CHADEMA wazungumze na Zitto na ACT

CHADEMA wazungumze na Zitto na ACT

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Posts
49,320
Reaction score
117,654
Wanaojua historia ya OAU na Morocco na mgogoro wa Sahara Magharibi watakumbuka alichowaambia Nyerere viongozi wenzie wa OAU wakati ule.

Nchi ya Morocco ilikuwa inakataa kila maazimio ya OAU ikisisitiza Sahara Magharibi ni ardhi yake Viongozi wengi wakasema dawa ni kuifukuza Morocco OAU.

Nyerere alipinga na hoja kubwa ilikuwa ukishaifukuza Morocco then what? utawezaje kuidhibiti wakati
sio member wako tena?si unaipa uhuru wa kufanya lolote? nguvu ya kidhibiti Morocco ni only kama Morocco ni member wa OAU...otherwise akishakuwa sio member hatalazimika tena kuisikiliza OAU.Viongozi hawakusikia the rest is history..mgogoro haujaisha hadi leo..

Ni kama ile hadithi ya mtoto anaekojoa sebuleni halafu unamfukuza anaenda kusimama nje anakojoa mkojo akitokea nje kupitia dirishani unaingia sebuleni tena...hujafanya kitu labda uongee na huyo mtoto ujue analilia nini labda kuna pipi tu karibu akipewa its done...

Kuelekea Uchaguzi 2015 CHADEMA now ndio chama cha upinzani chenye nguvu kuna UKAWA ambapo CHADEMA ndio wenye nguvu zaidi na sauti zaidi...Sasa ingawa CHADEMA wanashikilia msimamo wao ambao ni very 'radical' wa kutoongea na Zitto na kuwaita
ACT 'wasaliti' ukweli ni kwamba njia rahisi ya kuidhibiti ACT ni kuongea nao na kujua hasa 'wanataka nini' na kuwapa masharti ya kujiunga na UKAWA na vinginevyo ACT wanaweza kabisa 'kukojoa kutokea dirishani' na the rest ikawa historia.

ACT ikiwa ndani ya UKAWA ..CHADEMA watakuwa na uhakika wa baadhi ya viti vya ubunge watu kama Tundu Lissu,Mbowe na Halima Mdee watapata 'nafuu' ya kupambana na CCM only kuikataa ACT ni kuwaruhusu ACT waweke wagombea wao wa ubunge kwa Lissu,Mdee,Mbowe na wote wengine

sio lazima hao wagombea washinde..lakini wanaweza kugawa kura...the rest will be history.

Najua wapo watu ndani ya CHADEMA wana obsession ya kummaliza Zitto....tatizo ni kwamba 'no one knows the future' .....watu wenye akili hukubali ku negotiate when they have power and are strong watu wajinga huenda ku negotiate wakiwa wameshashindwa au kujeruhiwa.

CHADEMA now they have power....wasisubiri kujeruhiwa.
 
ACT-Wazalendo imeundwa kwa misingi ya kuwa anti-Chadema. Sasa utawashirikishaje kwenye UKAWA ambapo Chadema ndicho chama kikuu? Kajipange upya.

Hata Makaburu walizungumza na ANC licha ya kuwafunga na kuwaua
kuzungumza sio lazima mkubaliane...CHADEMA wanaweza kutoa 'masharti' ya kuikubali ACT ndani ya UKAWA
ikabaki kazi ya ACT kukubali au kukataa masharti
 
Makaburu walizungumza na ANC baada ya kuona kuwa hali huko mbele kwao si nzuri, hasa baada ya jeshi lao kushindwa kule Cuito Cuanavale, Angola na jeshi la Cuba/MPLA. They had lost the military leadership in South Africa.
Zitto amepoteza nini? He is anti-Chadema, and he is there kubomoa Chadema, kwa nini mtu kama huyu mmweke kwenye kundi lenu?
 
Ni kama unasema hadi Zitto apate nguvu ya kuijeruhi na kuiumiza CHADEMA ndo wakae nae kujadili
kama CHADEMA wanaamini Zitto is out to destroy CHADEMA that is a more reason to negotiate with him..
Zitto sio stupid anauwezo wa ku reason....ACT haiwezi moja kwa moja kuwa as big as CHADEMA overnight
it will take time...now kwa sasa watafute 'suluhu' ili wapeane space badala ya kutumia nguvu kubwa kujeruhiana...
 
...Najua wapo watu ndani ya CHADEMA wana obsession ya kummaliza Zitto....tatizo ni kwamba
'no one knows the future' .....watu wenye akili hukubali ku negotiate when they have power and are strong watu wajinga huenda ku negotiate wakiwa wameshashindwa au kujeruhiwa......CHADEMA now they have power....wasisubiri kujeruhiwa......
You might have had a valid argument lakini kwa tamko hili, umeharibu kila kitu. Unadai unajua wapo watu ndani ya CHADEMA wana obsession ya kummaliza Zitto! My God The Boss, are you serious? Je na mimi nikidai najua wapo watu ndani ya ACT wana mission/obsession ya kuidhoofisha Chadema? Kweli tutaelewana? La pili; upi ni ushauri wako kwa Zitto?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu unaweza ukawa unatumia busara bila kujua damage ambayo CHADEMA wameshapata tayari, wakati Zitto akiwa DGS, na Baada ya kufukuzwa....CHADEMA wko makini sana, kwa maoni yangu pengine this is beyond recovery, Zitto mwenyewe hayuko tayari kwa hilo, hakuna ambalo hakusikia hadi kuunda Chama ndani ya Chama na kujitaidi kuwashawishi wanachama waasi chama, mpinzani anapendwa na Chama tawala na kusifiwa sana, walau hata kupata rabsha ya kuwa mpinzani....... leo mnakaa meza moja kudiscuss..... ni kusaliti damu za watanzania Iringa, Morogoro na Soweto Arusha
 
Ni kama unasema hadi Zitto apate nguvu ya kuijeruhi na kuiumiza CHADEMA ndo wakae nae kujadili
kama CHADEMA wanaamini Zitto is out to destroy CHADEMA that is a more reason to negotiate with him..
Zitto sio stupid anauwezo wa ku reason....ACT haiwezi moja kwa moja kuwa as big as CHADEMA overnight
it will take time...now kwa sasa watafute 'suluhu' ili wapeane space badala ya kutumia nguvu kubwa kujeruhiana...
No, sijasema kuwa Chadema wazungumze na Zitto tu pale atakapokuwa na nguvu za kuijeruhi na kuimaliza Chadema. Tayari Zitto anaamini kuwa hizo nguvu anazo. Ninachosema ni kwamba Chadema isonge mbele without Zitto. Namfananisha Zitto na Zuberi Mtemvu 1959 alipojitoa TANU kwa kutokukubaliana na sera za TANU kuhusu uraia wa Tanganyika na kuanzisha chama chake cha Congress. Katika uchaguzi uliofuata TANU ilifunika na Mtemvu akawa history. The same fate awaits Zitto and his party.
 
Hata Makaburu walizungumza na ANC licha ya kuwafunga na kuwaua
kuzungumza sio lazima mkubaliane...CHADEMA wanaweza kutoa 'masharti' ya kuikubali ACT ndani ya UKAWA
ikabaki kazi ya ACT kukubali au kukataa masharti

Yaani kama kuna kosa kubwa na kihistoria ambalo Chadema watafanya ni kukubali ACT wajiunge Ukawa, Kutenda kosa si kosa ila kurudia kosa. Zitto siku zote huwa anaona mawazo yake ndiyo yanafaa na ni mtu anaependa madaraka. Mtu anayependa sifa sana. Ukawa itasambalatika endapo ACT itaungana nao. Tatizo sio ACT ila ni yule kiongozi mkuu. Na inawezekana ule mpango wa kuivuruga Chadema ulivyobuma inawezekana CCM wanataka ajiunge Ukawa ili aendelee kufanya kazi yao.
 
Mbona kuna nguvu kubwa sana kutaka ACT iwe sehemu ya ukawa na si TLP au UDP au DP n.k.? ACT inafahamika ni chama kilichoanzishwa baada ya kutofautiana ndani ya chama kimoja kinachounda ukawa, kama ilivyo chama (nafikiri ADC) kilichoanzishwa na Ahmed Rashid wa CUF, lakini sisikii kikitokea. Hapa kuna nini nyuma ya pazia? Viongozi wa ACT sijasikia wakisemea hili, lakini kwenye mitandao kila wakati hii imekuwa ajenda ya Kudumu. Ushirikiano unatakiwa uwe wa watu wenye misimamo au ajenda zinazofanana...
 
Mtoa maada umepagawa! Kurusi Zitto hawezi penya Jimboni kwa Lissu
 
Ni kama unasema hadi Zitto apate nguvu ya kuijeruhi na kuiumiza CHADEMA ndo wakae nae kujadili
kama CHADEMA wanaamini Zitto is out to destroy CHADEMA that is a more reason to negotiate with him..
Zitto sio stupid anauwezo wa ku reason....ACT haiwezi moja kwa moja kuwa as big as CHADEMA overnight
it will take time...now kwa sasa watafute 'suluhu' ili wapeane space badala ya kutumia nguvu kubwa kujeruhiana...

The boss uko vizuri bg up kwa logical argument
 
You might have had a valid argument lakini kwa tamko hili, umeharibu kila kitu. Unadai unajua wapo watu ndani ya CHADEMA wana obsession ya kummaliza Zitto! My God The Boss, are you serious? Je na mimi nikidai najua wapo watu ndani ya ACT wana mission/obsession ya kuidhoofisha Chadema? Kweli tutaelewana? La pili; upi ni ushauri wako kwa Zitto?

Ushauri wangu kwa Zitto nimeutoa humu
kuna thread nimesema Zitto ajifunze kusema 'we' na 'sisi'
kama anataka 'bright future'ya kisiasa..ukisoma between the line ni ushauri mkubwa

Kuhusu hiyo ya mimi kuamini wenye Obession...well you can ignore me
kumbuka CHADEMA hawa deal na mimi hapa......but Zitto is out there kuendelea kumuita msaliti na kum ignore
na the fact yeye Zitto ana 'machungu' yake binafsi na individuals ndani ya CHADEMA kutapekelea asiwe
na kizuizi cha kuweka wagombea kwenye majimbo ambayo tunapenda kuona wabunge wake wakirudi bungeni
hivi Suppose ACT waweke mgombea kwa Tundu Lissu achukue kura za kutosha hadi Lissu ashindwe
unafikiri hilo ni jeraha dogo?
the way kuzuia hilo ni ku negotiate na Zitto baasi
 
Najua wapo watu ndani ya CHADEMA wana obsession ya kummaliza Zitto....tatizo ni kwamba 'no one knows the future' .....watu wenye akili hukubali ku negotiate when they have power and are strong watu wajinga huenda ku negotiate wakiwa wameshashindwa au kujeruhiwa.

CHADEMA now they have power....wasisubiri kujeruhiwa.
Mkuu The Boss, hii ni kitu inayoitwa busara za hali ya juu!, it is very unfortunately, Chadema haina watu wenye busara za level hii, wengi wao wanatawaliwa na chuki dhidi ya Zitto, hawataki kuchukua 'tahadhari yoyote kabla ya hatari', bali wako tayari kwa 'majuto ni mjukuu!'. Maadam umesema kuhusu wenye akili wanafanya nini na wajinga watafanya nini, sisi tukiwaita watu ni wajinga humu, tutashutumiwa tunawatukana!, nasisitiza Watanzania kama hawako tayari kuwaingiza 'wajinga' kwenye ikulu yao!.

Kuliko kuingia ikulu na ujinga wao, bora wakae na ujinga wao huko huko, mpaka watakapo pata akili ndipo tuwakabidhi ikulu yetu!.

Pasco
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom