CHADEMA yaanza kujipanga zanzibar?

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,184
671
niliposoma hii makala suali la kwanza nililojiuliza hivi chadema wameanza kujipanga huko kwetu kwa kuanza na wasomi au vipi?

sawa tunawakaribisha

Wataka rais wa Z`bar awe Makamu wa Rais

2008-04-28 09:03:26
Na Mwinyi Sadallah, Zanzibar

Wanafunzi wa vyuo vikuu Zanzibar wamependekeza Rais wa visiwa hivyo ashike nafasi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, ili awe na hadhi ya kimataifa anapokuwa nje ya nchi.

Waliyasema hayo katika kongamano la vijana wa vyuo vikuu Zanzibar lililokwenda pamoja na maadhimisho ya miaka 44 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Kongamano hilo liliandaliwa na Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA).

Akizungumza katika kongamano hilo, mmoja wa wanafunzi Bw. Haji Habib Kombo, wa Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Zanzibar, alisema, marekebisho ya 11 ya Tanzania iliyofuta wadhifa wa Rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Rais yanapaswa kuangaliwa upya.

Alisema mfumo uliokuwa ukitumika miaka ya mwanzo ya Muungano ulikuwa mzuri kwa vile ulimwezesha Rais wa Zanzibar kuwa na hadhi ya kimataifa anapokuwa nje ya nchi kama kiongozi wa Tanzania.

Marekebisho ya katiba yaliyofuta Rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano yalifanyika mwaka 1995 na kuweka utaratibu wa kuwa na mgombea mwenza.

Alieleza kuwa mfumo wa uongozi katika serikali hivi sasa Waziri Mkuu anaonekana msaidizi wa Rais kuliko Makamu wa Rais.

Aidha, alisema kitendo cha Rais wa Zanzibar kuingia katika Baraza la Mawaziri wa Muungano kama Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum hakileti tafsiri inayokubalika katika kuimarisha Muungano.

Mwanachuo Yahya Alawi kutoka Chuo Kikuu cha Afya Mbweni alishauri kero za Muungano zitatuliwe haraka kwani zinachangia kuzorotesha maendeleo ya Zanzibar.

Alisema utatuzi ukiendelea kuchelewesha utaleta athari kwa vizazi vijavyo kwa vile wananchi hawatakubali kuendelea na Muungano usio na faida kiuchumi.

Alikumbusha kuwa wakati umefika hati ya Muungano kuonyeshwa hadharani ili kama kuna mapungufu yarekebishwe.

``Tuwe na Muungano unaokubalika baina ya pande zote, tunahofia vijana baadaye tutakuja kukamatana kutaka kujua faida na hasara za Muungano,`` alisema mwanafunzi huyo.

Issa Kheri kutoka Chuo Kikuu cha Elimu Chukwani alisema ni jambo la kushangaza tume nyingi zimeundwa kushughulikia kero za Muungano, lakini utatuzi haujafanyika.

Alisema iwapo mapendekezo ya ripoti ya Jaji Robert Kisanga yangetekelezwa kero nyingi zingekuwa zimetatuliwa.

Aliongeza kuwa kuna matatizo mengi ya Muungano na kutaka wananchi kupewa fursa ya kuamua kwa njia ya kura ya maoni kuhusu aina ya Muungano wanaotaka.

Akifungua kongamano hilo, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar, Bw. Said Mzee, alisema uwezo mdogo wa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi umesababisha visiwa hivyo kuwa na matatizo makubwa.

Alisema wawakilishi wanashindwa kukosoa serikali na kutetea kero za wananchi.

Bw. Mzee alisema wajumbe wa baraza hilo wanaburuzwa na serikali kutokana kuwa na uwezo mdogo ikilinganishwa na wenzao wa Bunge la Muungano.

SOURCE: Nipashe
 
Sifahamu kwa nini umeshangaa kwa CHADEMA kutimiza wajibu wake kwa watanzania, Chadema imekuwa ikifanya shughuli zake Zanzibar siku nyingi sana tu, tupo na tutaendelea kutimiza wajibu wetu kwa watanzania, ukija maeneyo ya Kidongo Chekundu karibu na Kidongo Chekundu Seondari utatukuta hapo, na utajua kwamba na sisi Zanzibar ni kwetu, taarifa uliyoisoma ni matokeo ya kongamano lililoandaliwa na Kurugenzi ya Vijana Ofisi ya Makao Makuu Zanzibar, ni sisi Wazanziri wenzako tulio na mawazo zaidi nje ya CCM na CUF, tunahitaji siasa ambazo hazitatufanya tuwachukie wengine hivyo moto huu tulioanza kuuwasha utaendelea na wewe kama ni mzalendo kweli unapaswa kuunga mkono juhudi hizi badala ya kukejeli.
 
Endeleeni na moyo huu huu.Siasa is uadui ni maisha ya wananchi mwisho wa siku .Maisha mazuri na maendeleo ya Nchi yanategemea na utashi wa wanasiasa na sera zao.Kila jambo jema Chadema Zanzibar
 
Kumfanya Rais wa Zanzibar kuwa makamu wa Rais sio sahihi hata kidogo!

Kwa sababu kumfanya makamu wa Rais unamaanisha anaweza kuwa Rais ikiwa matukio fulani yatatokea kwa Rais.

Hii ina maana kuna siku Tanzania itaongozwa na ni mtu aliyechaguguliwa na watu wachache sana; wapiga kura wa zanzibar ambao nadhani sio zaidi ya 350,000.

Najua kuna mtu atasema kwani Waziri Mkuu amechaguliwa na Watu wangapi... lakini mashariti ya katiba yanasema waziri mkuu lazima awe mbunge wa kuchaguliwa na pili lazima apitishwe na bunge hivyo basi... kwa kuwa anabitishwa na wawakilishi wa wananchi wote wa Tanzania ndio maana ana hadhi ya kumkaimu rais.
 
Chadema imekuwa ikijipanga zanzibar miaka ile ilipokuwa inaungana na CUF kwenye kukubali mgombea wa CUF kwenye nafasi ya uraisi.
 
CHADEMA ni chama chenye watu wastarabu sana, japo kuna kale kaukiritimba ka ukabila, tunategemea watajilekebisha,CHADEMA kujipanga hapa zanzibar ni siku nyingi ila lengo ni kuwaondoa ccm na kwa kuwa CUF wameshakuwa na pa kushika, basi waachiwe hapa zanzibar
 
Ni hatua nzuri lakini wanapashwa kuenda hatua nyingi mbele zaidi hasa kufungua matawi na kuhakikisha wanaweka viongozi makini wa matawi hayo wenye kueleza kwa ufasaha malengo ya chadema siyo kuishia mijini tu.
 
Sijui huyu mdudu ukabila CHADEMA ATAONDOKA LINI. Kuna maelezo mengi yameshatolewa kupinga hii dhana ya ukabila lakini watu bado wameshikia bango. Si vema kuanza kuangalia safu ya juu bila kuangalia ndani. Wale wanaoona ukabila si waje na data kuthibitisha kwa mfano wananchama kwa kabila. Labda inawezekana watu wa kabila la mwenyekiti hutamba kuwa wao ndio CHADEMA halisi sababu mwenyekiti mwanzilishi anatoka kabila moja na wa sasa. Hili ni potofu kwani Mtei hakuanzisha chama peke yake bali kulikuwa na wengine kama Bob Makani. Ikumbukwe uchaguzi ulifanywa kihalali na mgombea mmoja kushinda na hakukuwa na hoja ya ukabila kutumika kupata ushindi toka kwa wajumbe au wagombea wengine. Labda nikumbushe hoja hii ya ukabila ilivyowahi kujibiwa na Nyerere UDSM 1978 alipolalamikiwa kuhusu ukabila uliokuwepo katika kupandisha vyeo wanataaluma UDSM ukipendelea kabila la wachaga chini ya Prof. Kimambo, pengine kulikuwa na ukweli, jibu lilikuwa , je mwulizaji (Dr. Chemponda) kama angelifurahi kufika na kukuta wengi ni wa kwao? Japo ilikuwa ni puupu ya JKN ujumbe ulifika. Ilikuondoa hisia hizo basi watu wa makabila mengine wajiunge na CHADEMA ili uwingi wao ulete picha halisi 'wanayoipenda'. Kimsingi uwingi wa watu wa kabila moja kuwa wengi katika chama cha siasa hauepukiki kama kujiunga kutafuata wa kwetu. Kwa hili viongozi wa Chadema, walifanyie kazi kwa kupiga kampeni za kujenga chama kule ambako kuna wanachama wachache. Kelel hizi, japo hazina msingi, huweza kuyumbisha watu wakati wa upigaji kura ukiwadia na wapinzani wenu wakizitumia vizuri. Kuna wapigaji kura wachache sana ambao hupiga kura kimchama damudamu, wengi wao ni wale(undecided voters) ambao huamua ukaribiapo uchaguzi
 
Wakati wananchi wakipigana na ufisadi wa ccm kwenye kuiba na kuuza mali ya nchi. CCM na wapambe wao wanajaribu kupambana kwa kuonesha kuwa vyama vya upinzani ni vya kidini (CUF) na kikabila (CHADEMA) bila kukumbuka kuwa hapa JF kuna mtu pia alisema kuwa zaidi ya 75% ya viongozi wa ccm ni kutoka dini fulani na zaidi ya asilimia 50 ya watendaji wake wa juu ni kutoka sehemu fulani ya Tanzania.

Bado najiuliza kuwa nini kipimo gani kinatumika kujua kabila la mtu kama mwenyewe hajalisema?
 
Aunti:

Nje ya mada. Mimi nataka kujiunga na CHADEMA, kuna pilikapilika gani za kufuata?
 
Kumfanya Rais wa Zanzibar kuwa makamu wa Rais sio sahihi hata kidogo!

Kwa sababu kumfanya makamu wa Rais unamaanisha anaweza kuwa Rais ikiwa matukio fulani yatatokea kwa Rais.

Hii ina maana kuna siku Tanzania itaongozwa na ni mtu aliyechaguguliwa na watu wachache sana; wapiga kura wa zanzibar ambao nadhani sio zaidi ya 350,000.

Najua kuna mtu atasema kwani Waziri Mkuu amechaguliwa na Watu wangapi... lakini mashariti ya katiba yanasema waziri mkuu lazima awe mbunge wa kuchaguliwa na pili lazima apitishwe na bunge hivyo basi... kwa kuwa anabitishwa na wawakilishi wa wananchi wote wa Tanzania ndio maana ana hadhi ya kumkaimu rais.

Kasheshe bwana unanifurahisha sana siku hizi, yaani umeamua kutete kila kinachofanya/kilichofanywa na serikali ya CCM. Yaani siku zote tulikuwa na makamu wa Rais hapakutokea shida yeyote leo ndio unasema kwamba sio sawa kuongozwa na mtu aliyechaguliwa na watu 300,000? Wewe unafikiri hadhi ya kiongozi inatokana na idadi ya watu waliomchagua tu? Tulishakwambia kwenye ile thread ingine kuwa nchi haiwi kwa sababu tu ya idadi ya watu au sehemu ilipo kijiografia. Nchi inapatikana kwa sababu za historia za kujipambanua na kujikomboa. Usifanye mchezo mkuu, Zanzibar ni nchi kamili kabisa na walijiunga na Tanganyika kwa hiari na uhuru wao kabisa na wala muungano haukuwa na maana ya kuwanyang'anya utaifa wao. Kwa Rais wa Zanzibar ni kiongozi kamili mwenye hadhi sawa na nchi ingine yeyote na hili haliathiriwa na idadi ya watu waliomchagua.

Wenzako tunajua kwamba waliamua kutoa cheo cha makamu wa Rais kwa upande wa Rais wa Zanzibar kwa sababu ya kuogopa Rais wa Muungano w CCM kukaa meza moja na Rais wa Zanzibar ambaye alikuwa awe CUF. Sababu zilikuwa za kibinafsi na kiitikadi na wala sio hizo unazosema wewe. Ingekuwa swala ni hilo Mzee Karume, Jumbe na Abdul Wakil wasingepata kuwa makamu wa pili wa Rais ukizingatia kwamba kipindi hicho hawa watu walichaguliwa na watu wachache kabisa kuliko miaka ya hivi karibuni. Usiniambie kwamba historia hii ndogo umeshaisahau mara hii!
 
wasiende mijini tu hata vijijini wafike. Mimi ni mbara lakini nafikiri kama makubaliano ya mwanzo yalikuwa ni kuwa rahisi wa zanzibar awe makamu wa kwanza wa raisi nafikiri hili lazima wapewe nafasi yao. Hivi raisi wa zanzibar ana status gani akiwa nje ya nchi kikazi? inawezekana mimi sifahamu maana nilijua anapewa heshima kama raisi wa sehemu ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania
 
Good move Kitila. Ningeomba pia ukasaidia kujibu maswali kuhusu magugu wengine tuliyouliza ili iweze kusaidia kupata wanachama wengi zaidi wanaoiona CHADEMA kama chama cha kikabila.

.................................

Utaishia kubadili jina na kutumia lingine maana viongozi wa chadema hawana muda na mtu mwenye chuki za kikabila na kidini kama wewe!
 
Good move Kitila. Ningeomba pia ukasaidia kujibu maswali kuhusu magugu wengine tuliyouliza ili iweze kusaidia kupata wanachama wengi zaidi wanaoiona CHADEMA kama chama cha kikabila.

Vyama vyote kama sio ukabira basi vina udini, sioni sababu ya wewe kuwa na wasiwasi kama unataka kurudisha kadi ya kijani wewe rudisha tu.
 
Wakati wananchi wakipigana na ufisadi wa ccm kwenye kuiba na kuuza mali ya nchi. CCM na wapambe wao wanajaribu kupambana kwa kuonesha kuwa vyama vya upinzani ni vya kidini (CUF) na kikabila (CHADEMA) bila kukumbuka kuwa hapa JF kuna mtu pia alisema kuwa zaidi ya 75% ya viongozi wa ccm ni kutoka dini fulani na zaidi ya asilimia 50 ya watendaji wake wa juu ni kutoka sehemu fulani ya Tanzania.

Bado najiuliza kuwa nini kipimo gani kinatumika kujua kabila la mtu kama mwenyewe hajalisema?

Kwa mujibu wa Katiba Waziri Mkuu aweza kuwa Rais likitokea lolote. Lakini amechaguliwa na na chini ya watu wa Zanzibar. Mfano Pinda alichaguliwa na watu wachache tu wa Mpanda Mashariki lakini aweza kuwa Rais likitokea lolote.

Hivyo, hoja yako umeijenga ndivyo sivyo. Mimi nina mawazo tofauti kabisa kuhusiana na Mkuu wa serikali ya Zanzibar. Naungana nawe Rais wa Zanzibar asiwe Makamu wa Rais, lakni sio kwa hoja uliyoijenga hapo Juu.

Tukumbuke- kwa mujibu wa Makubaliano ya Muungano, Rais wa Zanzibar ndio Makamu wa Rais wa Muungano. Hamad, pigeni kazi Zanzibar
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom