Mtu wa Pwani
JF-Expert Member
- Dec 26, 2006
- 4,184
- 671
Sifahamu kwa nini umeshangaa kwa CHADEMA kutimiza wajibu wake kwa watanzania, Chadema imekuwa ikifanya shughuli zake Zanzibar siku nyingi sana tu, tupo na tutaendelea kutimiza wajibu wetu kwa watanzania, ukija maeneyo ya Kidongo Chekundu karibu na Kidongo Chekundu Seondari utatukuta hapo, na utajua kwamba na sisi Zanzibar ni kwetu, taarifa uliyoisoma ni matokeo ya kongamano lililoandaliwa na Kurugenzi ya Vijana Ofisi ya Makao Makuu Zanzibar, ni sisi Wazanziri wenzako tulio na mawazo zaidi nje ya CCM na CUF, tunahitaji siasa ambazo hazitatufanya tuwachukie wengine hivyo moto huu tulioanza kuuwasha utaendelea na wewe kama ni mzalendo kweli unapaswa kuunga mkono juhudi hizi badala ya kukejeli.
CHADEMA ni chama chenye watu wastarabu sana, japo kuna kale kaukiritimba ka ukabila, tunategemea watajilekebisha,CHADEMA kujipanga hapa zanzibar ni siku nyingi ila lengo ni kuwaondoa ccm.
Sijui huyu mdudu ukabila CHADEMA ATAONDOKA LINI. Kuna maelezo mengi yameshatolewa kupinga hii dhana ya ukabila lakini watu bado wameshikia bango. Si vema kuanza kuangalia safu ya juu bila kuangalia ndani. Wale wanaoona ukabila si waje na data kuthibitisha kwa mfano wananchama kwa kabila. Labda inawezekana watu wa kabila la mwenyekiti hutamba kuwa wao ndio CHADEMA halisi sababu mwenyekiti mwanzilishi anatoka kabila moja na wa sasa. Hili ni potofu kwani Mtei hakuanzisha chama peke yake bali kulikuwa na wengine kama Bob Makani. Ikumbukwe uchaguzi ulifanywa kihalali na mgombea mmoja kushinda na hakukuwa na hoja ya ukabila kutumika kupata ushindi toka kwa wajumbe au wagombea wengine. Labda nikumbushe hoja hii ya ukabila ilivyowahi kujibiwa na Nyerere UDSM 1978 alipolalamikiwa kuhusu ukabila uliokuwepo katika kupandisha vyeo wanataaluma UDSM ukipendelea kabila la wachaga chini ya Prof. Kimambo, pengine kulikuwa na ukweli, jibu lilikuwa , je mwulizaji (Dr. Chemponda) kama angelifurahi kufika na kukuta wengi ni wa kwao? Japo ilikuwa ni puupu ya JKN ujumbe ulifika. Ilikuondoa hisia hizo basi watu wa makabila mengine wajiunge na CHADEMA ili uwingi wao ulete picha halisi 'wanayoipenda'. Kimsingi uwingi wa watu wa kabila moja kuwa wengi katika chama cha siasa hauepukiki kama kujiunga kutafuata wa kwetu. Kwa hili viongozi wa Chadema, walifanyie kazi kwa kupiga kampeni za kujenga chama kule ambako kuna wanachama wachache. Kelel hizi, japo hazina msingi, huweza kuyumbisha watu wakati wa upigaji kura ukiwadia na wapinzani wenu wakizitumia vizuri. Kuna wapigaji kura wachache sana ambao hupiga kura kimchama damudamu, wengi wao ni wale(undecided voters) ambao huamua ukaribiapo uchaguzi
Wakati wananchi wakipigana na ufisadi wa ccm kwenye kuiba na kuuza mali ya nchi. CCM na wapambe wao wanajaribu kupambana kwa kuonesha kuwa vyama vya upinzani ni vya kidini (CUF) na kikabila (CHADEMA) bila kukumbuka kuwa hapa JF kuna mtu pia alisema kuwa zaidi ya 75% ya viongozi wa ccm ni kutoka dini fulani na zaidi ya asilimia 50 ya watendaji wake wa juu ni kutoka sehemu fulani ya Tanzania.
Bado najiuliza kuwa nini kipimo gani kinatumika kujua kabila la mtu kama mwenyewe hajalisema?
Aunti:
Nje ya mada. Mimi nataka kujiunga na CHADEMA, kuna pilikapilika gani za kufuata?
Kumfanya Rais wa Zanzibar kuwa makamu wa Rais sio sahihi hata kidogo!
Kwa sababu kumfanya makamu wa Rais unamaanisha anaweza kuwa Rais ikiwa matukio fulani yatatokea kwa Rais.
Hii ina maana kuna siku Tanzania itaongozwa na ni mtu aliyechaguguliwa na watu wachache sana; wapiga kura wa zanzibar ambao nadhani sio zaidi ya 350,000.
Najua kuna mtu atasema kwani Waziri Mkuu amechaguliwa na Watu wangapi... lakini mashariti ya katiba yanasema waziri mkuu lazima awe mbunge wa kuchaguliwa na pili lazima apitishwe na bunge hivyo basi... kwa kuwa anabitishwa na wawakilishi wa wananchi wote wa Tanzania ndio maana ana hadhi ya kumkaimu rais.
Aunti:
Nje ya mada. Mimi nataka kujiunga na CHADEMA, kuna pilikapilika gani za kufuata?
Karibu Bin Maryam. Ingia hapa na fuata maelekezo: http://www.chadema.net/maelezo/fomu/uanachama.php
Karibu Bin Maryam. Ingia hapa na fuata maelekezo: http://www.chadema.net/maelezo/fomu/uanachama.php
Good move Kitila. Ningeomba pia ukasaidia kujibu maswali kuhusu magugu wengine tuliyouliza ili iweze kusaidia kupata wanachama wengi zaidi wanaoiona CHADEMA kama chama cha kikabila.
.................................