Chadema wekeni wazi wagombea ubunge 2025 katika majimbo haya, mtashinda sababu wabunge waliopo wamekosa ubunifu

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
879
4,118
Majimbo yote ya Arusha na Kilimanjaro Kwa kuzingatia Aina ya nguvu ya upinzani huko na wabunge waliopo Kwa SASA NI wazi mkiwapelekea wananchi wagombea serious wanapata endorsement before 2025.

Mkoa mtwara majimbo yote hayana mtetezi wanasubiri watetezi wafike, anzieni kwenye mikutano ya adhara wananchi wanatamani watu wa kuwaamsha wabunge waliopo wakumbuke kurejea majimboni watoke DSM.

Iringa, Mbeya na Mbeya Panakosa thinkers, pamepooza na fursa za maendeleo zinaminywa. Uhalifu unaongeza kutokana na kuongezeka Kwa idle mind na mara zote ubongo usipotumikishwa unabaki kuwaza utovu.

Rukwa na Katavi hakuna wabunge kuna watu wanasubiri kumaliza muda wako, tumieni fursa ya mikutano ya sasa kupeleka watu watakaoibua Kero za wananchi Kwa maandalizi ya 2025.

Mwanza pambalu peke yake Naona amekimbiza vyakutosha na ngome za CCM zimetingishwa....bado mnapaswa kutafuta viumbe zaidi hasa wasomi wanaoweza kusimamia jiji lile liwe na tija Kwa wananchi. Ziwa Victoria limeachwa Bila kusimamiwa na mchango wake kwenye pato la Taifa unashuka...tumieni hii fursa kuamsha waliolala Ila epukeni kulala ninyi

Shinyanga Hali Kwa baadhi ya majimbo ikiwemo Shinyanga mjini inaridhisha, mnafanya vizuri Ila ongezeni nguvu eneo hili kutingisha ngome za CCM waamke wakawaletee wafugaji maendeleo

Singida Lisu anayo kazi yakufanya, Imani kubwa waliyonayo ndugu zake asiipoteze, atengeneze sussion plan Kwa kuandaa vijana na wazee wakumsaidia kupambana huu mkoa NAO uwe kwenye fomu.

Dar wala msitumie nguvu kubwa Kwa Sababu Ubungo pako wazi, kawe pako wazi, segerea pako wazi, mbagala hakuna mwakilishi, kigamboni hakuna kitu pale NI amasa Tu na kuchagua timu nzuri.....Kwa Mzee wa Tozo ilala tieni kiumbe mwenye nguvu kuondoa fikra za zamani kwenye ramani ya jiji.

Fikeni Morogoro, watu wameumizwa wanahitaji tumaini jipya; changamkeni tokeni ndani jamii inawategemea at list Mhe. Rais aone maeneo yenye shida na ajue namna ya kupanga safu na kuondoa viongozi mzigo kwenye mfumo wake.

Salum mwalimu anafanya vyema Zanzibar sajilini wachezaji wa ziada mtanishukuru.

Msipomsaidia Mama kuonyesha udhaifu Leo NI vigumu kwenu kwenda kuonyesha udhaifu kwenye kampeni 2025....muda NI sasa nisaidieni kuwaletea wananchi maendeleo
 
Ubabe aliotumia Magufuli kukata moto wa CHADEMA ni strategy nzuri sana lakini matunda yake ni mida mfupi-ingawa kwa mida huo mfupi CCM tunapata kuendelea kushikilia kijiti.

Inaweza ikawa rahisi kwa CDM kuibuka tena na vilevile inaweza kuwa ngumu-itategemeana na wao walivyojipanga.

By the way,CCM tupo tumeongoza mida mrefu tumechokwa hasa na vijana na watu ambao ni thinkers watu wanahitaji mabadiliko-tatizo hawapo tayati kuchukua effort kwa ajili ya mabadiliko.Katika hatua hii ndipo CDM wanapata kazi.
 
Hakuna Wabunge nchi nzima, Spika yule Fundi Cherahani lazima atoke Mbeya mjini
 
Ubabe aliotumia Magufuli kukata moto wa CHADEMA ni strategy nzuri sana lakini matunda yake ni mida mfupi-ingawa kwa mida huo mfupi CCM tunapata kuendelea kushikilia kijiti.

Inaweza ikawa rahisi kwa CDM kuibuka tena na vilevile inaweza kuwa ngumu-itategemeana na wao walivyojipanga.

By the way,CCM tupo tumeongoza mida mrefu tumechokwa hasa na vijana na watu ambao ni thinkers watu wanahitaji mabadiliko-tatizo hawapo tayati kuchukua effort kwa ajili ya mabadiliko.Katika hatua hii ndipo CDM wanapata kazi.
Nakubaliana nawe 100% na naimani wataanza kujijenga mapema kupitia mikutano hii ya hadhara kwaajili ya kujenga chama na kuvuna wanachama wapya. Hakuna namna zaidi ya kuongea madhaifu ya wawakilishi wa maeneo hayo bungeni na serikali kiujumla ili kuwashawishi wananchi waweze kuwaamini CDM.
 
Back
Top Bottom