jmushi!, Swala la Richmond halikuwa swala la taifa hata kama lingekuwa ktk serikali ya majimbo bado ni tatizo la mkoa wa Dar es salaam.
Sasa kama hawa viongozi wanaoendesha nchi nzima ndio mafisadi kisha tugawe nchi ktk majimbo kuwapa nafasi hata mafisadi wadogo kushika madarakka ya juu ktk kila Jimbo who will be responsible ikiwa leo hii swala dogo kaa la Richmond la mkoa ambalo tunashindwa kulishughulikia Kitaifa?..
Mkuu sijasema kwamba majimbo yatakuwa na mamlaka ya maswala ya Taifa isipokuwa nachojaribu kujenga hapa hoja yangu ni sawa na kusema hivi;- Tatizo letu kubwa la kiuchumi ni Uongozi wetu wala sio wa mtu mmoja isipokuwa viongozi wote wa juu kutowajibika. Tumewaona kina Yona, Karamagi, Lowassa, na pengine naweza sema mawaziri wote walioachishwa nafasi zao za Uongozi kumetokana na utendaji wao wa kazi na sio nguvu ya rais..
katika serikali ya Majimbo kina Karamagi watakuwepo bado kitaifa na poengine kuzaa kina Karamagi wengine ktk Majimbo kwa sababu kazi inayotakiwa kufanyika ni ile ile.
Nitakubali Majimbo ikiwa kuna utafiti wa kisayansi unaodhihirisha wazi kuwa kina Lowassa na kundi zima walishindwa kazi zao kutokana na ukubwa wa nchi ama system nzima iliyopo sasa hivi..badala ya kuwapa watu hawa nafasi wapate kuwa marais wadogo wa kanda zetu kwani wapo kina Karamagi wengi tu wanasubiri nafasi kama hizi. na ndio maana nikatoa mfano wa hizi Halmashauri za miji tulizojenga sasa hivi kuwa na madaraka ktk maendeleo ya sehemu zao zimegeuka kuwa sehemu baabu kubwa za Ulaji. Kila kijana leo hii Tanzania anatafuta kupata kazi City kwa sababu kuna Ulaji mkubwa. Nenda huko wilayani, Madiwani siku hizi wanajirusha na kuonekana wenye fedha yote haya ni matokeo ya kumpa mamlaka mtoto wa Fisadi...Barabara hazijengwi hadi utakapo fika wakati wa uchaguzi, yale mabillioni ya Kikwete yameliwa vibaya sana na viongozi wadogo wa mikoa ambao kesho watakuwa na madaraka zaidi chini ya serikali ya Majimbo....
Hivyo problem sio majimbo ila ni watu wenyewe na sio kusema ati nguvu ya rais peke yake ndio tatizo bali mfumo mzima wa sheria kutoheshimu rule of law kwa sababu ya kipengele kidogo kilichoundwa na serikali ya CCM kuweka maazimio kama Azimio la Zanzibar..
Ondoeni kwanza UFISADI, jenga mfumo wa uwazi na good governance kwa sababu Utawala bora haujengwi na mipaka bali watu wenyewe...
Kwa hao wanaosema Utawala wa mtu mmoja kuwa rais wanchi nzima sielewi hata wanachojaribu kusema hapa kwa sababu zipo nchi kibao zinazoendelea mfumo huo na wamefanikiwa. Binafsi siamini kabisa kwamba Botswana ingeweza kuwa na tofauti mbili za kiuchumi kama ingekuwa na mfumo fulani wa kuigawa/ kuunganisha nchi hiyo kwa mipaka yake, kwa sababu hawa jamaa zetu viongozi wake ni wawajibikaji kwanza na wote abide by the rule of law..hakuna Mungu mtu isipokuwa hapa kwetu Tanzania ambako tumeona haya yakijijenga taratibu mbele ya macho yetu. Kesho tukiumba Miungu wengine wadogo sidhani kama itaongeza uadilifu..
Enzi za mwalimu viongozi wetu waliheshimika lakini sasa hivi viongozi wetu wanaogopwa!.. Kwa mtazamo wa haraka unaweza sema tunawaheshimu kumbe kuogopa sio kabisa kuheshimiwa...