa hawana. Mfano wa mafanikio ya Watanzania ni hii JF, imagine hapa ukumbini kama tungeweka mbele ukabila badala ya Utanzania, sidhani kama JF ingekuwa na mafanikio makubwa kama iliyoyapata hadi sasa.

Bubu,

Ukabila ni natural instinct sawa na Udini, Usomi na Utabaka. We ca not avoid them. Baya Zaidi ni kuwa pamoja na intergration kubwa ya Jamii ya Watanzania through iner marriage za makabila na dini, bado kuna egemeo kubwa sana la ukabila.

Mkandara kaongea vizuri sana hilo la Msukuma na Dhahabu na Almasi kumsaidia Mhaya na Mkurya na ndizi na ng'ombe zao!

Tanzania imefanikiwa sana kwa kuishi kama Tanzania bula makundi ya Ukabila. Tumejisahau na kupuuzia suala la udini ambalo chimbuko lake nalo ndio lile lie tatizo kuu la Taifa, Maendelo ya watu.
 
Mushi,

(1)Kwa nini unakuwa mgumu kutuliza bongo na kufikiri kauli za watu? Nimesoma majibu yote anayokupa Mkandara ambayo yanafanana na hoja yangu, lakini ni upofu wa makusudi ndio unaokusumbua.

(2)Nilikuambia kule kwenye Tanzania Rich or Poor, take time to read, understand the speaker and know the speaker well, before you jump into conclusion and respond.

(3)Moelex kakufundisha vizuri sana, hata Biskuti kabainisha wazi kuwa usipoona vijineno fulani katika hoja, unakimbilia kusema hoja ni hewa.

Mimi nimesoma huo mchakato mzima walioletya Chadema and I am being honest kuwa ni Batili na Pungufu.

Acha kuchagua maneno ya kuwekea mkazo na rangi bwana. Soma hoja uelewe.

Mimi naandika kwa nafsi nyingi na si yangu pekee (kumbuka somo la fasihi?). Naelewa maendeleo ni nini na kwa nini Tanzania haina maendeleo. Ndio maana katika aya yangu ya mwisho nauliza kama hakuna ufanisi na uwajibikaji, kuna maana gani kuja na mfumo mpya wa utawala?

Read son, read!

Najaribu kuona kama kuna maana!
Sasa mimi nasoma lakini si ni lazima uwe na thesis?

1)Umenichekesha sana hapo unapodai kuwa mnakubaliana na Mkandara!
Weka hoja usitafute kukubaliana tu!
Tunakubaliana baada ya wote kuleta hoja!
Kama vile nilivyokubaliana na molex pamoja na kina Mkandara on some issues!

2)Kule kwenye ile mada ya Rich or Poor..Wewe ndio ume jump kwenye conclusion!
Kumbuka kuwa msingi wa mjadala ule ni ulitokana na comments za viongozi wetu pamoja na other dignitaries the way they perceive our country's well being.
Je hujui kuwa kauli zao zilikuwa zinatofautiana as to whether we're rich or poor?
Kauli ya muungawana, kauli ya Dr Slaa na kauli ya R.Mengi.

3)Hivyo vijineno unavyotaka nivione si ndio hivyo ninavyo vihighlight?
Na ndio maana nikasema post yako inafana na ile siku JK aliposema viongozi wasijali kuitwa mafisadi,kuwa waongezewe pesa huku akisema sisi ni masikini!
Wewe umezungumzia maendeleo huku ukidai huyajui maendeleo na huku uki suggest kuwa wananchi waulizwe maendeleo ni nini..Sasa what is what?
We unataka kuniambia wananchi bado hawajui kuwa maendelo ni nini?
Ama wewe huwezi kuwasaidia na kuwaambia kuwa maendeleo ni nini?
 
Ubatili na Ubutu wa Sera ya Chadema ya Majimbo

Chadema wana nia nzuri ya kuleta maendeleo kwa Wananchi na Taifa. Dhana ya kuwa na serikali za mitaa zilizo na nguvu kwa ajili ya maendeleo ya wananchi ni nzuri. Ama kuwepo kwa Serikali za Mikoa/Majimbo ambayo zinatokana na msukumo wa Wananchi wenyewe na si Uteuzi wa Ikulu pia ni jambo jema na ni wakati muafaka wa Wananchi kuwa na sauti kubwa zaidi ya Wabunge katika kutetea haki zao, kudai maendeleo na kurutubisha mapato na hali za maisha yao.​

Lakini jinsi CHADEMA walivyowasilisha huu mchakato wa Sera ya Majimbo, kuna upungufu mkubwa sana wa kisera na kiutendaji ambao unaifanya Sera hii iwe Butu na hata Batili.​

Chadema wamefanya kazi nzuri kubainisha mapungufu na matatizo ya migongano ya kiutawala katika nazi za mikoa wilaya na hata Serikali za mitaa kutokana na mvutano wa kiimla, kiutendaji na nguvu za kiutawala.​

Walichoshindwa Chadema kukifanya katika kuwasilisha maoni yao kwa Wananchi, ni kuonyesha ni jinsi gani mfumo wao wa Utawala wanaoupendekeza unaweza kuleta ufanisi na kuhamasisha uzalishaji mali na kuwa kichocheo cha maendeleo. Aidha wameshindwa kuoanisha mfumo wao kwa kutoa ama takwimu au vitendea kazi ambavyo vinaweza kuonyesha kuwa mfumo wao utakuwa bora kuliko wa sasa wa kiutawala.​

Zaidi, Chadema wameshindwa kuwa makini kwa kujikanganya mno katika kubainisha chimbuko la kudumaa kwa maendeleo ya Taifa, kudai kuwa mfumo wa uongozi na utawala ni mbaya na hatimaye kudai mfumo wao wa utawala utakuwa ni bora na kwa manufaa ya Taifa na jamii.​

Hii kauli ya Majimbo na hata kuundwa kwa majimo haya katika manifesto ya Chadema ni sawa na ile Sera ya TANU tulioishupalia na kuipiga vita ya Vijiji vya Ujamaa.​

Wengine wenu/wetu, tunashupalia sera lakini bado hatujakaa chini na kuchanganua ni kwa nini bado tuna umasikini, bado hatuna maendeleo madhubuti na kadhalika.​

Kama kawaida yetu, tumejiunga na wale wanaotafuta kila sababu kulaumu kushindwa kwa maendeleo ya Taifa. Tulianza na Fikra za Nyerere, tukaja Siasa ya Ujamaa, tukaegemea kwenye mambo ya Ruksa na sasa ni Ufisadi na Utawala.​

Lakini hizi ni sababu nyingi kama kete za drafti au bao. Hatujakaa chini kujiuliza je Mtanzania anataka maendeleo ya namna gani? hatujamhoji Mtanzania kujua tafsiri yake ya maendeleo ni nini!

Kama Chadema wangetamka kuwa wataboresha mfumo wa uongozi na utawala kwa kutumia vigezo vilivyopo sasa na kuleta maendeleo, ningewaelewa.​

Lakini Sera hii ni kama kibwagizo cha kujinadi ili wapewe kura. Kiutendaji, kamwe haitafanikiwa!​

Ili kufanikisha Sera hii ambayo wengine tunaishabikia bila kutafakari kunabidi kwanza kuwepo kwa mabadiliko ya Katiba ya Nchi. Hili Chadema wameligusia juu juu kwa kudai tuliunda katiba ya kumuiga mkoloni, lakini hawajaliweka mbele kuwa ili kuleta mabadiliko ya maana ya Kidemokrasia, Uongozi na Utawala ili Taifa liweze kuanza safari mpya ya maendeleo ni kubadilisha Katiba. Chadema hawajathubutu hata kidogo kuonyesha wazi kuwa kuna haja ya kuwa na Katiba mpya kwanza ambayo itasawazisha makosa yaliyopo sasa hivi ambayo yanadumaza maendeleo ya Taifa, yanapunguza Uwajibikaji na kuwa na Serikali yenye Nguvu nyingi zisizo milikiwa na Wananchi.​

Chadema hawajazungumzia wazi kwa wananchi kuwa mfumo huu ni Utashi wao (Chadema) na si wa Wananchi au mjumuiko wa Vyama vya Kisiasa. Sijawahi sikia kuwa Chadema walikusanya kura za maoni na kuwauliza Watanzania wanataka mfumo gani wa Utawala au Ushirikishi. Hivyo basi, Chadema wanataka kunda Sera ya kujenga mfumo mpya wa Utawala ambao kikija Chama kingine cha Siasa ambacho hakikubaliani na mfumo huo, basi Watanzania itabidi tujifunge mikanda na kujiandaa kuishi na kuongoza na mfumo mpya wa Kiserikali. Na hili ndilo linaloonekana wazi kuwa Chadema haikubaliani na mfumo wa sasa ambao tuliuunda baada ya Uhuru.​

Ama Chadema haitamki rasmi na wazi gharama kubwa za kuwa na mfumo kama huu. Chadema haitamki hatima ya hiyo mikoa ambayo itakusanywa kama fungu la nyanya kuunda Jimbo. Je Chadema imefanya tathmini gani kuona kuwa Singida na Dodoma ziko tayari kuunda Serikali ya mseto ya Jimbo? Je ni mfumo gani utatumika kugawa madaraka kwa hii mikoa itakayounda jimbo?​

Nitaleta jambo moja ambalo laweza kumuamsha Mkandara na kunikoromea, lakini hili ni muhimu wakati tunatafakari huku kuundwa kwa majimbo.​

Kanisa la Kilutheri Tanzania (KKKT) lilikuwa na majimbo (Dayosisi na Sinodi) ambayo yalikuwa sawa na hayo majimbo nane yanayotangazwa na Chadema. Baada ya miaka nenda rudi, waumini katika majimbo hayo, wakakataa kuwepo kwa muungano wa mikoa na hovyo kuishia karibu kila mkoa au sehemu kuunda jimbo (Dayosisi au Sinodi) yake!​

Je tutaweza kuwaweka Wahaya, Wakurya,Wakerewe, Wajaluo, Wajita Wasukuma na Wanyamwezi kama Jimbo moja?​

Chadema inazungumzia rasilimali na mapato yatumike kwa majimbo yaliyovuna. Hili ni sawa, lakini bado Chadema haijatueleza ni vipi Serikali kuu itajiendesha ama kuratibu Uendeshaji wa majimbo na hata mapato ya Taifa.​

Chadema inasema Serikali kuu itakuwa na Wizara nne tu, Hata Marekani yenye Majimbo/Mikoa 50 yanayojiendesha yenyewe, Serikali kuu inaongozwa na kadiri Wizara 12 za kudumu. Sisi tutajenga nchi gani isiyo na wizara ya mawasiliano na miundo mbinu, wizara ya sheria, wizara ya afya, wizara ya elimu, wizara ya biashara na viwanda, wizara ya kilimo? Ni nchi gani au Serikali gani ya Kitaifa tutaijenga yenye wizara za mambo ya nje, mambo ya ndani, fedha na ulinzi pekee?​

Huu ni udhaifu mkubwa sana ambao Chadema wanaonyesha katika kujiuza kwa wananchi na kama hili ndilo tegemeo lao kushika madaraka na kuongoza nchi, basi Mtanzania atasema heri tuendelee na CCM yetu maana hawa Chadema hawaeleweki.​

Kinachotakiwa si kubadilisha mfumo kila mara tunapoona mambo hayaendi sawa na yanakwenda kombo. La kujiuliza ni hili, je Chadema kwa kutumia mfumo uliopo watahakikishaje kuwa Ufanisi, Uwajibikaji, Ubunifu, Uchapa kazi, Mipango bora na Uadilifu vinakuwa ndio vigezo kamili vya kuleta maendeleo kwa Taifa letu?​

Mike Huckabee amesema juzi kuwa kama Wananchi hawawezi kujidhibiti, kujisukuma na kujitawala kwa uadilifu na kuchapa kazi, kamwe hawatakuwa huru na kuwa na maendeleo, hishia kuwa na Serikali inayoburuza, kuratibu na kutawala kwa nguvu ma kuamuru kila kitu.​

Tunahitaji sera na mwamko wa Uongozi ambao unafuata Haki, unajali Utu, ni Fanisi, Hodari, Nyenyekevu, Mahiri, Wenye Juhudi, Wajibikaji, Fuatiliaji, Bunifu, yenye Uwazi na hamasishaji. Hatuhitaji mfumo mpya wa Kiutawala ikiwa matokeo yatakuwa ni yale yale kwa kushindwa kutibu magonjwa yaliyopo.​

Umetaja neno maendeleo mara kumi na mbili lakini bado hujui maana yake?
Yani Reverand hapo juu ni vurugu tupu..Jipange upya!
Tukubali na kutokukubaliana sometimes...Haina shida..Saa nyingine tunaongozwa na mapenzi yetu binafsi..Ni ngumu kusema kweli!DUH!
 
Maendeleo ya Taifa letu yataletwa si kwa mgawanyo mpya wa makazi au mfumo wa uendeshaji. Yataletwa kwanza na Utashi wa wananchi kuwa na haya maendeleo kwa kutoa tafsiri na maana halisi ya maendeleo.

Kila jamii na jumuiya zina tafsiri tofauti sana za Maendeleo. Nitatoa mfano mmoja ambao ni wa karibu.

Wazazi wangu ni wa makabila mawili tofauti na yako mikoa mbali kabisa haipakani.

Alikozaliwa Mama yangu, tangu nikiwa mtoto, kulikuwa na umeme wa Jenereta, simu ya mkorogo, barabara ya vumbi, maji ya bomba na familia ilijimudu kwa shughuli za Kilimo. Leo hii, barabara ni ile ile, umeme ni wa Tanesco, simu ya kawaida, uzalishaji mali umeongezeka kwa babu na bibi yangu pamoja na majirani, lakini maisha yao ni yale yale ya miaka 35 iliyopita. Jamii na jumuiya ya sehemu alikotoka Mama yangu, imeridhika na ilichonacho ikiwa ni pamoja na zahanati, shule na miundo mbinu ile ile, ingawa kwa kipato wametajirika.

Kwa Baba yangu, hali ya miaka 50 iliyopita ni ile ile. Hakuna maji ya bomba, inabidi utembee maili moja kwenda mtoni au kisimani kuchota maji, Shule iliyoletwa na mkoloni ni ile ile hakuna msukumo wa asili wa Wananchi kutaka shule au zahanati, barabara ni vumbi bovu kukatiza kwenye mashamba, hakuna umeme au mkumo wa kuwa hata na umeme wa jenereta na zaidi na baya kuliko yote, ni kule kuridhika kwa jamii hii na majirani wao (vijiji mpaka wilaya) kwa maisha ya namna hii.

Labda mtasema ni mifano batili au si endelevu. Nitarudi Dar Es Salaam nilikokulia ambako ndipo tunadai kinara cha maendeleo ya Taifa kwa tafsiri zetu za maendeleo kuwa Barabara za lami, nyumba za tofali nabati la chuma, hospitali, shule, maji ya bomba na kuweko kwa tabaka la kati (middle class).

Hapa Dar, kuna mkusanyiko wa kila kitu wa maendeleo, elimu, afya, mali, nyumba bora na kadhalika. Lakini pamoja na kuwepo na vigezo hivi, bado kuna sehemu kubwa ya Wakazi wa Dar na vijiji jirani ambao mapokeo yao na tafsiri ya maendeleo si sawa.

Mfano, nina shamba na nimejenga nyumba yangu. Maji yangu ni kutokana na kuchimba bwawa na kujenga kisima. Mimi ni "msomi" mwenye upeo wa Maendeleo. Nimeleta haya "maendeleo" kijijini kwangu Boko. Lakini majirani zangu ambao ndiyo waliniuzia shamba na kiwanja, wao bado wanakataa kujishughulisha na shughuli za kufanya kazi za kuwapa kipato cha ziada ili waishi kwenye nyumba "bora" wawe na maji "safi" na kuwa wazalishaji mai mahiri.

Sasa kama wao wameridhika na hali zao za maisha kwa kukaa kwenye nyumba ya udongo na makuti, wakifurahia heka yao moja ya mhogo na mbaazi na wakikataa kulima heka kumi ambazo wana uwezo, je tutasema nini maana ya Maendeleo kwao?

Hivyo basi, ni lazima na ni wajibu wa sisi kama Taifa kutoa maana ya Maendeleo na kuoanisha na malengo ya kujenga Taifa letu.

Kwangu mimi na kama ningekuwa Chadema, sasa hivi kampeni yangu ingekuwa si kuunda mfumo mpya na kudai kuwa mfumo mpya utaleta maendeleo. Bali ningewekeza nguvu zangu kuonyesha umma wa Watanzania kuwa Chadema inaweza kufanya kazi borakuliko CCM ya kuleta Maendeleo na kuimarisha kipato cha Taifa ili upatikanaji wa huduma muhimu kwa jamii na taifa kama elimu, afya, maji , ajira an bei bora za mazao zitainua kipato cha Mtanzania kwa kutumia vitendea kazi vilivyopo.

Ningekuwa mimi Chadema, nisingetaka kuingia madarakani na kuchukua uongozi kwa kuuza sera mpya wakati sera zilizopo kilichoshindikana si sera bali ni ufanisi bora na uongozi mahiri wenye juhudi na maarifa kuleta maendeleo kwa Taifa.

Ningekuwa Chadema ningejiuza kwa kusema ni vipi ningeweza kutimiliza maendeleo ya nchi na mipango yote kama Mkukuta na mingineyo kwa kutumia hata Ilani ya CCM na kubainisha kuwa nina uwezo na motisha wa kufanikisha malengo hayo kwa ubora na ufanisi kuliko CCM.

Kuleta sera mpya ni kulizuga Taifa na kama Moelex alivyosema ni kuwachanganya Watanzania!

Lets focus to improve what we have at hand before we introduce something new!

Na kazi ya kwanza kuhakikisha Chadema, CUF, NCCR au TLP ni kuwaambia Watanzania, je watafanya nini ambacho ni bora kuliko CCM, practical items on board and not impractical plans!
 
Umetaja neno maendeleo mara kumi na mbili lakini bado hujui maana yake?
Yani Reverand hapo juu ni vurugu tupu..Jipange upya!
Tukubali na kutokukubaliana sometimes...Haina shida..Saa nyingine tunaongozwa na mapenzi yetu binafsi..Ni ngumu kusema kweli!DUH!

Mushi,

Unahakika wa unachoongelea? Nimekuuliza unaelewa maana ya fasihi? unaelewa maana ya abstract language? kwa nini unaendelea kujidhalilisha namna hii? Hivi mwalimu wako darasani anakufikiriaje?

Son, you need to calm the anxiety and try to comprehend what is at stake, take time to understand what is being said, absorb what is being stated before you make up your mind!
 
Back
Top Bottom