šHECHE AITAKA SERIKALI KUHARAKISHA MCHAKATO WA MARIDHIANO NCHINI
Na Mwandishi Wetu
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Heche, ameitaka serikali kuharakisha mchakato wa maridhiano nchini, akisisitiza kuwa hatua hiyo ndiyo njia sahihi ya kudumisha amani, utulivu na mshikamano wa kitaifa.
Akizungumza leo katika mkutano uliofanyika katika Kata ya Kibamba, Heche amesema kuwa maridhiano ni msingi muhimu wa kujenga taifa lenye umoja na maendeleo endelevu.
Alieleza kuwa jamii haiwezi kusonga mbele ikiwa itaendelea kugubikwa na migawanyiko na misuguano ya kisiasa, hivyo ni wajibu wa serikali kuweka kipaumbele katika juhudi za kuleta maelewano miongoni mwa wananchi.
āMaridhiano ni njia sahihi ya kudumisha amani na utulivu nchini. Serikali inapaswa kuharakisha mchakato huu kwa maslahi ya taifa letu,ā alisema Heche mbele ya wananchi waliojitokeza kwa wingi katika mkutano huo.
Katika hotuba yake, Heche pia aliwataka wananchi kuwakataa wanaharakati wanaochochea vurugu na migogoro nchini, akidai kuwa vitendo vya uchochezi vinaweza kuhatarisha amani iliyojengwa kwa muda mrefu.
Alisisitiza kuwa wananchi wanapaswa kuwa waangalifu na watu wanaotumia majukwaa mbalimbali kueneza chuki na kuwagawa Watanzania kwa maslahi binafsi.
āTusikubali kuyumbishwa na wale wanaotaka kuturudisha nyuma kwa kuchochea vurugu. Amani yetu ni tunu kubwa ambayo lazima ilindwe kwa nguvu zote,ā aliongeza.
Kauli hiyo imekuja wakati ambapo mijadala kuhusu maridhiano na mshikamano wa kitaifa inaendelea kushika kasi katika maeneo mbalimbali nchini.
Wananchi wa Kibamba waliohudhuria mkutano huo walionesha kuunga mkono kauli za Heche, wakisema kuwa amani na utulivu ni msingi wa maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.

- Tunachokijua
- April 27, 2026, Makamu Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) John Heche alienda Kibamba kuhudhuria mkutano maalum wa jimbo la Kibamba, wakati akielekea huko pia alisimamishwa na wananchi alipokuwa kwenye kituo cha mabasi cha Magufuli, Mbezi.
Madai
Baada ya kufanya mikutano hiyo kumeibuka taarifa kupitia mitandao mbali mbali ya kijamii ikieleza kuwa Heche ameitaka serikali kuharakisha maridhiano na pia akiwataka wananchi kulinda amani na kutowasikiliza wanaharakati.
Uhalisa wa Taarifa hizo
JamiiCheck imefuatilia hotuba ya John Heche aliyoitoa APril 26, 2026 akiwa Kibamba na kubaini kuwa hakutoa kauli hizo.
Ufuatiliaji zaidi umebaini kuwa hakuna chanzo chcochote cha kuaminika nchini kilichochapisha taarifa hiyo ama kumnukuu Heche kutoa ujumbe huo ukilinganisha na namna taarifa hiyo ingekuwa kubwa iwapo ingekuwa ya kweli.
Kupitia hotuba ilichopishwa katika mtandao wa Youtube wa Mwanzo TV, John Heche aligusia haswa kuhusu ripoti ya uchunguzi wa matukio ya uvunjifu wa amani ya Jaji Chande, Msemaji wa Serikali Gerson Msigwa kuwaita watu Nguchiro na mambo mengine