CHADEMA wazungumze na Zitto na ACT

CHADEMA wazungumze na Zitto na ACT

Zitto kama chuki na Mbowe ni shauri lake, lakini CHADEMA sio Mbowe wakati ACT ni Zitto. Ina maana bila Zitto ACT hamna lolote kwa sasa hivi, ila bila Mbowe CHADEMA ipo na itaendelea kuwepo. CDM sio chama cha msimu kama ACT. Usaliti wa Zitto hauna ubishi.[/QUOTE yero hayo maneno yako umeyaongea upo sawa! mbowe ndie kilakitu chadema yeye ndie mungu mtu wa cdm, naujue kelele zenu zote kwa ztt ni kupitia mbowe, mbowe ndie chanzo cha yote jua ACT haina mwaka lakin leo kila mkutano wa cdm lazima waizungumzie ACT
 
Last edited by a moderator:
Siku hizi umebaki kuandika utumbo tu huku,kibaraka wa zito wew ....

mjinga mwenyewe

Mnaji dhalilisha mkiwa mnajibu kwa jazba na kutoelewa
mtu akiandika 'wajinga' na akiandika wajinga ....hayo ni maneno mawili tofauti...
sasa wewe badala ya kuelewa unajibu kama umetukanwa...
 
Mkuu kuna vitu unapaswa kuviweka maanani pia
Zitto kama binadamu ana makosa yake....na ni binadamu mwenye emotions pia
anaamini sana kuwa ana mchango mkubwa kwa 'kukua kwa CHADEMA'
na yeye anaamini CHADEMA 'wamemsaliti' kwa hiyo kuwa na hasira nao kibinaadamu ni very obvious
kuhusu kuungwa mkono na CCM.....Zitto anaweza kuamini kuwa 'anawatumia' CCM to his advantages
ndo maana nasema in politics hakuna 'black or white' kuna so many colors

Hiyo imani ya ZZK kuwa amesalitiwa sidhani kama ni kweli kwa sababu yeye alivyoanza mchakato wake na waraka wake alifanya 'risk/benefit' analysis. Na kuna uwezekano mkubwa alijua atafukuzwa na ndio maana na ACT aliianzisha akiwa bado yupo CDM.

Hilo la kuamini kuwa 'anawatumia' CCM for his adavantages sio kweli, ukweli ni CCM ndio wanaomtumia for their advantages.
 
Kwani wameshindwana na CCM mpaka waanze negotiation na CDM??Na kwa nn negotiation iwe na act na siyo TLP au SAU???
Hayo maswari gani? kwani ukawa ni cdm? act wanataka kujumuika na ukawa na si cdm maana kuna cuf,nccr pia nld wacheni kujivika koti la ukawa kama mlivyo lalamikia Tanganyika dhid ya Znbr
 
The Boss naona kuna ukweli fulani. Hata Zito keshaona alivyofikiria sivyo. Kwahiyo atakuwa amejifunza kitu fulani na nirahisi kumfanyia monitoring akiwa ndani ya ukawa. Zito ameshambuliwa kuwa yeye strategic objective ya kushinda na vyama vya upinzani badala ya chama tawala kama kawaida ya vyama vya upinzani.
 
...Timu ya mpira kama Barcelona inachukua watoto masikini kama kina Messi
ina wa train na kuwapa kila kitu hadi wanakuwa 'masuper star' wakubwa
wakishakuwa wakubwa 'hawaitwi wasaliti' wakihama timu kutafuta maslahi.... vipi CHADEMA...why take the risks?

Vipi mchezaji anapouza mechi? Zitto wa sasa hana hadhi mnayopambana kumpa humu... FUNGU LA KUKOSA!
 
Hiyo imani ya ZZK kuwa amesalitiwa sidhani kama ni kweli kwa sababu yeye alivyoanza mchakato wake na waraka wake alifanya 'risk/benefit' analysis. Na kuna uwezekano mkubwa alijua atafukuzwa na ndio maana na ACT aliianzisha akiwa bado yupo CDM.

Hilo la kuamini kuwa 'anawatumia' CCM for his adavantages sio kweli, ukweli ni CCM ndio wanaomtumia for their advantages.

Kweli au si kweli ni maoni yako tu
ukweli halisi mimi na wewe hatuujui kama anatumiwa au anawatumia
only history will tell us
 
Hayo maswari gani? kwani ukawa ni cdm? act wanataka kujumuika na ukawa na si cdm maana kuna cuf,nccr pia nld wacheni kujivika koti la ukawa kama mlivyo lalamikia Tanganyika dhid ya Znbr

unakurupuka tu huelewi hata title ya thread inasemaje rudi kasome tena,ni wapi kuna neno UKAWA
 
Mkuu utaona sijasema akaribishwe moja kwa moja UKAWA
nimesema tu CHADEMA waanze kuzungumza nae...labda anataka majimbo mawili tu au matatu
aachiwe na UKAWA au jimbo lake tu moja....na wao wana UKAWA in return wanaweza kumpa masharti
labda ACT wasisimamishe mgombea kwa Lissu na Mdee....na hapo labda ukawa 'mwanzo mpya'

Wanasema in Politics there are no permanent enemies nor permanent friends....

Haina haja ya kujadiliana kuhusu kugawana majimbo, mbona haina ulazima. Yeye kama kiongozi wa chama anaweza kusimamisha wagombea katika majimbo yote 239 ya TZ. Mbona hujasema ukawa waongea na TLP, UDP, na wengineo. Mgombea wake akiweza kumtoa Lissu au Mdee basi, hawatakuwa wa kwanza kushindwa ubunge. Haina ulazima wa UKAWA kuzungumza na ZZK. Na kwanini utaje tu majimbo ya Lissu, Mdee hujui kuwa hapa TZ kuna majimbo mengine 237 hujayataja.
 
Vipi mchezaji anapouza mechi? Zitto wa sasa hana hadhi mnayopambana kumpa humu... FUNGU LA KUKOSA!

Mnazungumza kihisia au halafu mkidanganywa na viongozi wa CDM mnaamini
walimtuhumu kuwa alizungumza na Nimrod Mkono kumuachia jimbo for price
ukifuatilia zile tuhuma Zitto alikuwa ana report kwa mtu ndani ya CHADEMA
hakua na final say.....kote ambako CHADEMA hawakusimamisha wagombea Zitto hakua na final say
lakini in the end 'msaliti' ni Zitto but aliokuwa ana report kwao wenye final say sio wasaliti
bottomline maamuzi yote ya majimbo yapi CHADEMA waweke mgombea au la..Zitto hakua na final say..
kumuita msaliti kwa hilo ni kichekesho......kulikuwepo na mtu au watu wenye final say...je hawakupokea chochote?
 
Haina haja ya kujadiliana kuhusu kugawana majimbo, mbona haina ulazima. Yeye kama kiongozi wa chama anaweza kusimamisha wagombea katika majimbo yote 239 ya TZ. Mbona hujasema ukawa waongea na TLP, UDP, na wengineo. Mgombea wake akiweza kumtoa Lissu au Mdee basi, hawatakuwa wa kwanza kushindwa ubunge. Haina ulazima wa UKAWA kuzungumza na ZZK. Na kwanini utaje tu majimbo ya Lissu, Mdee hujui kuwa hapa TZ kuna majimbo mengine 237 hujayataja.

Lissu na Mdee kwangu ni watu muhimu bungeni
kama wewe ni mwana CHADEMA na unafikiri hao wako equal na wagombea wote wa CHADEMA kina
Shibuda na Msigwa basi hata wewe ni kazi bure kukuelewesha
sio Lissu na Mdee hata Mnyika anapaswa kupewa free pass na upinzani wote
 
Ukisema Zitto hana mchango wowote aliochangia CHADEMA hizo ndo hisia
hisia za chuki.......Ukisema Zitto ni msaliti kwa ukaribu wake na CCM unapaswa kujibu
mbona Mbatia ni mbunge wa kuteuliwa na Mwenyekiti wa CCM na mwenyekiti mwenza wa UKAWA?

Sijasema hana mchango wowote, actually anao mchango wake CHADEMA kufika hapo ilipo. Lakini yeye alihitaji kuwa juu CDM kwa njia za kugawa chama, alifanya waraka kwa siri na mengine kama hayo. Ni kwa sababu ya Intelligensia ya CDM iliomuumbua na waraka huo, ni kwa sabab ya intelligensia ilimuumbua Kagenzi, ni kwa sababu ya intelligensia ndio maana CDM wakasema anatumiwa na CCM kwa kupewa fedha kuvunja CDM. Hizo intelligensia ndio zinafanya asiaminiwe kwa sasa ingawa alishiriki kujenga chama kama wanachama wengine.
 
...
what if akiweza kupata viti viwili vitatu na CHADEMA wakapoteza watu muhimu kama Lissu?
kutazama future kwa mahaba na vyama sio sahihi....

Na wewe unacheza karata ya umimi.... Lissu au la, tunajenga taasisi. Hakuna COMPROMISE na wasaliti. Kuna pimbi alicompromise na wezi wa EPA!! NO WAY.....
 
Siamini kama unajua vizuri ulichokileta hapa. Otherwise I remain to believe that you have come to test the rate of polarity. We have data on trivial deeds that zitto attempted in the right to come up with his mission (ccm missions). we are not fool enough to reject the guy. Hata hivo, chadema imevumilia kwa kiasi kikubwa sana mienendo hasi dhidi ya chama (chadema). Hebu fikiri kitu kingine kuliko hiki, madhara unayoyasema ni madogo kuliko kunegotiate naye. Au umetumwa?...stop there...

Mkuu kuna vitu unapaswa kuviweka maanani pia
Zitto kama binadamu ana makosa yake....na ni binadamu mwenye emotions pia
anaamini sana kuwa ana mchango mkubwa kwa 'kukua kwa CHADEMA'
na yeye anaamini CHADEMA 'wamemsaliti' kwa hiyo kuwa na hasira nao kibinaadamu ni very obvious
kuhusu kuungwa mkono na CCM.....Zitto anaweza kuamini kuwa 'anawatumia' CCM to his advantages
ndo maana nasema in politics hakuna 'black or white' kuna so many colors
 
Zitto kama chuki na Mbowe ni shauri lake, lakini CHADEMA sio Mbowe wakati ACT ni Zitto. Ina maana bila Zitto ACT hamna lolote kwa sasa hivi, ila bila Mbowe CHADEMA ipo na itaendelea kuwepo. CDM sio chama cha msimu kama ACT. Usaliti wa Zitto hauna ubishi.[/QUOTE yero hayo maneno yako umeyaongea upo sawa! mbowe ndie kilakitu chadema yeye ndie mungu mtu wa cdm, naujue kelele zenu zote kwa ztt ni kupitia mbowe, mbowe ndie chanzo cha yote jua ACT haina mwaka lakin leo kila mkutano wa cdm lazima waizungumzie ACT

Mbowe sio kila kitu CDM, sio Kiongozi wa Chama mwenye mamlaka kama Zitto. Lakini pia CDM ilikuwa na wenyeviti kabla ya Mbowe, kwa sababu ilianza zamani. Kelele zote za Zitto ni baada ya kutochaguliwa kuwa Mwwnyekiti wa CDM, anapenda madaraka huyo jamaa. Watu wangapi wapo CDM vichwa lakini hawajaenda kuanzisha vyama vyao, ingekuwa hivyo tungekuwa na vyama vya siasa kama MIA. Kiukweli inaonekana hujasikia Afande Sele anavyoongelea CDM kwenye mikutano ya ACT
 
Last edited by a moderator:
Sijasema hana mchango wowote, actually anao mchango wake CHADEMA kufika hapo ilipo. Lakini yeye alihitaji kuwa juu CDM kwa njia za kugawa chama, alifanya waraka kwa siri na mengine kama hayo. Ni kwa sababu ya Intelligensia ya CDM iliomuumbua na waraka huo, ni kwa sabab ya intelligensia ilimuumbua Kagenzi, ni kwa sababu ya intelligensia ndio maana CDM wakasema anatumiwa na CCM kwa kupewa fedha kuvunja CDM. Hizo intelligensia ndio zinafanya asiaminiwe kwa sasa ingawa alishiriki kujenga chama kama wanachama wengine.

Kuna kitu naona baadhi ya wanachama wa CDM wengi huwa hawapay attention
CDM ku make deals na CCM ilikuepo zamani sana hata kabla Zitto hajawa mbunge
hata mwaka 2005 CDM walishapanga deals na watu CCM ..zipo taarifa Kikwete angehamia CDM then agombee
urais kama asingepitishwa na CCM...na wakati fulani wakati CUF walikuwa na nguvu CDM ndo walikuwa
wana tuhumiwa kusaliti 'upinzani' kwa ufupi ni kuwa 'behind the scene politics'
sio jambo jipya CDM na CCM ku make deals ndo maana Shibuda akaenda CDM huku moyo wake ni CCM..

Sasa ni jambo lipi mtu akifanya anakuwa 'msaliti' na lipi akifanya ni okay....
hilo wanalijua kina Mbowe........Jiulize tu swali moja
inawezekana vipi CDM wasisimamishe wagombea au wasifanye kampeni kwa baadhi ya majimbo
kama majimbo ya Nimrod Mkono,Pinda na Mengineyo...kama Mwenyekiti ni Mbowe na katibu ni Slaa?
Zitto aliwezaje pata all that power na asiadhibiwe?why tuhma zimlenge yeye tu?
 
Kweli au si kweli ni maoni yako tu
ukweli halisi mimi na wewe hatuujui kama anatumiwa au anawatumia
only history will tell us[/QUO

Sidhani kama unategemea mimi kwa juhudi zangu binafsi niwe na ushahidi kuhusu kutumiwa kwa wanasiasa hapa TZ. Intelligensia ya CDM ilikuwa na data 'beyond reasonable doubt' kuhusu fedha za CCM zinavyotumwa kutoka Germany na CRDB kwenda kwa Zitto na mawaciliano yake na Usalama wa Taifa. Alikana, lakini mwenendo wake baada ya hapo kila mtu hata wewe unauona.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Wanaojua historia ya OAU na Morocco na mgogoro wa Sahara Magharibi watakumbuka alichowaambia Nyerere viongozi wenzie wa OAU wakati ule.

Nchi ya Morocco ilikuwa inakataa kila maazimio ya OAU ikisisitiza Sahara Magharibi ni ardhi yake Viongozi wengi wakasema dawa ni kuifukuza Morocco OAU.

Nyerere alipinga na hoja kubwa ilikuwa ukishaifukuza Morocco then what? utawezaje kuidhibiti wakati
sio member wako tena?si unaipa uhuru wa kufanya lolote? nguvu ya kidhibiti Morocco ni only kama Morocco ni member wa OAU...otherwise akishakuwa sio member hatalazimika tena kuisikiliza OAU.Viongozi hawakusikia the rest is history..mgogoro haujaisha hadi leo..

Ni kama ile hadithi ya mtoto anaekojoa sebuleni halafu unamfukuza anaenda kusimama nje anakojoa mkojo akitokea nje kupitia dirishani unaingia sebuleni tena...hujafanya kitu labda uongee na huyo mtoto ujue analilia nini labda kuna pipi tu karibu akipewa its done...

Kuelekea Uchaguzi 2015 CHADEMA now ndio chama cha upinzani chenye nguvu kuna UKAWA ambapo CHADEMA ndio wenye nguvu zaidi na sauti zaidi...Sasa ingawa CHADEMA wanashikilia msimamo wao ambao ni very 'radical' wa kutoongea na Zitto na kuwaita
ACT 'wasaliti' ukweli ni kwamba njia rahisi ya kuidhibiti ACT ni kuongea nao na kujua hasa 'wanataka nini' na kuwapa masharti ya kujiunga na UKAWA na vinginevyo ACT wanaweza kabisa 'kukojoa kutokea dirishani' na the rest ikawa historia.

ACT ikiwa ndani ya UKAWA ..CHADEMA watakuwa na uhakika wa baadhi ya viti vya ubunge watu kama Tundu Lissu,Mbowe na Halima Mdee watapata 'nafuu' ya kupambana na CCM only kuikataa ACT ni kuwaruhusu ACT waweke wagombea wao wa ubunge kwa Lissu,Mdee,Mbowe na wote wengine

sio lazima hao wagombea washinde..lakini wanaweza kugawa kura...the rest will be history.

Najua wapo watu ndani ya CHADEMA wana obsession ya kummaliza Zitto....tatizo ni kwamba 'no one knows the future' .....watu wenye akili hukubali ku negotiate when they have power and are strong watu wajinga huenda ku negotiate wakiwa wameshashindwa au kujeruhiwa.

CHADEMA now they have power....wasisubiri kujeruhiwa.

Zitto should be given total blackout we already know alichokitaka ni kugawa kura so nini kijadiliwe? Akaribishwe tena ili avujishe siri za chama na kukidhoofisha zaidi.

Ni wakati wa kukutana uwanjani aisee. Athibitishe kwamba anaweza kujenga chama chenye itikadi ya kijmaa lakini viongozi ni mabepri.

Let Zitto prove Chadema wrong or otherwise. Mtoto akililia wembe dawa ni kumpa akijikata ndo ataelewa
 
Back
Top Bottom