CHADEMA yaiiga ODM kuhusu Sera ya Majimbo

CHADEMA yaiiga ODM kuhusu Sera ya Majimbo

chadema wamecherewa pwere
Hoja imeshawekwa mezani,unatakiwa utoe mchango kama demokrasia shirikishi inavyotaka.Kwa maoni yangu nafikiri baado unakumbatia mawazo ya viongozi kuhodhi fikra, hawa wamekufungulia utoe mawazo ya kuboresha mfumo bora wa wananchi kushiriki kwenye utawala wao wa kujiamulia mustakabali wao wa kisiasa,kijamii na kiuchumi.Naomba tufungue fikra zetu,tuache kufikiri kuwa viongozi wetu ndiyo wanastahili kufikri kwa niaba yetu. Njia ya viongozi kufikiri kwa niaba ya wananchi ilifanikiwa Singapore tu, chini ya Gen.Lee Kwan Yue na hamna sehemu nyingine ilikofanikiwa.Hivyo Ndugu yangu,Mtu wa Pwani anza wewe kujenga fikra za kujitegemea kimawazo ili uisaidie jamii kufikia maendeleo endelevu.
 
Naona Chadema wanataka kutimiza azma yao ya kuigawa nchi kabisaaaa
 
Na je,

Sehemu masikini Tanzania zitabaki bila maendeleo? Huu ni ubaguzi tu
 
Naona Chadema wanataka kutimiza azma yao ya kuigawa nchi kabisaaaa

Wana ccm sasa mnadhani kuwa mmepata pa kutokea. Kuigawa nchi ndio una maana gani hapa. Hoja hapa ni kuweka juhudi za maendeleo karibu na wananchi zaidi kuliko sasa hivi ambapo pesa zote zinakwenda hazina ili kutumiwa na ccm kwenye chaguzi hapo Tanzania.
 
Hapo m/kike umegonga penyewe, Nadhani kati ya mapungufu makubwa yaliyopo kwa mfumo wa sasa ni hii ya kukusanya kwenye kapu moja toka kila kona ya TZ afu ndo watu wachache waamue wanavo jisikia jinsi ya kurudisha makusanyo huku chini kwa kadri wanavo jisikia!

Hii imekuwa ikitoa mwanya kwa waroho wachache kujichotea wapendavo hela zetu! na kuto toa mwanya kwa mkazi wa Kasulu/Nanyamba/Nafuba kuelewa kinacho endelea juu ya pesa yake anayo tozwa kila kukicha!

Mambo ya ubinafsi wa mtu kuamua kwamba kwa vile ana madaraka ijengwe barabara fulani/viwanja vya ndege hata mahali ambapo si pa muhimu sana nadhani yatapungua kwa mfumo huu wa majimbo.
 
Mkuu Mnyika na Zitto ahsanteni sana kwa maelezo yenu.

Maswali:::::

1) Hivi kweli mko kwenye academic exercise au mnataka kuongoza nchi???
Hii issue ya majimbo ibaki kama research project tu lakini kwa Tanzania ni Dead on arrival. Kama ni kudiscuss tu pros/cons nakubali muendelee kudiscuss lakini kusema muanze kuwaeleza wananchi wakati huu ni wazimu wa hali ya juu na ukosefu wa kuelewa hasa nini wananchi wa Tanzania wanakihitaji.

2) Gharama za serikali ya majimbo itakuwa kubwa mno mpende msipende, kwa sababu mnaact as if serikali ya Tanzania sasa hivi ina balanced budget. Tunategemea wafadhili kwa asilimia 50%, sasa mnaposema majimbo yatajitegemea kutoka tax base ipi??? Kurun mabunge ya majimbo, kurun serikali za majimbo, kurun bunge la jamhuri, zanzibar blah blah hizo gharama hamzioni???

3) Yaani katika option zote za kudeal na CCM, hii ndio the best??

Hamna hata wabunge 10%, mnataka kubadilisha mfumo mzima from which mandate???
Kwa nini kama kweli nyie mnauelewa mkubwa, kwa nini mnashindwa kuchukua hata majimbo 5 katika nchi nzima?? How can U guys turn around and dare to say we want to change the whole system???

4) Issue kubwa sasa hivi ni rasilimali na uchumi wa nchi, mkishindwa kutokea hapo, TRUST ME mtakuwa mmepoteza upenyo ambao sijui utatokea lini tena.

Hivi kweli wale ndugu zangu pale Moshi, wakati huu suala la chakula la dunia na mafuta yanavyopanda, badala ya kuwahimiza kuwa kilimo kifufuliwe na rasilimali za nchi zisiibwe, unawaletea oh Jamani eeh kuna mfumo wa majimbo, AMA KWELI ISHI UONE VIOJA!!!!

Also for the sake of argument, let us look at this scenario::::

Sera ya Majimbo imekubalika na ndio sera ya Tanzania. What next?? Si CCM itashinda hayo majimbo na mabunge yake kama inavyoshinda sasa hivi, wabunge na madiwani?? Sasa kwa nini mnahangaika na suala gumu kama la majimbo ambalo hata kama likikamilika, still CCM ndio washindi??

Kwa nini system ya madiwani ambayo kwa kweli ndio iko karibu mno na wananchi, hamutafuti njia za kushinda huko??? Mkishinda hata Halmashauri say 50, kati ya hizo 100+, labda ndio muanze kuongelea mambo mengine.

sorry guys kwa maneno ya jazba, BUT I CAN NOT FATHOM WHAT U GUYS ARE TRYING TO DO> IT is a FIASCO OF BIBLICAL PROPORTION.
 
Zitto,
Premiers wa Mikoa (Gavana wa Majimbo) watakuwa wanawajibika kwa Baraza la Wawakilishi la Mikoa. Wawakilishi watapatikanaje? Hili suala la kufikriria kidogo. Mimi ushauri wangu ni kuwa Tarafa za sasa ziwe ni majimbo ya kuchagua wawakilishi katika Baraza la Kutunga sheria la Mkoa.

Hivyo kwa ufupi tutakuwa na vyombo vifuatavyo vya kutunga sheria kutokana na maeneo husika.
1. Bunge la Muungano - Dogo lenye wajumbe sawa kutoka Tanganyika na Zanzibar + Wakuu wa Mikoa (Provincial Premiers). Rais wa Muungango na Makamu wake (Makamu wa Rais kuwa Mkuu wa shughuli za Serikali ya Muungano katika Bunge la Muungano- Senate/National Council)
2. Bunge la Zanzibar na Bunge la Tanganyika. Waziri Mkuu Zanzibar na Waziri Mkuu Tanganyika
3. Baraza la Wawakilishi la Mkoa. Premier (Mkuu wa Mkoa)
4. Halmashauri ya Wilaya. Meya Mtendaji (Executive Mayor)

Mkuu nimekuelewa sana isipokuwa Hapa inaonyesha kutakuwa na vyombo vingi vya kutunga sheria ambazo pengine zinaweza kutofautiana mkoa hadi mkoa mbali kabisa hatujachukua serikali mbili kuu na ile ya Kitaifa (Muungano)..
halafu hofu yangu ni pale tutakapo kuwa na Mawaziri wakuu wawili ambao watakuwa chini ya Makamu wa rais, jambo ambalo kidogo linanipa utata jinsi watakavyo patikana hasa kwa kuzingatia uchaguzi mkuu. Kwa mfano sasa hivi tuna Rais, huyo makamu atapatikana vipi kama mgombea mwenza wa rais (mfumo uliopo) au tofauti na hao mawaziri wakuu watapatikana vipi...
Je, ikiwa Zanzibar wakishinda CUF na Bara CCM huo uongozi wa sehemu hizi mbili utakuwa wa aina gani ama ndio huo MSETO wanaozungumzia ktk Muafaka. Kidogo napata utata kuona mawaziri wakuu wawili ambao hadi sasa hivi sielewi upana wa kazi zao ktk serikali za ndani na ile ya Muungano..

Halafu mkuu bado nashindwa kuelewa haswa sababu kubwa ya kufikiriwa jambo hili ikiwa leo tunazo serikali kuu na zile za mitaa, zoezi ambalo ndiuo changa na linahitaji marekebisho kabla hatujafikia Uamuzi kuwa haiwezekani kutegemea fedha toka serikali kuu..Unajua mkuu mimi natazama sana makampuni makubwa ya huku ambayo yameweza kutawanyika dunia nzima kwa lengo la kuwafikia wananchi kirahisi lakini kamwe hawawezi kuweka maamuzi muhimu ya maendeleo ya kampuni hizo chini ya viongozi wa nchi hizo bado makao makuu wanayo nguvu kubwa ya kusukuma maendeleo ya kampuni hizo...
Sasa ikiwa kweli sisi tunashindwa kutoa maamuzi ya uwajibikaji ktk nchi ambayo huduma inaweza kufika mahala popote within a day inanipa shida zaidi kutazama mipaka badala ya kutazama viongozi wanaolaza kazi..
Nina mashaka makubwa kwa kiongozi anayeshindwa kutoa maamuzi ya maafa Bagamoyo kuwa ataweza kuwa na urahisi mtu huyo huyo akiundiwa Jimbo kupunguza paper work za taifa zima..
Chukulia maswala ya wale watoto waliokwama Urusi ktk masomo najaribu kuangalia tutaweza vipi kujipanga kukabiliana na swala kama lile ikiwa kila mmoja wao katoka jimbo tofauti...
Na mwisho kweli kabisa inaonekana rahisi sana lakini mkuu ktk utendaji kazi, sera kama hii itachukua miaka 20 kuweza kufanya kazi kwa ufanisi na kama tutakuwa na moyo kama huu wa kukata tamaa mapema wakati serikali za mitaa zimeanzishwa majuzi tu sidhani kama mfumo huo utaweza kudumu kwa sababu moja ya maradhi yetu ni SUBIRA..
Binafsi ninaamini kabisa kuwa hata mfumo huu uliopo unaweza kufanya kazi vizuri sana ikiwa Chadema mtautazama mfumo huu uliopo na kutafuta mapungufu ya mfumo wenyewe ama madaraka ya viongozi wawajibikaji. Kwa mfamo kwanza kuundwa kwa serikali ya Bara kuondoa mgogoro wa Muungano, Kuondoa baadhi ya nguvu za rais ikiwa ni pamoja na kupunguza madaraka ama kuwaondoa kabisa ma RC na DC wasiochaguliwa na wananchi badala yake wachaguliwe na wananchi. Nakumbuka kuna mambo mengi sana tuliwahi kuyajadili humu kama sio Tanzania Economic Forum (TEF) ama Bcstimes kuhusiana na mapungufu ya mfumo mzima wa serikali iliyopo.
 
Moelex23,
Mkuu kwa hakika hiyo ndio hofu yangu kubwa kabisa na kusema kweli nilishindwa kusema wazi kama ulivyofanya.. maneno yako mazito sana yanaweza kuuma lakini that is REALITY.. Mkuu shukran sana umeweza kutoa machungu yangu mimi..
 
Mkuu Mnyika na Zitto ahsanteni sana kwa maelezo yenu.

Maswali:::::

1) Hivi kweli mko kwenye academic exercise au mnataka kuongoza nchi???
Hii issue ya majimbo ibaki kama research project tu lakini kwa Tanzania ni Dead on arrival. Kama ni kudiscuss tu pros/cons nakubali muendelee kudiscuss lakini kusema muanze kuwaeleza wananchi wakati huu ni wazimu wa hali ya juu na ukosefu wa kuelewa hasa nini wananchi wa Tanzania wanakihitaji.

2) Gharama za serikali ya majimbo itakuwa kubwa mno mpende msipende, kwa sababu mnaact as if serikali ya Tanzania sasa hivi ina balanced budget. Tunategemea wafadhili kwa asilimia 50%, sasa mnaposema majimbo yatajitegemea kutoka tax base ipi??? Kurun mabunge ya majimbo, kurun serikali za majimbo, kurun bunge la jamhuri, zanzibar blah blah hizo gharama hamzioni???

3) Yaani katika option zote za kudeal na CCM, hii ndio the best??

Hamna hata wabunge 10%, mnataka kubadilisha mfumo mzima from which mandate???
Kwa nini kama kweli nyie mnauelewa mkubwa, kwa nini mnashindwa kuchukua hata majimbo 5 katika nchi nzima?? How can U guys turn around and dare to say we want to change the whole system???

4) Issue kubwa sasa hivi ni rasilimali na uchumi wa nchi, mkishindwa kutokea hapo, TRUST ME mtakuwa mmepoteza upenyo ambao sijui utatokea lini tena.

Hivi kweli wale ndugu zangu pale Moshi, wakati huu suala la chakula la dunia na mafuta yanavyopanda, badala ya kuwahimiza kuwa kilimo kifufuliwe na rasilimali za nchi zisiibwe, unawaletea oh Jamani eeh kuna mfumo wa majimbo, AMA KWELI ISHI UONE VIOJA!!!!

Also for the sake of argument, let us look at this scenario::::

Sera ya Majimbo imekubalika na ndio sera ya Tanzania. What next?? Si CCM itashinda hayo majimbo na mabunge yake kama inavyoshinda sasa hivi, wabunge na madiwani?? Sasa kwa nini mnahangaika na suala gumu kama la majimbo ambalo hata kama likikamilika, still CCM ndio washindi??

Kwa nini system ya madiwani ambayo kwa kweli ndio iko karibu mno na wananchi, hamutafuti njia za kushinda huko??? Mkishinda hata Halmashauri say 50, kati ya hizo 100+, labda ndio muanze kuongelea mambo mengine.

sorry guys kwa maneno ya jazba, BUT I CAN NOT FATHOM WHAT U GUYS ARE TRYING TO DO> IT is a FIASCO OF BIBLICAL PROPORTION.

Wewe ungekuwa kwenye kikao cha kuamua kama binadamu aende mwezini or not, sasa hivi tusingekuwa na satelite technology!
 
Mwafrika wa Kike,https://www.jamiiforums.com/showthread.php?t=13407&page=22
Bibe samahani huwezi kabisa kulinganisha satelite technology na swala linalozungumziwa hapa..Hata Iran wamerusha satelite..
Na kwa tabia kama hii ndio maana naogopa sana viongozi wa Tanzania ambao kila siku huja na sababu ambazo hazilingani na issue iliyopo ubaoni...
Sema tu Moelex23 kagusa pale panapo uma sana...
 
Mwafrika wa Kike,
Bibe samahani huwezi kabisa kulinganisha satelite technology na swala linalozungumziwa hapa..Hata Iran wamerusha satelite..
Na kwa tabia kama hii ndio maana naogopa sana viongozi wa Tanzania ambao kila siku huja na sababu ambazo hazilingani na issue iliyopo ubaoni...

Mkandara,

Mimi nakuelewa vizuri na muda wote nimekuwa kimya nasoma maoni yenu wakuu na kupata shule ya nguvu. Ninapinga tu swala la kukataa hii idea kwa sababu tu ya pesa.

Kusema kuwa hakuna pesa za kuendesha serikali za majimbo wakati mabilioni yanatumika kuendesha serikali kuu sasa hivi sio sababu ya msingi. Ni makosa kukataaa wazo zuri kwa vile tu hakuna pesa za kulifanya.

Nimelinganisha kukataa wazo hili na kupinga teknologia ya satelite kwa vile wapinzani wakubwa wa exploration ya mwezini miaka ya sitini walikuwa wanalalmikia gharama na sio idea yenyewe.

Ukiangalia moelex analalamikia gharama na sio wazo lenyewe.
 
Unajua nashindwa kujua watu .Yaani Chadema lazima iwe tofauti na CCM.Kila Chama na sera zake then tuone zipi zauzika .Maana zinaweza kuachwa lakini tunapo taka changes si viongozi pekee bali hata sera sasa utofauti huo bado unashangaa ?Well tuendelee na mjadala nitazama humo baadaye .
 
Mkandara,

Mimi nakuelewa vizuri na muda wote nimekuwa kimya nasoma maoni yenu wakuu na kupata shule ya nguvu. Ninapinga tu swala la kukataa hii idea kwa sababu tu ya pesa.

Kusema kuwa hakuna pesa za kuendesha serikali za majimbo wakati mabilioni yanatumika kuendesha serikali kuu sasa hivi sio sababu ya msingi. Ni makosa kukataaa wazo zuri kwa vile tu hakuna pesa za kulifanya.

Nimelinganisha kukataa wazo hili na kupinga teknologia ya satelite kwa vile wapinzani wakubwa wa exploration ya mwezini miaka ya sitini walikuwa wanalalmikia gharama na sio idea yenyewe.

Ukiangalia moelex analalamikia gharama na sio wazo lenyewe.

Tufanye hivi, wekeni kando kwa muda issue ya GHARAMA.
Tuangalie mengine aliyohoji mwenzetu moelex23

.
 
Tufanye hivi, wekeni kando kwa muda issue ya GHARAMA.
Tuangalie mengine aliyohoji mwenzetu moelex23

Hayo mengine ya Molex kama kusaidia chakula na mafuta ni mambo ambayo CHADEMA inayafanya kila leo. usisahau kuwa wanachadema nao ni watanzania.

kinachogomba ni ukimya wa serikali iliyoko madarakani - ya kifisadi ya ccm - kushindwa kuyashughulikia. Mengine yote anaeleza kitu kinachojulikana kuwa CHADEMA na vyama vya upinzani wanataka pia kushinda bunge na halmashauri na ndio maana wanasimamisha wagombea. Katika haya hakuna jipya.

Bado hajatoa sababu ya kupinga wazo la majimbo zaidi ya kungangania status quo kama mzee wetu Kingunge.
 
Mwafrika wa Kike,
Nakuelewa wewe pia lakini muhimu kabla mtu hujashutumu ni muhimu kumwelewa mtoa hoja kwa sababu kama utasoma kwa makini hoja ya Meolex utaona kuwa katazama matatizo tuliyokuwa nayo sasa hivi na jinsi gani ya kuyaondoa.. yawezekana kabisa option yake kubwa ni Chadema kupata ushindi First priority..
Kisha swala la fedha ni muhimu sana kwa sababu ufujaji wa fedha wa CCM hauwezi kupachikwa sera ambayo pia inafuja fedha vile vile kwa sasa hivi.. Ni kutazama kwenda mwezini wakati huna fedha wala techonologia ya kutengeneza baiskeli acha mbali chakula chenyewe kuwalisha watu wako huna.

Binafsi nimekubaliana sana na mawazo yake kwa sababu kuu muhimu kuwa Majimbo ni issue kubwa sana kwa macho ya watu hata sisi wengine ambao tayari tunaishji nchi zenye mfumo huo huwa tunaona matatizo ya kisiasa yanazikuta Province (states)zenye uchumi duni. hawa wamekjuwa ktk mfumo huo kwa miaka kama sio karne..Hata hao South Africa kuna sehemu ukienda utafikiria sio nchi hiyo..
Chadema wanatakiwa kutazama sera ambazo zitaleta mageuzi ya matumizi ya fedha za serikaliili kuwafikia wananchi haraka iwezekanavyo, pengine within 100 days za kushika kwao madaraka, watu wataweza kuona tofauti kubwa ya utendaji kazi..

Lunyungu,
Changes ambazo zinaweza kuuzika sasa hivi ndio deal kubwa na mara nyingi changes watu huzitegemea ktk taratibu za uzalishaji kabla ya kufikiria changes za kugawana mavuno. Hii sera ya Majimbo ime base zaidi ktk kugawana umaskini, yaani Tajiri apate kuona Utajiri wake na maskini atajiju...Tatizo langu ni kwamba ikiwa leo tunashindwa kuondoa gap kubwa iliyopo kati ya matajiri na maskini kisha tunaunda mfumo ambao sasa utaingia level nyingine ya kuweka level ya tabaka za wealth inanitisha zaidi.
Asikuambie mtu hakuna kabisa kitu kinachosema kwamba ati majimbo watashindana.. hakuna nchi zinashindana kiuchumi acha majimbo.. Tanzania hatushindani na Kenya kwa maendeleo wala Marekani haishindani na UK ama China isipokuwa kila mmoja wao anajaribu kuwekesha zaidi ktk Uuzalishaji..Majimbo haina guarantee ya uzalishaji na hii ndio hofu yangu kubwa kwamba hakuna kipengele chochote ndani ya kupanga uongozi kinachomfanya mwananchi afikirie kuzalisha zaidi isipokuwa kutugawa makundi kama ktk mkeka wa kisomo cha Hitma...watu watasubiri hilo pilau toka kwa viongozi hawa.
Mfumo mzima wa Majimbo hauna jibu wala motivation ktk uzalishaji, uwajibikaji ambao hivi sasa ndilo tatizo letu kubwa..
 
Back
Top Bottom